Tamko la kamati ya madaktari baada ya serikali kutoa taarifa ya mgomo bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la kamati ya madaktari baada ya serikali kutoa taarifa ya mgomo bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by asakuta same, Feb 3, 2012.

 1. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  TAARIFA YA KAMATI YA MUDA YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI KUFUATIA TAMKO LA BUNGE (ILIYOTOLEWA LEO KWENYE VYOMBO VYA HABARI);
  Baada ya taarifa ya bunge kuwasilishwa leo ijumaa, kamati ya madaktari inaazimia haya yafuatayo;
  • Kamati inalishukuru bunge la jamhuri ya muungano kupitia mwongozo wa spika kwa kuiagiza kamati ya kudumu ya huduma za jamii kuanza kazi mara moja ya kukutana na jumuiya madaktari.
  • Kamati pamoja na jumuiya ya madaktari ipo tayari kukutana na kamati ya huduma za jamii.
  • Kwa kuwa suala hili ni la umuhimu na dharura kubwa, Mkutano wa jumuiya ya madaktari unatarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 04/02/2012 kuanzia saa 4 asubuhi.
  • Kamati inasikitika kuwa kauli ya waziri wa afya iliyotolewa bungeni ilijaa upotoshaji mkubwa kwa jamii na wabunge na kwa kuwa busara za naibu spika zilitoa ufafanuzi kuwa kauli hiyo ni ya upande mmoja na wangependa kusikia kutoka kwa madaktari lakini kanuni haziruhusu,kamati imeona kuwa ni muhimu kufafanua baadhi ya masuala yaliyopotoshwa na ambayo hayajatolewa ufafanuzi wowote;
  1. Si kweli kuwa huduma zinaendelea kama kawaida katika hospitali tajwa,kwa mfano KCMC taarifa za jana zinaonyesha kuwa hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kusitisha huduma zote kasoro huduma ya magonjwa ya ngozi ,hali hiyo ililazimu Askofu mkuu wa KKKT kufika hospitalini hapo kuwasihi madaktari,jambo ambalo lilishindwa kutatua tatizo. Propaganda za waziri ni msiba mkubwa kwa taifa.
  2. Si kweli kuwa madaktari bingwa walikataa kwenda mikoani,taarifa ya kweli ni kuwa taratibu hazikufuatwa kabisa,badala yake kejeli na ubabe ulitumika huku madaktari bingwa wengi kati yao wakihamishwa kupitia magazetini. Mfano upo wa madaktari ambao walienda kuripoti mikoani wakasumbuliwa na kuzungushwa kupewa masurufu ya safari,hospitali ya mkoa ikimuelekeza kuwa jukumu hilo ni la wizara na wakati huo huo wakienda wizarani wanaambiwa jukumu hilo ni la mikoa.
  3. Mojawapo ya madai ya madaktari ni suala la uboreshaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira ya kazi, waziri amelikwepa na kupoteza muda wa wananchi kuzungumzia propaganda zisizo na tija.
  4. Suala la bima ya afya kwa watumishi wa afya hajatolea tamko lolote.
  5. Suala la uwajibishwaji wa watendaji wa wizara ya afya akiwemo yeye, amelikwepa kabisa.
  6. Serikali inazungumzia na kutoa ahadi siku zote bungeni kuwa inapeleka watumishi wa afya wilayani na vijijini lakini Mh Waziri akifahamu kuwa dai mojawapo la madaktari ni kuomba serikali iingize posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa afya wanaopelekwa maeneo ya mazingira magumu mojawapo ikiwa mikoa ya pembezoni mfano ni Rukwa anapotokea waziri mkuu, hili hajalitolea tamko wala kulizungumzia kabisa.
  7. Bw Waziri ametumia muda mrefu kupiga propaganda za mshahara badala ya kusema wao wanatoa ofa gani ili tuelekee kwenye meza ya mazungumzo.

  • Mwisho kabisa , jumuiya ya madaktari inaona kuwa serikali haina nia ya dhati kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.
   
 2. m

  mwana wa africa JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  silaha ya wanyonge ni umoja. tafuteni hakizenu kwa gharama zozote!
   
 3. b

  busar JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hivi jukumu la kusimamia afya ya watz ni la Drs? Au serikali inayoongozwa na ccm?
   
 4. c

  chayowa1981 JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  TAARIFA YA KAMATI YA MUDA YA KUSHUGHULIKIA MADAI YA MADAKTARI KUFUATIA TAMKO LA BUNGE (ILIYOTOLEWA LEO KWENYE VYOMBO VYA HABARI);
  Baada ya taarifa ya bunge kuwasilishwa leo ijumaa, kamati ya madaktari inaazimia haya yafuatayo;
  • Kamati inalishukuru bunge la jamhuri ya muungano kupitia mwongozo wa spika kwa kuiagiza kamati ya kudumu ya huduma za jamii kuanza kazi mara moja ya kukutana na jumui...ya madaktari.
  • Kamati pamoja na jumuiya ya madaktari ipo tayari kukutana na kamati ya huduma za jamii.
  • Kwa kuwa suala hili ni la umuhimu na dharura kubwa, Mkutano wa jumuiya ya madaktari unatarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 04/02/2012 kuanzia saa 4 asubuhi.
  • Kamati inasikitika kuwa kauli ya waziri wa afya iliyotolewa bungeni ilijaa upotoshaji mkubwa kwa jamii na wabunge na kwa kuwa busara za naibu spika zilitoa ufafanuzi kuwa kauli hiyo ni ya upande mmoja na wangependa kusikia kutoka kwa madaktari lakini kanuni haziruhusu,kamati imeona kuwa ni muhimu kufafanua baadhi ya masuala yaliyopotoshwa na ambayo hayajatolewa ufafanuzi wowote;
  1. Si kweli kuwa huduma zinaendelea kama kawaida katika hospitali tajwa,kwa mfano KCMC taarifa za jana zinaonyesha kuwa hali ilikuwa mbaya sana kiasi cha kusitisha huduma zote kasoro huduma ya magonjwa ya ngozi ,hali hiyo ililazimu Askofu mkuu wa KKKT kufika hospitalini hapo kuwasihi madaktari,jambo ambalo lilishindwa kutatua tatizo. Propaganda za waziri ni msiba mkubwa kwa taifa.
  2. Si kweli kuwa madaktari bingwa walikataa kwenda mikoani,taarifa ya kweli ni kuwa taratibu hazikufuatwa kabisa,badala yake kejeli na ubabe ulitumika huku madaktari bingwa wengi kati yao wakihamishwa kupitia magazetini. Mfano upo wa madaktari ambao walienda kuripoti mikoani wakasumbuliwa na kuzungushwa kupewa masurufu ya safari,hospitali ya mkoa ikimuelekeza kuwa jukumu hilo ni la wizara na wakati huo huo wakienda wizarani wanaambiwa jukumu hilo ni la mikoa.
  3. Mojawapo ya madai ya madaktari ni suala la uboreshaji wa huduma kwa wagonjwa na mazingira ya kazi, waziri amelikwepa na kupoteza muda wa wananchi kuzungumzia propaganda zisizo na tija.
  4. Suala la bima ya afya kwa watumishi wa afya hajatolea tamko lolote.
  5. Suala la uwajibishwaji wa watendaji wa wizara ya afya akiwemo yeye, amelikwepa kabisa.
  6. Serikali inazungumzia na kutoa ahadi siku zote bungeni kuwa inapeleka watumishi wa afya wilayani na vijijini lakini Mh Waziri akifahamu kuwa dai mojawapo la madaktari ni kuomba serikali iingize posho ya mazingira magumu kwa watumishi wa afya wanaopelekwa maeneo ya mazingira magumu mojawapo ikiwa mikoa ya pembezoni mfano ni Rukwa anapotokea waziri mkuu, hili hajalitolea tamko wala kulizungumzia kabisa.
  7. Bw Waziri ametumia muda mrefu kupiga propaganda za mshahara badala ya kusema wao wanatoa ofa gani ili tuelekee kwenye meza ya mazungumzo.

  • Mwisho kabisa , jumuiya ya madaktari inaona kuwa serikali haina nia ya dhati kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.
   
 5. U

  UNIQUE Senior Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Madaktari kanyaga twende hapa kinachotakiwa ni fedha siyo maneno. Rate, bei. Mmekoswa kukatwa shingo kwa kufukuzwa sasa na nyinyi msiwaonee huruma. Wenyewe wanapiga hela ndefu halafu wanaleta maneno ya kitoto. Lazima mlipwe
   
 6. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  namshukuru sana Ndugai, he has been a really gentleman today!
   
 7. Mbutunanga

  Mbutunanga Senior Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 183
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimejua leo kuwa mheshimiwa Lema alikuwa sahihi alivyosema Pinda alidanganya. Leo tena mponda kadanganya, at least yeye alikuwa anatetemeka maana alijua alichokuwa anafanya.

  Hivi ni kweli serikali na inteligensia yake yote haioni aibu kupaza sauti kubwa na kusema Steven Ulimboka si daktari? Mponda naweza elewa maana alishindwa kumtofautisha intern doctor na mwanafunzi wa mwaka wa tano, na leo anaonyesha kuwa hajui kuwa ukishagraduate degree ya udaktari hauwezi kufutiwa ingawa unaweza usifanye kazi ya udaktari.! Tehe
   
 8. tonnyalmeida

  tonnyalmeida JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madaktari kazeni kamba hawa watawala wasioweza kufikiri watanyooka tu?.

  haijalishi ulimboka ni daktari au la, serikali inapaswa kutoa majibu ya hoja za msingi za wtaalamu wetu.
  hivi propaganda zitawafikisha wapi? unaposema hali ni shwari unamdanganya nani wakati wananchi ndo tunaokwenda mahospitalini tunaona?
  SHAME ON YOU MPONDAJI..
   
 9. vimon

  vimon Senior Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  mponda kapotea
   
 10. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Masaburi tupu R.I.P Mponda Utapondwa wewe sasa!
   
 11. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hivi huyo mizengo akiugua ataenda kutibiwa wapi!
   
 12. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Madaktari komaeni kwani kwa kufanya hivyo hakuna mtakachopoteza isipokua ni minyororo mliyofungwa siku nyingi

  kama kufa tulisha uliwa siku nyingi na serikali ya CCM,
   
 13. CR wa PROB

  CR wa PROB Senior Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ebwanae wadau hv yale madudu yaliyoelezwa na Mponda kuhusu Dk Stevene Ulimboka yana ukweli ndani yake???? na kama kweli huyu jamaa sio daktari iatakuwaje hawa madaktari wampe kuongoza harakati kama zile??? HONGERENI SANA MADAKTARI WETU KWA KUITIKISA SERIKALI, ENDELEENI HIVYO HIVYO kwani hii nchi imekuwa kama KA**** LAND,
   
 14. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  India. Mkuu umesahau?
   
 15. chubulunge

  chubulunge Senior Member

  #15
  Feb 4, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kitaelewaka tu
   
 16. Kabakabana

  Kabakabana JF-Expert Member

  #16
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 5,559
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  atakuwa alisahau
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Feb 4, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndugai ni mtu anayefikiria ndani na nje ya ccm isipokuwa kwenye posho alijisahau kidgo
   
 18. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #18
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kapota ama kapotoshwa? Yale sio ya kwake aliandikiwa akasoma tu. Yaani hata yeye ukimuuliza ukweli anaujua ila nasikitika sana linapokuja suala la kitaalamu watu wanafanya kisiasa zaidi bila kujali utaalamu zaidi. Hivi Dr Mponda ni daktari wa magonjwa ya binadamu ama ni wale madoctor wengine. Nafikiri kama ana taaluma kama ya hawa walogoma basi angekuwa hata anaujua wimbo wanaouimba! Yaani yeye keshajitenga as if hawajui kabisa! Sijui asipochaguliwa tena kuwa waziri atarudia kazi yake ya utabibu ama ataendelea na nini!
   
 19. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #19
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kaza buti ulimboka udaktiri wako hautaondolewa kwa propaganga na maneno ya wanasiasa maana wakati unakoomaa muhimbili na kupata mnyonyo wa internal medicine mponda hakuwepo na wal a hajui thamani yako .madaktari tumekuamini na tukakuchagua utuongoze.keep it up.
   
 20. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #20
  Feb 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Kesho Jakaya atalalamika lalamika sana juu ya swala hili huko mwanza kwenye
  kusanyiko la ccm
   
Loading...