Tamko la NEC ya CCM juu ya kupanda kwa gharama za maisha nchini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la NEC ya CCM juu ya kupanda kwa gharama za maisha nchini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, May 17, 2012.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,088
  Likes Received: 2,220
  Trophy Points: 280
  Posted by dosama | May 15, 2012

  TAMKO LA NEC JUU YA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA NCHINI.

  Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imejadili kwa kina suala la kupanda kwa gharama za maisha nchini. NEC inakiri kwamba ni kweli lipo tatizo la kupanda kwa gharama za maisha nchini. Tatizo hili pia limezikumba karibu nchi nyingi za Afrika Mashariki na kwakweli karibu sasa lipo dunia nzima. Baadhi ya sababu za kupanda kwa gharama za maisha hapa nchini ni pamoja na;

  1. Hali mbaya ya mavuno inayotokana na uhaba wa mvua au mvua kunyesha kipindi cha nje ya msimu katika maeneo mengi nchini.

  2. Kuongezeka kwa bei ya mafuta duniani, hivyo kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wa bidhaa na usafirishaji wa mazao.

  3. Kuyumba kwa thamani ya dola ya Marekani.*

  4. Kuwepo kwa soko huria ambapo sasa *mazao ya chakula yanapata soko nje ya nchi, na wakati mwingine kuuzwa nje kwa njia ya magendo na hivyo kusababisha uwepo wa ukubwa wa mahitaji na hivyo kuongezeka kwa bei ya chakula nchini.*

  5. kuongezeka kwa walaji wakati uzalishaji ukiwa mdogo.

  6. kutofanikiwa (ikiwemo kuhujumiwa na wafanyabiashara wasio waaminifu) kwa baadhi ya mikakati ya kudhibiti mfumko wa bei.

  Uwamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

  1. Pamoja na Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na wa kati za kukabiliana na tatizo hili, CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka za muda mfupi ikiwemo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na kodi ya ongezeko la thamani VAT katika sukari.

  2. Utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea upanuliwe ili kunufaisha wakulima wengi.

  3. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kwa kupitia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa, ikiwa ni pamoja na kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula katika maeneo ya uzalishaji wa mazao, na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo. Pamoja na hili, mipango ifanywe kuongeza uwezo wa wakulima kuhifadhi chakula chao wenyewe na kupunguza upotevu baada ya mavuno (post-harvest losses).*

  3. Serikali iendelee kupanua utaratibu wake wa kutumia Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (SGR) kama nyenzo ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula. Wakati wa uhaba wa vyakula katika maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji wa chakula utumike ili walaji, na sio wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike.

  4. Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kilimo nchini, hasa ASDP na SAGCOT, ambayo itasaidia kumaliza tatizo la chakula nchini na kuongeza ajira na kipato kwa Watanzania walio wengi.

  5. Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa dola za kimarekani. Aidha, Serikali iongeze udhibiti wa Maduka na mahoteli yanayofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii.*

  6. Waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha.

  7. Serikali iweke jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri.

  Nape Moses Nnauye Chama Cha Mapinduzi Ideology and Publicity Secretary
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Upumbavu, narudia tena Upumbavu, chama gani hiki tapeli?.
  .
  "HERI KIJANA MASKINI MWENYE HEKIMA, KULIKO RAIS MPUMBAVU ASIYE NA AKILI".
   
 3. k

  kaka miye Senior Member

  #3
  May 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 157
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo ndo ccm ya jk
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hv ccm huwa wanapigiwa kura na nan maana kila kwenye kusanyiko hakuna anayeishabikia ccm!
   
 5. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wanauzunguka mbuyu kwani serikali ni ya nani jamani? Kwanini wasiwauzie wananchi hayo mahidi hizo kampuni wanazoipa tenda si bi epa nyingine
   
 6. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wanajifanya hawajui kuwa hata mlo mmja umekuwa tabu kwa mtanzania wa kawaida,ambaye anashinda amevaa t-shirt ya chagua kikwete.Si kwa kuipenda hana nguo ya kubadilisha.
   
 7. frema120

  frema120 JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 5,103
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  tamko! kumbe mi ccm nayo yana Tamko....
   
 8. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mengi ni matokeo ya utendaji mbovu wa serikali yetu inayoongozwa na CCM.
  Huwezi ukachukulia failure yako na kusema nchi nyingi imetokea.
  Nishati ya umeme na mfumo wa usafirishaji mbovu umesababisha uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa kuwa mgumu. Upande wa kilimo ukame sio ishu, kuna nchi kama israel mvua kuiona shida lakini wanalima kama mchwa hivyo ni mipango mibovu ya serikali yetu ya CCM. Nyinyi mumekalia kujaza matumbo yenu tu
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kuamini kuwa tamko kama hili linaweza kutolewa na chama kinachounda serikali na ambacho kimeng'ang'ania madarakani kwa miaka nenda rudi! NEC ya CCM inatoa tamko hili la kisanii ili iweje? Kama huku si kuonesha dharau kubwa kwa wananchi ni kitu gani! Hata hivyo faraja pekee analoweza kubaki nalo mwananchi ni kuwa siku za genge hili la wezi na wapuuzi kubaki madarakani zinazidi kuyoyoma.
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,956
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Eti tunaongozwa na rais mchumi! Kama wachumi ndo performance zao ziko hivi, mi basi tena. Afadhali walimu na makanjanja.
   
 11. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  What about Dutch Desease!. Hivi CCM inawasomi kweli??. du!!!. Mnahimiza soko huria na kuruhusu resources na ajira kuchukuliwa na wageni huku mkiwazuia wakulima kuuza mazao yao nje, are you crazy!!!!
   
 12. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Acha matusi toa mawazo mbadala, tukutane CCM hakuwezi kuwa sera mbadala wala hawezi kusifiwa kwa utalaamu aw uchumi kwa kuporomosha matusi.
   
Loading...