Tamko la Lissu kuhusiana na sakata la kesi ya Arusha; Mbowe naye alonga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Lissu kuhusiana na sakata la kesi ya Arusha; Mbowe naye alonga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Regia Mtema, Jun 3, 2011.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari!!

  Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Tundu Lissu na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Freeman Mbowe leo wamezungumza na vyombo vya habari kwenye Ofisi za Kambi ya Upinzani DSM kuhusiana na amri ya mahakama kutaka kumkamata Kamanda Mbowe.

  Jisomeeni wenyewe!!

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  BUNGE LA TANZANIA

  Simu Na. 026 2322761-5
  Fax Na. (255) 026 2324218
  E-Mail: mbowe2008@gmail.com


  (Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa
  Kiongozi wa Upinzani)
  OFISI YA BUNGE

  S.L.P. 941 DODOMA  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  AMRI YA KUMKAMATA KIONGOZI WA KAMBI RASMI YA UPINZANI YAINGILIA UHURU WA BUNGE, YAHATARISHA DEMOKRASIA!!!
  Dar es Salaam, Juni 3, 2011:

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imepokea kwa mshtuko, masikitiko na mshangao mkubwa taarifa za Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha kutoa amri ya kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe. Mheshimiwa Mbowe pamoja na Wabunge, viongozi na wanachama kadhaa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanakabiliwa na mashtaka kadhaa yanayotokana na maandamano tarehe 5 Januari 2011 katika Jiji la Arusha yaliyopelekea Jeshi la Polisi kuua wananchi watatu na kujeruhi wengine wengi. Taarifa zinaonyesha kwamba amri hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mheshimiwa Charles Magessa, siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2011 na kurudiwa tena jana, yaani tarehe 2 Juni 2011.

  Mheshimiwa Mbowe hakuhudhuria mahakamani katika tarehe zote mbili kwa vile amekuwa akihudhuria vikao vya Kamati mbali mbali za Bunge vilivyoanza tarehe 23 Mei 2011 na ambavyo vinaendelea hadi hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaotazamiwa kuanza tarehe 7 Juni hadi tarehe 7 Septemba 2011. Kama Mbunge na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Mbowe ni mjumbe wa Kamati mbali mbali za Bunge kama vile Kamati ya Uongozi, Kamati ya Kanuni za Bunge na Kamati ya Fedha na Uchumi. Aidha, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ni mjumbe katika Tume ya Utumishi wa Bunge na ndiye msemaji mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na amri ya kumkamata Mheshimiwa Mbowe kwa vile inakiuka moja kwa moja sheria, mila na desturi za miaka mingi zinazohusu kinga, haki na mamlaka ya Bunge na ambazo ndio msingi mkuu wa demokrasia yetu ya kibunge. Ibara ya 100 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatambua na kulinda "uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge." Uhuru huu wa kikatiba umetiliwa mkazo katika vifungu vya 5, 6 na 11 vya Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge ya mwaka 1988 vinavyokataza Mbunge kukamatwa au kupewa amri ya kuhudhuria mahakamani wakati akiwa ndani ya eneo la Bunge au wakati Bunge limekutana bila kuwepo kwa kibali cha Spika.

  Maneno ‘eneo la Bunge' limetafsiriwa na kifungu cha 2 cha Sheria hiyo kumaanisha "ukumbi ambao hutumiwa kwa vikao vya Bunge, pamoja na ofisi, vyumba, vibambaza (lobbies), maeneo ya wageni (galleries), courtyards, bustani na maeneo mengine yaliyowekwa kwa ajili ya matumizi au malazi ya wajumbe, maafisa au wageni wa Bunge pamoja na njia zinazounganisha maeneo hayo na maeneo mengine yanayoweza kutangazwa na Spika kuwa ndani ya maeneo ya Bunge." Kwa maana hiyo, Mbunge anapokuwa anahudhuria vikao vya Bunge au Kamati zake au anapokuwa mahali pengine popote kwa kuitikia wito wa kuhudhuria vikao hivyo vya Bunge hawezi akakamatwa ili kutekeleza amri ya Mahakama au ya chombo kingine chochote nje ya Bunge.

  Kufuatana na mila na desturi za kibunge za Jumuia ya Madola ambazo nchi yetu imezikubali na inatakiwa kuzifuata, kinga ya Wabunge dhidi ya kukamatwa inakuwa na nguvu wakati wa mkutano wa Bunge pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha' kabla na baada ya mkutano wa Bunge. Kwa mujibu wa Erskine May, mwandishi maarufu wa mila na desturi za mabunge ya Jumuia ya Madola, "muda muafaka na wa kutosha umechukuliwa kwa ujumla kuwa ni siku arobaini kabla na baada ya mkutano wa Bunge." Kwa mantiki hiyo, wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha inatoa amri dhidi yake, Mheshimiwa Mbowe alikuwa analindwa na kinga ya Bunge. Aidha, Mheshimiwa Mbowe ataendelea kulindwa na kinga hiyo kwa kipindi chote cha Mkutano wa Nne wa Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na ‘muda muafaka na wa kutosha' - kama unavyotambuliwa katika mila na desturi za Mabunge ya Jumuia ya Madola - utakapokwisha baada ya Mkutano huo!

  Kwa upande mwingine, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeshangazwa na unafiki na ubaguzi wa wazi unaoonyeshwa na Jeshi la Polisi juu ya Wabunge wa vyama vya upinzani. Hii ni kwa sababu wakati Jeshi la Polisi limekuwa likiwakamata Wabunge wa Upinzani bila kuomba kibali chochote cha Spika kama inavyotakiwa na Sheria ya Kinga, Mamlaka na Haki za Bunge - kama ilivyotokea kwa Wabunge wa CHADEMA Waheshimiwa Mbowe, Godbless Lema (Arusha Mjini), Phillemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Joseph Selasini (Rombo), Meshack Opulukwa (Meatu), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Esther Matiko (Viti Maalum, CHADEMA) na Magdalena Sakaya (Viti Maalum, CUF), wabunge wa CCM – na ambao wanakabiliwa na tuhuma za makosa makubwa zaidi – wamekuwa wanaombewa kibali cha Spika kabla ya kukamatwa. Kwa hili, tuna ushahidi wa barua ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mwanza SP B.M. Wakulyamba kwa Katibu wa Bunge ya kumwomba Mheshimiwa Titus Mlengeya Kamani (Busega, CCM) ili akahojiwe na Jeshi la Polisi kuhusu kuhusika kwake na njama za kutaka kumwuua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Busega Dk. Raphael Masunga Chegeni. Barua hiyo ya tarehe 31 Mei 2011 ilinakiliwa kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, Makao Makuu ya Polisi DCI Robert Manumba. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CHADEMA au chama kingine cha upinzani ambaye – kwa taarifa zetu – amewahi kuombewa kibali cha kukamatwa na Polisi kama inavyoonekana kwa Wabunge wa CCM. Hii inadhirihisha upendeleo wa wazi wa Jeshi la Polisi kwa Wabunge wa CCM

  Kwa sababu hizo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitarajii, na itapinga kwa nguvu zake zote, kitendo chochote cha kumtishia au kumkamata Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kwa kipindi chote ambacho ana kinga ya Bunge kama inavyotambuliwa na Katiba na sheria zetu pamoja na mila na desturi za kibunge ambazo tumechagua kuzifuata kwa hiari yetu wenyewe. Aidha, tunatarajia Mahakama pamoja na vyombo vingine vyote vilivyoanzishwa na vinavyofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi yetu vitatumia busara ili kuiepusha nchi yetu na fedheha ya kuonekana inakamata Wabunge wake wakati wakiwa wanatekeleza wajibu wao wa kibunge!  ------------------------------------
  Tundu A.M. Lissu (MB.)
  Mnadhimu Mkuu
  KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI


  Aluta Continua
  Kutoka Ofisi ndogo za Bunge

  Regia E Mtema
  Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa sijui hii! I bet hata jk hajui, wala wasaidizi wake hawajui!
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Nitarudi baadae kuisoma kwa undani zaidi, nipate msosi kwanza....
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Mimi kuna kitu huwa sijakielewa bado, yaani Kiongozi wa kambi ya upinzani aache majukumu ya Kitaifa kwenda Arusha kumsikiliza tu hakimu anavyohairisha kesi mpaka tarehe nyingine, is it make any sense? Ninachowashauri wanasheria wa CHADEMA ni kumkataa huyo hakimu moja kwa moja maana sioni kama anaweza kutenda haki, na haki ionekane kweli imetendeka. SIAMINI.
   
 5. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... Wanafunzi wanaopata Mimba ni kwa sababu ya kiherehere chao" JK 2010

  Statesman, my foot!
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Crap
  Hajajibu chochote hapo zaidi ya porojo nyingi zisizo na mashiko kabisa. Mdhamini wake mbona nae hakufika ? Mbowe hana kinga hiyo na akamatwe kwa kuidharau mahakama. Yeye avunje sheria eti ni kiongozi wa kambi kivuli ya upinzani. Mkae mkielewa kivuli, maana yake si halisi, hivyo yeye ni kiongozi wa kambi isiyo halisi hana nguvu.
   
 7. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  Tanzania Security Sector Reform (SSR) has become imperative.
   
 8. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #8
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Aibu hata kwa hakimu aliyetoa amri hiyo
   
 9. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hii imetulia, ndio uzuri wa kupeleka wabunge Bora Bungeni na wala sio bora wabunge kama chama kile kingine sijui magamba kinavyofanya, hongera Mh Tundu Lisu ki ukweli mimi umenipa Shule leo.

  Nilikuwa najiuliza siku zote mbona wabunge wetu wanakamatwa bila utaratibu? ila nijuavyo ni kwamba polisi bado wana uccm ndio sababu,

  Aksante kwa kutuelimisha wengi.
   
 10. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #10
  Jun 3, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi kumbe ndivyo sheria inavyosema. Kwa hiyo wabunge wa upunzani si wabunge tuliowachagua ila wabunge ni wale wa CCM tu. Bado tupo kwenye mfumo wa chama kimoja hakika!!
   
 11. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,420
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180

  Wewe ni Genius?!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 12. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  siyo kosa la hakimu, tatizo hawa mahakimu wa mahakama za mwanzo na vijiji hawajui hizi sheria, na isitoshe wanazozijua wamekariri.
   
 13. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mwambie IGPa2me vibaraka wake wakamkamate bs.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sure! Kamkamate basi acha maneno mengi.
  Au mtumie msg Said akamkamate, si yupo hapo mjini kati!?
   
 15. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naona hujasoma between lines kuelewa kilichoandikwa.
   
 16. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hawa magamba kiboko yao ni vitu vya namna hii maana ni wavivu wa kusoma, CDM has to step smartly always if they want to frustrate them more. Tumieni akili zaidi maana ndiyo mtaji wa masikini, wao wanahela na dola nyie mna akili na nguvu ya umma tuone mwisho wake!
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Akamatwe kama amri inavyotaka, hakuna aibu yoyote hapo ! yeye ni kiongozi wa kambi feki bungeni hana hadhi ya kutokamatwa ( kivuli = feki )
   
 18. k

  kbhoke Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Crap vipi? Sheria ya kinga inayotajwa na Lissu inawahusu wabunge wanapofanya kazi zao. Kipi hakieleweki hapo. Wabunge waupinzani ni wabunge!
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  crap madrasa
   
 20. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  lissu, the driving force of the revolution...
   
Loading...