Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
Rostam Azizi anashirikiana na Kikwete kwenye ufisadi wake. Only Kikwete can do something about Rostam Azizi. Hawa wengine wote wataendelea kujaribu.
 
Niliwahi kuuliza which is supreme the Governmnet or the CCM Central Committe? Mkiweza kunijibu hapo ndio mtapata picha ya nini Ndg Mengi anafanya. na ninawahakikishia nan baraka zote za JK. Kabla ya kumtosa Lowassa Jk aliwatumia wazee kibao tu wamwambia aachie ngazi.

Hizi ni ngoma za JK tu.

Haiwezekani mafisadi papa na wengine wote wenye tuhuma mbaimbali wakaka katika CC ya CCM inaleta picha gani, watolewe humo waje mitaani hawa nia vibaka tu!!!!. Bora Mkapa tunaye mitaano huku!!! sio kwenye CC ya CCM watoke wenyewe ama sivyo patakuwa hapatoshi wezi wakubwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwakuwa viongozi wetu wansukumwa na donors anachofanya mengi ni kuwa alert donors kuwa lipo tatizo la mapap wa ufisadi na Iam sure kuwa baada ya muda kidogo domors wakiagiza hatua zitachukuliwa tuu. Bravo Mengi

Viongozi wetu ndio mafisadi hao hao sasa wakiamua kuchukua hatua ina maana watajichukulia hatua wenyewe? I don't see that happening...sorry....

Halafu hata hizo hatua zikichukuliwa (sijui na nani) wataanzia wapi? Is there a cutoff line? Kwa sababu tokea niko dogo ufisadi uliokithiri umekuwepo.....
 
Pinda aliposema wauwaji wa albino na wao wauliwe, tulisema hakuwa sahihi kwa kauli yake, haikuwa na maana kuwa tulikuwa tukiunga mkono mauwaji ya albino, kilichokuwapo ni kuwa zipo hatua ambazo tumejiwekea na kkubaliana kuzifuata katika kushungulikia matatizo hayo, na kwa hili la Mengi kama kweli alifahamu kuwa hawa ndo mafisadi na ushahidi anao kwanini asifuate taratibu zinazoeleweka na yeye Mengi anazifahamu, hawa watu wakashughulikiwa kwa njia hizo badala ya kubwatuka na kuw "sensitize" Watz (ambao tokea hapo weshadata kwa ugumu wa maisha), wakajenga chuki za bure?
Hoja ni kwanini asifate sheria, wakati hakuzuiliwa kufanya hivyo na mtu yeyote, hata hao aliowaita mafisad papa.
sasa hatari yake ndo hii, heshima yake Mengi, imepotea, anaonekana ovyo tu kama aliyechanganyikiwa na nini sijuwi.
Kama alitafuta ziada ya umashuhuri, angetumia staili ile ile ya Mtikila, Mtikila anajuwa pahala pa kutafuta ugomvi na watu.

Mkuu, taratibu zipi hizo?

Zinaeleweka kwa akina nani?

Kutoa maoni sio kama kupeleka posa.

Eti taratibu zinazofahamika...
 
Let me make one thing clear here, am not in support of RA, Manji or Mengi. To me they all bunch of nuisance old businessmen who are driving this nation to its grave.

The biggest fool is The Executive Chairman of IPP Media, and Chairman of Media Owner Association of Tanzania plus holder of many other top position in bussness related associations, Mr powermonger, Reginald Mengi.

Inawezakana vipi akurupuke kuita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja na kuwatuhumu wenzake kwa kile anachodai ufisadi papa? Anataka kutuambia nini watanzania, mahakama zetu na vyombo vya dola vimeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo, je yeye nani katika nchi hii hadi ifike wakati aende kifua mbele kuwatuhumu watu atakavyo.

Nakubali kuwa RA na kundi lake limetajwa sana kuhusika na vitendo vya kifisadi lakini jukumu la kuthibitisha hayo lipo mikono mwa polisi na si vinginevyo....mbona hatujamuona huyu mzee mnafiki kwenda kupiga kura kwenye ile kampeni yetu ya kuwataja watu wanaohusika na vifo vya maalbino na wahalifu wakubwa wakiwemo mafisadi. Ni kweli Bwana Mengi anauchungu na nchi hii? Kwanini hakupeleka ushahidi wake polisi na kisha kuja kututangazia umma kuwa yeye ameshalabidhi ushahidi na yuko tayari kuwa shahidi namba moja katika kesi dhidi ya watu hao?

Kusema kweli tabia ya mengi inakera sana hasa kwa nchi ambayo inafuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria kama Tanzania. Kwahiyo baada ya kuwataja alikuwa anatarajia nini kiendelee, au angejisikiaje kama sisi wananchi tungejichukulia sheria mkono kama ilivyokuwa kwa bwana Balali ambapo wananchi waliamua kujigawia mashamba yake kwa hasira. Mi simuelewi huyu mzee hata kidogo....kama ni ushindani kibiashara angetafuta njia nyingine si staili hii ya kuchonganisha wenzake. Hali hii inafanya niamini kuwa Mengi ameanzisha kikundi chake cha Kimafya ili kuspy wanayofanya wenzake...where else he would have gotten all these information and this guts to stand up in public and declare oother guilt without being prosecuted in court of law.

Najua wapo watu humu ndai wanajenga mapenzi kwa mtu yeyote anaelekea kuwasakama watuhumiwa hawa wa ufisadi, na hali hii inawezakana kuwapofusha hata warevu wachache kuona ukweli wa mambo. Kama mnapenda kusikia RA na wenzake wanakwenda mahakamani iweje msitoe hamasa hiyo hiyo kwa Bwana Mengi kwenda mahakamani au ndo ule usemi wa kiswahili usemao "Nani atamfunga paka kengele?". Let's not rejoice for anyone who break the law under the name of saving the nation unless we are all agree that our Jurisdictions can not be trusted and only then let take matter on our own hand as per Mr. Mengi point of view. Period

Utaenda motoni.Kuna watu mil.40 au zaidi wanataabika sababu kwa namna moja au nyingine ni kwasababu ya huyu mswahili na wenzake.Umenitoa machozi,i wonder kama wewe sio Balile.
 
Tamko gani hili....Siku zote zilijua Rostam ana akili sana, kumbe ndondocha..!!

Hili tamko halina hata dhamani ya hiyo karatasi iliyoandikwa...
 
Mkuu nafikiri umemsikia Prof. Lipumba alivyompa somo Mengi, vp alitakiwa afanye na siyo ku behave kama "juha" au punguwani vile vyombo vya kushughulikia mambo hayo si vipo, angelikwenda TAKUKURU akawapa ushahidi na vielelezo vya madai yake, kama hatua singelichukuliwa ndo angekuja akawambia watu kupitia vyombo vya habarik, tungemuelewa.
Na kutoa maoni ni haki ya kila mtu lakini ina taratibu zake,zinafahamika, si kila maoni yoyote yanasemwa popote, kama Mengi angelijua pa kusemea maneno yake(on the right forum) asingelaumiwa na yeyote.
 
Jamani mbona mnashindwa kuconnect the dots. Huu ubavu wa Manji kwenda mahakamani kufungua kesi na hii sasa ya Rostam kutoa vitisho wanaupata wapi ? Jibu liko wazi - ni baada ya Sophia na Mkuchika kuiingiza serikali ya Jamhuri kwenye utetezi wa mafisadi. Hawa wawili ni mawaziri - je walitumwa ? Je ni uchungu wa mwana, aujuaye baba ?

Usemi wa Rostam umenikumbusha ule wa waziri moja anayeitwa Masha, aliyeamua kumshughulikia Mengi na kutoa siku saba - sasa naye Rostam katoa masaa 48. Huu ni muda mwafaka wa kujipanga kuingia vitani - ama upo upande wa mafisadi au dhidi yao - wazungu husema, the daggers are drawn, na sasa hakulaliki mpaka kieleweke, mafisadi kaeni chonjo.

Mafisadi wameiweka serikali nzima ya CCM mfukoni.​
 
Mafisadi wameiweka serikali nzima ya CCM mfukoni.

No, ni hivi....CCM ndio hao hao mafisadi. Serikali ni ya CCM therefore, serikali, from top on down, they are all mafisadi.

Sijui kwa nini watu wanaogopa kusema kuwa Kikwete naye ni fisadi. Sijui mnamwogopa au mnamuonea aibu. Hapa ni kujikoma tu (kumkoma Nyani)...lol
 
Are you trying to suggest tutetemekee wahindi ndani ya nchi yetu? Kama umeamua wahindi wawe mabwana wako mie simo!!

Mara ngapi? mbona wanatetemekewa tangu enzi hizo?

No, ni hivi....CCM ndio hao hao mafisadi. Serikali ni ya CCM therefore, serikali, from top on down, they are all mafisadi.

Sijui kwa nini watu wanaogopa kusema kuwa Kikwete naye ni fisadi. Sijui mnamwogopa au mnamuonea aibu. Hapa ni kujikoma tu (kumkoma Nyani)...lol

Kaka umenena, kila anayezungumzia ufisadi anamkwepesha JK! KAMWE KATIKA MAISHA YANGU SITAKUBALIANA KUMTENGA JK NA UFISADI , SO , MENGI JUZI KAFANYA HIVYO HIVYO, ANASEMA TUMSAIDIE RAIS!!!!!

HUU NI UHUNI NA KAMA KAWAIDA YA WADANGANYIKA WAMEISHAINGIA KING!

UMSAIDE JK MWENYE DOLA? NA KILA AINA YA RESOURCES??
 
Mara ngapi? mbona wanatetemekewa tangu enzi hizo?



Kaka umenena, kila anayezungumzia ufisadi anamkwepesha JK! KAMWE KATIKA MAISHA YANGU SITAKUBALIANA KUMTENGA JK NA UFISADI , SO , MENGI JUZI KAFANYA HIVYO HIVYO, ANASEMA TUMSAIDIE RAIS!!!!!

HUU NI UHUNI NA KAMA KAWAIDA YA WADANGANYIKA WAMEISHAINGIA KING!

UMSAIDE JK MWENYE DOLA? NA KILA AINA YA RESOURCES??

Ndo maana nasema hadi hapo atakapotokea mtu na kutamka kuwa Rostam ni fisadi JUST LIKE JK himself, yote haya mi naona ni mazingaombwe tu!
 
Mara ngapi? mbona wanatetemekewa tangu enzi hizo?



Kaka umenena, kila anayezungumzia ufisadi anamkwepesha JK! KAMWE KATIKA MAISHA YANGU SITAKUBALIANA KUMTENGA JK NA UFISADI , SO , MENGI JUZI KAFANYA HIVYO HIVYO, ANASEMA TUMSAIDIE RAIS!!!!!

HUU NI UHUNI NA KAMA KAWAIDA YA WADANGANYIKA WAMEISHAINGIA KING!

UMSAIDE JK MWENYE DOLA? NA KILA AINA YA RESOURCES??

Aiding and Abetting/Accessory
--------------------------------------------------------------------------------
A criminal charge of aiding and abetting or accessory can usually be brought against anyone who helps in the commission of a crime, though legal distinctions vary by state. A person charged with aiding and abetting or accessory is usually not present when the crime itself is committed, but he or she has knowledge of the crime before or after the fact, and may assist in its commission through advice, actions, or financial support. Depending on the degree of involvement, the offender's participation in the crime may rise to the level of conspiracy.

For example, Andy draws a floor plan of a bank, knowing of Dan's intention to rob it. After Dan commits the robbery, Alice agrees to let him store the stolen money at her house. Both Andy and Alice can be charged with aiding and abetting, or acting as accessories to the robbery.
 
Jamani mbona mnashindwa kuconnect the dots. Huu ubavu wa Manji kwenda mahakamani kufungua kesi na hii sasa ya Rostam kutoa vitisho wanaupata wapi ? Jibu liko wazi - ni baada ya Sophia na Mkuchika kuiingiza serikali ya Jamhuri kwenye utetezi wa mafisadi. Hawa wawili ni mawaziri - je walitumwa ? Je ni uchungu wa mwana, aujuaye baba ?

Usemi wa Rostam umenikumbusha ule wa waziri moja anayeitwa Masha, aliyeamua kumshughulikia Mengi na kutoa siku saba - sasa naye Rostam katoa masaa 48. Huu ni muda mwafaka wa kujipanga kuingia vitani - ama upo upande wa mafisadi au dhidi yao - wazungu husema, the daggers are drawn, na sasa hakulaliki mpaka kieleweke, mafisadi kaeni chonjo.

Mafisadi wameiweka serikali nzima ya CCM mfukoni.​

Serikali ikijichomeka kutetea watu kwenye hili la Mafisadi Shark utetezi wao utatupwa kapuni mara moja. Huko nyuma serikali iliwahishitaki watu kijinga jinga hivi hivi ikajikuta ikibwagwa chini kwa aibu kubwa.Mafisadi Papa ni maafisa wa juu kabisa katika ngazi za uongozi wa CCM kudhihirisha kwamba CCM ni kinara cha ufisadi na inategemea moja kwa moja mshiko wa wizi wa Mafisadi Papa kuendelea kukalia kiti kinundanunda.
 
Hivi huyu waziri Simba na watu wengi kwa nini wanadhani kwamba Mengi kama raia hawezi kutoa maoni yake na kuaccuse watu kuwa ni wezi????

Kama Mengi amekosea, inabidi wale waliokuwa accused waende mahakamani kumshitaki Mengi kwa defamation au na wao kumaccuse Mengi kuwa ni mwongo.

Sasa Waziri Simba anaposema Mengi amepata wapi haki ya shutuma zake si ameipata kwenye Katiba au???

Halafu kama Jeetu ana kesi mahakamani, Waziri Simba anasema eti Mengi kumdiscuss kuwa ni fisadi ni makosa, kwa sheria ipi??? Kwani mengi ni serikali au yeye ni raia tu??

Mbona huyu mama anaonyesha kutokuelewa tofauti baina ya raia na serikali??

Mengi ameshutumu raia wengine, ni vipi Waziri Simba kama serikali kuingilia lawama hizi especially kama inavyosemwa kuwa ni uongo???

Naomba waziri Simba apewe mwongozo wa kisheria ili ajitulize na ujinga wake huko aliko!!
 
Kwa nini kila litajwapo kundi la Fisi Rostam yumo?

Hajajiangalia katika kioo aone anafafanaje?Mtu mmoja anweza kukusingia kwamba wewe ni Fisi na nunda mkubwa, lakini endapo kila asimamaye kutaja Mafisi jina la Mzalendo Rostam Azizi halikosekani hapo nadhani kuna kijambo.

Kiongozi wa serikali ukisha rambishwa Rushwa unakuwa kama Malaya.Malaya kamwe haoni aibu kuweka hadaharani uchi wa akili yake.

Kiongozi wa serikali aliye hodari wa kula rushwa kamwe haoni sababu ya kuficha uchi wa akili yake. Ndiyo maana Mawaziri wazima pamoja na heshima utukufu na shule zao wanasimama wima kwa miguu miwili kutetea uchi wa akili ya Fisadi Rostamu kwa gharama ya kuweka nyuchi za akili zao wazi ili zionwe na kila Mtanzania.

Ukishaonyesha uchi wa akili yako, ubakizacho ni kuonyesha uchi wa roho yako.
 
Last edited:
Jana asubui nilifanikiwa kuona interview TBC1 ya Waziri Sophia Simba kuhusu sakata la Mengi na wale aliowaita mafisadi papa. Mambo aliongelea kama waziri ndio msimamo wa serikali. Binafsi naona msimamo huo wa serikali una kasoro.

1) Kama serikali ilitaka kutoa tamko ingemtafuta waziri ambaye ni "eloquent" wa kuweza kuzungumzia swala nyeti kama hili la ufisadi. With due respect kwa Mheshimiwa Simba alijigonga gonga kuhusu maswali aliyokuwa anaulizwa. Majibu yake hayakuwa "factual" enough na hivyo kuoneka anapwaya! Kwa mfano mdogo, Marin Hassan alimuuliza dhana ya kutengenisha baishara na siasa na yeye akajibu kwamba katika wale watuhumiwa watano hakuna mwana siasa hata mmoja! Duinia nzima inajua kwamba Mhe. Rostam Aziz ni mbunge wa Igunga na mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Juzi Mama Simba amenukuliwa kwenye gazeti akisema kwamba Kamati ya Maadili ya Viongozi haipaswi kujishugulisha pesa za viongozi zilizoko nje ya nchi! My foot!! Maoni yangu ni kwamba serikali ikiachia watu kama waziri Simba kuelezea msimamo wake katika mambo nyeti kama hili tunaweza tukaishia kama swala la Zitto Kabwe na Buzwagi. That issue was mishandled by the government at a high political cost.

2) Historia inatukumbusha kwamba mwaka juzi wakati swala la EPA lilipoibuka kwenye mtandao na Dr. Slaa kulileta Bungeni, Waziri Meghji (akiwa waziri-Fedha) na Spika walimbeza (skepticism) wakisema hakuna ushaidi na hayo ni mambo ya mitandao. Waingereza wanasema " It came to pass". Leo hii kesi za EPA zinanguruma mahakamani na waziri Meghji sio waziri tena!

3) Katika nchi yetu sio mara ya kwanza kutaja wazi wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi. Septemba 2007 Dr. Slaa na wenzake walitaja majina kumi ya watuhumiwa wa ufisadi pale MwembeYanga, Temeke. Baadhi yao walicharuka na kutishia kwenda mahakamani kwa kuchafuliwa na wengine wakasema hakuna ushaidi. Mpaka leo hakuna hata kesi moja ilifunguliwa mahakamani kwa "uzushi" huu! Leo hii Mhe. Lowassa, Karamagi na Chenge wako nje ya Baraza la Mawaziri kwa tuhuma kama walizosema kina Dr, Slaa. Mhe, Mramba, Yona na Mgonja wako mahakamani kwa tuhuma kama hizo. Rais mstaaafu Ben Mkapa halali usingiz mzurii kwa kutuhumiwa na umma kwa kutumia madaraka vibaya. Kinachoshangaza wakati wote huu sijaona serikali ikitoa msimamo wake mkali (kama Mama Simba) kuhusu watuhumiwa wa Dr. Slaa. Kulikoni sasa waziri anakuja mbogo kwa kutajwa mafisadi watano tu? Labda kwa kuwa limeongezeka neno " papa"? Mbona serikali haijatoa tamko kuhusu kutuhumiwa Rais mstaafu?

4) Mhe. Rostam Aziz amekuwa akitajwa tajwa katika haya mambo ya ovyo. It is not by coincedence, I believe. Alitajwa Mwenbeyanga, anatajwa katika wizi wa EPA, alitajwa na Tume ya Mwakyembe kuhusu Richmond na Dowans na sasa anatuhumiwa na Mengi kuwa ni fisadi "papa" . Huyu ni sawa na "Yuda Iscariot" kwa kuisaliti CCM hapaswi kula meza moja na viongozi wetu labda kama nao ni "birds of the same feathers"? Kwa nini asitolewe kamati kuu CCM hadi hatakapojitakasa? Bila hivyo maswali yataulizwa tu. Wakubwa wapende wasipende.

5) Tanil Somaiya amefadhili uchaguzi wa juzi wa UV-CCM kwa "mchango" wa shs. 400 milioni. Je waziri Simba hakuona kwamba kwa utetezi wake kwa hawa watuhumiwa kunaweza kukatafusiriwa kwamba serikali ya CCM inalipa fadhila? Je wananchi wakisema CCM imetekwa na matajiri kuna wakubisha?

6) Mama Simba anasema Mengi kama ana ushahidi aupeleke kwenye vyombo husika hususan TAKUKURU. Tunauliza TAKUKURU ipi? Hii inayoongozwa na Hosea? Kuna azimio la Bunge kuhusu kiongozi huyu kwa kuboronga uchunguzi wa ufisadi Richmond. Mengi kama mtu mwelevu hawezi kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere. Na hata wananchi hawana imani na Polisi katika mambo haya. Kama imani ingekuwepo serikali hii isengeitisha kura za maoni kutafuta wauaji wa Maalbino. Watu wangewataja watuhumiwa kwa jeshi la polisi na Polisi wangeisha maliza tatizo hili. Iko wapi ile orodha ya wauza unga aliyotuaaidi Mhe. Mwapachu akiwa waziri wa Usalama wa Taifa?

7) Sio mara ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho kwa Mengi kuzozana hadharani na wafanya biashara wenzake. Walikwaruzana na Yusuf Manji mpaka wakafikishana mahakamani. Mengi alizozana na Rostam kuhusu Rostam kuzindua album katika kanisa moja la Kiluteri mpaka (tunaambiwa) mchungaji akachukuliwa hatua. Hakuna jipya na sisi hatuoni kwa nini serikali inaigilia mzozo huu. Kuna sheria zinazohusu kafsha na kama waliotajwa na Mengi wanafikiri wameonewa Mengi kwa kauli yake atafurahi kukutana nao. Manji ameshatinga mahakani ni Rostam aende huko. Why is the minister poking her nose in the affairs that do not concern her? Ana kihele hele. Kwa hili yeye ndie KACHEMSHA na aambiwe hivyo.

8) Swala la Ubaguzi wa rangi halina mashiko. Hatuwezi kuogopa kutajana na kusutana eti tutaambiwa ni wabaguzi. Kama Wahaya kumi ni wezi wa mali ya Umma nawatajwe. Mbona wachaga wanasemwa kwa kujazana TRA kwa misingi ya Ukabila na hawajalalama? Lipumba na wenzake walikuwa wapi wakati Salum Mohamed Salum akibaguliwa wazi wazi wakati wa mchakato wa Urais ndani ya CCM 2005 na hakuna aliyenyosha kidole? Rostam should not hide behind racism veil to justify his misdeeds.

Nimalizie kwa kutoa mfano wa Biblia. Yesu alipowasema sana mafarisayo, mazudakayo na wakuu wa dini ya kiyahudi walipanga njama ya kumuua. Na katika kuhalilisha kifo chake Kuhani Mkuu wa wakati ule jina lake Keyafa aliwashauri kwamba " inabidi mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi". Baadhi ya magazeti yamesema Mengi kwa kufanya alichofanya anajitoa mhanga. Inawezekana lile neno likatimia. Hatuwezi kuendelea na uoza huu katika nchi yetu. Tanzania bila Ufisadi inawezekana.

Bysel, hapo umenena. Tuko pamoja

Tiba
 
Mkuu nafikiri umemsikia Prof. Lipumba alivyompa somo Mengi, vp alitakiwa afanye na siyo ku behave kama "juha" au punguwani vile vyombo vya kushughulikia mambo hayo si vipo, angelikwenda TAKUKURU akawapa ushahidi na vielelezo vya madai yake, kama hatua singelichukuliwa ndo angekuja akawambia watu kupitia vyombo vya habarik, tungemuelewa.
Na kutoa maoni ni haki ya kila mtu lakini ina taratibu zake,zinafahamika, si kila maoni yoyote yanasemwa popote, kama Mengi angelijua pa kusemea maneno yake(on the right forum) asingelaumiwa na yeyote.

Junius,

Can you please dont mind to mention what is the so called "right forum"

Tiba
 
Kama huna la kusema si lazima uandike. Mengi ame-practice uhuru wake; he selected to speak on this issue; and this was his prioritity(maybe); how can you select his priorities? wewe kula dona ulale!

Wewe umehongwa tu haiwezikani...hebu soma kwa makini afu ujibu tena. Mbona watu mnapenda kukurupuka humu ndani...no wonder umechagua kumsupport huyo jamaa. Mengi hakupractice uhuru bali amepass on judgement...Hatuishi maporini mkuru where no rules can be applied...hapa kwetu kama ulikuwa hujui, tuna katiba ambayo pia imetoa mipaka na wajibu wa kila mtu. Hata humu ndani ukienda kinyume unapigwa chini.

Usikurupuke na kutafuta umaarufu.
 
Junius,

Can you please dont mind to mention what is the so called "right forum"

Tiba

Right forum ni sehemu iliyowekwa kisheria au kiutaratibu kuzungumzia shauri fulani. Kwa mfano ukitaka kuzungumzia habari za mapenzi hapa JF uwanja huu si mahala pake, michezo pia si pahala pake. Kwa hiyo Mengi hakuchagua uwanja sahihi kuzungumzia TUHUMA ZAKE. Ilimpasa apeleke kwenye uwanja wa Mahakama ili waamue ukweli wa aliyoyasema. Therefore he went off the topic from that venue.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom