Tamko la serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam juu ya ripoti ya makinikia

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,875
2,000
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU DAR ES SALAAM (DARUSO) TAMKO LA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM JUU YA RIPOTI YA TUME YA PILI YA KUCHUNGUZA KIWANGO CHA MADINI KWENYE MAKONTENA YA MCHANGA (MAKINIKIA) Ndugu wanahabari sisi WANA DARUSO tunapenda kuchukua fursa hii adhimu kwa mara ya pili ya kumpongeza Mh. Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi ngumu za kizalendo anazoendelea kuzifanya kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Kwanza, ndugu Wana habari sisi wana DARUSO tumefarijika sana kwa kazi ya Mh. Rais wetu alivyolishughulikia suala hili la Mchanga wa Madini (Makinikia). Tofauti na wale wanasiasa wanaobeza juhudi zake sisi wana DARUSO tunapenda kumuhakikishia Mh. Rais wetu kuwa tuko pamoja nae kifikra, kimikakati na kimaombi kuhakikisha kuwa fedha iliyopaswa kulipwa na ACACIA kwa Tanzania tangu 1998 hadi 2017 zinalipwa mara moja. Ndugu wana habari tunasema kwa masikitiko makubwa sana kuona nchi yetu inageuzwa kuwa “SHAMBA LA BIBI” kwani ripoti ya kamati iliyoongozwa na Professor Ossoro imebainisha kuwa “Pesa zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu ama kujenga reli ya standard (gauge) kutoka Dsm mpaka Mwanza!” Kwa pesa ya kiwango hiki ndugu wana habari kwenye huduma za jamii kila mtoto mwanafunzi wakitanzania angepaswa kupata kitabu chake binafsi cha kusomea cha kila somo na asingekosa dawati la kukalia na wale wa vyuo vya elimu ya juu hawakupaswa kwa nyakati tafouti wagome kwanza ndio wapatiwe fedha za mikopo ya kujikimu. Pili, ndugu wana habari tunapenda kumpongeza Mh. Rais kwa muelekeo mzuri wa juhudi zake za Kizalendo zilizomfanya Mwenyekti Mtendaji wa Kampuni ya (Afica) Barrick Gold Mining Professor John Thornton kuja Tanzania kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu kama alivyonukuliwa kusema: “I have assured the president we are very interested in…..reaching resolution which is a win-win situation. A win for Tanzania, a win for Barrick and our subsidiary company
ACACIA.” (John Thornton, 14.06.2017, STATE HOUSE DAR ES SALAAM). Hivyo basi ndugu wanahabari kutokana na maelezo ya hapo juu tunawaomba watanzania wa makundi yote tuungane ili tukumuunge mkono Mh. Rais na tuache kubeza juhudi zake za kizalendo na zakihistoria katika kupigania uhuru na ukombozi wa kiuchumi wa Taifa letu. Tatu, ndugu wanahabari pamoja na hayo yote yaliyoainishwa hapo juu tunapenda kushauri: Mh. Rais asiwateue kwenye timu ya majadiliano wale wanasiasa wote wanaobeza na kupinga juhudi zake katika suala la madini ili kuleta ufanisi wa matokeo chanya ya majadiliano hayo yenye maslahi makubwa kwa Taifa letu. Nne, ndugu wana habari tunatanabahisha kuwa wanasiasa hawa ni wakuogopwa kama “UKOMA” kwa usaliti huu wa “KI-SAVIMBI” na ni watu hatari kwa UHAI na USALAMA wa Taifa letu kwa kuwatetea MABEBERU na kuweka pembeni na kutelekeza maslahi ya Taifa letu. Kitu kibaya zaidi hawa wanasiasa ni wanasheria na wachumi waliosoma UDSM. Je hayo ndio malipo yao kwa watanzania? Sisi wana DARUSO tunasema wameitia aibu taasisi yetu na hawakustahili kusoma kwa kodi za watanzania na kupata Digrii ya chuo chetu. Kwa usaliti wa kiwango hiki wanasiasa hawa hawatofauitishwi na YUDA ESCARIOT aliyemsaliti YESU KRISTO na kama wangekuwa kwenye timu ya waliopigania na kuutafuta Uhuru wa Tanzania kwenye miaka ya 1960 chini ya Mwl JK Nyerere na Mzee Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) wasingejali kuwasaliti waasisi wa Taifa kwenye harakati za kuikomboa nchi yetu kwenye Makucha ya WAKOLONI. Pia wanasiasa hawa wangekuwa sambamba na Mzee wetu Abeid Amani Abeid Karume kule Zanzibar basi Mapinduzi matukufu 1964 yasingepatikana kwa usaliti wa kiwango hiki cha kujali sana kuweka mbele maslahi binafsi. Mwisho, Wana DARUSO tunapenda kukumbusha kuwa vita hii sio ya chama chochote cha siasa bali ni vita ya watanzania wote kwa hivyo tusimame na kuungana na Mh. Rais wetu Dkt. JPM kwenye mapambano haya. Asanteni sana kwa kunisikiliza, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki DARUSO na Mungu M-bariki Rais wetu Mpendwa Dkt. JPM Imetolewa na DARUSO na kusomwa na Rais wa DARUSO Engineer John Jeremiah Jilili (+255 687 548 035) tarehe 16.06.2017
 

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
636
1,000
Andiko murua kutoka Kwa wanaojiita wasomi!
Ni kweli kwamba watu hao mnaowaeleza kuwa wapingaji hawakustahili kupata hilo li digrii la hicho chuo, kwani ni aibu kupata hilo li digrii katika chuo chenye wasomi wa aina hii, tena wanaowakilisha wanachuo wenzao.
Kama viongozi ndio mko hivi, hao wengine wakoje?
Duh, wasomi wasiofahamu historia ya taifa Lao, wako wapi na tunatakiwa kwenda wapi!
Eti karume aliongoza mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya 1964!
Kuwa Na wasomi wa aina ya kupongeza na kusifia vitu bila utafiti ni heri kuwa na kundi la watoto wa chekechea ambao watauliza na kudadisi kabla ya kutoa mtazamo wao kama hawa wasomi.
Poleni wana habari, nafikiri nisingevumilia kusikiliza utumbo huu hata kama ninaandikia gazeti la Uhuru
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom