Tamko la pamoja kati ya vyama vya wafanyakazi na asasi za kiraia

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
TAMKO LA PAMOJA KATI YA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA ASASI ZA KIRAIA KUHUSU MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII UNAOKWENDA KUZUIA FAO LA KUJITOA

Ndugu Waandishi wa habari , kwanza tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa namna mnavyoendelea kutupatia ushirikiano katika kutimiza wajibu wetu wa kudai, kulinda na kutetea masilahi ya wafanyakazi wa nchi hii na taifa kwa ujumla. Tunaomba muendelee na moyo huo ili tusaidiane kuijenga Tanzania tuipendayo.

Sisis sote kwa pamoja kupitia Jumuiya mbalimbali za wafanyakazi Tanzania kama vile NUMET, TUCTA, RAAWU, TUIKO, CWT, CHODAWU na Mitandao ya Asasi za Kiraia Tanzania chini ya Mwamvuli wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), tumepokea kwa masikitiko makubwa lengo la serikali kutaka kuondoa kabisa utataratibu wa Fao la Kujitoa( Withdrawal Benefit) kupitia Mswada wa Sheria ya Mifuko ya Jamiii unategemewa kujadiliwa Bungeni Muda wowote.

Mchakato huu wa kubadilisha Sheria za Mafao ulipaswa kuwa shirikishi kwa kuwahusisha wenye mifuko hiyo wenyewe (yaani wafanyakazi) kupitia vyama vyao na vikundi vyao vinavyotambuliwa kisheria. Kinachoshangaza ni usiri mkubwa katika zoezi hili hasa lengo la kutaka kupeleka Mswaada huu kwa hati ya dharura bungeni bila kutoa ushiriki wa wadau kikamalifu.

Ndugu, waandishi wa habari pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye Mswaada huo, kwa leo tumeona ni vyema tulizungumzie suala moja la muhimu ambalo litakwenda kuumiza sana watanzania wafanyakazi hasa wale wanaofanya kazi katika maeneo yasiyokuwa na ajira za kudumu kama migodini, viwandani, mashambani na kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali (AZAKI). Suala hilo ni haki ya Fao la Kujitoa kwa mfanyanyakazi anaecha kazi ama kumaliza muda wake wa kazi kabla ya umri wa kustaafu.

HISTORIA FUPI YA SAKATA LA FAO LA KUJITOA

Yafuatayo ni maelezo juu ya Fao la kujitoa, tunaomba kila mmoja wenu asambaze taarifa hii kwa wabunge, viongozi wa serikali na wafanyakazi wote nchini hususan wale wanaofanya kazi katika tasnia za migodi , viwanda, biashara, nishati, taasisi za kidini, taasisi za kitaaluma, mashirika ya kiserikali na asasi za kiraia nchini.

Sote tunakumbuka kuwa, tatizo hili liliibuka kwa mara ya kwanza mwaka 2012 baada ya Sheria ya udhibiti wa mifukoyahifadhiyajamii (SSRA) kupitishwa Bungeni mwezi April, 2012 na kusainiwa na Mheshimiwa Raisi wa JamuhuriyaMuungano wa Tanzania Dr. JakayaMrishoKikwete.

Sheria hiyo pamoja na mambo mengine iliondoa fao lakujitoa (withdrawal benefit) ambalo lilikuwepo kisheria katika baadhi ya mifuko na mingine ilikuwa ikilitoa kwasababu ilionekana ni muhimu sana fao hili kutolewa, lakini sheria ikapitishwa na kumtaka mfanyakazi kutochukua mafao yake hadi atakapofikisha umri wa kustaafu yaani miaka 55 au 60.

Baada ya Sheria hiyo kupitishwa, iliiibuka mijadala mingi kutoka kwa wafanyakazi hasa wa Sektabinafsi kama vile, migodini, ujenzi, mashambani, mashirika yasio ya kisherikali, Asasi za kiraia n.k hali iliyopelekea baadhi makampuni na mashirika kusitisha shughuli zake na baadhi ya wafanyakazi kupoteza ajira zao.

Baadae wabunge mbalimbali walipaza sauti zao bungeni kupinga sheria hiyo iliyokuwa na mapungufu mengi, hadikupelekea Mh. Seleman S. Jafo, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, kupeleka hoja binafsi katika kikao cha 41 cha mkutano wa 8 cha Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Baada ya Mjadala mrefu Bungeni serikali iliunda Kikosi kazi kilichozunguka kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ndani na njeyanchi.

Baada ya kikosi kazi kukamilisha kazi yake na kupeleka taarifa yake serikalini, Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Kazi na Ajira alitoa kauli ya serikali bungeni kuwa Fao la kujitoa litaendelea kutolewa kama ilivyo kuwa kabla ya mabadiliko ya sheria na pia, Serikali iliomba Bunge liipatie muda ili kuleta muswada mpya wa Sheria ya marekebisho ya mifuko ya hifadhi ya jamii itakayo kuwa endelevu na itakayojumuisha maslahi yawadau na kutoa wito kwa wadau kuendelea kutoa maoni yao juu ya maboresho ya jambo hili. Baada ya kauli hiyo, hali ilirejea kuwa ya utulivu na amani, na fao liliendelea kutolewa kama kawaida.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida siku ya tarehe 23/05/2016, msemaji wa PPF alinukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema PPF wameamua kusitisha utoaji wa fao hilo kwa sababu hakuna sheria inayowataka kutoa fao hilo. Wafanyakazi kupitia vyama vyao walifanya jitihada za kutafuta ukweli huo kutoka SSRA lakini hakuna majibu yaliyotolewa kufafanua jambo hili hadi vyama vilipokutana na waziri mwenye dhamana ambaye alithibitisha kupata taarifa hizo na kuahidi kuzifanyia kazi na kutoa taarifa baada ya kuwasiliana na waziri wa fedha mwenye dhamana ya mfuko wa PPF na Mkurugenzi wa SSRA. Hata hivyo TAMKO lililotolewa na SSRA lilikwepa hoja ya wafanyakazi na kuongelea fao la kutokuwa na ajira.

KWANINI FAO LA KUJITOA NI MUHIMU

Wafanyakazi hasa wa sekta binafsi walipeleka sababu zao za ni kwanini fao la kujitoa ni muhimu kuendelea kutolewa kwa wafanyakazi hasa wale wanafanya kazi katika Asasiza za Kiraia, Mashirika ya Kiserikali, Migodini, Viwandani, Majumbani na sector zote binafisi. Zifuatazo ni sababu kuu muhimu;

1. Ajira katika sector binafisi siyo ya kudumu, ni ya mikataba ya muda mfupi kati ya miaka 2-5.
2. Wanafunzi wengi wanapomaliza shule au vyuo hupenda kufanya kazi kwa muda na baadaye kutumia fao la kujitoa kujiendeleza kielimu.
3. Watu wengi wanapoacha kazi au mikataba yao inapokuwa imekwisha katika maoneo ya kazi, hupenda kufungua biasha binafsi badala ya kuajiriwa upya, na mtaji unaotegemewa ni hilo fao la kujitoa.
4. Watu wengi wanaofanya kazi katika sector binafsi wanaacha kazi au mikataba kwisha wakiwa katika umri mdogo (25-40), hivyo hutegemea sana fao la kujitoa katika kuboresha maisha yao na familia zao.
5. Ni vigumu sana kuingia kichwani kama leo hii tumefikia hatua ya kutaka mtu anaecha kazi akiwa na mika 25 au 30, akae hadi afike miaka 60 ndipo achukue pesa zake sawa na yule anaefanya kazi hadi kufikia miaka hiyo 60 na kustaafu. Hapa inaoneka wameshindwa kuelewa matumizi ya pensheni, lengo la mafao haya ni kumsaidia yule mfanyakazi anapokoma kufanya kazi maisha yake yaendelee kuwa kama alipokuwa kazini na si kumfikisha miaka ya kustaafu. Hivyo anamaliza kazi akiwa na umri unaotakiwa kustaafu kisheria na yule anaondoka kazini kwa sababu mbalimbali kabla ya umri wa kustaafu wote wanahitaji kutumia mafao yao kuendelea kuboresha maisha.
6. Tofauti na sekta zingine, migodi ina ukomo wa maisha. Kwa mfano kwa taarifa tulizo nazo maisha ya migodi mikubwa ya Tanzania ni kama ifuatavyo;

i. Bulyanhulu Gold Mine Ltd miaka 19 kutoka sasa
ii. Geita Gold Mining Ltd miaka 10 kutoka sasa
iii. North Mara Gold Mine miaka 6 kutoka sasa
iv. Buzwagi Gold Mine miaka 4 kutoka sasa
Pia, ikumbukwe kuwa Migodi ya Tulawaka, Resolute na Buhemba imeishafungwa hadi sasa. Hivyo wafanyakazi wote wenye umri mdogo na wenye umri wa kustaafau wote watahitaji mafao yao. Kwa upande wa kampuni za utafiti wa magfuta na gesi kampuni kama Petrobras Tanzania ilianza utafiti mwaka 2010 na kufunga utafiti na ofisi zake hapa nchini mwaka 2016. Kutokana na mifano hiyo ni dhahiri kuwa sekta ya nishati na madini ina ukomo wa maisha.
7. Kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na asasi za kiraia, mara nyingi zinakuwa na ajira za muda mfupi kulingana na miradi wanayokuwa wanashughulikia kwa wakati maalum. Mashirika mengi na miradi mbali mbali isiyo na idadi imeishafungwa na wafanyakazi wako mitaani hawana kazi za kufanya na hivyo hutegemea zaidi mafao yao kujiendeleza kimaisha. Hutegemea mafao yao angalau kuendeleza huduma za lazima kama malazi, chakula, matibabu, mavazi na kusomesha watoto.

8. Uzalishaji katika sekta ya nishati, madini na viwanda huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya bei (price elasticity –elastic), na hivyo waajiri hukimbilia kupunguza wafanyakazi kama njia ya kupunguza gharama za uendeshaji ili kukabiliana na mabadiliko hayo ya bei.
9. Wafanyakazi katika makampuni ya ujenzi wa barabara na majengo hupata ajira ya muda mfupi maana miradi mingi huwa ni ya muda mfupi, pia wafanyakazi wa mashambani huajiriwa kwa msimu na kwa kuwa ni wazoefu katika maeneo hayo tu si kazi rahisi kupata ajira katika maeneo mengine hasa ukizingatia wengi wao sio wataalaam (non professionals) na ukosefu wa ajira Tanzania ni tatizo kubwa.

10. Pia wanahabari wengi wanamikataba mifupi na waajiri wao, hivyo kujitkuta wanamaliza mikataba katika umri mdogo unaohitaji pesa katika kuendesha maisha ya kila siku. Na wengi hutegemea mafao ya kujitoa kuendesha maisha huku wakitafuta ajira nyingine.

11. Pia wabunge na wanasiasa humaliza muda wao wa Ubunge ambao ni wa miaka 5, na kutegemea mafao hayo kujiimarisha kisiasa au kuendesha maisha nje ya siasa kama kufungua bishara nk. Hivyo kwa sasa sheria hiii itawaumiza hadi wabunge na wanasiasa wanaofanya kazi kuwa vipindi vya mika mitano mitano.

12. Matatizo ya magonjwa yatokanayo na kazi na ajali kazini huwasababisha wafanyakazi kuacha kazi au kuachishwa kazi kwa sababu hawana uwezo wa kufanya kazi tena, pia kuna baadhi ya wafanyakazi ambao huacha au kuachishwa kazi na baadae kujigundua kuwa wameathirika na magonjwa yatokanayo na kazi wakati huo wakiwa hawana chanzo chochote cha kipato hutumia mafao haya kujitibu.Hivyo kumwambia mfanyakazi anaecha kazi akiwa na umri kati ya 25-35 asubiri mafao yake tangu hadi afikishe miaka ya kusataafu ni sawa na kumwambia hatolipwa hadi kifo.

13. Wafanyakazi wengi katika sector binafsi hulipwa mshahara kidogo sana ambao huwezi kujikimu kwa mwezi mzima na kuacha akiba kwa ajili ya kujitafutia vyanzo vingine vya mapato kama vile ujasiriamali. Chukulia mfanyakazi sekta ya ulinzi ambaye sheria imepitishwa kwamba kima cha chini ni Sh. 105,000/=. Mfanyakazi huyu anakaa lindoni kwa saa zisizopungua 12, kwa siku 30 kwa mwezi , na mwisho wa mwezi anapokea kiasi hicho cha pesa, anayo familia inayomtegemea kwa kila kitu, ataishije baada ya ajira kukoma? . Kwa maanake huyu akifanya kazi kwa mkataba wa miaka 5, mafao yake yatakuwa ni madogo sana kiasi kwamba unapomwabia asubiri hadi uzeeni ndio aichukue ni sawa na kumwambia ulifanya kazi bila kuwa na mafao yoyote.

14. Wafanyakazi wengi wa sekta binafsi hawakopesheki;- kutokana na usalama mdogo wa kazi (job insecurity) wafanyakazi wa sekta binafsi hawakopesheki na taasisi za fedha na hivyo hawawezi kupata mitaji ya kufanya miradi yoyote ya maendeleo wanapokuwa kazini. Na kwasababu mshahara wanaolipwa ni mdogo siku zote huishi maisha ya kubahatisha, na mfanyakazi huishi bila hata akiba ya shilingi moja katika maisha yake yote ya utumishi wake. Hivyo kumnyima tena hicho kidogo alichodunduliza kwa muda huo mfupi wa kazi ni sawa na kuzalisha taifa la mafukara wasioweza kubudu maisha ya kawaida.

15. KUKOSA SIFA ZA MAFAO YA UZEENI;-Wastani wa Umri wa wafanyakazi katika migodi yote hapa nchini ni miaka 35, hata wafanyakazi wengi wanaoacha au kuachishwa kazi katika maeneo mbali mbali ya ajira kwenye sekta binafsi wana umri huo. Ukifanya utafiti migodini, mashambani, makampuni ya ujenzi, asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini, wafanyakazi walio wengi wamefanya kazi kati ya miaka 0 hadi 5, na asilimia ndogo sana wapo kati ya miaka 5-10.

16. Muda wa uchangiaji katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa mfanyakazi wa tasnia ya nishati na madini ni miaka mitano (5) badala ya miaka 15 ya sheria.Wengi hutoka kazini wakiwa na umri wa miaka 35 badala ya 55 ya sheria. Kwa maana hiyo wafanya kazi wengi katika sector binafsi huacha kazi bila kufika ule umri wa miaka 15 kisheria ambao ndio unastahili kulipwa pensheni baada ya kustaafu, hasa pensheni ya kila mwezi. Ikimbukwe kuwa mu anapostaafu baada ya kufanya kazi hadi umri wa kustataafu, hulipwa mafao yake yote kwa mkupu pamoja na pensheni ya uzeeni kila mwezi had atakapokufa.

17. Kutokana na upungufu mkubwa wa ajira nchini, wafanyakazi wanapoondoka kazini hawana uhakika wa kupata ajira nyingine. Na pia wakati huo hawatakuwa katika mfumo wa pensheni kila mwezi. Manake ni kwamba serikali inajali zaidi maisha ya mtanzania huyu tu akifika miaka 60,na kumwacha bila kipato chochote miaka yote hiyo alipoacha kazi hadi kufikia miaka 60 huku pesa zake zikitumiwa matumizi ya watu wengine.

18. Waajiri hasa wa kampuni zilizowekeza kwenye sekta binafsi hawapendi wafanyakazi kazi kudai haki zao, inapotokea mfanyakazi ameachishwa kazi hata kwa kuonewa, akaenda kwenye vyombo vya haki mfano Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) au Mahakama Kuu ya kazi, waajiri humuwekea mfanyakazi huyo kitu kinachoitwa “red flag” au black list, hii ni alama ambayo mfanyakazi akiwekewa basi hatoajiriwa mahali popote kwenye makampuni ya namna hiyo kwasababu wao wamejiwekea utaratibu huo wa siri na huwa wanapeana taarifa juu ya wafanyakazi kabla ya kuwaajiri.

19. Kutokana na ukweli kwamba, kwa muda mrefu thamani ya Shilingi ya Tanzania imekuwa ikishuka kwa kasi sana, ni wazi kwamba mfanyakazi anayepoteza ajira akiwa na umri wa miaka 35 leo, atapaswa kusubiri miaka 20 ili aweze kuingia kwenye mfuko wa malipo ya uzeeni (pension). Na kwakuwa kanuni ya ukokotoaji wa mafao inazingatia mshahara wa mwisho wa mfanyakazi, ni dhahiri mshahara wa mwisho utakuwa ni wa miaka 20 nyuma ambao utakuwa umeathiriwa sana na mabadiliko ya thamani ya pesa ( low value). Hivyo mtu huyu kama alipaswa kulipwa million 10 mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 35 atakuja kulipwa hiyo hiyo milioni 10 mwaka 2036 akiwa na umri wa miaka 55, kitu ambacho ni kibaya sana kwani million kumi wakati huo itakuwa ni sawa na miliono moja kwa sasa. Ikumbukwe pesa hizi haziongozeki, hivyo leo ukimzua mfanyakazi aliecha kazi akiwa na umri wa mika 35, asichukue fao lake mfano wa miliono 20, badaye miaka 20 hatoweza itumia pesa hiyo kwa thamani ya leo.

MSWAADA UNASEMAJE KUHUSU FAO LA KUJITOA

Kwa kifupi muswada huu umeondoa kabisa fao la kujitoa na badala yake unapendekeza kuwepo kwa fao la kutokuwa na ajira. Fao la kutokuwa na ajira linamruhusu mwanachama wa mfuko ambaye ameachishwa kazi (hakuacha kazi kwa hiyari yake / resignation), na amechangia zaidi ya miezi kumi na nane (18), kuomba alipwe asilimia thelathini (30%) ya mshahara wake wa mwisho baada ya kupoteza ajira, na atalipwa kwa miezi sita (6) mfululizo tu, na baada ya hapo malipo hayo yatasitishwa. Baada ya miaka mitatu (3) tangu kusitishwa/ kuisha kwa hilo fao la kutokuwa na ajira, mfanyakazi atakayekuwa bado hajapata ajira ataruhusiwa kuomba michango kuhamishwa kutoka kwenye mfuko wa lazima (compulsory scheme) kwenda kwenye mfuko wa hiari (supplementary scheme), baada yamichango yake kuhamishwa, hapo ataweza kuendelea kuchangia kwa hiari na kufuata utaratibu wa kila mfuko kuomba kuchukua michango yake. Kwa mfanyakazi ambaye amechangia chini ya miezi kumi na minane (18%), na ameachishwa kazi (hakuacha kazi kwa hiyari yake / resignation), atakuwa na haki ya kurudishiwa asilimia hamsini (50%) ya michango yake.

Aidha Mswaada unasema kuwa malipo ya fao la kujitoa hayatazidi jumla ya miezi kumi na nane (18) sawa na mwaka mmoja na nusu katika maisha ya ajira. Manake ukifanya kazi kwa miaka 2 na kuendelea huwezi pata fao la kujitoa, badala utapata fao la kutokuwa na ajira baada ya miaka 3 tangu ulipoacha kazi na utaweza pata fao la kutokuwa na ajira kwa asilimia 50% tu baaada ya kuhamishia kwenye mfuko wa hiari. Pia watu wanaocha kwa kazi kwa hiari yao na magonjwa haijulikani hatma yao.

MAPENDEKEZO YETU KWA UJUMLA
(A) Kwa Serikali,
1) Kwakuwa hadi sasa fao la kujitoa halitolewi tena wakati bado sheria haijatungwa, tunaitaka serikali itoe tamko mara moja la kuruhusu mafao hayo kutolewa kwa wafanyakazi ambao hawako kazini kwa sasa.

2) Kutokana na sababu tulizozitoa hapo juu, ni dhahiri kwamba hakuna namna unavyoweza kuondoa fao hili la kujitoa bila kuathili maisha ya wafanyakazi hasa katika sekta binafsi. Hivyo tunaishauri serikali iache utaratibu uliokuwepo uendelee kwa maana kwamba, mfanyakazi awe na hiari ya kuchukua mafao yake au kusubiri kustaafu badala ya kuwawekea vikwazo kwenye pesa zao.

3) Fao la kutokuwa na ajira ni takwa la mikataba ya ILO hivyo litolewe na bila vikwazo na serikali ilisimamie hili, aidha fao hili lisiishie kwa wale waliopoteza ajira tu, bali kama linavyoitwa fao la kutokuwa na ajira, basi lipelekwe kwa watanzania wote wenye sifa na haki ya kuajiriwa lakini kutokana na ukosefu wa ajira nchini wameshindwa kupata ajira hiyo. Lakini pia, wadau wote washirikishwe katika kuweka utaratibu wa kutengeneza viwango vya malipo hayo ya fao la kutokuwa na ajira.

4) Serikali ihakikishe inashirikisha wadau wote katika kutunga sheria na masuala mengine yote yanayo wahusu wafanyakazi. Ifahamike kuwa kushirikisha wadau wachache kwenye masuala muhimu Kama haya ni kuwanyima wafanyakazi na wadau wengine haki ya kutoa maoni yao.

5) Fao la kujitoa libakie kuwa ni haki kwa wafanyakazi wa ajira za muda usiozidi miaka 15.

B) KWA WABUNGE
6) Tunawasihi wabunge Kama wawakilishi wetu, na wao kama waathirika wa mabadiliko haya, kusitisha majadlilano ya Mswada wa mabadiliko ya sheria ya mifuko ya hifadhi ya jamii unaotarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza kwenye vikao vinavyoendelea vya Bunge la 4 usisomwe hadi serikali irejeshe kipengele cha fao la kujitoa.
C) KWA JUMUIYA ZA WAFANYAKAZI
6. Watumie muda kutetea maslahi ya wafanyakazi wao, kwani kutokufanya hivyo kunaweza leta tafsiri mbaya ya kuwepo kwa jumuiya hizi.
7. Watanzania wote wapaze sauti kukataa Mswaada huu kwani unakwenda kubinya haki za watanzania wengi wanaofanya kazi kwa jasho lao katika maeneo mbalimbali.

D) KWA WANAHABARI
8. Tunawasihi wanahabari wote hapa nchini kutumia muda huu mchache kutoa elimu kwa wananchi,wafanyakazi na hata viongozi wetu juu ya madhara yatakayojitokeza endapo wafanyakazi wa muda mfupi watanyimwa mafao yao hadi uzeeni.

MWISHO

Tunaamini kabisa tamko hili litawafikia viongozi wetu na wabunge wetu huko bungeni, na hatimaye wataungana na sisi katika hoja zetu za msingi hapo juu kuhusu umuhimu wa kuendelea kuwepo kwa fao la kujitoa hasa kwa wafanyakazi wa sector binafsi. Na Kama sauti hii itapuuzwa, wafanyakazi wanaweza chukua hatua mbalimabli Kama vile kwenda mahakamani, kugoma na kujitoa kwenye mifuko hiyo. Pia waajiri wanaweza sitisha pelekea michango kwenye mifuko hiyo na kufungua account za mafao hayo hadi hapo usalama wa fedha za wafanyakazi utakapopatikana katika mifuko ya jamii hasa suala hili la fao la kujitoa.

TAMKO HILI LIMEANDALIWA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI PAMOJA NA ASASI ZA KIRAIA NCHINI ,09/09/2016.

Imesainiwa kwa Niaba na:

Gratius Mkoba, Rais TUCTA/ CWT

Onesmo Olengurumwa, Mratibu Kitaifa THRDC/AZAKI

Nicomemas Kajungu,
Katibu Mkuu NEMET
National Union of Mine & Energy Workers of Tanzania (NUMET)

B. Majura Katibu Mkuu, TUICO

Adv. Kasambala -Naibu Katibu MKuu- TPAWU

Ramadhani Mwendwa- Katibu RAAWU-Kanda ya Kati
 
Lawama zote kwenye huu mswada zielekezwe kwa wabunge wa CCM nyie ndiyo mna majority votes.
Wabunge wa CCM Mungu anawaona.
 
M nimegoma kupelekewa makato yang mpaka nihakikishe naweza kuyatoa pind kaz ya mwaka mmoja itakapo isha

Kwa mwendo hu serikal haipat chenji yang nitajitunzia
 
Lawama zote kwenye huu mswada zielekezwe kwa wabunge wa CCM nyie ndiyo mna majority votes.
Wabunge wa CCM Mungu anawaona.

Hapa pana matatizo mawili.

La kwanza ni uelewa, waelimishwe tu wataelewa umuhimu wa kufutwa fao hili na kuwataka wahusika wajibidiishe kutafuta kazi ingine. Mtu wa miaka 25 anataka mafao ya uzeeni ya nini wakati bado ana miaka 35 ya taabu huko mbele? Si atavute kazi ingine?

La pili of course ni siasa. Kuna vinara wa UKAWA humu ndani - wako tayari kufanya chochote ili tu amani ivurugike.
 
Wewe ni mmoja wa watoto wa wenye ccm yao bila shaka. Umezaliwa ukakuta kila kitu kipo hivyo hauna shida.
 
Nil
Hapa pana matatizo mawili.

La kwanza ni uelewa, waelimishwe tu wataelewa umuhimu wa kufutwa fao hili na kuwataka wahusika wajibidiishe kutafuta kazi ingine. Mtu wa miaka 25 anataka mafao ya uzeeni ya nini wakati bado ana miaka 35 ya taabu huko mbele? Si atavute kazi ingine?

La pili of course ni siasa. Kuna vinara wa UKAWA humu ndani - wako tayari kufanya chochote ili tu amani ivurugike.
Nilitamani nitoe neno chafu juu yako
 
Tafiti zinaonyesha wengi wa waliojitoa walipata kati ya Tshs 400'000-1'000'000. Je hizi zinatosha kuanza Biashara?
Au kuna Siasa ndani yake?
 
Tumia hata robo ya ubongo wako kuwaza... Ndorobo mkubwa we mtu wenywe ugari kwa kengele unajua hata uchungu wa kusaka hela na kufanya kazi mwehu we
 
Hapa pana matatizo mawili.

La kwanza ni uelewa, waelimishwe tu wataelewa umuhimu wa kufutwa fao hili na kuwataka wahusika wajibidiishe kutafuta kazi ingine. Mtu wa miaka 25 anataka mafao ya uzeeni ya nini wakati bado ana miaka 35 ya taabu huko mbele? Si atavute kazi ingine?

La pili of course ni siasa. Kuna vinara wa UKAWA humu ndani - wako tayari kufanya chochote ili tu amani ivurugike.

Ni bora usingejibu chochote mana umeharisha vibaya mno ,dehydration iliotokea Ni Paka kwa ubongo,unahitaji monitoring wewe
 
Naona akili zimeanza kuja. Tutafika tu.
 
Hapa pana matatizo mawili.

La kwanza ni uelewa, waelimishwe tu wataelewa umuhimu wa kufutwa fao hili na kuwataka wahusika wajibidiishe kutafuta kazi ingine. Mtu wa miaka 25 anataka mafao ya uzeeni ya nini wakati bado ana miaka 35 ya taabu huko mbele? Si atavute kazi ingine?

La pili of course ni siasa. Kuna vinara wa UKAWA humu ndani - wako tayari kufanya chochote ili tu amani ivurugike.
Toto kakojoe ulale kesho shule.Maana hujajua wakubwa zako wanatetea nini
 
Tafiti zinaonyesha wengi wa waliojitoa walipata kati ya Tshs 400'000-1'000'000. Je hizi zinatosha kuanza Biashara?
Au kuna Siasa ndani yake?
Kama kwako ni kidogo kwa mwenzio huo ni mtaji tosha kwa biashara ya genge la matunda na mboga za majani.acha kashfa kijana.
 
Tafiti zinaonyesha wengi wa waliojitoa walipata kati ya Tshs 400'000-1'000'000. Je hizi zinatosha kuanza Biashara?
Au kuna Siasa ndani yake?
Anegeziacha hadi afikishe miaka 60 angepata nini? Thamani yake kwa wakati huo ingekuwaje?
 
Wanaotunga sheria hizo hawaguswi na makali ya msumeno hivyo hawawezi kuwajali wafanyakazi.

Mfumo ndio tatizo kuu!
 
Back
Top Bottom