Tamko la serikali kuhusu mgomo wa madktari

jamani yaani hatuli tukashiba; madaktari madaktari, hatuogi tukatakata: mgomo mgomo, hatupigi stori tukacheka; pinda pinda. mbona serikali ilishatoa tamko lake siku ya Jumapili kuwa daktari ambaye ataendelea na mgomo ifikapo jumatatu (jana) ajihesabu kuwa hana kazi. tamko gani tena linatakiwa?

Kamanda ni afadhali na wewe umesema bana! yaani hatuna muda wa kujadili mambo mengine kila wakati ni hayo hayo tu?
 
mawaziri na wabunge msijidai kuwa mgomo huu unaathiri walalahoi pekee.kama sio ndugu yako basi hata wewe unaweza kukuathiri.leo hii ukipata ajali mitaa ya bombo ni lazima ufikishwe hapo bombo kabla ya kwenda india?je ukikuta bombo wamegoma utapona kweli?hili linawahusu tusijisahau....
 
jamani yaani hatuli tukashiba; madaktari madaktari, hatuogi tukatakata: mgomo mgomo, hatupigi stori tukacheka; pinda pinda. mbona serikali ilishatoa tamko lake siku ya Jumapili kuwa daktari ambaye ataendelea na mgomo ifikapo jumatatu (jana) ajihesabu kuwa hana kazi. tamko gani tena linatakiwa?
Haya tungelee mambo ya Davos, anza!

Kamanda ni afadhali na wewe umesema bana! yaani hatuna muda wa kujadili mambo mengine kila wakati ni hayo hayo tu?
mkuu kinachojadiliwa ni uhai wa mtanzania.sijui utajadili na nani kama watu watapoteza maisha.
 
Serikali gani tena mkuu...mhimili yote chali...hatuna watu wa kutoa maamuzi mpaka mwananchi ukaona kweli tuna watawala. Kule juu kumepwaya vibaya mno...hapa kati kwa mawaziri hakuna kitu blah blah na siasa ndio nyingi!!!utawasikia mara tuko kwenye process mara cijui mchakato...hakuna kitu full longolongo. Bunge ndio kabisaaaa...wengi ni watu wa ndioooo wakiongozwa na bi mkora......pembeni kule kwenye mashirika ya umma kila mtu anaangalia tumbo lake....full ufisadi. Hii nchi tumepoteza dira... kosa letu kubwa watanzania ni watu wa kutake easy mambo ambayo ni serious kwa taifa, kusahau ishu nyeti kwa muda mfupi, uoga n.k. SISI NDIO WAAJIRI WA HAWA WATAWALA....NA SISI NDIO WENYE JUKUMU LA KUWAWAJIBISHA...KWA HIYO KAMA TUNASHINDWA KUCHUKUA HATUA INABIDI TUJILAUMU WENYEWE...HAIJALISHI KWA NJIA GANI....
 
Wafanyabiashara ya mafuta walipogoma jambo hili lilijadiliwa bungeni. Nadhani hili la Afya za

watanzania ni la umuhimu zaidi.
 
Acha unafiki bana,
Kupotoshwa? My underwear!
Mgogoro umedumu zaidi ya wiki tatu tangu madaktari interns walipoacha kazi kudai malipo yao.
Attempts zimefanyika nyingi za kuwasiliana na waziri mkuu na chama cha madaktari (MAT).
Hadi MAT wakaenda ofisini kwake na kagoma kuongea nao akawasakizia na secretari wake.
Mgomo ukaitishwa rasmi na ukadumu siku sita hali akijua madaktari wanamtaka wamalize mgogoro.
Ana vyombo vya usalama vinampelekea taarifa hata kama viongozi wa wizara ya afya wangem-disinform.
Alikuwa akijua yote na kuamua jinsi tulivoona.
Tusimtetee kuwa kapotoshwa.
Mkapa kakaa ikulu miaka 10 hatujawahi kusikia kapotoshwa.
kila leo JK kapotoshwa, Pinda kapotoshwa!
ehe! Potoshapotosha syndrome!

Mkuu hapo kwenye wekundu umenena la mbolea. Badala ya kupambana na malaria na kugawa vyandarua ambavyo watu wanalimia mchicha na kuvulia dagaa, wangejitahidi sana kutafuta tiba ya liugonjwa hili (Potoshwa Potoshwa Virus)
 
Acha unafiki bana,
Kupotoshwa? My underwear!
Mgogoro umedumu zaidi ya wiki tatu tangu madaktari interns walipoacha kazi kudai malipo yao.
Attempts zimefanyika nyingi za kuwasiliana na waziri mkuu na chama cha madaktari (MAT).
Hadi MAT wakaenda ofisini kwake na kagoma kuongea nao akawasakizia na secretari wake.
Mgomo ukaitishwa rasmi na ukadumu siku sita hali akijua madaktari wanamtaka wamalize mgogoro.
Ana vyombo vya usalama vinampelekea taarifa hata kama viongozi wa wizara ya afya wangem-disinform.
Alikuwa akijua yote na kuamua jinsi tulivoona.
Tusimtetee kuwa kapotoshwa.
Mkapa kakaa ikulu miaka 10 hatujawahi kusikia kapotoshwa.
kila leo JK kapotoshwa, Pinda kapotoshwa!
ehe! Potoshapotosha syndrome!

Hapana usimtetee Mkapa yeye ni sehemu kubwa ya matatizo tuliyo nayo. Amedai mara nyingi kuwa kapotoshwa alikuwa na ni mpotoshaji mkubwa. Ufisadi mkubwa nchini kaufanya yeye mpaka akanenepeana kama Tembo, miguu ikashindwa kuhimili uzito, ikabidi twende kumtibu Uswisi mwezi mzima.

Kwa hiyo kutaka kutofautisha kati ya Kikwete na Mkapa ni kama kutofautisha kati ya kitumbua na chips kwamba nani ana mafuta zaidi. Kwangu mimi hawana tofauti.
 
Ilikuwa mapema sana kwa serikali kutumia silaha kali na ya mwisho ya kutishia kufukuza kazi madkatari jumapili.
Matokeo yake ni total shutdown ya hospitali kama Muhimbili na MOI

Ndiyo matatizo ya siasa na uongozi wa kutotumia common sense...Bora boss wake ameamua kuwa mbayu wayu!!

PM alisahau kwamba wenzake hawana mzaha katika hili na siyo legelege kama wao...Sasa amejaribu kubeep, wakamtwangia; tena bila kujali gharama au kama international call...Anasubiri nini kukata hizo simu na kuomba msaada??

PM amepoteza credibility na serikali yote imezamishwa kwenye matope....Nangojea ultimatum ya specialists!!

Pinda na wenzake are in deep trouble!!

DC
 
Hapana usimtetee Mkapa yeye ni sehemu kubwa ya matatizo tuliyo nayo. Amedai mara nyingi kuwa kapotoshwa alikuwa na ni mpotoshaji mkubwa. Ufisadi mkubwa nchini kaufanya yeye mpaka akanenepeana kama Tembo, miguu ikashindwa kuhimili uzito, ikabidi twende kumtibu Uswisi mwezi mzima.

Kwa hiyo kutaka kutofautisha kati ya Kikwete na Mkapa ni kama kutofautisha kati ya kitumbua na chips kwamba nani ana mafuta zaidi. Kwangu mimi hawana tofauti.

Kweli kaka,

Baada ya Nyerere (pamoja na ubaya wake wote), CCM haijawahi kutupa kiongozi makini...Na kadri wanavyozidisha mizengwe na majungu...huko mbele ya safari kuna hatari wakatuletea mabomu ya kutisha na ambayo yatatulipukia any time...

Si unaona sasa hivi nchi inavyoishi kwa matumaini utadhani hatuna hata mtu mmoja wa kutupa ARVs??

DC
 
mbona kamati ya madaktari inayoratibu mgomo huu intoa taarifa mara kwa mara?iweje serikali ikae kimya?wabunge kama kweli mnawakilisha wananchi na kama kweli sis tuliwachagua basi hakuna budi kuwakilisha mawazo yetu.

Mkuu signature yako mie hoi hakika .Nimeipenda naomba ruhusa niitumie pia mkuu .
 
najua wengi wetu tunatamani kusikia tamko la serikali kuhusu mgomo wa madaktari.haieleweki kama serikali imewatimua madaktari waliogoma au la.haieleweki kama mgomo umekwisha au la.hatuelewi nini kinaendelea,je serikali imefanikiwa kudhibiti hali mbaya ya huduma kwenye mahospitali yaliyoko kwenye mgomo au la.pinda alisema tuvumilie sasa tunavumilia mpaka lini?mponda alisema yuko tayari kwa mazungumzo je madaktari wamekutana naye?ana makinda alisema tutarajie taarifa kutoka serikalini je tutasubiri mpaka lini?watanzania wanaendelea kufa au kuumia kwa kukosa huduma stahiki je tusubirie mpaka lini?tunawezaje kulazimisha tamko la serikali litoke ?je swala la mgomo wa madaktari sio kipaumbele kwa wabunge wetu?nahitaji tamko la serikali kama mwananchi niliyeathirika na mgomo huu.hatuwezi na kamwe tusikubali swala hili liende bila watu kuwajibika.mbunge wangu nifikishie ujumbe huu bungeni!wanajf na wananchi tushinikize kutolewa kwa tamko la serikali lenye muelekeo wa kuhitimisha mgogoro huu.

Nimeshasema hapa kwamba Serikali hii imejaa mataahira na ushahidi wa hili jinsi mambo yalivyo hivi sasa shaghala baghala. Rais wa nchi hata kusimama mbele ya Umma wa Watanzania kuongelea kuhusu hili swala la posho kunamshinda!!!! Swala muhimu kama hili anaongea kupitia kurugenzi yake ya Mawasiliano!!!!! Pia mgomo wa madakatari unaoendelea zaidi ya wiki sasa Rais wa nchi hajatia neno!!!! Huku Watanzania wakiendelea kufa na wengine kukosa huduma muhimu kwa matibabu mbali mbali wanayoyahitaji.

Kungekuwa na watu wenye akili timamu katika Serikali hii iliyopoa madarakani basi yote haya yangekuwa yameshazungumziwa kwa kinaga ubaga na kusingekuwa na utata wowote ule lakini kutokana na kujaa mataahira ndani ya Serikali hii kitu ambacho kimesababisha ombwe kubwa sana la uongozi nchini haijulikani nini kinachoendelea kuhusiana na mgomo wa madaktari na pia ongezeko la posho ya Wabunge. Wamethubutu wameweza na sasa wanasonga mbele!!!! Walidhani Urais ni lelemama na kuchekacheka!!!! Mungu inusuru nchi yetu.

I dont expect anything good from this country espeially from my lazy crazy government, The PM is on top bt infinite times he did so many blunders in his carrier. He is totally failure figure in the gava.

Less expectations, less dissapointments. Kwa hii nchi expect zero from gov ili uishi stress free
 
Acha unafiki bana,
Kupotoshwa? My underwear!
Mgogoro umedumu zaidi ya wiki tatu tangu madaktari interns walipoacha kazi kudai malipo yao.
Attempts zimefanyika nyingi za kuwasiliana na waziri mkuu na chama cha madaktari (MAT).
Hadi MAT wakaenda ofisini kwake na kagoma kuongea nao akawasakizia na secretari wake.
Mgomo ukaitishwa rasmi na ukadumu siku sita hali akijua madaktari wanamtaka wamalize mgogoro.
Ana vyombo vya usalama vinampelekea taarifa hata kama viongozi wa wizara ya afya wangem-disinform.
Alikuwa akijua yote na kuamua jinsi tulivoona.
Tusimtetee kuwa kapotoshwa.
Mkapa kakaa ikulu miaka 10 hatujawahi kusikia kapotoshwa.
kila leo JK kapotoshwa, Pinda kapotoshwa!
ehe! Potoshapotosha syndrome!

Miaka hii ya viongozi wasanii tutasikia mengi - mara kapotoshwa mara kashauriwa vibaya... yote hii ni USANII tu .. Mkuchika alishauriwa vibaya...

Hivi haya maelezo ya kupotoshwa na kushauriwa vibaya yana nafasi gani katika uwajibikaji ?

Kwa bahati mbay ni awamu hii hii iliyokuja na msemo wa ushauri wa mwenzako ogeza na za kwako---USANII..USANII ni aibu tupu ... leo naye na Shigela kwa macho maangavu kabisa, wanakuja kushauri [KUPOTOSHA??] baada ya mambo kudoda kama vile wametokea kwa jirani -hivi huko inner circles za Magamba huwa wanaongea nini?
 
Back
Top Bottom