Tamko la Serikali dhidi ya Reginald Mengi na Rostam Aziz

3. Kwa mfano, tarehe 23 Aprili, 2009, Bwana Reginald Mengi aliandaa Mkutano wa Waandishi wa Habari (Press Conference) ambapo aliyataja makampuni na wafanyabiashara watano wa hapa nchini, akiwamo Mheshimiwa Rostam Aziz, akiwaita kuwa ni "MAFISADI PAPA" na kuwaornba wananchi kuungana nave iIi kupambana na "mafisadi" hao.
8. Aidha, Serikali imebaini kwamba katika malumbano haya kumekuwepo na "matumizi mabaya" ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Bwana Mengi, (televisheni, magazeti na radio), na kwa Mheshimiwa Rostam Aziz, (magazeti). Kila mmoja ametumia vyombo vya habari anavyomiliki kwa manufaa yake binafsi kinyume na maelekezo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003, inayobainisha wazi kwamba:-
• Chombo eha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji bali kitatumiwa kwa manufaa ya umma;
• Chombo eha habari kiongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika; na
• Chombo eha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuehoehea uhasama.
10. Kutokana na hali hiyo basi, Serikali inawataka Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kupitia vyombo vya habari, na badala yake wawasilishe madai na vielelezo vyao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe,na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.

.
12. Aidha, Serikali inawataka Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz kuvitumia vyombo vyao vya habari kwa manufaa ya Wananchi wote wa Tanzania, na si kwa manufaa yao binafsi. Wakumbuke kwamba malumbano yao hayo kwa kutumia vyombo vyao binafsi, na wakati mwingine kuonekana kana kwamba wanalihutubia Taifa, ni kutowatendea haki watu wengine ama kampuni/mashirika ambayo yametajwa katika malumbano hayo, lakini hawana vyombo binafsi (redio, televisheni, rnagazeti) ambavyo wangeweza kuvitumia kujieleza na kujitetea kama walivyofanya Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Azizi.
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.
14. Aidha, Serikali inawatahadharisha Wahar;,.i wa Wanahabari kwa ujurnla kuwa makini katika kutirniza wajibu wao kwa weledi na kuzingalia maadili ya taalurna yao, badala ya kuandika au kutangaza habari kulingana na matakwa ya mmiliki wa chombo kinachohusika.

16. Mwisho, Serikali kwa mara nyingine inasisitiza kwamba mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi bade yanaendelea, na inawahimiza wananchi wote wenye taarifa za vitendo kama hivyo watoe taarifa hizo kwenye vyombo vya dol a vilivyopewa majukumu hayo, iIi hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.


Sina shaka yale niliyoyasimamia katika majadiliano humu jamvini serikali imeyaona na kuyachukua na kuyafanya kama sehemu ya tamko lake. Kufikiria huko hakuhitaji PhD bali ni uwezo wa kawaida tu wa kufikiri.
Sasa wale mabingwa wa kufabricate na kubadilisha maneno ili wawalishe wachangiaji wengine waendelee kufanya hivyo bila ya kuwa sahau wale wenye user ID zaidi ya moja nao waendelee kujaza threads.
Kwaaaheriii!!!!
 
Last edited:
Wewe bendera unakubali kutumiwa na wanaume wenzio kuonge urojo wa pweza!

Eti taifa limegawanyika makundi mawili. Umefanya utafiti gani. Kama ni makundi basi kuna kundi kubwa la watu wasiotaka ufisadi na kikundi kidogo cha kuwatetea wakina Rostam. Hii haitishii amani ya nchi. Hebu acheni ujanja wenu wa kuzima mjadala.

Maneno yako hayana tofauti na aliyoyasema Rostam, unashambulia kidogo upande wake ili uonekane neutral?

Nimekudharau sana leo, unaaabisha

Asha
 
Kwa hiyo Rostam anamiliki pia Habari Leo na Daily News. Hebu Bendera kuwa serious sio unakuwa Bendera kufuata upepo. Huku Pinda anasema lake kibendera nacho kinaanyooshwa upande wake! Hapo ni mwanzo tu mnaelekea kutaka kumshughulikia Mengi. wakati magazeti yaandika uwongo CHADEMA imemuua Wangwe na Mbowe amefukuzwa na mapanga hivi hamkuona uchochezi dhidi ya amani? Au akiguswa Rostam kwa ufisadi wake wa kweli ndio mnaanza kukurupuka?

Asha
 
Halafu huyo Naibu Waziri si anapaswa kushughulika na michezo huyo? Naona amevamia tasnia ya habari, anasema wamevunja sera ya habari ya mwaka 2003. What on hell? Sera ni mwelekeo tu. Hebu tuonyesheni basi sheria ambavyo imevunjwa. kama Sheria ingekuwa imevunjwa serikali gani inayotoa tu matamko ya kukemea badala ya kuwataka walioguswa kwenda mahakamani? Au kwanini isingetumia vyombo vyake? Ina TCRA kwa vyombo vya electoniki na ina MAELEZO kwa magazeti. na kuna baraza la hiyari la habari(MCT). Hebu bendera acha kutupotosha. Mnataka tuache kujadili ili mfunike kombe. Nitavishangaa vyombo vya habari kama vitaingia huu mtego na kuacha kuendelea kuandika. Itakuwa mmeingia mtego wa mafisadi. Hawa ni kuendelea kuwabana na huo ufisadi wao papa, kwanza wengine walishatajwa kwenye orodha ya aibu toka Septemba 15 mwaka 2007 na Dr Slaa pale mwembe Yanga!

Asha
 
Wakubwa nashukuruni kwa taarifa mliyotupatia kama ilivyosainiwa na Tariq Azizi. Maswali yote yamejibiwa
 
mkuchika mtu wa kukurupuka tu, Mengi katufungua watanzania masikio yetu mimi nasema mengi endeleeeeeeeea
 
Yaah true man this Mkuchika never stop to amaze me. Analaumu vyombo vya IPP na vya Rostam Aziz na kuisahau TBC1 ambayo iliandaa kipindi maalumu kwa ajili ya Rostam. TBC ni chombo cha umma au cha Rostam? Nakumbuka nilihoji hapa jamvini wengine wakaniambia (moja wapo Dar es salaam) kwamba ninawivu. Hivi Rostam ni nani mpaka apewe kipindi maalumu TBC? je ni Rais au VP wa nchi?

This Mkuchika could have blamed it strongly and ordered immediate measures to Tiddo Mhando and his comrades. Kwa tamko hili la Serikali takata rufaa.


Na si hivyo tu hata daily news na Habari Leo wamekua wakiandika kishabiki kumtetea mbunge? Kulikoni vyombe vya serikali?
 
Tamko la serikali kuhusu Mengi na Rostam limetushangaza wengi na limetuacha na maswali magumu. Serikali isutufanye kwamba sisi wote ni mbu mbu! Watu wana akili ya kutambua nyuma ya hilo tamko kuna nini hasa? Ni wazi tamko hilo pamoja na kuwaonya Mengi na Rostam kuacha malumbano hadharani tamko lenyewe linalenga kumlinda zaidi mtuhumiwa mmoja. Kwa jana Joe Bendera ameonyesha kwamba Rostam Aziz ni " Mungu Mwana" wa nchi yetu Tanzania. Tunajiuliza;

1) Hivi kwa nini Rostam akiguswa serikali na CCM wanakuja juu? Juzi juzi Mwakyembe alipozozana na Rostam serikali na chama tawala wakaigilia. Na Mwakyembe akauliza; Kulikoni?

2) Kwa nini serikali inalia na kupiga mayowe kuliko wafiwa? (Why is the Government crying more than the breaved?). Kama ni Mengi tayari yuko mahakamani na Rostam kapeleka ushahidi Takukuru. Kwa nini Joe Bendera na wenzake wasisubiri sheria ichukue mkono wake?

3) Mbona hatujasikia kelele za serikali kukemea wanaomwandama Rais mstaafu Ben Mkapa kwa mambo kama haya haya? Si magazeti, bungeni na vijiweni mbona hatujasikia serikali ikisema jambo hili litatugawa wananchi hivyo tuliache na mwenye ushaidi apeleke kwenye vyombo husika? Nani wa kutetewa zaidi kati ya Rais mstaafu, Ben Mkapa na Mengi na Rostam?

4) Mbona mgawanyiko haukutokea wakani Dr. Slaa na wenzake walioowataja watuhumiwa wa ufisadi (akiwamo Rais wa sasa) pale Temeke 2007. Kwa nini mvutano kati ya Mengi na Rostam upewe umuhimu na serikali kuliko ule wa Mwembe Yanga amabao hata nchi za magharibi ziliingilia?

5) Kwa nini serikali haikulaani matumizi ya vyombo vya habari vya kitaifa Kama TBC1, Daily News na Habari Leo ambavyo vilutumiwa kutangaza mapigo ya Rostam dhidi na Mengi bali serikali inavilaumu IPP ma New Habari Corporation kwa kutummiwa vibaya? Na TBC1 je? Jana Joe Bendera alishikwa na kigugumizi alipoulizwa kuhusu matumizi mabaya ya TBC1 katika sakata hili.

6) Waliotajwa na Mengi kama mafisadi papa wote kwa namna moja au nyingine wanajulikana kuifadhili CMM huko nyuma. Juzi juzi Tanil Somaiya aliwafadhili UV-CCM katika uchaguzi. Hivi serikali haioni kwamba watanzania wanajua kwamba anayelipa mpiga zumari ndiye uchagua wimbo gani utapigwa? (Who pays the piper call the tune) Watu sio wajinga.

7) Hivi nchi yetu ikipata msukosuko kama uliyoipata nchi ya Guinea Bissau juzi juzi (Mungu apishe mbali) kati ya Mengi na kina Rostam nani atakuwa wa kwanza kukimbia nchi? Your guess is as good as mine.
 
Nakumbuka wakati wa maandamano ya wanafunzi dsm, watoto wetu walitufumbua macho kwa kuiita serikali ya JK kuwa ya KISHIKAJI, sasa inajidhihirisha. Mzee Mwanakijiji katupangia orodha yao humu, inathibitisha kauli ya wanafunzi kwamba ni serikali ya kishikaji, hivyo Watanzania tusitegemee jipya kutoka kwa kundi hili la manyang'au.

Leo tunashangaa TBC kutumiwa na mifisadi, kwani aliyemweka Tido pale ni nani kama sio hao hao mafisadi? Tido alitumika wakati wa kampeni kumpigia debe muungwana kupitia BBC, au tumesahau kura ya maoni ya BBC wakati wa mchakato, ambayo Prof Mwandosya aliikejeli baada ya naye kupata ujumbe mfupi wa simu ukimtaka kutuma jina la JK kwenda BBC!

Hawa kina Mkuchika, Bendera nk ni matarumbeta tu ya mabwana zao, wameruhusu vyombo vinavyoendeshwa kwa kodi zetu kutumika kuficha uchafu wa mabwana zao, ni aibu kubwa, na siku zote hujitutumua pale anapoguswa mfadhili wao, ni aibu kubwa kwa taifa kuwa na viongozi wa jinsi hiii.

Hawa jamaa hivi sasa wamekamata takribani vyombo vyote vya habari hapa nchini, kwa Mengi kuvielekeza vyombo vyake vya habari dhidi ya kundi hili ndogo la mafisadi ni mchango mkubwa kwa taifa kwa sababu anatoa uwanja kwa wtz kupaza sauri zao kupinga dhuluma za mafisadi, hivyo tumuunge mkono na si kumbeza.
 
Back
Top Bottom