Tamko la Rostam Aziz dhidi ya Reginald Mengi na yatokanayo. Amuita fisadi Nyangumi

Status
Not open for further replies.
In other words in 48 hrs Mengi and the like will be dead or what????? This justify Mengis paranoia that they want to kill me.It will be Rostam wants to kill me. How fablous. Thats why the whole government is afraid of him????? Blackmailing them and if it wont work he will kill them eh.
 
"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly. Alternatively he is it to apologize to me personally within 48 hours, failing all of which, I reserve the right to exercise any appropriate actions in order to expose his wrongdoings"

Inakuwaje hii nchi inakuwa na viongozi wanaojua kuwa kuna mtu ana maouvu lakini hawasemi au kuwafikisha waovu hao mbele ya sheria? Statement kama hii inatosha kabisa kumwondoa mtu katika uongozi. Hafai kuwa kiongozi wa Watanzania.

Kama anajua maovu ya Mengi, angelikuwa mstari wa mbele kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria yashughulikiwe na siyo asubirie maovu yake yatajwe ndiyo naye aseme "mbona huyu naye ana maovu."

Hadi Amir Jeshi Mkuu naye ana style hii hii ya kuwa na orodha za wauza unga na watoa rushwa.... Kama wanajua maovu kwanini wasiyapeleke kwenye vyombo vya sheria mara moja? Wanasubiria aina gani ya mabaya yatokee ndiyo hayo maovu tuyajue?

What a bunch of disgraced leaders! Shame.
 
"I am therefore calling upon Mr. Mengi to either surrender whatever evidence he has to support his wild accusations and to appoint the appropriate legal bodies or state organs to act accordingly."

Mengi alishasema kwamba kama itawachoma wao waende mahakamani na hapo ndipo atakapotoa huo ushahidi, sasa tunashangaa huyu mbwana anasema anaonewa na anataka Mwengi hampe ushahidi, inaelekea huyu bwama upeo wake wa kuelewa mambo yaliyo nje ya Ufisadi ni mdogo sana, kama kweli kaonewa na anataka kuprove kwa wananchi kuwa kaonewa basi aende mahakamani hapo ndipo tutakapomwana mengi kama ni uzushi au ni mambo ya kweli
 
Hapa jamaa kachemsha na inaonekana hata washauri wake ni wavivu wa kufikiri kwani aya ya mwisho inamuonyesha kuchanganyikiwa hivyo kujaribu kumtisha Mengi kuona kama kweli atamuomba radhi ili iwe njia ya kujisafisha. Heri angekaa kimya, maisha magumu!
 
Hapa jamaa kachemsha na inaonekana hata washauri wake ni wavivu wa kufikiri kwani aya ya mwisho inamuonyesha kuchanganyikiwa hivyo kujaribu kumtisha Mengi kuona kama kweli atamuomba radhi ili iwe njia ya kujisafisha. Heri angekaa kimya, maisha magumu!


Huyu jamaa naona anataka waanze kucheza kidali po! Nani atalala nacho? Kwa hiyo naye atamtuhumu Mengi ili Mengi ndiye aende mahakamani. Hii ngwe bado sana! Ila kama serikali ingekuwepo sasa tungepata mapapa 6 badala ya 5. Mengi alitaja 5 na RA anamwongeza Mengi wenye orodha. Serikali iko wapi jamani? Orodha hiyo tayari inatosha, kwa nini hatuanzi kazi?
 
- Rostam Aziz, mbunge na mjumbe wa CC aliyeapa kulinda taifa, siku zote hizi anafahamu kwamba Mengi kama raia na mfanyabiashara amekwua akivunja sheria za jamhuri ambazo yeye kama mbunge ameapa kuzilinda kwa nguvu zake zote lakini ameshindwa, sasa anangojea nini kujiuzulu?

- Kwa nini anatishia nyau, badala ya ku-deal straight with the ishu ya Mengi kwamba yeye ni fisadi? Wananchi tunataka ukweli nothing but the truth bila kujali sura ya mtu hapa, wala rangi hii ishu haina siasa ila ni ufisadi tu, nani ni fisadi na nani siye!

- Wananchi wa Tanzania tumechoshwa na Ze-Comedy, sasa ukweli uwekwe wazi, Rostam aende kwenye sheria aseme ya kwake na Mengi ajibu, tusije tena kusikia busara za Spika.

Siasa zisiingizwe kwenye hii ishu ambayo ni 100% legal, na wananchi tusiyumbishwe hapa kwa kuweka mayai yetu yote kwenye kikapu kimoja, tunachotaka ni ukweli bila ya kujali sura ya mtu, Mengi alianza kwa maneno, Rostam amejibu kwa maneno na vitisho, sasa next step iwe kwenye sheria! Kwa sababu Rostam ndiye aliyeanza kulilia sheria, sasa ni wakati wa yeye kuwahi Kisutu! Ingawa record yake hapa inamsuta sana maana kwa kawaida yake angeshausema wazi ukweli alinao mbona kwenye Mtikila hakudai kuombwa radhi na kutishia sheria this time ana ushahidi dhidi ya Mengi lakini anataka radhi kwanza?

Something is not right!

FMES
 
Watu wameanza kutapatapa. Msaada wa utawala bora unahitajika haraka kunusuru mifadhaiko
 
Kama sikosei Pinda kaweka sawa mambo bungeni katika maswali ya papo kwa papo!!!???
 
Mad in Tanzania;

Ni TANZANIA TU, HUWA HAIWASHTAKI WATU, LA INASUBIRI MTU ALIYEAMBIWA MWIZI NDIYE AENDE MAHAKAMANI!!!

wote mnaotaka wezi waende kushtaki mahakamani, ni kipimo tosha kuwa hamna la kuwafanya mafisadi! na haya ni mawazo mabaya kabisa,

Mengi alitakiwa aende mahakamani! la akae kimya, maana hakuwa na jipya, pili tabia hii ni sawa na kuwapiga mawe vibaka, tunaposema utwala wa sheria nadhani JF tuwe tunaongoza, tunapokuwa na double standard, kuna siku tutaULIZWA!
 
How can Rostam run away from this? I need to know, how in the world huyu jamaa anakuwa na mikwara mingi?

from that letter i can say this, Rostam hajaandika bali ni mwanasheria wake sababu ya uchaguzi wa meneno unaonyesha. On top of that Rostam is empty head.

Jamani naomba niwe racist for a second, How is possible MUIRAN akacontrol maisha ya watu million 40? I just think Rostam doesn't care about Tanzania sababu He don't know nothing about Tanzania. Does Rostam know the struggle of majority of Tanzanian? Does he know the pain that watanzania wanapitia sababu ya mtandao wake. God help us, i lay my case mbele ya Mungu.... It seems no one can either defeat this guy.... Tanzania we have problem.
 
- Mkuu Steve, Smart? with all due respect not really ila kwa sababu ni Tanzania tu!

FMES

Ni ile impact yake katika jamii yetu, mbaya au nzuri haijalishi... ni kule kusikika kila sehemu kuwa mhusika ni huyu na ndiyo yule yule... ni kule kutegemea kuwa mtu aliye nyuma ya haya mambo yoooote hawezi kutoa statement kama hiyo!... statement imetoka, huyu (Mh.) siyo smart na siyo mtetezi wa katiba aliyo apa kuitumikia na kuitetea. He should go on that grounds alone!
 
Let me make one thing clear here, am not in support of RA, Manji or Mengi. To me they all bunch of nuisance old businessmen who are driving this nation to its grave.

The biggest fool is The Executive Chairman of IPP Media, and Chairman of Media Owner Association of Tanzania plus holder of many other top position in bussness related associations, Mr powermonger, Reginald Mengi.

Inawezakana vipi akurupuke kuita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja na kuwatuhumu wenzake kwa kile anachodai ufisadi papa? Anataka kutuambia nini watanzania, mahakama zetu na vyombo vya dola vimeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo, je yeye nani katika nchi hii hadi ifike wakati aende kifua mbele kuwatuhumu watu atakavyo.

Nakubali kuwa RA na kundi lake limetajwa sana kuhusika na vitendo vya kifisadi lakini jukumu la kuthibitisha hayo lipo mikono mwa polisi na si vinginevyo....mbona hatujamuona huyu mzee mnafiki kwenda kupiga kura kwenye ile kampeni yetu ya kuwataja watu wanaohusika na vifo vya maalbino na wahalifu wakubwa wakiwemo mafisadi. Ni kweli Bwana Mengi anauchungu na nchi hii? Kwanini hakupeleka ushahidi wake polisi na kisha kuja kututangazia umma kuwa yeye ameshalabidhi ushahidi na yuko tayari kuwa shahidi namba moja katika kesi dhidi ya watu hao?

Kusema kweli tabia ya mengi inakera sana hasa kwa nchi ambayo inafuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria kama Tanzania. Kwahiyo baada ya kuwataja alikuwa anatarajia nini kiendelee, au angejisikiaje kama sisi wananchi tungejichukulia sheria mkono kama ilivyokuwa kwa bwana Balali ambapo wananchi waliamua kujigawia mashamba yake kwa hasira. Mi simuelewi huyu mzee hata kidogo....kama ni ushindani kibiashara angetafuta njia nyingine si staili hii ya kuchonganisha wenzake. Hali hii inafanya niamini kuwa Mengi ameanzisha kikundi chake cha Kimafya ili kuspy wanayofanya wenzake...where else he would have gotten all these information and this guts to stand up in public and declare oother guilt without being prosecuted in court of law.

Najua wapo watu humu ndai wanajenga mapenzi kwa mtu yeyote anaelekea kuwasakama watuhumiwa hawa wa ufisadi, na hali hii inawezakana kuwapofusha hata warevu wachache kuona ukweli wa mambo. Kama mnapenda kusikia RA na wenzake wanakwenda mahakamani iweje msitoe hamasa hiyo hiyo kwa Bwana Mengi kwenda mahakamani au ndo ule usemi wa kiswahili usemao "Nani atamfunga paka kengele?". Let's not rejoice for anyone who break the law under the name of saving the nation unless we are all agree that our Jurisdictions can not be trusted and only then let take matter on our own hand as per Mr. Mengi point of view. Period
 
Jana asubui nilifanikiwa kuona interview TBC1 ya Waziri Sophia Simba kuhusu sakata la Mengi na wale aliowaita mafisadi papa. Mambo aliongelea kama waziri ndio msimamo wa serikali. Binafsi naona msimamo huo wa serikali una kasoro.

1) Kama serikali ilitaka kutoa tamko ingemtafuta waziri ambaye ni "eloquent" wa kuweza kuzungumzia swala nyeti kama hili la ufisadi. With due respect kwa Mheshimiwa Simba alijigonga gonga kuhusu maswali aliyokuwa anaulizwa. Majibu yake hayakuwa "factual" enough na hivyo kuoneka anapwaya! Kwa mfano mdogo, Marin Hassan alimuuliza dhana ya kutengenisha baishara na siasa na yeye akajibu kwamba katika wale watuhumiwa watano hakuna mwana siasa hata mmoja! Duinia nzima inajua kwamba Mhe. Rostam Aziz ni mbunge wa Igunga na mjumbe wa kamati Kuu ya CCM na alikuwa Mweka Hazina wa CCM. Juzi Mama Simba amenukuliwa kwenye gazeti akisema kwamba Kamati ya Maadili ya Viongozi haipaswi kujishugulisha pesa za viongozi zilizoko nje ya nchi! My foot!! Maoni yangu ni kwamba serikali ikiachia watu kama waziri Simba kuelezea msimamo wake katika mambo nyeti kama hili tunaweza tukaishia kama swala la Zitto Kabwe na Buzwagi. That issue was mishandled by the government at a high political cost.

2) Historia inatukumbusha kwamba mwaka juzi wakati swala la EPA lilipoibuka kwenye mtandao na Dr. Slaa kulileta Bungeni, Waziri Meghji (akiwa waziri-Fedha) na Spika walimbeza (skepticism) wakisema hakuna ushaidi na hayo ni mambo ya mitandao. Waingereza wanasema " It came to pass". Leo hii kesi za EPA zinanguruma mahakamani na waziri Meghji sio waziri tena!

3) Katika nchi yetu sio mara ya kwanza kutaja wazi wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi. Septemba 2007 Dr. Slaa na wenzake walitaja majina kumi ya watuhumiwa wa ufisadi pale MwembeYanga, Temeke. Baadhi yao walicharuka na kutishia kwenda mahakamani kwa kuchafuliwa na wengine wakasema hakuna ushaidi. Mpaka leo hakuna hata kesi moja ilifunguliwa mahakamani kwa "uzushi" huu! Leo hii Mhe. Lowassa, Karamagi na Chenge wako nje ya Baraza la Mawaziri kwa tuhuma kama walizosema kina Dr, Slaa. Mhe, Mramba, Yona na Mgonja wako mahakamani kwa tuhuma kama hizo. Rais mstaaafu Ben Mkapa halali usingiz mzurii kwa kutuhumiwa na umma kwa kutumia madaraka vibaya. Kinachoshangaza wakati wote huu sijaona serikali ikitoa msimamo wake mkali (kama Mama Simba) kuhusu watuhumiwa wa Dr. Slaa. Kulikoni sasa waziri anakuja mbogo kwa kutajwa mafisadi watano tu? Labda kwa kuwa limeongezeka neno " papa"? Mbona serikali haijatoa tamko kuhusu kutuhumiwa Rais mstaafu?

4) Mhe. Rostam Aziz amekuwa akitajwa tajwa katika haya mambo ya ovyo. It is not by coincedence, I believe. Alitajwa Mwenbeyanga, anatajwa katika wizi wa EPA, alitajwa na Tume ya Mwakyembe kuhusu Richmond na Dowans na sasa anatuhumiwa na Mengi kuwa ni fisadi "papa" . Huyu ni sawa na "Yuda Iscariot" kwa kuisaliti CCM hapaswi kula meza moja na viongozi wetu labda kama nao ni "birds of the same feathers"? Kwa nini asitolewe kamati kuu CCM hadi hatakapojitakasa? Bila hivyo maswali yataulizwa tu. Wakubwa wapende wasipende.

5) Tanil Somaiya amefadhili uchaguzi wa juzi wa UV-CCM kwa "mchango" wa shs. 400 milioni. Je waziri Simba hakuona kwamba kwa utetezi wake kwa hawa watuhumiwa kunaweza kukatafusiriwa kwamba serikali ya CCM inalipa fadhila? Je wananchi wakisema CCM imetekwa na matajiri kuna wakubisha?

6) Mama Simba anasema Mengi kama ana ushahidi aupeleke kwenye vyombo husika hususan TAKUKURU. Tunauliza TAKUKURU ipi? Hii inayoongozwa na Hosea? Kuna azimio la Bunge kuhusu kiongozi huyu kwa kuboronga uchunguzi wa ufisadi Richmond. Mengi kama mtu mwelevu hawezi kupeleka kesi ya nyani kwa ngedere. Na hata wananchi hawana imani na Polisi katika mambo haya. Kama imani ingekuwepo serikali hii isengeitisha kura za maoni kutafuta wauaji wa Maalbino. Watu wangewataja watuhumiwa kwa jeshi la polisi na Polisi wangeisha maliza tatizo hili. Iko wapi ile orodha ya wauza unga aliyotuaaidi Mhe. Mwapachu akiwa waziri wa Usalama wa Taifa?

7) Sio mara ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho kwa Mengi kuzozana hadharani na wafanya biashara wenzake. Walikwaruzana na Yusuf Manji mpaka wakafikishana mahakamani. Mengi alizozana na Rostam kuhusu Rostam kuzindua album katika kanisa moja la Kiluteri mpaka (tunaambiwa) mchungaji akachukuliwa hatua. Hakuna jipya na sisi hatuoni kwa nini serikali inaigilia mzozo huu. Kuna sheria zinazohusu kafsha na kama waliotajwa na Mengi wanafikiri wameonewa Mengi kwa kauli yake atafurahi kukutana nao. Manji ameshatinga mahakani ni Rostam aende huko. Why is the minister poking her nose in the affairs that do not concern her? Ana kihele hele. Kwa hili yeye ndie KACHEMSHA na aambiwe hivyo.

8) Swala la Ubaguzi wa rangi halina mashiko. Hatuwezi kuogopa kutajana na kusutana eti tutaambiwa ni wabaguzi. Kama Wahaya kumi ni wezi wa mali ya Umma nawatajwe. Mbona wachaga wanasemwa kwa kujazana TRA kwa misingi ya Ukabila na hawajalalama? Lipumba na wenzake walikuwa wapi wakati Salum Mohamed Salum akibaguliwa wazi wazi wakati wa mchakato wa Urais ndani ya CCM 2005 na hakuna aliyenyosha kidole? Rostam should not hide behind racism veil to justify his misdeeds.

Nimalizie kwa kutoa mfano wa Biblia. Yesu alipowasema sana mafarisayo, mazudakayo na wakuu wa dini ya kiyahudi walipanga njama ya kumuua. Na katika kuhalilisha kifo chake Kuhani Mkuu wa wakati ule jina lake Keyafa aliwashauri kwamba " inabidi mtu mmoja afe kwa ajili ya wengi". Baadhi ya magazeti yamesema Mengi kwa kufanya alichofanya anajitoa mhanga. Inawezekana lile neno likatimia. Hatuwezi kuendelea na uoza huu katika nchi yetu. Tanzania bila Ufisadi inawezekana.
Mafisadi papa should be put on notice kuwa endapo Mengi atadhulika kwa namna yeyote ile, wao na washirika wao wanaowalinda wataiwasha nchi hii moto!!
 
How can Rostam run away from this? I need to know, how in the world huyu jamaa anakuwa na mikwara mingi?

from that letter i can say this, Rostam hajaandika bali ni mwanasheria wake sababu ya uchaguzi wa meneno unaonyesha. On top of that Rostam is empty head.

Jamani naomba niwe racist for a second, How is possible MUIRAN akacontrol maisha ya watu million 40? I just think Rostam doesn't care about Tanzania sababu He don't know nothing about Tanzania. Does Rostam know the struggle of majority of Tanzanian? Does he know the pain that watanzania wanapitia sababu ya mtandao wake. God help us, i lay my case mbele ya Mungu.... It seems no one can either defeat this guy.... Tanzania we have problem.

Huyu jamaa sio muiran ni mTanzania, sema umeshindwa umfanye nini umeamua kuingiza point ya uiran, amepewa kura na watanzania kama wewe, hajateuiwa huyu, sijaona point ya uian inakuja wapi, MKUU UKISEMA HIYO NDIYO KAMA VILE INAONYESHA YALE MAGEREZA NI YA WEUSI TU KAMWE HUTAKUTA WAHINDI NA WAARABU! huna jinsi na kamwe hatakuwa muiran ni mtanzania, mwenye tuhuma za ufisadi! swala ni kwa nini yuko huru? kwa nini hajafunguliwa mashtaka, kwa nini mnamuinua sana huyu jamaa??
 
Mafisadi papa should be put on notice kuwa endapo Mengi atadhulika kwa namna yeyote ile, wao na washirika wao wanaowalinda wataiwasha nchi hii moto!!


Tanzania haina historia hiyo kaka, Mengi wanaweza kumlima risasi sasa hivi na bado kesho jamaa akawa mbunge, JAMANI MATATIZO NI SISI WENYEWE!!!!!!!!!!
 
Let me make one thing clear here, am not in support of RA, Manji or Mengi. To me they all bunch of nuisance old businessmen who are driving this nation to its grave.

The biggest fool is The Executive Chairman of IPP Media, and Chairman of Media Owner Association of Tanzania plus holder of many other top position in bussness related associations, Mr powermonger, Reginald Mengi.

Inawezakana vipi akurupuke kuita waandishi wa habari na kuanza kubwabwaja na kuwatuhumu wenzake kwa kile anachodai ufisadi papa? Anataka kutuambia nini watanzania, mahakama zetu na vyombo vya dola vimeshindwa kufanya kazi yake ipasavyo, je yeye nani katika nchi hii hadi ifike wakati aende kifua mbele kuwatuhumu watu atakavyo.

Nakubali kuwa RA na kundi lake limetajwa sana kuhusika na vitendo vya kifisadi lakini jukumu la kuthibitisha hayo lipo mikono mwa polisi na si vinginevyo....mbona hatujamuona huyu mzee mnafiki kwenda kupiga kura kwenye ile kampeni yetu ya kuwataja watu wanaohusika na vifo vya maalbino na wahalifu wakubwa wakiwemo mafisadi. Ni kweli Bwana Mengi anauchungu na nchi hii? Kwanini hakupeleka ushahidi wake polisi na kisha kuja kututangazia umma kuwa yeye ameshalabidhi ushahidi na yuko tayari kuwa shahidi namba moja katika kesi dhidi ya watu hao?

Kusema kweli tabia ya mengi inakera sana hasa kwa nchi ambayo inafuata misingi ya demokrasia na utawala wa sheria kama Tanzania. Kwahiyo baada ya kuwataja alikuwa anatarajia nini kiendelee, au angejisikiaje kama sisi wananchi tungejichukulia sheria mkono kama ilivyokuwa kwa bwana Balali ambapo wananchi waliamua kujigawia mashamba yake kwa hasira. Mi simuelewi huyu mzee hata kidogo....kama ni ushindani kibiashara angetafuta njia nyingine si staili hii ya kuchonganisha wenzake. Hali hii inafanya niamini kuwa Mengi ameanzisha kikundi chake cha Kimafya ili kuspy wanayofanya wenzake...where else he would have gotten all these information and this guts to stand up in public and declare oother guilt without being prosecuted in court of law.

Najua wapo watu humu ndai wanajenga mapenzi kwa mtu yeyote anaelekea kuwasakama watuhumiwa hawa wa ufisadi, na hali hii inawezakana kuwapofusha hata warevu wachache kuona ukweli wa mambo. Kama mnapenda kusikia RA na wenzake wanakwenda mahakamani iweje msitoe hamasa hiyo hiyo kwa Bwana Mengi kwenda mahakamani au ndo ule usemi wa kiswahili usemao "Nani atamfunga paka kengele?". Let's not rejoice for anyone who break the law under the name of saving the nation unless we are all agree that our Jurisdictions can not be trusted and only then let take matter on our own hand as per Mr. Mengi point of view. Period

Rostam ni raia na mbunge. Aliapa kuitetea katiba ya jamhuri. Mengi hajaapishwa mbele ya katiba. Rostam anajua kuwa Mengi ni mtu mwenye maovu lakini kaamua kuyakalia. Je, kama hayo maovu ya Mengi yatakuja kuwa na madhara kwa wananchi hapo mbeleni (hata kama hayatakuja kuwa), kwa nini huyu aliyeapishwa kutuwakilisha anaficha maovu?
 
Tusimbeze Rostam, hatikisi kiberiti


Mwandishi Wetu
Aprili 23, 2008
rC.jpg

WIKI iliyopita nilikusanya magazeti yote ya wiki. Niliyasoma kijuu juu, ila nilipata fursa ya kuyapitia kwa ufasaha Jumapili nilipotoka kanisani.
Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wanahabari kwa kazi nzuri wanayofanya kuelimisha, kuburudisha na kuhabarisha jamii. Kimsingi nimekuta magazeti mengi kwa asilimia kubwa yakilifahamisha Taifa letu nini kinaendelea katika jamii.
Hata hivyo, wakati napitia gazeti la Raia Mwema, toleo namba 025, nilikutana na makala ndefu iliyochapishwa ukurasa wa nne na kuendelea ukurasa wa 22. Mwandishi wa makala hii ni Lula wa Ndali Mwananzela.
Makala hii ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho: "Sipendi Rostam Aziz atikise kiberiti bungeni." Alichambua na kuhoji Rostam alitaka kuzungumza nini bungeni hadi nchi nzima ikatetemeka.
Katika moja ya aya zake anasema: "Kitu gani hasa alitaka kusema kiasi kwamba kwa nyakati tofauti imeonekana kana kwamba ana ‘jambo' kubwa ambalo lingeweza kuleta vurugu bungeni?"
Anafafanua kuwa Rostam alitaka kupeleka maelezo ya ufafanuzi kuhusiana na mkataba wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond.
Makala hiyo inasema Rostam angetumia muda huo kujisafisha, na si ajabu angefika na vielelezo vyake zikiwamo fomu za BRELA zenye kuonyesha wamiliki halisi wa Richmond, na hivyo kujisafisha yeye na washirika wake.
Ameandika mengi, anayojua aliyatoa wapi, lakini pengine ninukuu aya ifuatayo iliyonifanya kuandika makala hii: "Hivi ni lini mara ya mwisho kwa Rostam kutoa mchango bungeni na alichangia nini? Ni kitu gani ambacho Rostam Aziz alisema bungeni katika mijadala ya bajeti au mingineyo ambayo inaweza kukumbukwa? Kama huko kote hajasema jambo lolote la kukukumbukwa, iweje leo tugwaye kama Taifa eti Rostam anataka kusema? Huku ni kujifanya duni kusiko na sababu."
Nimeamua kuijibu makala hii baada ya kuona tabia inayoibuka katika jamii yetu inastahili kukemewa vinginevyo itatupeleka pabaya. Namchukulia Rostam Aziz kama raia yeyote wa nchi hii mwenye haki ya msingi ya kujitetea anapokuwa ametuhumiwa.
Ni wiki iliyopita tu, tumeshuhudia Spika wa Bunge Samuel Sitta akijikanyaga juu ya uamuzi muhimu unaohusu kanuni za Bunge. Spika ni mhimili wa kanuni hizi, akijua kuwa jambo lililoamuliwa na Bunge haliwezi kujadiliwa katika muda wa miezi 12, katika mkutano wa 10, akasema Rostam angelazimika kuthibitisha tuhuma dhidi ya kamati ya Dk. Harrison Mwakyembe.
Rostam alikuwa akidai kutotendewa haki na kwamba kamati ilifanya kazi nje ya muda wake, hivyo aliamini kuwa ilifanya kazi kisiasa. Kama kweli wangekuwa na nia ya kumhoji wangeweza kumhoji, ila kumhoji kwao kungeweza kuvuruga mchezo wa kisiasa ulionuiwa.
Bunge la Mkutano wa 11 Sitta alikubali kumpa Rostam nafasi ya kutoa maelezo yake, lakini akatoa sharti kuwa shurti yaandikwe. Rostam alipoyaandika, Spika akabadili milingoti ya goli. Akasema kanuni za Bunge haziruhusu jambo lolote lililoamuliwa na Bunge kujadiliwa upya katika kipindi cha miezi 12!
Mwandishi wa makala ile anakiri nguvu na umuhimu wa Rostam Aziz katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kuwa nguvu kubwa aliyonayo ndani ya chama hicho ilimwogofya Spika Sitta,, pale anaposema: "Sasa kama mmoja wa mashabiki wake (Rostam) naye ataanza kumtwanga mangumi, basi si tu inawezekana kupata ufa mkubwa, lakini yaweza kabisa kusarambatika".
Mwandishi huyu huyu anayekiri nguvu ya Rostam, ndiye anadiriki kuhoji Rostam angesema nini na aliwahi kusema nini bungeni.
rostam_5.jpg


ROSTAM Aziz
Kilichonisikitisha zaidi, mwandishi wa makala hiyo naye ameangukia katika mkumbo. Anamwagia matope Rostam, bila kuchunguza na wala sijui kilichomtuma afanye hivyo.
Sitaki pia kuamini kama kweli mwandishi huyu anaishi nchini na ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya kisiasa.
Sina sababu ya kutumia nguvu kuonyesha ukweli umelala wapi katika kueleza Rostam alipata kuchangia nini akiwa bungeni. Kwa uchache niorodheshe matukio haya aliyotenda kwa ufasaha wa hali ya juu na kutikisa nchi akiwa bungeni.
Mwaka 1994 Taifa lilikumbwa na mfumuko wa bidhaa kutoka Zanzibar. Bidhaa hizo zilikuwa zikipita kwa njia ya panya, maarufu kama ‘Zanzibar route.' Zilikuwa azikiingia nchini bila kulipa kodi na kufurika madukani. Rostam alisimama bungeni, akajenga hoja na Serikali ikachukua hatua za haraka kudhibiti hali hiyo.
Alidiriki kuwatuhumu hata viongozi wa Zanzibar kuhusiana na biashara hiyo. Hapo alionyesha ujasiri wa kwanza akiwa mbunge kijana kuliko wote wakati huo.
Mwaka 1977 Rostam alikuwa mbunge pekee aliyekataa kuunga mkono muswada wa Sheria ya Madini. Alisema muswada huo ulikuwa na upungufu mkubwa wa msingi na akaonya kuwa iwapo ungepitishwa, vizazi vijavyo vingewahukumu wabunge kwa uamuzi huo. Leo kamati ya Madini ya Rais, chini ya Jaji Mark Bomani, imeipitia sheria hii. Si ajabu matokeo yatakuwa sawa na alivyokuwa amependekeza Rostam.
Mwaka 1999 Rostam huyu huyu ambaye mwandishi hakumbuki iwapo aliwahi kusema lolote bungeni, aliweka historia katika chama tawala. Akiwa mbunge wa chama tawala, aliongoza kundi la wabunge 50 kupinga iliyoitwa kesi ya uhaini dhidi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF).
Kumbuka CUF ni chama cha upinzani. Kesi hii ilikuwa imepandikizwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, akidai wabunge hao walikuwa na njama za kumpindua. Baada ya hoja ya Rostam, muda mfupi baadaye watuhumiwa wote waliachiwa.
Mwaka huo huo, kwa ujasiri mkubwa, Rostam aliongoza mapambano dhidi ya Dk. Salmin aliyetaka kubadili Katiba ya Zanzibar na kuongeza muda wake wa kuwa madarakani.
Yapo mengi, ila nikumbushe hata hili. Rostam huyo huyo anayebezwa, mwaka 2001, alisimama kidete kupinga mabadiliko ya Katiba yaliyokuwa yakimpa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka makubwa zaidi, ikiwa ni pamoja na kuteua wabunge 10.
Lakini si vibaya nikakumbusha kwamba pamoja na mengi yaliyozungumzwa na Rostam bungeni, na ambayo yamekuwa na manufaa kwa Taifa ni pamoja na lile la mwaka 2004 bungeni.
Katika mkutano wa Bunge la Bajeti, Rostam alimbana vilivyo aliyekuwa Waziri wa Uchumi na Mipango, Dk. Abdallah Kigoda juu ya kazi za wizara hiyo.
Nakumbuka vizuri sana suala hili. Hasa kutokana na ujasiri wake wa kuzuia shilingi, akitaka apewe majibu ya hoja kadhaa. Mosi, ilikuwa akitaka ahakikishiwe kuwa wizara hiyo inaachana na mpango wa kukusanya takwimu za uchumi, badala yake ibuni mipango thabiti ya uchumi na kuisimamia ipasavyo.
Akapendekeza Wizara ya Uchumi na Mipango iunganishwe na Wizara ya Fedha, kwani kazi zake zilikuwa pacha na zilizohitaji kuwa chini ya kiongozi mmoja. Leo suala hilo limetekelezwa na Seriakali iliyo madarakani.
Akataka uwepo udhibiti wa hali ya juu ili shilingi isiporomoke kila uchao, kwani athari za kushuka kwa thamani kulikuwa kunayumbisha uchumi.
Mjadala ulikuwa mkali mno, na wote walioshuhudia wanakumbuka vizuri hoja za Rostam ambazo baadaye zimetekelezwa.
Sipendi kuendelea zaidi ya hapo. Natumaini mwenye macho haambiwi tazama. Wapo wabunge wa kubezwa, lakini Rostam Aziz si mmoja wao, mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
Nimjuavyo Rostam Aziz, kwa ujasiri aliouonyesha ni kweli angetikisa nchi. Hata hivyo, hoja zinazopenyezwa kuwa angeweza kukiumbua chama chake, Chama Cha Mapinduzi, inaelekea wanaozitoa hawamfahamu vilivyo.
Kwa jinsi anavyojulikana, Rostam atakuwa mtu wa mwisho kukiumbua chama chake, hofu inayoonekana inatokana na ujasiri uliowekwa wazi na sehemu ya historia niliyoonyesha hapo juu.
Kwa vyovyote iwavyo, Mwananzela hakumtendea haki Rostam. Uandishi wa aina hii ni hatari kwa ustawi wa Taifa. Ninashauri bora kutoandika pale tusipokuwa na taarifa sahihi, vinginevyo tunaishia kujiumbua na kulipotosha Taifa.

source: http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=599

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=599

Jamani nimeweka hii hapa ili tumfahamu huyu jamaa, na njia pekee ya kupambana naye ni kuindoa CCM madarakani, nje ya hapo atabaki na atendelea tu!
 
Rostam ni raia na mbunge. Aliapa kuitetea katiba ya jamhuri. Mengi hajaapishwa mbele ya katiba. Rostam anajua kuwa Mengi ni mtu mwenye maovu lakini kaamua kuyakalia. Je, kama hayo maovu ya Mengi yatakuja kuwa na madhara kwa wananchi hapo mbeleni (hata kama hayatakuja kuwa), kwa nini huyu aliyeapishwa kutuwakilisha anaficha maovu?

Tunacho kifanya hapa JF ni sawa na unakuta watu wanakimbiza mwizi na wewe bila kujua kaiba nini unatoa mchango wako kumshughulikia matokeo yake watu wengi wasio na hatia wamepoteza maisha yao au kupata vilema vya maisha. Mengi anajua fika uwepo wa vyombo vya kisheria katika suala hilo na hata sisi sidhani kama tumefikia hatua ya kutoviamini vyombo hvi.

Hoja yako haina mashiko kwasababu suala la kula kiapo halihusiani na jambo hili, basi kama ndo hivyo tuwape wabunge mabunduki ili tujue moja kuwa na wao wanafanya kazi ya usalama wa raia. Zipo taasisi maalum zilizopewa mamlaka kisheria kufuatilia nani anakosa na hana...wabunge hawahusiki katika mchakato huu. Kama RA hakuamua kupeleka taarifa kunakohusika haina maana na yeye ahukumiwe kwa hilo...pleeeeaaasseee wajameni wake up, Mengi anaitumia hii forum kwa taarifa yenu ngoja niwaleteeni ushahidi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom