Tamko la madaktari bingwa MNH, MUHAS na ORCI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la madaktari bingwa MNH, MUHAS na ORCI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Jun 29, 2012.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  TAMKO:
  Tamko la Madaktari Bingwa wa mkoa wa Dar es salaam
  (MNH, MOI, Ocean Road na Hospitali za manispaa ya mkoa wa Dar es salaam)

  Kutokana na kikao kilichofanyika leo tarehe 29/06/2012 madaktari bingwa tumeamua yafuatayo:


  • Tunalaani kwa kauli moja kitendo alichofanyiwa daktari na kiongozi wa jumuiya yetu dr stephan ulimboka cha kutekwa kuumizwa na kutupwa msitu wa mabwe pande kitendo hiki kimetuhuzunisha, kimetufadhaisha na kutufanya kuishi katika hofu ya hali ya juu.
  • Unazitaka mamlaka husika kutuhakikishia mustakabali wa usalama wetu sasa na siku za mbeleni katika nchi yetu.
  • Tunalaani juhudi zinazofanywa na wathalimu wote katika fani ya udaktari
  • Tunalaani vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa madaktari wenzetu sehemu mbalimbali kama bugando, dodoma na mbeya na kwingineko.
  • Tunatamka wazi kuwa kitendo cha kuwafukuza, kuwanyima mshahara na haki nyingine za mwezi juni ni udhalilishaji na kinyume na amri ya mahakama.
  • Kutokana na vitendo vyo te hapo juu (yaani kutekwa na kuteswa kwa dr ulimboka, unyanyasaji wa madaktari wenzetu) na pia kutoka na ukweli kwamba hali ya dr ulimboka inazidi kudorora, vile vile kwakuwa siku zote serikali imekuwa ikikubali kuwa madai yetu ni ya msingi (lakini haiyatafutii ufumbuzi wowote) tumeamua kusitisha kutoa huduma katika hospitali zote tunazofanyia kazi yaani Muhimbili, MOI, Ocean Road, Amana, Mwananyamala nk. Hadi hapo madai yetu ya msingi yatakaposikilizwa na kutekelezwa.
  • Tunaomba madaktari bingwa wote hapa nchini watuunge mkono katika harakati hizi za kuiboresha sekta nzima ya afya.


  Imetolewa na Dr C. Mng'ong'o
  Mwenyekiti wa Madaktari Bingwa Kanda ya Dar es salaam   
 2. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shiriki maandamano tarehe 04.07 2012 ubungo mataa kuwa shaidi wakudai huduma bora ya afya mwambie na mwenzako
   
 3. b

  bgmy Member

  #3
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandamano hayana Tija....wasomi kuweki makini na mambo mnayoyafanya
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ninahofia akipelekwa nje watammalizia hukohuko.
   
 5. m

  maingu z Senior Member

  #5
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo ndo hatua za wanaume, big up nawapongeza kwani inaweza kuwa chachu ya ukombozi wa nchi hii, damu ya dr ulimboka ni sawa ya jesus haitapotea bure, kwani naamini kuwa ukombozi halizi huja kwa kumwaga damu. Mungu akupe afya njema pamoja na juhudu za madaktari wenzako. Nashauri madaktari wote hata wasio maspecialist wagome pia kuunganisha nguvu,
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,832
  Trophy Points: 280
  Saafi sana tuko pamoja
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Madaktari wanatakiwa wajitahidi sana kuwasilisha vilio vyao kwenye vyombo vya kimataifa mfano UN, Amnesty International, ICC n.k tena haraka, vinginevyo wataokotwa wengi kwenye msitu wa Mabwepande.
   
 8. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hapo penye red sijakuelewa vizuri nadhani panahitaji marekebisho
   
 9. 4

  4change JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 535
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  this is news!we were waiting for it.everybody everywhere anatakiwa astand up against hii serikali dhaifu na ya wauaji
   
 10. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukomo wa akili zako sawa na urefu wa kidole chako kidogo.
  Tunisia, Misri,.... hata ikifika huko, so be it.
   
 11. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Good move, tuko pamoja.
   
 12. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani unge edit hapo, the post is too religious
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280

  kuna mahali katika statement hiyo hapo juu kuna mahali mameandikwa maandamani??
   
 14. Litvinienko

  Litvinienko JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika vitisho vingine, MOI pia imeagizwa na serkali kuwaandikia barua madktari wote warudi kazini by jumatatu saa tatu, beyond which atakuwa kajifukuzisha kazi
   
 15. Unkolonized

  Unkolonized Member

  #15
  Jun 29, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena wafanye haraka kutoa taarifa Amnest Intl na kwingineko! Mie naomba maandamano yawe ni kwa nchi nzima sio ubungo tu!
   
 16. Pena

  Pena Member

  #16
  Jun 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Serikali leo imetoa ofa ya kulipia gharama zote za matibabu, madaktari wamekataa... Wamesema hawataki fedha ya yuda iskarioti.
   
 17. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ... The truth shall come strong whatever the circumstances !!!! ...The Government shouldn't get any difficulty on learning and adapting to the Truth ... The only Saviour in the Moment NOW!!!!
   
 18. M

  Mundu JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ile ya Yuda Iskariote iliandikwa...na ilipaswa iwe vile ili mambo yote ya nyuma yaliyotabiriwa yapate kuwa! Hii ya Serikali ni yako na Yangu..kodi na maliasili zetu...wasiikatae...
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hii ndio kitu nisichokubaliana nacho kabisa!.. Sasa hawa madaktari wanapogoma ndio kusema Dr.Ulimboka kapigwa na wananchi kiasi kwamba wao ndio wachukue adhabu hii?

  Halafu wanaombwa wananchi wale wale waliadhibiwa kuchangia tiba ya Ulimboka wakati wengine tuna wagonjwa wanaotaka huduma tu wapone lakini wanatufia mkononi kwa sababu ya mgomo huu..Nawaomba Madaktari iadhibuni serikali na sii wananchi walipa kodi ambao hawana makosa kabisa.

  TUCTA wametoa kauli na wito kwamba swala hili litafikishwa ktk vyombo vya kimataifa, na hatuelewi mazungumzo baina ya serikali na shirikisho la madaktari limeenda vipi au wamekwama wapi..

  Tunaona migomo hadi Bugando na Hospital za makanisa halafu tukisema mfumo mbaya na wapi penye mapungufu watu wanakuja juu kutetea kanisa ilihali vyombo hivi havifanyi kazi inavyohitajika.

  Kazi kusubiri fedha za donors na misamaha wajirushe kwa sifa ya huduma ambayo haitusaidii wananchi ktk kupunguza gharama za Afya na sasa ndio hatutibiwi kabisaa wakati kodi zetu wanakula.

  Kinachofanywa na madaktari hakina tofauti na UAMSHO, wao wanaona kila haki ya kuchoma makanisa au kugoma lakini wanashindwa kuidhibu serikali yenyewe. Kesho ukisikia Sheikh mkubwa wa UAMSHO kafanyiziwa, utawasikia Wazanzibar na Waislaam wakilaani Wakristu na serikali lakini hawapimi kitendo cha kuchoma makanisa yasiyohusika na mgogoro ndio unafiki ulipoanzia. Vitendo vyetu sisi wenyewe ktk kuwaadhibu wananchi ndivyo vinavyozidi kutugawa.

  Sioni sababu ya madaktari kugoma pasipo kuwashirikisha wananchi, kulifanya swala hili ni lao wao wenyewe kwa kuwasulubu wananchi ii kuikomoa serikali.. Watu wanakufa jamani, muwe na huruma japo kidogo wakati tunaitafuta suluhu.

  TUCTA wamesema watalipeleka swala hili ktk vyombo vya kimataifa, muda wote kwa nini wasihusishwe mapema tukatafuta suluhu badala ya kuwaadhibu wananchi?..
   
 20. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,632
  Trophy Points: 280
  msipeleke mje kama mmeshindwa kumtibia waiteni madokta bingwa wastaafu, swala lake sio ugonjwa ni kipigo tu, mkipeleka nje watamwakwembe bure.
   
Loading...