EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Jakaya Mrisho KikweteAibu tupu...... Wanajamvi hembu nijuzeni Ni wajumbe wangapi au ni akina nani ni Wajumbe wa CC ya CCM na pia ni Mawaziri ktk Serikali hii ya Sasa?
Jakaya Mrisho KikweteAibu tupu...... Wanajamvi hembu nijuzeni Ni wajumbe wangapi au ni akina nani ni Wajumbe wa CC ya CCM na pia ni Mawaziri ktk Serikali hii ya Sasa?
Hapa sasa ndo kifo cha magamba make Nape ajiandae kujibu maswali magumu juu ya mapacha wa3,huyu Vasco kweli ni 'changanya za kwako',sasa balaza la mawazili ni ccm tupu walipokaa wakaona mafuta ya taa yapande bei,leo kwenye cc anawaongoza wenzie waseme mafuta ya taa yashushwe bei,sasa sijuhi huku alimwogopa nani kubadilika hivi ama anaonesha uzuzu wa cabinet yake kwamba hawakumshauri rais wao?
a contradicting decision,na ndo maana hata mawaziri wake hawamwelewi kwa maana anakaa nao wanaelewana hivi alafu akienda huku anaongea vinginevyo,kumbe yeye ndo chanzo namba1 cha serikali yake kupwaya hivi na hata kama ni hujuma yeye ndo anajihumu,maamuzi ya hivi nayakumbuka kama ile ishu ya bomoabomoa pale Ubungo,uzinduzi hoteli pale Arusha n.k
Nalazimika kukiri kwamba kwa stairi hii si ajabu hii nchi yetu ikawa imeuzwa kiasi ambacho hatujajua na tukija kujua tutakuja kujuta na tutalia sana!
...Kweli haya sasa ni maigizo, Mhe. amepitisha bajeti na kukubali bei ya mafuta ya taa ipande akiwa kama mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, then huku akiwa kama mwenyekiti wa CC anasema hapana bei ya afuta ya taa ishushe tena anaiamuru serikali hiyo hiyo anayoongoza yeye!!
Only in TanzaniaYani kwenye kikao cha baraza la mawaziri wameamua mafuta ya pande bei, kwenye halmashauri ya magamba wanasema bei ishuke eti inamuumiza mtu wa chini, vikao vyote hvyo mwenyekiti mmoja. Hakika bora tz bora hata tungempa DOVUTWA tujue moja.
Hapo kwenye Black, huyo kwisha habari yake hana lolote. hapo kwenye red hao wameshakula ban ni washenzi sana, na kwenye blue huyo ndio umsahau kabisa maana ana gari mpya Nissan yeye sasa hivi kazi yake ni misele tu kwenye mitaa ya New York, USA.
Huyo namba 9 ni kama katoon huwa hata hajui kama yupo facebook au yupo JF, huyo namba 10 kuondoka kwa Makamba kwenye secretarit kumemuathiri sana maana hayupo kwenye payroll ya Nape. sasa hivi anafanya propaganda kwa kinyongo
Wana jf nisaidieni, kwenye nec kuna watu waliopo serikrini. Kwenye ccm kuna watu wliopo serikarini. Bungeni kuna watu waliopo serikarini. Sasa vikao vya juu magamba wanapo sema wataishauri serikari ipunguze bei ya mafuta ya taa na kusolve tatizo la umeme, je hao walioamua hayo, je,baadhi yao si ndo hao hao wamo humo humo serikarini? Wakiwa huku wanaamua hivi na wakiwa kule wanaamua vile. Je si ndio wale wale kwenye serikari ile ile? Sasa wataishauri serikari ipi? Au wakati hayo yanaamriwa na wananchi wanalalamika masikio yao na macho yao yalikuwa yameziba?

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemaliza kikao chake cha siku moja usiku wa tarehe 31/07/2011 mjini Dodoma chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeamua yafuatayo;

1. Imefanya uteuzi wa makatibu ishirini na saba (27) kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika wilaya hizo. (majina na wilaya zao yameambatanishwa). Pamoja na uteuzi huo, Kamati Kuu imetengua uteuzi wa Makatibu wa Wilaya watatu (3) katika kuboresha ufanisi wa kazi katika wilaya hizo.(majina na wilaya zao yameambatanishwa).

2. Kamati Kuu imepokea na kuridhia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kuwakilisha Mkoa wa Tabora, Ndugu Rostam Aziz. Aidha imempongeza kwa uamuzi huo uliozingatia maslahi mapana ya chama chake.

3. Kamati Kuu imepokea pia taarifa ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Ndugu Rostam Aziz na kuagiza chama kupanga ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga itakayozingatia ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uteuzi wa mgombea. Aidha Kamati Kuu imeagiza shughuli zote za kampeni kutafanywa na CCM Mkoa, Wilaya na ngazi zote za chama wilayani Igunga. CCM Taifa watashiriki kuongeza nguvu. Chama kinatoa wito kwa wana CCM, wapenzi na wakereketwa wa chama chetu kushiriki kwa pamoja kuhakikisha jimbo linabaki kwa CCM.

4. Kamati Kuu haijaridhishwa na kiwango cha bei ya mafuta ya taa nchini kwa kuwa ndio nishati inayotumiwa na wananchi wengi wenye kipato cha chini. Aidha Kamati Kuu haikuridhishwa na maelezo ya kupandishwa kwa bei ya mafuta hayo kwa kisingizo cha kuzuia uchakachuaji wa mafuta mengine.  Hivyo basi, Kamati Kuu imeiagiza Serikali kutafuta njia za kushusha bei ya mafuta ya taa na kuvitaka vyombo vya Serikali vinavyohusika na usimamiaji wa ubora wa mafuta, vihakikishe vinatimiza wajibu wake kuzuia kabisa mtindo wa uchakachuaji wa mafuta nchini na si kupandisha bei ya mafuta ya taa kama suluhisho.

5. Kamati Kuu inasikitishwa na tatizo la umeme nchini kwani athari zake kwa uchumi wa Taifa na mtu mmoja mmoja ni kubwa. Hivyo basi imeitaka Serikali kutumia muda iliyopewa wa kurekebisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kuja na mpango wa dharura wa kunusuru hali hii na kisha kulimaliza kabisa tatizo la umeme nchini.

6. Aidha Kamati Kuu imejadili masuala mengine kama; migogoro ya ardhi, tatizo la bei ya pamba, tatizo la uuzaji wa mahindi, migogoro migodini, masuala yanayohusu kero za Muungano na kuagiza Serikali kuyashughulikia kwani yanatatulika.

7. Kamati Kuu imeipongeza Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kazi nzuri ya kutekeleza maamuzi ya NEC na kuitaka iongeze kasi katika utekelezaji huo, ili kuhakikisha mageuzi yaliyokusudiwa yanatekelezwa kwa wakati. Aidha imejadili na kupitisha miundo mipya ya Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

8. Kuhusu suala la maadili ndani ya Chama, Chama kinaendelea kusimamia maadili, na kuwataka wale waliotakiwa kujipima na kuwajibika watumie muda huo, kujipima na kuwajibika kwa masilahi mapana ya chama. Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi Septemba, ambapo pamoja na mambo mengine itatathimini utekelezaji wa maamuzi yake.  Imetolewa na:-

Nape M. Nnauye (MNEC)

KATIBU WA NEC, ITIKADI NA UENEZI

DODOMA

1/8/2011