Tamko la Lissu kuhusiana na sakata la kesi ya Arusha; Mbowe naye alonga

Kwa nini haya hayakuwekwa kwenye taarifa rasmi iliyotolewa na Mh Lissu? Au hii habari ilikuwa ni kwa ajili ya magazeti tuu? Ingekuwa vizuri kama nayo ingewekwa kwenye taarifa ya Mh Lissu. Yaani hapa umedhibitisha tuu kuwa taarifa ya Mh Lissu ina gaps. Hii ni fact muhimu sana. Ingewekwa kwenye hiyo taarifa na pia tupewe ufafanuzi hayo maombi yalitumwa lini na yali-cover muda gani. Kumbuka Mh hakwenda mahakamani mara mbili. Je, hayo maombi yanacover hizo non-appearances mbili au moja tuu? Chadema kinajitambulisha kama chama makini, kwa hiyo kinabidi kuwa makini pia katika kutoa taarifa muhimu kama hizi.

Kumbuka washtakiwa Joseph Selasini na Dadi Igogo pia hawakuwepo mahakamani jana, lakini mahakama haikuamuru wakamatwe kama ilivyo kwa wenzao kutokana na wadhamini wao kujitokeza na kuwaombea udhuru. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani hapo, Selasini alikuwa anahudhuria vikao vya Kamati ya Bunge mjini Bagamoyo na Igogo alikuwa kwenye mitihani jijini Dar es Salaam. Sasa kama Mh Selasini aliweza kutoa udhuru kupitia kwa mdhamini, kwa nini Mh Mbowe alishindwa? It doesn't make any sense at all.



Hii pia ingeelewa zaidi kama Mh Lissu angeghusia hili kwenye kwenye taarifa yake rasmi. Inaonyesha kama kama vile kilichozungumzwa mbele ya waandishi wa habari ni tofauti kidogo na kilichopo kwenye taarifa rasmi. Kwa maneno mengine aliyoyasema Mh Mbowe mbele ya waandishi wa habari hayakuwekwa kwenye taarifa ya Mh Lissu. Kwa nini?



Kwa hiyo ina maana kuwa kama asingekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni asingedhalilishwa? Mboa Dk Willibrod Slaa naye ameamuriwa kukamatwa na hili jalizungunzwi? Ay naye hadhalilishwi? Mbona Mh Godbless Lema nae ameamriwa akamatwe na kufikishwa mahakamani hapo baada ya kushindwa kuhudhuria mara kadhaa mahakani. Naye yuko kwenye vika vya kamati za bunge?

Mkuu argument yangu inabase kwenye taarifa rasmi iliyotolewa na Mh Lissu ambaye ni mnadhimu mkuu kambi ya upinzani bungeni. Ile taarifa ameitoa kama kiongozi bungeni. Ile taarifa itaingia kwenye records za bunge. Kwa sababu hiyo basi inabidi iwe self sufficient. Hatuwezi kutumia magazeti ili tuweze kuielewa taarifa rasmi. Kama hayo yote yalisemwa kwenye mkutano na waandishi wa habari, why then hawakuweka kwenye hiyo taarifa rasmi? Kwa nini wawake vitu nusu nusu? Tunachotaka ni transparency and consistence on what exactly happened. Whatever the case vipengele vingi alivyotumia Mh Lissu sio relevant kwenye hii issue.

Nashukuru. Taarifa ya kibunge ya Tundu Lisu is one issue, amri ya mahakama ya Mbowe kukamatwa is a different issue, Madhumuni ya mahakama na utaratibu wake kwenye kesi (yaani kuwapotezea muda watuhumiwa wasifanye shughuli za kitaifa) is another issue. Any way kama nilivyosema hapo juu, mwenendo wa jeshi la polisi, mahakama na wenye madaraka (mind you not mamlaka) yanatia shaka. Polisi wanayumbishwa na kuyumba wenyewe kwenye kutekeleza majukumu yao, Mahakama ina virusi vya kutumia umahakama (ujinga wa wengi wetu kuhusu sheria) kuwatiisha watu kwa vitisho, wenye madaraka wame unsurp hata majukumu ya wengine ili wajinufaishe na amri zisizo halali (mimi naamini wanamkono kwenye hili shauri).

My take wanasema usipojielimisha jaribu ujinga. Hapa nchini tupo kwenye lindi la ujinga wa kisheri (elimu ya kwanza ya raia ye yote kuhusu haki za kisheria) kiasi ambacho mambo yanayoendelea nchini yapo hapa tu na si mahali pengine duniani. Kama tunavyokanganywa na hili tukio toka mauaji, kesi mahakamani kudhalilishana eti kwa kwa kuwa mmoja ni polisi, mwingine hakimu, mwingina kiongozi wa upinzani na nyuma ya pazia kuna mwenye madaraka (siyo uongozi) kwa chama kilichopigika. Mwisho tunataka kufanikisha nini kama siyo kufarakana na kupalilia chuki baina yetu.
 
Lissu the Dragon.Anakwambia Musa alitumwa akawakomboe wana wa isirael pale misiri.Walitumia miaka mingi sana njiani hadi kufika ile inchi ya ahadi.Kuna waliokatatamaa,waliokufa,waliozaliwa na hatawaliosalitiana ktk safari hiyo tena ya jagwani.Lakini walifika licha ya kukutana na vizingiti na mambo kadha wa kadha ya kukatisha tamaa.
 
Kuna watu humu waliongea hadi mapovu mdomoni tukawaambia kwa hili serikali haina ubavu wa kumkamata Mh. Mbowe hata wao (CCM) wanalijua hilo wanachofanya ni siasa za kuuza magazeti tu.
 
Back
Top Bottom