Tamko la kuondoa wamachinga mijini liende sambamba na kuwaondoa watoto wa vigogo kwenye ajira Serikalini

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
25,290
2,000
Inasikitisha mno,

Namna maskini asiye na kipato akinyanganywa fursa yake hata ndogo tu ya kuilisha familia yake.

Wakati haya yakiendelea.

Watoto wa vigogo wamezijaza nafasi zote za ajira huko serikalini.

Huku wale maskini wakiambiwa wakajiajiri kwakua ajira hakuna.

Lakini wanapotaka kujiajiri wanaambiwa hawana haki ya kujiajiri.

Nani mtetezi wa kada hii ya chini.

Aliyepo ajitokeze.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,512
2,000
Acha wivu basi. Tunakula malupulupu ya wazee wetu. Tuamini watoto wa vigogo wasio na uhalali walitumbuliwa enzi za Hayati Magufuli
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,980
2,000
Hivi machinga wameondolewa kwa maana ya kutofanya biashara au wamehamishwa kwenda maeneo maalum waliyotengewa?!! Mbona kuna uzungumzaji fulani ni km vile wamefukuzwa kabisa yaani!
 

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
15,934
2,000
Tumechoka na watetezi wenu wa kada ya chini, tunataka watetezi watakaotutoa kwenye uchumi wa umachinga, bodaboda na mama ntilie.
 

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
25,290
2,000
Kuna vita ukianzisha haiwez kuisha ndo km hyo ya kuondoa watt wa vgogo serikal. Mm naamin hat ww ungekua na kitengo kizur serikalin usingemsahau mwanao
tatizo ni kuwa wanatukandamiza sana mkuu,

yaani hata tukijiajiri hawataki tupange vitu vyetu mjini.

Huko mjini wanataka waishi wao tu na tusiwabugudhi wanapopita na magari yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom