Tamko la Lissu kuhusiana na sakata la kesi ya Arusha; Mbowe naye alonga

Akamatwe kama amri inavyotaka, hakuna aibu yoyote hapo ! yeye ni kiongozi wa kambi feki bungeni hana hadhi ya kutokamatwa ( kivuli = feki )
Duu sijui wewe ni gamba au polisi mtandao?Waambie magamba na taasisi zake waje na fact kama ndugu Tundu lisu wasiwe waropokaji na kutoa kauli wasizoweza kuzitetea,mbona wanajisikilizia kumkamata sasa wakati hajajificha kama Liyumba alivyo fanya.
Pipoooooooooooooooooooooooz Pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa:grouphug::grouphug::grouphug:
 
Alitoa taarifa Hakimu akakataa, wewe tushauri ulitaka Mh Mbowe afanye nini?

Labda nifahamishe taarifa hiyo alitoa kwa mdomo au kwa maandishi? Na kwanini hakimu akatae taarifa za maandishi? na kama kweli alikataa taarifa hiyo ya maandishi basi alitakiwa aliwakilishe kwa spika ili kuthibitisha ushiriki wake katika shughuli hizo mbalimbali za bunge.

Naomba jibu hapo kama taarifa hiyo aliitoa kimaandishi na tujiulize kwanini hakimu aikatae?
 
MIe nachukulia chadema kama mwalimu wa walimu.... kila magamba wakija na viroja wanakutana na hoja!!! Yaani hamna hata haja ya somo la uraia aisee, shule yote siku hizi ipo available free from CDM

Ngoja tusubiri na hili chiligati atajibu nini.... hakawii kusema kama hamtaki akamatwe basi nikamateni mimi! mie sikatai kitu!!
 
Labda nifahamishe taarifa hiyo alitoa kwa mdomo au kwa maandishi? Na kwanini hakimu akatae taarifa za maandishi? na kama kweli alikataa taarifa hiyo ya maandishi basi alitakiwa aliwakilishe kwa spika ili kuthibitisha ushiriki wake katika shughuli hizo mbalimbali za bunge.

Naomba jibu hapo kama taarifa hiyo aliitoa kimaandishi na tujiulize kwanini hakimu aikatae?
Kwani hujawahi kusikia hakimu amekataa taarifa ya maandishi?? maswali mengine kama yanatokea jupiter aisee.. wa wap i weye??
 
Ulitaka kujua kama alitoa taarifa nimekujuza sasa maswali mengine muulize Hakimu Magamba mwenzao.
 
Hakuna Kitu hapo zaidi ya porojo zisizo na mashiko. Yeye wakati Mbowe anaandamana alikuwa anafanya kazi ya kibunge ? ametenda kosa la jinai kwa kusababisha mauaji ya watu , Mbowe ni muuaji, leo hii anataka kukamtwa eti kinga ya bunge. Kinga ya bunge haipo kwa mbunge anae fanya kosa la jinai, akamatwe na afikishwe mahakamani. Acheni kuwa mchicha mwiba !

nimekaa kimya ila sio vizuri. kwenye bold umekosea ndugu yangu nimenukuu kutoka katika katiba TUKUFU ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu cha 13(6) B kinachosema

(b) ni marufuku kwa mtu aliyeshtakiwa kwa kosa la jinai
kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka
itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo.

ndugu yangu nakushauri ujisomehe angalau kwa kidogo kuliko kwenda kwa pupa na kujibu hoja. asante
hilo;
 
Mbowe hayuko juu ya Sheria, lazima sheria za nchi zifuatwe!. kama alikuwa na majukumu ya kikazi za kibunge, ni lazima angetuma mwakilishi(mdhamini) wake hapo mahakamani. Sheria iheshimiwe, hatuwezi kuendesha nchi kikanjnja na personality

We kweli ni gamba la nyoka,wastahil liondolewe,taka usitake litaondolewa hilo!
 
Hakuna Kitu hapo zaidi ya porojo zisizo na mashiko. Yeye wakati Mbowe anaandamana alikuwa anafanya kazi ya kibunge ? ametenda kosa la jinai kwa kusababisha mauaji ya watu , Mbowe ni muuaji, leo hii anataka kukamtwa eti kinga ya bunge. Kinga ya bunge haipo kwa mbunge anae fanya kosa la jinai, akamatwe na afikishwe mahakamani. Acheni kuwa mchicha mwiba !

waambie wamkamate!! usitupigie kelele.
 
Ratiba ya Vikao vya Bunge vinajulikana hata kwetu sisi watu wa kawaida sembuse Mahakama, soma maelezo ya Mh Lisu ukiwa umetulia then utajua watu wanatakiwa kufanya kazi sio kukurupuka tu.

Naomba ujue kuwa mahakama haiendeshwi na porojo, siasa wala habari za mitaani. mahakama inaendeshwa kwa vielelezo thabiti. Hivyo Mbowe alitakiwa kutoa taarifa za maandishi kwa hakimu kumweleza kuwa anashiriki katika vikao vya kamati za Bunge na si kazi ya hakimu kusoma na kujua hilo kupitia magazeti.

WanaCHADEMA jamani jifunzeni japo kidogo sheria za nchi yenu na kuacha siasa mnapokuwa mahakamani
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Hapa ndio siku zote ninapoingia kiwewe na wanasheria au wana taaluma mbalimbali huko Tanzania. Kwani wanaonekana wanakuwa wazuri sana wanapokuwa nje ya siasa lakini wakiingia kwenye siasa tu basi na taaluma zao zinapotea.

Sasa hapa namshangaa sana mwanasheria mahiri Tindu Lissu. Amesahau kabisa kujua kuwa DOULA ina mihimili mitatu nayo ni Serikali, Mahakama na Bunge na kila kimoja kina kanuni zake.

Kinachoweza kuviunganisha hivi ni TAARIFA na si vinginevyo. Kwa mujibu wa hapa Mbowe ana makosa ya Kudharau mahakama ambao ni muhimili unaojitegemea kabisa kwani Hakimu Hana taarifa ya vikao vyake vya Bunge. Ilimpasa MBOWE atoe taarifa ya maandishi kwa hakimu kuwa nina shughuli za Kibunge basi mambo yangeisha na hapa sasa mila na desturi zinakuwa applied.

Hakimu hawezi soma kutoka kwenye magazeti au kusikia radioni kuwa Mbowe anahudhuria Bunge.

Vile vile Polisi ni sehemu ya muhimili wa Serikali. Sioni kwa nini wanachanganya mada hapo. Polisi wanakazi kubwa ya kuhakikisha sheria zinafuatwa. Na mtuhumiwa akifikishwa mahakamani basi pale atakuwa chini ya kanuni za mahakama mpaka atakapopata hukumu yake.

Naomba Lissu na wabunge wenzako muangalie sheria na sio kuleta dharau dhidi ya mihimili mingine ya doula.

No mzee, uchambuzi wako sio genuine! Hizi kinga za wabunge ni kwa mujibu wa sheria za nchi, sio sheria za bunge. Mahakama kama ilivyo kwa bunge au serikali inafuata sheria za nchi. Kuhusu point kuwa Mbowe angetoa taarifa kuwa ana majukumu ya kibunge, sio sawa kwa sababu Mbowe ni mbunge kila siku (kwa kipindi chake) na hakimu analijua hilo. Hakimu ndiye alipaswa kuwasiliana na bunge kujua kama warrant or arrest iko applicable for the mean time bila au kwa uwepo wa kibali cha spika.
Sheria hizi hazimkatazi mbowe kwenda mahakamani, bali zinazuia kukamatwa na polisi, na hata kama Mbowe angetoa taarifa, ingeweza kukubaliwa au kutaliwa, kwa sababu hakuna sheria inayozuia mbunge kufika mahakamani, bali inazuia kukamatwa (katika kipindi fulani).
So, kesi hapa ni Mbowe kutofika mahakamani bila taarifa maalumu, then what follows ni kuwa kwa mujibu wa sheria nini kifanyike, akamatwe, lakini kwa mujibu wa sheria hizo hizo, akamatweje.., kwa kibali cha spika. Hapo ndipo hesabu zilipomshinda hakimu kidogo... or may be kibali kimetolewa na spika labda, hilo hatujui. Na spika akitoa hicho kibali (kama alivyotoa kwa huyo mbunge wa busega pengine), Mbowe hana cha kujitetea...
 
hakimu alikua busy sana kiasi kwamba alikisahau kifungu hicho cha sheria naimani akilisoma tamko hili
atafuatilia na kuubadilisha uamuzi wake hakimu nae mwanadamu japokua hapa kunakila chembechembe za maagizo toka kwa MAGAMBA
 
Kwani hujawahi kusikia hakimu amekataa taarifa ya maandishi?? maswali mengine kama yanatokea jupiter aisee.. wa wap i weye??

Kisheria Hakimu haruhusiwi kukataa taarifa zozote za maandishi labda ziwe na matatizo kisheria. labda hakuna taarih, hakuna saini n.k.

nakuomba ulielewe hilo.

Jamani tusimtetee mtu aliyekula kiapo cha kulinda sheria za nchi yenu.
 
Wakuu habari!!

Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe leo wamezungumza na vyombo vya habari kwenye Ofisi za Kambi ya Upinzani DSM kuhusiana na amri ya mahakama kutaka kumkamata Kamanda Mbowe.

Jisomeeni wenyewe!!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Simu Na. 026 2322761-5
Fax Na. (255) 026 2324218
E-Mail: mbowe2008@gmail.com

(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa
Kiongozi wa Upinzani)

OFISI YA BUNGE

S.L.P. 941 DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

AMRI YA KUMKAMATA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YAINGILIA UHURU WA BUNGE, YAHATARISHA DEMOKRASIA!!!
Dar es Salaam, Juni 3, 2011:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha kutoa amri ya kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Mheshimiwa Mbowe pamoja na Wabunge, viongozi na wanachama kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yanayotokana na maandamano tarehe 5 Januari 2011 katika Jiji la Arusha yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua wananchi watatu na kujeruhi wengine wengi. Taarifa zinaonyesha kwamba amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Charles Magessa, siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2011 na kurudiwa tena jana, yaani tarehe 2 Juni 2011.

Mheshimiwa Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa vile amekuwa akihudhuria vikao vya Kamati mbali mbali za Bunge vilivyoanza tarehe 23 Mei 2011 na ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011. Kama Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ni mjumbe wa Kamati mbali mbali za Bunge kama vile Kamati ya Uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Fedha na Uchumi. Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni mjumbe katika Tume ya Utumishi wa Bunge na ndiye msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ndio msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge. Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge. Uhuru huu wa kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza Mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika.

Maneno eneo la Bunge limetafsiriwa na kifungu cha 2 cha Sheria hiyo kumaanisha ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza (lobbies), maeneo ya wageni (galleries), courtyards, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge. Kwa maana hiyo, Mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au Kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya Mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

Kufuatana na mila na desturi za kibunge za Jumuia ya Madola ambazo nchi yetu imezikubali na inatakiwa kuzifuata, kinga ya Wabunge dhidi ya kukamatwa inakuwa na nguvu wakati wa mkutano wa Bunge pamoja na muda muafaka na wa kutosha kabla na baada ya mkutano wa Bunge. Kwa mujibu wa Erskine May, mwandishi maarufu wa mila na desturi za mabunge ya Jumuia ya Madola, muda muafaka na wa kutosha umechukuliwa kwa ujumla kuwa ni siku arobaini kabla na baada ya mkutano wa Bunge. Kwa mantiki hiyo, wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri dhidi yake, Mheshimiwa Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge. Aidha, Mheshimiwa Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na muda muafaka na wa kutosha - kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuia ya Madola - utakapokwisha baada ya Mkutano huo!

Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa na unafiki na ubaguzi wa wazi unaoonyeshwa na Jeshi la Polisi juu ya Wabunge wa vyama vya upinzani. Hii ni kwa sababu wakati Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata Wabunge wa Upinzani bila kuomba kibali chochote cha Spika kama inavyotakiwa na Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge - kama ilivyotokea kwa Wabunge wa CHADEMA Waheshimiwa Mbowe, Godbless Lema (Arusha Mjini), Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo), Meshack Opulukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) na Magdalena Sakaya (Viti Maalum, CUF), wabunge wa CCM na ambao wanakabiliwa na tuhuma za makosa makubwa zaidi wamekuwa wanaombewa kibali cha Spika kabla ya kukamatwa. Kwa hili, tuna ushahidi wa barua ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwa Katibu wa Bunge ya kumwomba Mheshimiwa Titus Mlengeya Kamani (Busega, CCM) ili akahojiwe na Jeshi la Polisi kuhusu kuhusika kwake na njama za kutaka kumwuua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Masunga Chegeni. Barua hiyo ya tarehe 31 Mei 2011 ilinakiliwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, Makao Makuu ya Polisi DCI Robert Manumba. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye kwa taarifa zetu amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na Polisi kama inavyoonekana kwa Wabunge wa CCM. Hii inadhirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa Wabunge wa CCM

Kwa sababu hizo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitarajii, na itapinga kwa nguvu zake zote, kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kwa kipindi chote ambacho ana kinga ya Bunge kama inavyotambuliwa na Katiba na sheria zetu pamoja na mila na desturi za kibunge ambazo tumechagua kuzifuata kwa hiari yetu wenyewe. Aidha, tunatarajia Mahakama pamoja na vyombo vingine vyote vilivyoanzishwa na vinavyofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu vitatumia busara ili kuiepusha nchi yetu na fedheha ya kuonekana inakamata Wabunge wake wakati wakiwa wanatekeleza wajibu wao wa kibunge!

------------------------------------
Tundu A.M. Lissu (MB.)
Mnadhimu Mkuu
KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

Aluta Continua
Kutoka Ofisi ndogo za Bunge

Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira

Nachelea kusema kwamba kuna upotoshaji unafanyika na sijui ni kwa hasara ya nani.

Mhe. Mbowe ana Makosa ya wazi kabisa ya kudharau Mahakama, si jambo zuri kwa kiongozi Mkuu wa aina yake.

Mhe. Lissu ni Mwanasheria makini, hivi ana amini hilo tamko linatosha kuzuia utekelezaji wa Amri ya Mahakama?

Tusipumbazane hapa, kama sijasahau Sheria, Tamko hilo lingekuwa na Makali kama lingefuatana na Amri ya Mahakama ya juu kusitisha/kuzuia kwa muda utekelezaji wa Amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha.

I stand to be corrected!
 
They have been using our ignorance to oppress and abuse our freedom of speech for so long!!!. This time wataipata yupo baba mnadhimu aliyeisoma sheria neno kwa neno! Hatubabaiki! Utaona kama watamgusa!

PP daima!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Dola haitishwi ww, na huna uwezo wa kubishana na dola . Mbona hapo kabla aliisha kamatwa, ulifanya nn sasa kumtoa ili hali alilazwa sakafuni na kipigo juu

Sawa dola haitishiwi kama itakuwa inafanya kazi yake ya kueleweka sio longo longo za huyu hakimu. Kwa taarifa walizotoa wabunge mwanzoni angewasiliana nao kwanza kabla ili asiumbuke. Inabidi mkamrudishe darasani asiwe anapiga chabo kwa wengine. Yeye hakimu alikuwa amekaa dawati moja na askari akapiga jicho akaona alichoandika polisi nae akaparamia hicho hicho, badala ya kufanya kazi yake. kamata riiireteee hapa, rinajifanga rinajua sheria tutarionyesha sheria za kibongo bongo. Yeye alishindwa kufanya kazi ya hakimu akawasaidi polisi na kazi yake kaiweka pembeni..
Haya sasa Mh Lissu amemrahisishia sehemu ya kusoma ili mtihani ujao afaulu. Ole wake afeli tena.
 
Dola haitishwi ww, na huna uwezo wa kubishana na dola . Mbona hapo kabla aliisha kamatwa, ulifanya nn sasa kumtoa ili hali alilazwa sakafuni na kipigo juu
Unafurahia ujinga, mbunge wako anadharirishwa na kupigwa wewe kwa akili yako finyu unafurahi????? Huoni huo ni ukiukwaji wa haki za msingi za bunge, mbali na haki za binadamu. Wewe zezeta unajiita genius brains!!!!! Mpaka mpelekwe The Hague ndio mjue haki za binadamu ni nini??????????
 
No mzee, uchambuzi wako sio genuine! Hizi kinga za wabunge ni kwa mujibu wa sheria za nchi, sio sheria za bunge. Mahakama kama ilivyo kwa bunge au serikali inafuata sheria za nchi. Kuhusu point kuwa Mbowe angetoa taarifa kuwa ana majukumu ya kibunge, sio sawa kwa sababu Mbowe ni mbunge kila siku (kwa kipindi chake) na hakimu analijua hilo. Hakimu ndiye alipaswa kuwasiliana na bunge kujua kama warrant or arrest iko applicable for the mean time bila au kwa uwepo wa kibali cha spika.
Sheria hizi hazimkatazi mbowe kwenda mahakamani, bali zinazuia kukamatwa na polisi, na hata kama Mbowe angetoa taarifa, ingeweza kukubaliwa au kutaliwa, kwa sababu hakuna sheria inayozuia mbunge kufika mahakamani, bali inazuia kukamatwa (katika kipindi fulani).
So, kesi hapa ni Mbowe kutofika mahakamani bila taarifa maalumu, then what follows ni kuwa kwa mujibu wa sheria nini kifanyike, akamatwe, lakini kwa mujibu wa sheria hizo hizo, akamatweje.., kwa kibali cha spika. Hapo ndipo hesabu zilipomshinda hakimu kidogo... or may be kibali kimetolewa na spika labda, hilo hatujui. Na spika akitoa hicho kibali (kama alivyotoa kwa huyo mbunge wa busega pengine), Mbowe hana cha kujitetea...
.

hapo nilipoRED nafikiri Mh Lissu amepafafanua vizuri katika tamko lake. Soma vizuri kisha lete hoja
 
Nachelea kusema kwamba kuna upotoshaji unafanyika na sijui ni kwa hasara ya nani.

Mhe. Mbowe ana Makosa ya wazi kabisa ya kudharau Mahakama, si jambo zuri kwa kiongozi Mkuu wa aina yake.

Mhe. Lissu ni Mwanasheria makini, hivi ana amini hilo tamko linatosha kuzuia utekelezaji wa Amri ya Mahakama?

Tusipumbazane hapa, kama sijasahau Sheria, Tamko hilo lingekuwa na Makali kama lingefuatana na Amri ya Mahakama ya juu kusitisha/kuzuia kwa muda utekelezaji wa Amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha.

I stand to be corrected!

soma vizuri kanuni za bunge la jumuia ya madola ambayo Tanzania imeridhia - baada ya hapo tutakusaidia.
 
Back
Top Bottom