Tamko la NCCR Mageuzi kuhusu bajeti ya mwaka 2011/12

Dec 2, 2010
15
2
TAMKO LA NCCR MAGEUZI KUHUSU BAJETI YA MWAKA 2011/12
2011-06-12
BUNGENI DODOMA

1.0 UTANGULIZI
Tunawashukuru wanahabari kwa kuja kupokea maoni yetu na kuwafikishia watanzania kuhusu maoni yetu wabunge wa NCCR Mageuzi kuhusu hali ya uchumi na mwelekeo wa Bajeti ya 2011/2012. Tukiwa tunakwenda kujadili Mkakati wa Uchumi wa miaka mitano kuanzia Jumatatu na hatimaye Bajeti ya 2011/2012, tungependa kutoa maoni yafuatayo kuhusu mwelekeo mzima wa bajeti hii ambayo itakuwa ya kwanza kuelekea nusu karne ya Uhuru wa Taifa letu miezi michache.

2.0 KUHUSU UKUAJI WA UCHUMI NA MAENDELEO YA UCHUMI
Msimamo wa NCCR Mageuzi ni kwamba tatizo la Tanzania sio ukuaji wa uchumi(Economic Growth), ni Maendeleo ya uchumi(Economic Development). Ukuaji wa uchumi unapimwa kwa kiwango cha uzalishaji ndani ya nchi, Maendeleo ya uchumi yanapimwa kwa kiwango cha namna mapato hayo ya nchi yanavyotumika kuboresha maisha ya binadamu ndani ya Taifa.

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania wa asilimia 7 mpaka sasa ni ukuaji wa juu sana kwani mpaka sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 zenye kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani lakini kwasababu ya udhaifu katika mfumo wa ukuaji wa uchumi ni Tanzania hiyohiyo imekuwa miongoni mwa nchi 20 masikini duniani.

Pia nidhamu ya ukuaji uchumi wetu bado ina walakini kutokana na serikali kushindwa kuhakikisha uimara wa sarafu yetu kuishindani na mfumko wa bei usio na tija katika uchumi mpana na wenye madhara katika uchumi mdogo na hivyo kusababisha kupanda kwa gharama za maisha kusikoendana na pato la mtanzania na hivyo kuibuka kwa jamii pana inayoshindwa kumudu gharama za maisha.

Ndio maana wakati serikali ya awamu ya nne ikiweka rekodi ya kupandisha mapato ya nchi kutoka 260 bn mwaka 2005 mpaka 470bn mwaka 2011 kama ongezeko la asilimia 80% ,ukweli huo sio ukuaji halisi wa makusanyo kwa mwezi bali ni matokeo ya udhaifu wa sarafu kiushindani. hii ni kwasababu mwaka 2005 wakati mapato ya ndani yakiwa 260bn thamani ya sarafu imara kama dola ilikuwa Tsh1000 kwa Dolla1. Na leo wakati mapato ni 470bn , dola1 ni sawa na Tsh1600. hivyo basi kwa Tafsiri ya dola, mapato yetu kwa mwezi yamepanda kutoka dola 260m mwaka 2005 mpaka dola 269m 2011 sawa na ongezeko la asilimia 13% na sio asilimia80%.

Ndio sababu hadi sasa, zaidi ya muongo mmoja sasa, ukuaji wa uchumi umeshindwa kutafsiri Maendeleo ya uchumi. Msingi wa tatizo hili kwanza; sekta za kilimo( kwa maana pana ya mazao, uvuvi na ufugaji) na biashara ndogondogo zinakuzwa kwa kasi ndogo sana ya asilimia 4 hali inayosababisha umasikini kuongezeka mwaka hadi mwaka. kufikia mwaka 2005 idadi ya fukara ilikuwa millioni 11, serikali ya CCM ikaahidi kupunguza umasikini kwa asilimia 50 na hivyo watanzania wakatarajia fukara wangepungua kutoka milioni 11 hadi milioni 5.5 lakini ukweli ni kwamba idadi ya masikini kufikia 2009 ilifikia 12.9milioni (Poverty and Human development report 2009).

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya REPOA umebainisha wazi kwamba kama sekta ya kilimo kwa maanapana itakuzwa kwa asilimia 10 kwa miaka 3 mfululizo tunaweza kupunguza umasikini wa kipato kwa asilimia 50. Mwenendo huu wa ukuaji wa sekta ya kilimo kwa maana pana kwa miaka zaidi ya 10 ni kielelezo kwamba mlinganyo wa kutafsiri ukuaji wauchumi kwenda maendeleo ya uchumi hauwezekani kwa sera za CCM.

3.0 KUHUSU DENI LA TAIFA, MISAADA NA MIKOPO
Mwenendo wa uchumi wetu umekabiliwa na deni kubwa kwa muda sasa, tulitegemea kwamba deni hili liende sambamba na kasi ya maendeleo. hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Economist kupitia kitabu cha The Pocket world in Figure 2011), tatizo sio deni, tatizo ni huo mkopo umetumikaje kujenga maendeleo ya uchumi. Inasikitisha Taifa lenye deni la zaidi ya dola 11billion bado tunazalisha 800MW za umeme.. Robo ya deni hili zingetosha kabisa kumaliza tatizo la umeme kwa kuzalisha 3000MW za umeme ambazo leo tunaweka mikakati ya kuzalisha ndani ya miaka mitano na haitawezekana.

NCCR Mageuzi tunaitaka serikali kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya mikopo ili ukubwa wa deni uweze kuendana na kiwango cha maendeleo.

Wataalamu wa uchumi duniani wanabainisha wazi kuwa sababu kuu mbili za umasikini kwa nchi za Afrika ni migogoro ya ndani ambayo misingi yake ni ukabili, ukanda, udini na uchu wa madaraka pamoja na ufisadi mambo ambayo kwa ujumla yanadhoofisha kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, tofauti na nchi zote Afrika, Tanzania bado ni nchi yenye isiyo na migogoro wa kidini, kikabila, kikanda lakini imeshindwa kuendelea hali inayothibitisha kuwa tatizo la msingi kwetu bado ni ufisadi unaochagizwa na mfumo mbovu wa kiutawala.

Ni aibu Waziri wa fedha kuendelea kulilia misaada kwa wahisani na kulalamika wanaposhindwa kutekeleza. Ifahamike wazi kwamba mpaka sasa Tanzania ni nchi ya saba duniani kwa kupata misaada mingi duniani ikiwa kundi moja na Iraq, Afghastanistan, Ethiopia, West Bank and Gaza, Vietnam na Sudan ( The Econimist 2011. Nchii zilizopo kundi moja na Tanzania kwa kupata misaada mingi nyingi ni kwasababu ya vita na hali mbaya kiusalama, ni aibu Tanzania kusaidiwa sawa na mataifa yenye hali tete kiusalama ilhali tukiwa Taifa salama.

4.0 KUHUSU VIPAUMBELE
Tunatambua kwamba msingi wa kupanga vipaumbele ni hoja ya kiuchumi kwamba hatuwezi kutekeleza kila kitu..ni kwa msingi huo tunapaswa kupanga vipaumbele kwa kuzingatia vile vitu ambavyo vikitekelezwa vinaweza kuleta mabadiliko chanya(impacts) katika maeneo mengi zaidi.

Kwa nchi masikini kama yetu,sekta yenye kuweza kuleta mabadiliko chanya katika maeneo mengi bado ni elimu. bado elimu lazima ibaki kuwa kipaumbele hasa kipindi hiki ambacho taifa linashuhudia anguko kubwa la elimu kupata kutokea. Tunaamini hatua ya kwanza ya kuleta maendeleo ni kuboresha rasilimali watu, tunaamini katika maendeleo ya watu kabla ya vitu, na hatua ya kwanza ya maendeleo ya mtu ni kuboresha uimara wake katika elimu.

Kipaumbele cha pili ni Nishati. Hii inachangia kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya uchumi. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na REPOA2010, imebainishwa wazi kuwa kama serikaliingeweza kuunganisha wateja laki 5 kwa miaka mitano itazalisha ajira zaidi ya milioni moja za moja kwa moja, Aidha Benki ya dunia inabainisha wazi kuwa Nishati ya umeme ndio nguzo kuu katika kusukuma uchumi kokote duniani na kwamba katika kukuza uchumi na maendeleo inachangia asilimia 40.hii ni kutokana na ukweli kuwa umeme; unachochea ukuaji wa sekta ya viwanda na hivyo biashara ambavyo kwa pamoja kukuza ajira na pato la mwananchi hivyo kupunguza umasikini wa kipato. hata ripoti ya Hali ya Umasikini na Maendeleo Tanzania 2009(poverty and Human Development Report) inabainisha kuwa mgawo wa umeme unasababisha hasara ya kati ya Tsh milioni 10 mpaka Tsh50 kwa mwaka kwa wafanyabiashara wa kawaida.

Waziri amedanganya kuhusu tatizo la umeme;

Waziri wa fedha ametangaza sana mwaka huu kama mwaka wa umeme kama kipaumbele kwa kutenga bajeti ya wizara nzima kuwa 530bn lakini ukifanya rejea za nyuma utabaini kuwa waziri amecheza siasa katika eneo hili kwani mwaka 2006/2007 ambapo bajeti ya maendeleo ilikuwa 1734526 millioni , sekta ya umeme peke yake ilitumia asilimia 24,mwaka 2007/2008 ambapo bajeti ya maendeleo ilikuwa 2,201,095 millioni sekta ya umeme ilitengewa asilimia 13.9..na hata mwaka 2008/2009 ambapo bajeti ya maendeleo ilikuwa 2491480 millioni, sekta ya umeme ilitengewa asilimia 12.6. Sasa kama katika miaka hiyo tatizo mgawo haukumalizika, kwanini waziri awadanganye watanzania kukabili mgawo wa umeme kwa kutenga bajeti nzima kuwa 530bn?..ingawa hakueleza kiasi gani ametenga kwa ajili ya umeme lakini bajeti nzima ya miradi ya maendeleo ni billioni trilioni 4.9 na kwa wizara nzima ya Nishati na Madini imetengwa 325bn sawa na asilimia 6.6 ya bajeti yote ya maendeleo. Huu ni ushahidi kwamba bajeti ya umeme 2011/2012 haijapewa uzito mkubwa ukilinganisha na miaka tajwa hapo juu.

Sio hayo, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na REPOA kwa kushirikiana na Taasisi ya Skills Gap International imeshauliwa wazi kwamba ili kufikia malengo ya millenia na MKUKUTA ambayo serikali inadai kutekeleza, pamoja na mambo mengine, mwaka 2011 TANESCO inapaswa kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani 687.2millioni kiasi ambacho ni zaidi ya 1000bn kwenye miradi mbalimbali ya umeme iliyobainishwa.

5.0 KUHUSU MATUMIZI YASIYO YA LAZIMA
NCCR Mageuzi tumekuwa tukisisitiza siku zote tatizo la mfumo wa kiutawala wa Taifa hili ambao unanyonya sehemu kubwa ya mapato ya Taifa hili ambayo yangeweza kupunguza makali ya umasikini. Waziri wa fedha amesema katika bajeti hii atapunguza matumizi mengi yasiyo ya lazima(haya huwa yanakuwa kwenye fungu la OC-other charges), kauli hii sio ya kweli ndio sababu waziri wa fedha ameshindwa kubainisha wazi serikali itaokoa kiasi gani cha fedha kwa kuondoa matumizi hayo yasiyo ya lazima, lakini zaidi fungu lenye matumizi hayo limeongezwa kutoka 2.8trilioni mwaka 2010/2011 hadi 3trilioni 2011/12.

Inasikitisha kwamba wakati bajeti ya maendeleo ni trilioni 4.9 sawa na asilimia 36% ya bajeti yote ya trilioni 13.5 lakini bado mchango wa fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni trilini 1.8 sawa na asilimia 13% ya bajeti yote. Hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi na ni kielelezo cha uduni wa kujitegemea

Kwakuwa moja ya tatizo ni sehemu kubwa ya mapato kutumika kushibisha mfumo mkubwa na dhaifu wa kiutawala pamoja na ufisadi , Wabunge wa NCCR Mageuzi Katika kusimamia hoja hii, tayari tumeandaa barua ambazo kesho jumatatu tutaziwasilisha kwa Waziri wa Fedha na Nakala kwa Spika tukimwomba fedha zote za posho za vikao kwa wabunge wa NCCR Mageuzi zipelekwe kwenye fungu(vote74) ambalo ni fungu la miradi ya maendeleo kwa mkoa wa Kigoma. na zaidi ya kupendekeza posho za vikao kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo pia tutapendekeza posho zote zikatwe kodi ili kuongeza mapato ya ndani katika miradi ya maendeleo.

Lakini pia tutaendelea kusisitiza mabadiliko ya mfumo wa utawala kwani katika eneo moja tu la kuondoa wakuu wa wilaya na makatibu tarafa nchini na tukabaki na uongozi wa halmashauri kusimamia majukumu yote ndani ya wialaya tungeweza kuokoa 51,350,221,000(zaidi ya 52bn) au zaidi ya 200bn ambazo zinatosha kununua mitambo mipya yenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya 200MW za umeme, hiki ni kiasi kikubwa ikizingatiwa kuwa katika miaka mitano iliyopita, serikali ilizalisha 160MW tu.

Mwisho tunapenda kusisitiza umuhimu wa serikali kudhibiti mapato katika sekta za uvuvi, utalii, wanyama pori na madini kwani haya ni maeneo ambayo bado serikali imeshindwa kuyatawala na tunapoteza kiasi kikubwa cha mapato ambayo yangeweza kupunguza kodi kwa bidhaa za masikini.
NCCR Mageuzi tumependa kutoa maoni haya ya jumla ya kimwelekeo na tunaahidi kuchangia kwa kina maeneo haya wakati wa mjadala Bungeni.

Tamko limesainiwa na;
David Kafulila(MB)
Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi.
0716 42 62 20
 
Kafanya vema lakini ni kama kwamba hamna solutions kwa kila kitu bali malalamiko, nini kifanyike kama bajeti inapanda kwa 13% tangu 2005, solution hamna ni malalamiko tu bado sana
 
Ukuaji wa uchumi wa Tanzania wa asilimia 7 mpaka sasa ni ukuaji wa juu sana kwani mpaka sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 zenye kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani lakini kwasababu ya udhaifu katika mfumo wa ukuaji wa uchumi ni Tanzania hiyohiyo imekuwa miongoni mwa nchi 20 masikini duniani.

Ni aibu na fedheha...

kufikia mwaka 2005 idadi ya fukara ilikuwa millioni 11, serikali ya CCM ikaahidi kupunguza umasikini kwa asilimia 50 na hivyo watanzania wakatarajia fukara wangepungua kutoka milioni 11 hadi milioni 5.5 lakini ukweli ni kwamba idadi ya masikini kufikia 2009 ilifikia 12.9milioni (Poverty and Human development report 2009).

Ni aibu na fedheha

Ni aibu Waziri wa fedha kuendelea kulilia misaada kwa wahisani na kulalamika wanaposhindwa kutekeleza. Ifahamike wazi kwamba mpaka sasa Tanzania ni nchi ya saba duniani kwa kupata misaada mingi duniani ikiwa kundi moja na Iraq, Afghastanistan, Ethiopia, West Bank and Gaza, Vietnam na Sudan ( The Econimist 2011. Nchii zilizopo kundi moja na Tanzania kwa kupata misaada mingi nyingi ni kwasababu ya vita na hali mbaya kiusalama, ni aibu Tanzania kusaidiwa sawa na mataifa yenye hali tete kiusalama ilhali tukiwa Taifa salama.

Ni aibu na fedheha....Tukianza kupigana itakuwaje???..

Mwisho tunapenda kusisitiza umuhimu wa serikali kudhibiti mapato katika sekta za uvuvi, utalii, wanyama pori na madini kwani haya ni maeneo ambayo bado serikali imeshindwa kuyatawala na tunapoteza kiasi kikubwa cha mapato ambayo yangeweza kupunguza kodi kwa bidhaa za masikini.
NCCR Mageuzi tumependa kutoa maoni haya ya jumla ya kimwelekeo na tunaahidi kuchangia kwa kina maeneo haya wakati wa mjadala Bungeni.

Nafikiri kama wabunge inabidi kuipigia serikali kelele kuhusiana na Udhibiti wa Mapato pamoja na Matumizi mabovu. Wakati chama kama cdm wakipigania serikali kubuni mbinu za vyanzo vya maendeleo ya uchumi, na vyema na nyie mkaungana na Watanzania kuifanya serikali ibane matumizi...

Gap kati ya maskini ni tajiri ni kubwa sana kwa sasa
 
Ingekua vema na jamaa magamba wakatoa tathmini yao!!ingependeza zaidi...
 
Ingekua vema na jamaa magamba wakatoa tathmini yao!!ingependeza zaidi...
Magamba wameshasema, piga ua posho watachukua. Si tunajua hawa magamba wengi zile khanga na pilau ziliwacost, lazima wachukue hizo posho wakalipe madeni.

Big up NCCR, wabunge wote wa upinzani susieni hizo posho ili mkawashitaki vizuri wabunge wenye magamba kwa wananchi, mkianzia na spika wao.
 
Kafanya vema lakini ni kama kwamba hamna solutions kwa kila kitu bali malalamiko, nini kifanyike kama bajeti inapanda kwa 13% tangu 2005, solution hamna ni malalamiko tu bado sana

Nilitamani angetoa solution au msimamo wao kwa kila kipengele kama alivyofanya kwenye posho. Mengi naona kama alikuwa anachangia kama tulivyozoea kuwaona wabunge wa CCM. "Naungu mkono mia kwa mia lakini ....... !!
 
Kafanya vema lakini ni kama kwamba hamna solutions kwa kila kitu bali malalamiko, nini kifanyike kama bajeti inapanda kwa 13% tangu 2005, solution hamna ni malalamiko tu bado sana

Nadhani hujaisoma barua vizuri wamependekeza masuala mbali kwa njia ya kukusoa. Nakusisitiza isome vizuri hiyo barua. Labda nikupatie dondoo tu:-
a. Bajeti hii haina lengo la kumsaidia maskini bali ina lengo la kumkandamiza mlalahoi soma hapa anasema hivi nanukuu:

Ndio sababu hadi sasa, zaidi ya muongo mmoja sasa, ukuaji wa uchumi umeshindwa kutafsiri Maendeleo ya uchumi. Msingi wa tatizo hili kwanza; sekta za kilimo( kwa maana pana ya mazao, uvuvi na ufugaji) na biashara ndogondogo zinakuzwa kwa kasi ndogo sana ya asilimia 4 hali inayosababisha umasikini kuongezeka mwaka hadi mwaka. kufikia mwaka 2005 idadi ya fukara ilikuwa millioni 11, serikali ya CCM ikaahidi kupunguza umasikini kwa asilimia 50 na hivyo watanzania wakatarajia fukara wangepungua kutoka milioni 11 hadi milioni 5.5 lakini ukweli ni kwamba idadi ya masikini kufikia 2009 ilifikia 12.9milioni (Poverty and Human development report 2009).

Pia amezungumzia suala la deni la taifa na kupendekeza kuwa kukopa ndio tukope ila sio kuendesha serikali bali ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo namnukuu:-

NCCR Mageuzi tunaitaka serikali kuhakikisha nidhamu ya matumizi ya mikopo ili ukubwa wa deni uweze kuendana na kiwango cha maendeleo.

Pia kuhusu umeme wamelizungumzia nanukuu:

mwaka 2011 TANESCO inapaswa kuwekeza kiasi cha dola za kimarekani 687.2millioni kiasi ambacho ni zaidi ya 1000bn kwenye miradi mbalimbali ya umeme iliyobainishwa.

Sio kila kitu mnacriticise au kwa vile hakijatoka kwenye mdomo wa chama cha chadema tuwe na moyo wa uzalendo saa zengine. CCM mwaka 2015 nawaonea huruma chakula kitawakaa kooni maana wamejisahau sana..
 
Back
Top Bottom