karama kaila
Senior Member
- Jan 30, 2015
- 122
- 60
Ndugu Waandishi wa Habari
Tunawashukuru kwa mwitikio wenu wa kukutana nasi hapa leo ni matumaini yetu makubwa kuwa mtatufikishia kwa umma ujumbe tunaokusudia uwafikie
Kikubwa tulichodhamiria mtusaidie kufikisha kwa umma ni mustakabali wa Taifa letu na mwelekeo wake kwa siku zijazo hasa katika nyanja ya elimu, sisi ngome ya vijana ya chama cha ACT-Wazalendo tunajukumu la kuangalia maslahi yanayowagusa vijana wa leo na kesho, katika sehemu kubwa ambayo inaweza ikaamua hatma yetu
Ndugu waandishi wa Habari
Kama mnavyofahamu na kuamini kuwa Elimu ni uti wa mgongo wa maendeleo ambayo serikali inapaswa kuwekeza kwa kiasi cha kutosha ili vijana wanaotoka katika familia za kimaskini nao waweze kujikwamua kupitia elimu bora isiyo na vikwazo
Sisi vijana wa ACT Wazalendo tunaamini kuwa bila kuwekeza kikamilifu katika na kuhakikisha watu wengi wanapata elimu bora basi mipango mingi ya kimaendeleo haitaweza kufanikiwa
Ndugu Waandishi wa Habari
Nyie ni mashahidi wa matukio kadha wa kadha yaliyoweza kutokea katika taifa letu na mabadiliko mbali mbali yanayogusa sekta ya Elimu, Tumeona baadhi ya makundi yamejitokeza kukosoa na machache kuunga mkono mabadiliko hayo. Na kwa nafasi yetu sisi vijana wa Ngome ya ACT-Wazalendo tunajitokeza hadharani kutoa maoni yetu na matakwa yetu juu ya mustakabali wa vijana wa Tanzania kama ifuatavyo;
Kufahamu hatma ya Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kozi maalum ya Stashahada ya Elimu....Ndugu Waandishi wa Habari sote kwa pamoja tumefuatili mchakato mzima wa kuanzishwa kwa kozi hiyo maalum ya ualimu wa masomo ya Sayansi baada ya taifa kukumbwa na uhaba mkubwa wa walimu wa masomo hayo.
Madhumuni ya kuanzishwa kwa Kozi hiyo ilikuwa na nia njema na serikali chini ya serikali ya awamu ya nne hatua iliyofuata taratibu zote zilizotakikana kufuatwa na kushirikisha wadau mbalimbali wa Elimu ikiwepo wizara ya Elimu yenyewe, TCU, NACTE, WOLRD BANK, Watalaam wa Elimu, na baadhi ya Vyuo vilivyokubali kupokea vijana hao.
Baada ya kuingia awamu hii ya tano tumeona ikiwafukuzia mbali vijana hao wa UDOM bila kuangalia athari za maamuzi hayo kwa taifa, kama yanatoa faida au hasara?
Ndugu Waandishi wa Habari
Katikakti ya uamuzi huo wa kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM kukaibuliwa lugha za udhalilishaji zikiwalenga vijana hao wazalendo kwa kuitwa VILAZA bila kuangalia athari za kisaikolojia kwao, Sisi kwa nafasi yetu ya vijana tunalaani vikali udhalilishaji huo mbali ya kulaani tunaitaka serikali ituambie na kutujibu juu ya masuala haya
• Ukweli juu ya sakata hilo la wanafunzi wa kozi maalum UDOM, Je ni kweli tatizo lilikuwa udahili haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha baada ya wafadhili kujitoa kama tunavyosikia?
•Tunataka uwazi juu ya mchakato wa kuwapata hao 300 na zaidi waliokidhi vigezo vya kurudi chuo na tufahamu hawa 7000 na zaidi waliokosa sifa kwa matokeo yao kuwekwa hadharani, ili kuondoa sintofahamu
•Vijana hawa wanadaiwa kukosa sifa ya elimu maalum pale UDOM waliandaliwa kwa ajili ya kozi hiyo maalum sasa serikali imewapeleka katika vyuo vingine je wanaenda kuendelea na elimu waliyoianza awali au watakuwa na mwanzo mwingine
MATABAKA YANAINYEMELEA TAIFA LETU.
Ndugu Waandishi wa Habari
Serikali imekuwa ikitumia nguvu kubwa kwenye kupanga ada elekezi kwa shule binafsi badala ya kutumia nguvu kubwa katika uboreshaji wa shule za umma, ambapo ndo watoto wengi wanasoma huko na wakiwemo watoto wengi wa masikini.
Tungependa kuishauri serikali endapo shule za umma zikiboreshwa hakuna mzazi atakayepeleka mtoto wake shule binafsi na uboreshaji huo uanzie kwenye taaluma (Content) hapa tunazungumzia Walimu na utoaji mzima wa maarifa pamoja na vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji. Suala hili likiwekwa sawa litafutiliambali utabaka mkubwa uliojitokeza katika taifa letu kati ya watoto wa walionacho na wasionacho.
Tunamtaka Rais Magufuli kama ana nia ya dhati ya kuboresha elimu katika shule zetu atoe agizo sasa kwa watumishi wa umma na viongozi wote wa kisiasa ambao ni wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, na mawaziri kuwa ni lazima watoto wao wasome shule za umma.
Agizo hilo litakuwa mwanzo wa mwarobaini wa uboreshaji wa shule za umma. Tunasema haya kwa sababu hawa ndio wadau wakuu wanaopanga na kuzisimamia sera za Elimu kwa hiyo watoto wao wakisoma shule za umma watatunga sera nzuri na kuzisimamia vizuri kwa sababu zinaenda kugusa vizazi vyao, uamuzi wa aina hii utafanya elimu yetu kuwa moja na yenye usawa kwa wote.
KUPANDISHWA KWA ALAMA YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU
Ndugu waandishi wa Habari
Kupandishwa kwa alama za ufaulu wa kujiunga vyuo vikuu, tunaamin ni kutengeneza kwa matabaka kati ya walionacho na wasionacho na hapa tunaomba mtuelewe vizuri kwa sababu zifuatazo;
•Sisi sote tunafahamu fika shule zinazoongoza kwa kufaulisha na kutoa viwango vya juu vya ufaulu ni shule binafsi kwa 80% na shule za umma wanaobahatika kufaulu ni 20%. Kupandishwa kwa viwango hivyo vya ufaulu ni sawa na kuwaambia watoto wa shule binafsi ambao wengi ni watoto wa wenye nacho kuwa ruksa kupata elimu ya chuo kikuu na watoto St.Kayumba kupotelea mitaani na kukosa fursa ya kupata Elimu ya chuo kikuu.
Kwa hiyo hili lisipoangaliwa kwa jicho la tatu litakuja kutuumiza na kuhatarisha amani yetu huko mbeleni kwa sababu watoto watakaokuwa na Elimu nzuri, kazi nzuri watakuwa ni watoto wa wenye nacho waliosoma shule nzuri na wachache sana kutoka shule za umma. Tuikumbushe tu serikali na umma kwa ujumla “Kupandishwa kwa viwango vya ufaulu sikupatikana kwa Elimu bora bali Elimu bora ni maarifa yenye tija yatolewayo kwa mwanafunzi”
Ndugu Waandishi wa Habari
Inasikitisha sana nchi yetu ni miongoni mwa mataifa 3 Afrika na Duniani kuwa na watu wenye elimu ya juu kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza ambapo ni 2.4% ya watanzania. Leo ndio wa kwanza kupunguza goli la watu kujiunga na Elimu ya chuo kikuu kwa kigezo Eti ! wanaboresha Elimu
Hitimisho
Ndugu waandishi waandishi wa habari,
Tunaomba ushirikiano wenu na umma kwa ujumla ilikupambana na kuinua Elimu yetu na kuondoa kasoro mbali mbali na kuwadhibiti mawaziri na kukomesha kasumba yao ya kila waziri wa elimu anayekuja kuvuruga Elimu yetu aidha kwa makusudi au kwa kutafuta ujiko pia kuisukuma serikali kuunda chombo huru kitakacho simamia Mfumo wa Elimu ambacho kitaundwa kisheria kwa kuhusisha wadau wote wa Elimu.
Chombo hicho ndio kitakuwa kinapokea na kupitisha mapendekezo yoyote yale ya Mabadiliko ya Mfumo wa Elimu yetu.
Pia tutatembelea taasisi mbalimbali za vijana za kivyama na za kijamii ilikuzungumza nao watuunge mkono juu ya kuishinikiza serikali kuunda tume huru ya wataalamu ya kusimamia Elimu na kuunga mkono mapendekezo yetu kama yalivyokuwa kwenye ilani ya uchaguzi.
Imetolewa leo Agosti 3
Ndugu Kitentya Luth
..................................
Mratibu Elimu Ngome ya Vijana Taifa.