Tamko la Kubenea kuhusu kukamatwa kwa Meya wa Ubungo Boniface

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,120
2,000
*TAARIFA KWA UMMA*

NIMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Yakoub amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya "wanaodai wako madarakani."

Kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Mhe. Sumaye alikuwa na ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ziko chini ya vyama vinavyounda umoja wa UKAWA.

Napenda kuufahamisha umma kuwa amri; na au maelekezo yoyote yaliyotolewa iwe na polisi au mkuu wa mkoa ama wilaya juu ya kukamatwa kwa Meya ni batili na haikubariki.

Hivyo basi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunapigana kufa na kupona kutetea haki za wananchi waliotuchagua na kuhakikisha Meya wetu anakuwa huru kwa gharama yoyote ile.

Ninawaomba wanachama, viongozi na wananchi wa jimbo la Ubungo na Kanda ya Pwani kusimama nasi, pamoja na Meya wetu katika kipindi kigumu cha kudai demokrasia ya kweli ndani ya Nchi yetu.

Ninaahidi kuwa mstari wa mbele kutetea wananchi na kuhakikisha haki zao zinapatikana.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha "udikteta ulioanza kuingia nchini taratibu," unatokomezwa.

Taifa hili siyo mali ya CCM. Ni letu sote.

*Saed Kubenea*
Mbunge wa Ubungo, M/M- Kanda ya Pwani.
 
Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,477
2,000
Mmeshaambiwa "mtashughulikiwa" ohoo!! hapa kasababu katapatikana na ngonjera ya makinikia itazimwa sasa hivi achilia mbali single ya ESCROW na RUGEMALILA inayoanza kunyemele kuzamisha makinikia kwenye chati
 
COPPER

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
2,117
2,000
*TAARIFA KWA UMMA*

NIMEPOKEA kwa masikitiko makubwa taarifa kuwa Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Yakoub amekamatwa na jeshi la polisi kwa amri ya "wanaodai wako madarakani."

Kukamatwa kwake kunatokana na hatua yake ya kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Mhe. Sumaye alikuwa na ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ziko chini ya vyama vinavyounda umoja wa UKAWA.

Napenda kuufahamisha umma kuwa amri; na au maelekezo yoyote yaliyotolewa iwe na polisi au mkuu wa mkoa ama wilaya juu ya kukamatwa kwa Meya ni batili na haikubariki.

Hivyo basi, ni jukumu letu kuhakikisha kuwa tunapigana kufa na kupona kutetea haki za wananchi waliotuchagua na kuhakikisha Meya wetu anakuwa huru kwa gharama yoyote ile.

Ninawaomba wanachama, viongozi na wananchi wa jimbo la Ubungo na Kanda ya Pwani kusimama nasi, pamoja na Meya wetu katika kipindi kigumu cha kudai demokrasia ya kweli ndani ya Nchi yetu.

Ninaahidi kuwa mstari wa mbele kutetea wananchi na kuhakikisha haki zao zinapatikana.

Ni jukumu letu sote kuhakikisha "udikteta ulioanza kuingia nchini taratibu," unatokomezwa.

Taifa hili siyo mali ya CCM. Ni letu sote.

*Saed Kubenea*
Mbunge wa Ubungo, M/M- Kanda ya Pwani.

Kwani utaratibu uko vipi?
 
ushanga

JF-Expert Member
Jan 5, 2017
457
250
Hawa mbwa ccm wanaendelea na figisu zao za tangu miaka 50 ambazo zimepitw na wkt...

Yaani huyu ng'ombe from chattle yeye wachawi wa nchi hii ni wapinzani wkt ccm walipitisha kila kitu
Ss kwa kweli hta km ungekuwe ndio unaitwa mbwa huu ndio upizani huu mbona hamuweki wzi sbb za kkamatwa kwake zai ya maneno ya kashif kma hya kuweni wastarabu jeuri haiwasaidii ktu
 
Mbulu

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
5,449
2,000
Mungu hawezi kutusaidia kabisa kwa ujinga tunaouendekeza,jamaa washatuona mazuzu sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom