Tamko la Serikali dhidi ya Reginald Mengi na Rostam Aziz

serikali itawaadhibu vipi sasa hawa? kwa nini serikali iingilie malumbano ya watu? Miafrika bana....

Serikali ya kiswahiliswahili unategemea nini?? Mambo ya maana wanakaa kimya. Halafu leo wanataka kuingilia ugomvi wa mme na mke!!!!!!!!!!!!!
 
Hapa sirikali wanajiona wasanii wababe lakini hawampumbazi yeyote mwenye akili hata kama hana nguvu ya kusema. Shutuma ni nzito na ahadi ya hatua za kisheria ilitolewa. Leo kaigeuza nani. Imethibitika vipi kuwa wote, RA na Mengi ni wakosaji bila hata ya kuwakalisha kisheria na wakashindwa kutetea matamshi yao? Unawashauri eti wote mmekosa na nawasamehe msirudie, bila kuwataka hata mmoja kutetea alichodai ni ukweli?
Hapa sirikali ya kifisadi sasa yahofia kuumbuka na yataka kufanya iwezavyo kuyazima kabla hayajawa wazi zaidi. Je watawezaa? Hapo ni kuzuia maji ya mto ulofurika kwa tuta la udongo. Muda si mrefu tuta litabomoka na maji yataendela kwa kasi kubwa zaidi pamwe na tope lako! Mwisho wa ufisadi waja na tena sasa umekaribia!!
 
Kama walivyoimba, humu duniani kuna watu na viatu, naona pia kuna viongozi na viatu!
 
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.

aisee Serikali imekuwa msemaji wa mahakama siku hizi!
 
Wakuu JF.

Nimesoma kwenye mtandao kuwa Tariki Azizi wa TZ leo angetoa tamko la Serikali Kuhusu Mengi.

Tafadhali mlioko nyumbani tupasheni habari kama kalitoa na amesema nini.


Tarik aziz ni nani mkuuu...hahaha..mbona wa nchekesha mie
 
Aaa! kumbe TBC aliyotumia Rostam kumkashifu Mengi nayo ni ya Rostam. Sasa nemeelewa!

Yaah true man this Mkuchika never stop to amaze me. Analaumu vyombo vya IPP na vya Rostam Aziz na kuisahau TBC1 ambayo iliandaa kipindi maalumu kwa ajili ya Rostam. TBC ni chombo cha umma au cha Rostam? Nakumbuka nilihoji hapa jamvini wengine wakaniambia (moja wapo Dar es salaam) kwamba ninawivu. Hivi Rostam ni nani mpaka apewe kipindi maalumu TBC? je ni Rais au VP wa nchi?

This Mkuchika could have blamed it strongly and ordered immediate measures to Tiddo Mhando and his comrades. Kwa tamko hili la Serikali takata rufaa.
 
BREAKING NEWS!!! TAMKO LA SERIKALI
JAMHURI VA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICfIEZO


TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALUMBANO KATI YA MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP, BWANA REGINALD MENGI, NA MBUNGE WA IGUNGA, MHESHIMIWA ROSTAM AZIZ
1. Takribani wiki mbili sasa, kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Taifa limegubikwa na malumbano makali kati ya wafanyabiashara wawili, Bwana Reginald Mengi, Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, na Mheshimiwa Rostam Aziz, Mbunge wa Igunga, malumbano ambayo yamejikita katika suala la Ufisadi na Mafisadi.
2. Wafanyabiashara hawa wawili, Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz, kwa nyakati tofauti, wametumia vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo wanavyomiliki huku kila mmoja akimtuhumu rnwenziwe kuwa fisadi.
3. Kwa mfano, tarehe 23 Aprili, 2009, Bwana Reginald Mengi aliandaa Mkutano wa Waandishi wa Habari (Press Conference) ambapo aliyataja makampuni na wafanyabiashara watano wa hapa nchini, akiwamo Mheshimiwa Rostam Aziz, akiwaita kuwa ni "MAFISADI PAPA" na kuwaornba wananchi kuungana nave iIi kupambana na "mafisadi" hao.
4. Sikuchache baadaye.mmoja wa waliotajwa kuwa "Mafisadi Papa", Mheshimiwa Rostam Aziz, alijibu taarifa ya Bwana Mengi kupitia mkutano wa waandishi wa habari, akikanusha tuhul11a hizo. Aidha, alimtaja Bwana Reginald Mengi kuwa ni "FISADI NYANGUMI" na kuorodhesha tuhuma kadhaa za ufisadi zilizofanywa na Bwana Mengi.
5. Serikali imeyatafakari malumbano ya wafanyabiashara hawa na kubaini kwamba yanalipeleka Taifa letu mahali pabaya, kwani malumbano have yana mwelekeo wa uvunjaji wa amani kama yataachiwa kuendelea.

6. Ni Kweli kwamba Katiba ya Nchi yetu inatoa uhuru wa kila mwananchi kuongea, kutoa na kupokea habari; lakini I
7. Serikali imebaini kuwa malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi yamewagawa wailanchi katika makundi mawili; ya wale wanaounga mkono kauli ya Mheshimiwa Rostam Aziz, na wale wanounga mkono kauli ya Bwana Reginald Mengi.
8. Aidha, Serikali imebaini kwamba katika malumbano haya kumekuwepo na "matumizi mabaya" ya vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Bwana Mengi, (televisheni, magazeti na radio), na kwa Mheshimiwa Rostam Aziz, (magazeti). Kila mmoja ametumia vyombo vya habari anavyomiliki kwa manufaa yake binafsi kinyume na maelekezo ya Sera ya Habari na Utangazaji ya Mwaka 2003, inayobainisha wazi kwamba:-
• Chombo eha habari kisitumiwe kwa manufaa binafsi ya mmiliki au mtendaji bali kitatumiwa kwa manufaa ya umma;
• Chombo eha habari kiongozwe na maadili ya taaluma na jamii husika; na
• Chombo eha habari kisitangaze habari kwa misingi ya ubaguzi wa rangi, kabila, dini, jinsia au ulemavu au kuehoehea uhasama.
9. Katika hali hiyo malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi yakiachiwa kuendelea yanaweza kulitumbukiza Taifa letu katika uvunjaji wa amani.
10. Kutokana na hali hiyo basi, Serikali inawataka Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi kuacha mara moja malumbano kupitia vyombo vya habari, na badala yake wawasilishe madai na vielelezo vyao kwa mamlaka husika ili hatua zinazofaa zichukuliwe,na wananchi wapewe taarifa na vyombo hivyo.

11. Serikali haitakubali kusikia malumbano ya Mheshimiwa Rostam Aziz na Bwana Reginald Mengi ambayo yanaweza kuleta uvunjaji wa amani nchini, yakiendelea. Serikali pia haitavumilia kuona vyombo vya habari nchini vikichangia kliligawa Taifa katika makundi, na kudumaza maendeleo.
12. Aidha, Serikali inawataka Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Aziz kuvitumia vyombo vyao vya habari kwa manufaa ya Wananchi wote wa Tanzania, na si kwa manufaa yao binafsi. Wakumbuke kwamba malumbano yao hayo kwa kutumia vyombo vyao binafsi, na wakati mwingine kuonekana kana kwamba wanalihutubia Taifa, ni kutowatendea haki watu wengine ama kampuni/mashirika ambayo yametajwa katika malumbano hayo, lakini hawana vyombo binafsi (redio, televisheni, rnagazeti) ambavyo wangeweza kuvitumia kujieleza na kujitetea kama walivyofanya Bwana Reginald Mengi na Mheshimiwa Rostam Azizi.
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.
14. Aidha, Serikali inawatahadharisha Wahar;,.i wa Wanahabari kwa ujurnla kuwa makini katika kutirniza wajibu wao kwa weledi na kuzingalia maadili ya taalurna yao, badala ya kuandika au kutangaza habari kulingana na matakwa ya mmiliki wa chombo kinachohllsika.
15. Hivyo basi kuanzia sasa, Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wamiliki wa vyombo vya habari ambao hawatazingatia weledi (professionalism), Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 na Sheria ya Utangazaji ya Mwaka 2003, katika kutekeleza kazi zao za I

16. Mwisho, Serikali kwa mara nyingine inasisitiza kwamba mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi bade yanaendelea, na inawahimiza wananchi wote wenye taarifa za vitendo kama hivyo watoe taarifa hizo kwenye vyombo vya dol a vilivyopewa majukumu hayo, iIi hatua ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria. Hivyo basi, Serikali inawataka wananchi wote kufuata taratibu na Sheria za nchi yetu katika kuwasilisha hoja zao, iIi kuendelea kudumisha amani ya nchi yetu.
Kapt. (Mst) George H. Mkuchika (Mb) WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO
11 Mei,2009

source: mjengwa
 
Hawa akina chili na tomato watambue kuwa kuna siku tu wata acha hayo madaraka. Sijui kama miwaziri yetu inaakili na kama inaakili basi imejaa tamaa. Mnamtetea rostam mnajua anamipango gani na hii nchi??

Lawama zangu pia ni kwa hawa vijana wetu waliokaa na mabomu na misiles ambazo wanajua kabisa muda wa matumizi salama umekwisha lakini kwa sababu ya ufisadi pesa za mazoezi ili mabomu hayo yatumike mapema zililiwa kwa kununua vifaru na helkopta hewa (mambo ya mboma na waitara).

Wanalalamika chini chini tu.... kwa nini msimwambie JK kwamba nchi imemshinda ??
 
Hii ndio turufu ya serikali fisadi watawafunga mdomo wadanganyika ambao wameamka sikuhizi wakidai mambo ya uwazi na ukweli kwani maisha bora yameonekana ni kwa mafisadi papa. In real fact hapa ndo watakuwa wamevunja amani nchini. It is enugh. And enough is enough. Siku yeyote chochote kinaweza kuwa matokeo ya serikali kuchukua hatua mkononi. Wananchi wakichukua hatua mkononi haitashangaza sana. Kama wasemavyo mwanamke mpumbavu huivunja nyumba yake mwenyewe. At least this is my own opinion.
 
Quote:
13. Serikali imesikitishwa na kitendo eha Bwana Reginald Mengi eha kuzungumzia kesi ambazo tayari ziko Mahakamani. Sheria za nchi zinakataza mtu, watu kuzungumzia ama klljadili suala ambalo tayari liko Mahakarnani. Kwa kufanya hivyo, Bwana Reginald Mengi arnewahukumu watuhumiwa l1ao na kuwatia hatian; bila wao kupewa fursa ya kusikilizwa ("They have been condemned unheard''). Kwa mujibu wa Sheria za nehi, Mal1akama peke yake ndiyo inayoweza kumtia hatiani mtuhurniwa.

________________________
aisee Serikali imekuwa msemaji wa mahakama siku hizi!
_______________________

Nziku na wengine: Hiyo kesi aliyoizungumzia Mengi ni ipi? Aliwataja wadosi watano wanaotuhumiwa na kashfa mbali mbali za ufisadi, lakini katika hao ni mmoja tu -- Jitu Tapeli -- sorry Jeetu Patel, ndiyo ana kesi mahakamani, kesi ya EPA. Lakini Mengi hakutaja tuhuma zipi zinamhusu mtuhumiwa yupi. Ukiacha EPA Jeetu Patel ana tuhuma za Commodity Import Support (CIS), drug traficking, na nyingine.

Huyu Bendera kapangwa na hao mafisadi kuchomeka hilo la "kuingilia mahakama". Na tangu lini serikali ikaguswa na hilo, na siyo mahakama yenyewe ambayo ndiyo "inayoingiliwa?" mahakama haijasema kitu, kama vile imekuwa haisemi kitu chochote kuhusu kesi nyingine ambazo ziko mahakamani na ambazo vyombo vya habari vinazizungumzia kila siku.

Kwa mfano, mbona serikali haijaguswa na habari zinazoandikwa katika baadhi ya magazeti kuhusu kesi ya Zombe, habari ambazo zinaonekana moja kwa moja kumhukumu Zombe?

Halafu huyo huyo Bendera aliwahi kumhukumu Mengi Bungeni wakati aliposimamama na kusema kwamba kufuatana na sheria sa Hatimiliki, Za Comedy walikuwa halali kuhama kutoka Channel 5 kwa jina lao! Hapo kesi tayari ilikuwa mahakamani.

Kwa ujumla hili suala la serikali kila mara kuonekana inakerwa na watu wanaowasakama mafisadi linashangaza kweli kweli. Serikali inatia aibu vita nzima dhidi ya ufisadi.
 
Yaah true man this Mkuchika never stop to amaze me. Analaumu vyombo vya IPP na vya Rostam Aziz na kuisahau TBC1 ambayo iliandaa kipindi maalumu kwa ajili ya Rostam. TBC ni chombo cha umma au cha Rostam? Nakumbuka nilihoji hapa jamvini wengine wakaniambia (moja wapo Dar es salaam) kwamba ninawivu. Hivi Rostam ni nani mpaka apewe kipindi maalumu TBC? je ni Rais au VP wa nchi?

This Mkuchika could have blamed it strongly and ordered immediate measures to Tiddo Mhando and his comrades. Kwa tamko hili la Serikali takata rufaa.

Nziku uko sahihi.

Kwangu mimi Mkuchika,Waziri Simba na Tido ni amplifier za mafisadi.

Viongozi wa serikali kusimama kidete bila haya mchana kweupe kuwasemea individuals mafisadi na kuwa mdomo wao kwa kutumia nafasi zao ambazo zinalipiwa kodi za umma na Kutumia TVT ambayo inaendeshwa kwa kodi za umma kama platform ya mtu binafsi kama Rostam kuitumia kibinafsi ni ukosefu wa adabu wa hali ya juu kwa walipa kodi ambao kodi zao zatumika kuendesha chombo hicho.Mengi alitumia private media lakini mtu kuchukua public media Kama TVT kwa ajili ya private affairs zake kama Rostam alivyofanya si sahihi.

Sielewi kwa nini TIDO MHANDO bado yuko TVT.Anyway time will tell.Sidhani walioko serikalini wataendelea kuendesha serikali kipumbavu kwa remote ya mafisadi na watoto wa wakulima tuendelee kukaa kimya milele.Tutafikia mahali tutasema enough is enough.Cha muhimu mtu asije kulaumu mtu au fisadi itabidi ajilaumu mwenyewe na upumbavu wake mwenyewe.

Kwa ufupi things are not OK as they appear to be.USIONE KOBE(wananchi watoto wa wakulima wako kimya. wanatunga sheria sio kwamba ni wajinga hawaoni.

Viongozi walioko serikalini wasijiamini sana serikali hii sio yao peke yao ni yetu wote.Kupewa madaraka hugeuki kuwa demi-god. Anything can happen to you anytime Kama utendaji wako mbovu.Nani alijua Waziri Mramba au Yona wangepanda karandinga kwenda mashabusu ? Huwezi jua siku moja kukuta waziri Simba,Mkuchika au Tido Mhando nao wakijiunga nao kupanda Karandinga pia kwa kuchezea nafasi zao ZA UMMA na vyombo vya UMMA vilivyo chini yao kwa manufaa ya mafisadi wakati huo hao wanaowatetea watakuwa wameshatimua mbio nchini wanawaacha wao wanasota gereza la keko kwa kukosa dhamana.
 
Mkuu Zak Malang,
aliyetoa taarifa hii ni yule yule Waziri mwenye matamko tata Kapt. (Mst) George H. Mkuchika. Mi nimeshangaa sana kujifanya msemaji wa mahakama. Kesi anayosema ndo hiyo ya Patel. anatia aibu huyu Waziri...
 
Back
Top Bottom