Tamko la madaktari bingwa MNH, MUHAS na ORCI

Binafsi siafiki kupelekwa nje,labda wakaombe ufadhili katika balozi za nje ili wao ndo wampeleke and in that way it will bw easier kwa hao jamaa kumlinda akiwa huko nje. Hawa Wao-M ni hatari sana wanaweza kumfatilia hukohuko nje.

Naomba mgomo uwe MKUBWA SANA mpaka tuone hawa akina Pinda na wenzake viburi vyao vinaishia wapi.

Eti wagonjwa wapelekwe Lugalo?Hivi hiyo Lugalo ina madaktari wangapi?
 
Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii? Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.

TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi.. Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika. Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.

Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa. Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi, kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu. TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..

Naunga mkono hoja
 
Maandamano hayana Tija....wasomi kuweki makini na mambo mnayoyafanya

maandamano ni haki yangu ya kikatiba,wewe kula zako posho,ukiugua katibiwe nje kwa raha zako,tumia pesa za kodi yetu wakati ni wako,ila kumbuka 2015 si mbali (hata kabla ya hapo,lolote la weza tokea).mimi mwenye dhiki nipatae mateso na manyaso ndani ya nchi yangu niache nikadai haki yangt,kwan haki aiombwi bali udaiwa,ntadai haki popote pale,na nipotayari kufa huku nikiwa nadai haki yangu
 
Naunga mkono wagome nchi nzima kabisa.
Sawa unaunga mkono lakini mbona wanamtibu Ulimboka? Kama wamegoma sii wagome hata kumtibu Ulimboka kwani yeye sii Mtanzania mlipa kodi aliyelazwa kama wale wagonjwa wengineo!
Unapogoma unagoma hata kumtibu mzazi wako sio kuchagua!
 
please please please tusiishie kwenye keyboard tu wadau! mimi naiamini JF na naamini kuna watu makini sana humu ndani! naomba kama wewe ni mwandishi wa habari, kama ni polisi, kama ni mbunge, waziri, mkulima, mfanyabiashara, kama ni mama wa nyumbani, baba, kijana,mzee, au mwajiriwa wa serikalini, usalama wa taifa, mfanyabiashara n.k n.k n.k..popote pale ulipo kama ww ni mTanzania kweli, kama ni mzalendo na umeguswa na hili suala la mgogoro wa serikali na madaktari naomba uchangie matibabu ya Dr Ulimboka, na uchangie kwa namna yoyote ile kulingana na uwezo na nafasi yako, kuhakikisha kuwa tunawashinda WADHALIMU, TUNAWASHINDA WAHUNI WANAOIJIITA VIONGOZI WETU.

Natoa pongezi zangu za dhati kwa madaktari wote nchini kwa busara, mshikamano na moyo wa kizalendo waliouonyesha tokea mwanzo wa mgogoro huu, hadi sasa hivi.

MUNGU IBARIKI JAMII FORUM, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU MBARIKI Dr. ULIMBOKA!

SOLIDARITY FOREVER!
 
Damu ya mtu haimwagiki bure, wao walijua tutaokota maiti lakn sisi tukamwokota Doctor yuko mahututi!
 
Madaktari wanatakiwa wajitahidi sana kuwasilisha vilio vyao kwenye vyombo vya kimataifa mfano UN, Amnesty International, ICC n.k tena haraka, vinginevyo wataokotwa wengi kwenye msitu wa Mabwepande.

siyo madokta tu hata sisi raia ambao tumechoshwa na mkoloni mweusi ccm.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Ni msimu wa maumivu kweli kweli dhidi ya sisi raia tusio na hatia!
Watanzania tupo tofauti sana;ingekuwa nchi nyingine,uzembe wa serikali kushughulikia madai ya madaktari ungetosha kutufanya tuingie mtaani na kudai serikali hii iondoke madarakani!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Sasa wakigoma kutoa huduma za afya huyo doctor aliyepigwa atatibiwaje au yeye ni exceptional case
 
Ninahofia akipelekwa nje watammalizia hukohuko.

hata mim nahsi hvyo. Abaki hapohapo. Hata kati ya hao madaktari kuna mashushushu wa usalama wa taifa. Wanaweza kutoa proposal wamtoe hapo kwenye ulinzi mkali wa madaktari wenzake ili wampeleke huko iwe rahisi kummaliza.
Kwanza amepata tatizo gan ambalo halitibiki had wampeleke nje? #Madaktari au wenye ujuzi jibuni plz.
 
Kwa kuwa CCM na serikali yake wamezidisha propaganda dhidi ya kitendo cha madakatari tunaomba mtuwekee hapa madai oroginala ya madakatari ili tuweze kuwakumbusha wananchi wote kama njia mojawapo ya kushinda hizo propaganda
 
Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii?

Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.

TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi..

Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika.

Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.

Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa.

Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi, kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu.

TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..

Si wananchi ndo mloichagua CCM! tulieni.
 
Hapa ndipo nashindwa kuelewa huwa tunafikiri kwa kutumia kiungo gani!!!!!!!!!! Hivi wote tunaochangia kuhusu mgomo wa madaktari tunazijua hoja za madaktari kugoma?????????

Tumezifanyia upembuzi yakinifu au tunachangia tu kwa mkumbo? Naomba kila anayechangia afuatilie kwanza jinsi madaktari wanavyolipwa ukilinganisha na kada nyingine katika utumishi wa umma halafu ndipo uje uchangie kwa upya. Kuhusu vifaa, ni sawa wana haki ya kulalamika na kudai vifaa ili waweze kutoa huduma vizuri; na nia yake ni ili kupunguza vifo vya watanzania. Hebu jiulize wakati wakiwa kazini na vifaa hivyo vilivyopo bado watu walikufa, sasa wamegoma, maana yake madaktari na vifaa angalau hivyo vilivyopo vyote havipo, je unategemea nini?

Maana daktari angekuwepo hata kwa vifaa duni vingeweza kusaidia wale ambao wangeweza kusaidika na vifaa hivyo. Je sasa lengo lao la kutoa huduma nzuri au kupunguza vifo sasa linafanikiwa au kwa kuendeleza mvutano wao na Serikali ndio wananchi wasio na hatia wanaendelea kuteseka na kufa zaidi? Tusishabikie tu kwa sababu tuna uwanja wa ushabiki. Leo hii ukiondoka ukifika nyumbani ukakuta mkeo/mumeo/mwanao/mzazi wako au ndugu yako yuko hoi utaona mgomo wa madaktari ni wa maana sana kwa upande wako? Utaenda kuandamana au kutafuta jinsi utakavyookoa mgonjwa wako.

Mimi sina ugomvi sana na wao kudai wanachodai lakini wasiadhibu wananchi ambao hawana hatia na kila siku tunalipa kodi tena katika mazingira haya magumu. Jamani hatuhitaji kuongezewa ugumu wa maisha tulio nayo bali tupate angalau kiahueni fulani katika maisha haya. Mgomo ambao mimi ningeuunga mkono ni kuwagomea kuwatibu hao wakubwa na familia zao na hata kutowarefer huko nje, ili sote tuone uchungu n.k.
 

Tamko la Madaktari Bingwa wa mkoa wa Dar es salaam
(MNH, MOI, Ocean Road na Hospitali za manispaa ya mkoa wa Dar es salaam)

Kutokana na kikao kilichofanyika leo tarehe 29/06/2012 madaktari bingwa tumeamua yafuatayo:

  • Tunalaani kwa kauli moja kitendo alichofanyiwa daktari na kiongozi wa jumuiya yetu dr stephan ulimboka cha kutekwa kuumizwa na kutupwa msitu wa mabwe pande kitendo hiki kimetuhuzunisha, kimetufadhaisha na kutufanya kuishi katika hofu ya hali ya juu.
  • Unazitaka mamlaka husika kutuhakikishia mustakabali wa usalama wetu sasa na siku za mbeleni katika nchi yetu.
  • Tunalaani juhudi zinazofanywa na wathalimu wote katika fani ya udaktari
  • Tunalaani vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa madaktari wenzetu sehemu mbalimbali kama bugando, dodoma na mbeya na kwingineko.
  • Tunatamka wazi kuwa kitendo cha kuwafukuza, kuwanyima mshahara na haki nyingine za mwezi juni ni udhalilishaji na kinyume na amri ya mahakama.
  • Kutokana na vitendo vyo te hapo juu (yaani kutekwa na kuteswa kwa dr ulimboka, unyanyasaji wa madaktari wenzetu) na pia kutoka na ukweli kwamba hali ya dr ulimboka inazidi kudorora, vile vile kwakuwa siku zote serikali imekuwa ikikubali kuwa madai yetu ni ya msingi (lakini haiyatafutii ufumbuzi wowote) tumeamua kusitisha kutoa huduma katika hospitali zote tunazofanyia kazi yaani Muhimbili, MOI, Ocean Road, Amana, Mwananyamala nk. Hadi hapo madai yetu ya msingi yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
  • Tunaomba madaktari bingwa wote hapa nchini watuunge mkono katika harakati hizi za kuiboresha sekta nzima ya afya.

Imetolewa na Dr C. Mng'ong'o
Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa Kanda ya Dar es salaam
 
Back
Top Bottom