Tamko la Rais kuhusu benki ya walimu kuyumba ni hatari kwa ustawi wa benki

celinawetu

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
1,331
1,059
Ni majuzi akiongea na walimu huko dodoma alisema benki ya walimu inayumba..
Najiuliza hivi alidhamiria kutoa hilo tamko au bahati mbaya. Anajua athari zake kwa benk kwa yale matamshi au mdomo ulimteleza kama alivyoteleza pale aliposema yeye na mkewe wanajua namna ya kumalizana hadi mkewe akaangalia chini kwa aibu.

Kimsingi ile kauli ni moja ya mwanzo wa kuyumba kwa ile benk kwani wateja watakosa imani na kukimbilia kuchukua hela zao.

Hivi ni lini atajifunza aseme nini wapi na wakati gani,

A shameful statements ...
 
kwa hiyo benki inayofanya vibaya ifichiwe mabaya yake siku wateja wakikosa huduma muilaumu serikali...

haya mambo ya taifa starz haya timu inafanya vibaya lakini inasifiwa tu imejitahidi kila siku
 
Pia hajali kama ni Bank wanawake au wanaume, ikiyumba anaifunga. Yeye ni BoT na kila kitu. Lakini kwenye mkutano wa UWT kasema wakaifufue ile Bank. Hivi ya UWT? Au wanawake wote bila kujali vyama vyao?
Kauli zake zinaonyesha uelewa mdogo wa masuala mbalimbali.
 
Unazungumzia kuhusu bank ya walimu kuyumba , then ishu ya mke wake imeingiaje hapo!
Ujinga bado unatusumbua watanzania wengi kama hata kueleza hoja yako umeshindwa.
 
Benki ya waalimu ikifa Watanzania wengi sana waliowekeza hisa zao wataathirika.

Kwanza kabisa, Soko la hisa lilifanya makosa kuruhusu benki ambayo ilikuwa haijaanza kufanya kazi kujiandikisha katika soko la hisa.

Serikali wakati huo haikusema lo lote; wakati walijua kabisa kuwa taratibu zilikiukwa.

Sasa hivi ndiyo serikali inaona kuwa benki inayumba..!
 
We ni mwehu maneno yote aliyaongea siku hyo nahoji alijisahau kwa yote maneno mawli, ya benk na yake na mkewe?
UNGEFUNGUA UZI MBILI TOFAUTI MKUU MOJA YA MKEWE NA YA BANK,kama ulimsikiliza kwa makini alisema kutokana na taarifa alizozipata toka BOT hyo bank iko shakani inaweza kufutwa na akalaumu mikopo wanakua hawapewi mikopo wanakopa wasio walimu na wameshindwa rejeshabank iko taabani sasa ni kosa la nani, unataka nchi ndo iweke pesa pale ama kufutwa?
 
Ni majuzi akiongea na walimu huko dodoma alisema benki ya walimu inayumba..
Najiuliza hivi alidhamiria kutoa hilo tamko au bahati mbaya. Anajua athari zake kwa benk kwa yale matamshi au mdomo ulimteleza kama alivyoteleza pale aliposema yeye na mkewe wanajua namna ya kumalizana hadi mkewe akaangalia chini kwa aibu.

Kimsingi ile kauli ni moja ya mwanzo wa kuyumba kwa ile benk kwani wateja watakosa imani na kukimbilia kuchukua hela zao.

Hivi ni lini atajifunza aseme nini wapi na wakati gani,

A shameful statements ...

Hii alifanya pia dhidhi ya twiga bancorp. Washauri wake wanastahili lawama zote.

Ni dhahiri kuwa mheshimiwa hapati ushauri mzuri katika maswala ya uchumi na commerce. Mambo mengi anayoganya yanapelekea uchumi kuporomoka zaidi hata kama nia yake siyo hiyo.

Benki inayoyumba kuna utaratibu mahsusi wa namna ya kuisalimisha ili wenye amana wasiumie. BOT inafahamu huu utaratibu, ambao unatekelezwa kwa BOT kuja siku isiyotangazwa na kuichukua benki na kuiweka under administration. BOT haiendi majukwaani na kuanzw kuiponda benki husika kabla ya yukio kwa sababu kufanya hivyo kutapelekea wenye amana zao ku rush hiyo benki na kuiangamiza kabisa, hata kama ingewezekana kuinusuru.
 
UNGEFUNGUA UZI MBILI TOFAUTI MKUU MOJA YA MKEWE NA YA BANK,kama ulimsikiliza kwa makini alisema kutokana na taarifa alizozipata toka BOT hyo bank iko shakani inaweza kufutwa na akalaumu mikopo wanakua hawapewi mikopo wanakopa wasio walimu na wameshindwa rejeshabank iko taabani sasa ni kosa la nani, unataka nchi ndo iweke pesa pale ama kufutwa?

Kama uko timamu ungekubali pale hapakuwa platfom ya kuongelea, angeacha BOT wafanye mkakati kui stabilize, kitakachotokea ni wsteja kukimbia hivyo ku accelerate kulelekea kufa, nchi hii imekuwa na marais wanne kabla ya huyu hawskuwahi kuwa waropokaji kwa vitu vilivyo na impact mbaya ktk maendeleo,
Ndo maana nauliza alimaanisha nn huyu bwana
 
Hii alifanya pia dhidhi ya twiga bancorp. Washauri wake wanastahili lawama zote.

Ni dhahiri kuwa mheshimiwa hapati ushauri mzuri katika maswala ya uchumi na commerce. Mambo mengi anayoganya yanapelekea uchumi kuporomoka zaidi hata kama nia yake siyo hiyo.

Benki inayoyumba kuna utaratibu mahsusi wa namna ya kuisalimisha ili wenye amana wasiumie. BOT inafahamu huu utaratibu, ambao unatekelezwa kwa BOT kuja siku isiyotangazwa na kuichukua benki na kuiweka under administration. BOT haiendi majukwaani na kuanzw kuiponda benki husika kabla ya yukio kwa sababu kufanya hivyo kutapelekea wenye amana zao ku rush hiyo benki na kuiangamiza kabisa, hata kama ingewezekana kuinusuru.
MKUU TUSIWALAUMU WASHAURI WAKE ALISHA SEMA "SIPANGIWI"
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom