Tamko la serikali kuhusu malalamiko dhidi ya matokeo ya somo la isamic knowledge kidato cha sita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la serikali kuhusu malalamiko dhidi ya matokeo ya somo la isamic knowledge kidato cha sita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Jul 1, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

  TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA 2012

  1.0 UTANGULIZI
  Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi.

  Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:
  Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na
  Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).

  2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI

  Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi.

  Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya "Paper" tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.

  2. Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una "paper" mbili na siyo "paper" tatu.
  Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia "paper" tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia "paper" mbili.

  3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
  Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na "paper" zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.

  Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012.

  Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012.

  Pia walifahamishwa kuwa matokeo yaoyote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama
  yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.

  Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.

  Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara yaElimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.

  4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU
  Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki.

  Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.

  5.0 HITIMISHO
  Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini.

  Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa.

  Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.
  Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa.

  Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini. Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu anayependekezwa kusahihisha mitihani.

  4. Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa ku.pendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata.

  Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili.

  Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.

  Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge.

  Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.

  IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA
  WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
  TAREHE 07/06/2012

  Kiganyi, JF.
  Mwanzo - wotepamoja.com
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Asante kwa taarifa,,,,makosa ya kibinadamu ni makosa kama yalivyo makosa mengine,,,,,,,,
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Yani wakuu wa shule za Kiislamu wana lalamikia kuhusu ufaulu wa somo hilo? Si ni wao ndiyo wanaolifundisha? AU?
   
 4. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  waislamu wenye akili na upeo tumewaelewa.. Hao wengine ponda n co.ltd achaneni nao
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Tunakushukuru waziri Kawambwa kwa ufafanuzi makini sana.Tumekuelewa.
   
 6. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Poor u NECTA.
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  kwahiyo hilo somo ndio msaada kwao? hawa ndio wale Division One HKL unakuta mtu ana A ya somo la dini mengine ubabaishaji tu
   
 8. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Sasa hilo somo lita wapeleka chuo kikuu?

  Halisaidii chochote kupata chuo!

  Labda kama kuna chuo cha usheikh!
   
 9. J

  John W. Mlacha Verified User

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  wataenda kusoma jinsi ya kuchoma makanisa
   
 10. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii barua ni ya muda mrefu kidogo! hata hivyo binafsi ninaishukuru wizara kwa kufuatilia malalamiko ya Waislamu.
  Baada ya shukrani ningeomba serikali itutoe wasiwasi kuhusu hili la kuwa mitihani baada ya kusahihishwa hukaa na watu fulani hivi kwa muda wa miezi miwili,hasahasa tukizingatia kuwa wasiwasi wetu hauko kwenye usahihishaji.
   
Loading...