Tamko la MUWAZA – Udhalilishaji wanaofanyiwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la MUWAZA – Udhalilishaji wanaofanyiwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Apr 26, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by administrator // 26/04/2012 // Habari // 1 Comment


  23/04/2012
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
  Ikulu
  Zanzibar
  YAH: UDHALILISHAJI WANAOFANYIWA WANANCHI KWA KISINGIZIO CHA KUULINDA MUUNGANO
  Kwa heshima tafadhali husika na mada ya hapo juu.
  Itakumbukwa hivi karibuni kumeanzishwa Tume ya kuratibu maoni juu ya katiba mpya ambayo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano ambayo inatarajiwa kufanya kazi zake wakati wowote kuanzia sasa. Kwa upande wa Zanzibar, wapo Wananchi wengi ambao wanaonelea kuwa kwanza ifanyike kura ya maoni kwa kuulizwa kama wanautaka au hawautaki huo unaoitwa eti Muungano na ikiwa kama watakubaliana na hilo ndio ufanyike huo mchakato wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya.
  Hakuna asiyejuwa ukiwemo na wewe kuwa huo unaoitwa Muungano umeanzishwa kimabavu na Madikteta wawili ambao ni Karume na Nyerere bila ya ridhaa za Wananchi wa pande mbili yaani Tanganyika na Zanzibar na kusababisha kuipora Zanzibar kila kilicho chake kutoka Uraia, Uchumi, Siasa … n.k.
  Hivi karibuni tumeshuhudia udhalilishaji mkubwa unaofanywa ma Jeshi la Polisi kwa vikundi mbali mbali ambavyo vimeonesha hisia zao za kupinga UKOLONI WA KITANGANYIKA katika ardhi za Zanzibar kwa kisingizio cha kuwa eti wanaupinga huo unaoitwa Muungano.
  MUWAZA inasikitishwa zaidi kuona kuna baadhi ya Viongozi wetu wa juu katika Serikali wakitowa kauli za vitisho kwa Viongozi wa dini na vikundi mbali mbali vinavyo vinawaelimisha Wananchi udhalimu wa huo unaoitwa eti Muungano ambayo ni haki yao kufanya hivyo maana huo unaoitwa Muungano haukutoka mbiguni kwa Mwenyezi Mungu ila umeanzishwa kwa mabavu na watu wawili waliojifungia kwa siri bila ya ridhaa ya Wananchi wa pande mbili ya Tanganyika na Zanzibar ambao tokea awali umeonesha kuwa hauna nia njema wala maslahi ya Wananchi ila una maslahi kwa Viongozi wachache waliopo madarakani.
  Kutokana na hayo, Jumuiya ya MUWAZA inakuomba kuliingilia kati suala hili haraka kwa kuwaadhibu Viongozi wako wanaotowa kauli za vitisho kwa Wananchi wa Zanzibar ili tusiweze kuridishwa huko tulikotoka ambapo hatupataki kurudi. Pia, MUWAZA inakuomba kuwa Wananchi wote waliokamatwa kwenye Viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuonesha hisia zao juu ya huo Muungano wafutiwe kesi zao mara moja kwani tunaamini walilolifanya ni haki yao ya kupinga kitu ambacho kinawadhalilisha kwa miaka mingi.
  MUWAZA inatarajia barua hii utaipa mashirikiano makubwa
  Tunakutakia kila la kheri
  KATIBU
  Jumuiya ya MUWAZA
  UK
  Nakala: Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – UK
  Balozi wa Kenya – UK
  Balozi wa Rwanda – UK
  Balozi wa Uganda – UK
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  what is muwaza?
   
 3. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  muislamu wa zanziba
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Kazi kweli kweli.
  Lakin kumbuka Zanzibar ni 99.5% wa dini hiyo.
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Acha upotoshaji wewe,
   
Loading...