Tamko la maimamu kuhusu kuuliwa kwa imam na polisi

Happy nation

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
679
591
Nimesikiliza kwa makini na sipati jibu,hivi kama mtu anavamia atm na kila atm kuna camera kwa nini wasitoe picha?

Majambazi wengi wanauliwa kati yao wako waislamu na wakristo ni kwanini mashekhe hawa wote waseme huyu hakuwa jambazi?

Hatujawahi kusikia maimamu wakilalamika kuhusu hao wengine,
Unajua amani tuliokuwa nayo siyo ya polisi ni ya watanzania wote,tunasikia mashehe wanalalamika wenzao wako magereza bila ushahidi miaka zaidi ya tatu,tuna nyamaza.

Leo wanasema mwenzao kauliwa tunanyamaza ,wanalalamika vijana rufiji wakituhumiwa tu basi wanauliwa,hivi kazi ya mahakama ni nini?Tukiacha huu upuuzi uendelee na huku Tunataka amani haitaenda,lazima serikali iunde tume kuchunguza madai yao,mwisho wa kuuwa bila kufuata sheria siyo mzuri,

Naamini kabisa serikali inaweza kutatua manung'uniko yao kabla hali haija mbaya,hatuwezi tukawa tunasema kuna amani kama askari au vyombo tulivyoviamini vitulinde ndiyo ihatarishe maisha yetu na kutunga uwongo wakikosea,tizama ya nape aliomtolea silaha hajachukuliwa hatua,malima askari kapiga risasi kizembe kwa kutumia mkono moja na malima ndiyo kashitakiwa,amani inaenda sambamba na haki watu wakikosa haki amani hupotea.
 
Jambazi gani hajakamatwa na silaha yeyote ile hata manati hakuwa nayo ?

Jambazi alikuwa anatembea zake kawapa mgongo kaitwa hajasikia kamiminiwa risasi wakati alikuwa kawapa mgongo hivyo hapakuwepo na threat yeyote ile ?

Kwanini wasingempiga mguuni mtu ambaye kakupa mgongo anatembea hana threat kwako wewe ?.

Kiukweli maswali yapo mengi sana
 
Hakika polisi wajiangalie maana wanakuwa kama wanalipizak isasi kwa watu wasio na hatia kutokana na kuuliwa wale askari nane kibiti operesheni haiendi hivo mnatakiwa mjiongeze katika kutafuta ukweli na kuwabaini wahusika sio kila mtu mnaingiza mambo ya dini katika operation zenu mtaleta machafuko nchini nawaambia fanyeni kazi zenu kwa mujibu wa sheria na weledi sio kuuwa uwa ovyo
 
Hatari kubwa sana ni pale tunapoanza kuzoea taratibu hali hii....lakin pia kale kadhana ka kuona baadhi ya watu/jamii ni second class citizen...hili jambo gharama yake ni kubwa sana hasa pale hawa walalamikaji watakapozifikia kingo za uvumilivu.

Rai yangu....watu wote wenye nia njema tukatae hali hii kwa faida ya taifa zima. Tusikubali maelezo mepesi pale vyombo vya dola vinapopindukia mipaka.
Tukatae si kwa sababu ya dini zetu wala makabila yetu....tukatae kwa sababu utaifa wetu...kwa sababu ya amani yetu...lakin above all...tukatae kwa sababu ya utu wetu....tukatae maovu!
 
Nafikiri maneno yao yamenyooka na kueleweka na kila mwenye akili timamu. Hoja hujibiwa na hoja na sio vitisho. Maimamu wana hoja.
 
Hii kaZi ya Magwanda Bora mtu akawa Jobless kuliko kuvaa gwanda kwaajili ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia lakini ipo siku ya Malipo bila Shaka itakuja!!!
 
Mtoa mada uko sahihi sana,
polisi ndio mnavunja na mtakaovunja amani hapa nchini,huku jaribu na bungu mmeua watu zaidi ya 4,na yule mliempiga risasi palea mwanambaya mkuranga,akiwa na bodaboda yake aliwakosea nini?
Tunavyoandika humu kuna mipumbavu inaona kama tunawasakama polisi,lakini mngekua mnakaa kibiti,bungu au jaribu nadhani mngeelewa,
acheni mambo hayo,dunia tunapita tu.
 
Back
Top Bottom