Tamko la Kamati Kuu ya CCM kuhusu DOWANS na hali ya kisiasa nchini

Taarifa ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi

CCM1-1.JPG


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ilikutana jana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Katika kikao hicho Kamati Kuu ilijadili na kutolea maamuzi kuhusu masuala mbalimbali kama ifuatavyo:-

1. SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA CCM KUTIMIZA MIAKA 34

Kamati Kuu imejadili na kupitisha ratiba ya Sherehe za CCM kutimiza miaka 34 ambazo Kitaifa sherehe za Uzinduzi zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 1/2/2011 na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Mhe. Aman A. Karume na kilele cha maadhimisho Kitaifa yatafanyika Dodoma ambako Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni rasmi. Kila Mkoa na Wilaya wataandaa ratiba zao kulingana na mazingira ya maeneo yao. Katika wiki hiyo ya sherehe wana CCM na wanachama wa Jumuiya za Chama watafanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Uwakilishi na Madiwani.

Aidha sherehe hizi zitatumiwa kufanya mikutano ya Matawi na Kata kufanya tathmini kuhusu Uchaguzi uliopita na kuweka mikakati ya kujiandaa kwa Uchaguzi ujao.

Sherehe hizi pia zitaambatana na Matembezi ya Mshikamano yatakayofanywa nchi nzima asubuhi ya siku ya kilele, yaani tarehe 5/2/2011; haya ni matembezi yanayofanywa kila mwaka wakati wa sherehe hizi ili kudumisha umoja na mshikamano ndani ya chama na nchi kwa jumla; pia huwa ni fursa kwa wana CCM kuchangia Chama chao.






2. VURUGU KATIKA MANISPAA YA ARUSHA

Kamati Kuu imesikitishwa na tukio la vurugu za kisiasa zilizotokea tarehe 5 Januari, mwaka huu katika Manispaa ya Arusha ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa pamoja na uharibifu mali. Kamati Kuu inawapa pole waliofiwa, waliojeruhiwa na wale ambao mali zao ziliharibiwa. Aidha ni matumaini ya Kamati Kuu kwamba tukio hili halitarudiwa tena hapa nchini kwani lengo letu sote ni kudumisha amani na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao. Kuhusu maandamano yaliyozuiwa na Jeshi la Polisi lakini baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakachochea yafanyike na hatimaye kusababisha wananchi kupoteza maisha yao, na wengine kujeruhiwa na uharibifu wa mali, kwa vile suala hili sasa lipo Mahakamani Kamati Kuu haitapenda kulizungumzia kwa undani. Imetoa angalizo kwa viongozi wa siasa wa vyama vyote kuwa wajibu wao wa kwanza ni kulinda amani na utulivu, na kujiepusha kabisa na uchochezi wenye kuleta chuki na ubabe wa kutunishana misuli na vyombo vya dola ambavyo ndiyo muhimili wa ulinzi na usalama wa nchi yetu na wananchi wote na mali zao.

3. UCHAGUZI WA MEYA MANISPAA YA ARUSHA
Kwa kuzingatia kwamba umekuwepo upotoshaji mkubwa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, na hata kusababisha malalamiko mengi na vurugu, Kamati Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-

Kwanza:
· Matokeo ya Udiwani Manispaa ya Arusha yalikuwa ifuatavyo: Madiwani wa Kata: CCM 10, CHADEMA 8 na TLP 1 – Jumla viti 19.
· Madiwani Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
· Wabunge Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.

Matokeo ya jumla: CCM – Viti 16, CHADEMA 14 na TLP 1. Jumla Viti 31.

Pili:

Siku ya kupiga kura (tarehe 18/12/2010) Mkutano ulipoanza wajumbe 14 wa CHADEMA hawakuwepo. Waliofika ni wajumbe 16 wa CCM na 1 wa TLP, jumla wajumbe 17 ambao ni zaidi ya nusu ya wajumbe wanaotakiwa ili mkutano uwe halali kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira haya Msimamizi wa Uchaguzi aliendesha uchaguzi ambapo Ndugu Gaudence Vicent Lyimo wa CCM alipata kura 17, hivyo kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Umeya na Ndugu Michael Kivuyo wa TLP alipata kura 17 na kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Naibu Meya.

Kwa hiyo wanaosema uchaguzi huo haukuwa halali ama hawajui sheria au wanajiingiza tu katika ushabiki wa kisiasa.


Tatu:

CHADEMA wanadai katika wale wajumbe 16 wa CCM, mmoja wao (Mhe. Mary Chatanda) hakuwa mjumbe halali kwa kuwa katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum aligombea kupitia Mkoa wa Tanga.

CHADEMA, kupitia Msimamizi wa Uchaguzi waliomba ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume ya Uchaguzi, Katibu wa Bunge na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Ofisi zote hizo tatu zilitoa jibu kwamba Mhe. Mary Chatanda alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, na kwamba Wabunge Viti Maalum ni Wabunge wa Kitaifa na vyama vyao ndivyo vinawapangia Halmashauri za kufanyia kazi. Mhe. Mary Chatanda anaishi Arusha akifanyakazi kama Katibu wa CCM wa Mkoa huo hivyo CCM ilimpangia hapo hapo Arusha ndipo afanyie kazi za Halmashauri kama Diwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliarifiwa kuhusu uamuzi huu kama sheria inavyotaka.

Ni ufafanuzi huo huo ndio CHADEMA waliutumia kushinda kiti cha Halmashauri ya Hai baada ya kuwapangia kufanyakazi katika Halmashauri hiyo Wabunge 2 wa Viti Maalum na ambao si wakaazi wa Wilaya hiyo. Kura hizo mbili ndizo ziliwapa CHADEMA ushindi; na CCM tumekubali matokeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo CHADEMA hawakuvunja sheria.

Uhalali wa Mhe. Mary Chatanda kupiga kura Manispaa ya Arusha ni sawa sawa na uhalali wa Wabunge wawili wa Viti Maalum wa CHADEMA walivyopiga kura Hai.

Jambo hili CHADEMA wanalijua vizuri lakini wanapotosha umma kwa makusudi wakitumia vyombo vya habari ambavyo bila kufanya utafiti navyo vimekuwa vinashabikia suala hili.

Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.

4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.

5. MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU

Kamati Kuu imejadili hali inayojitokeza ya migomo ya wanavyuo na Wahadhiri katika vyuo mbali mbali kwa madai ya mikopo, na Wahadhiri kupunjwa mishahara. Kamati Kuu imeitaka Serikali ifuatilie kwa karibu sana madai ya Wanavyuo na Wahadhiri na yale matatizo ya dhati hatua za haraka zichukuliwe kuyapatia ufumbuzi ili wanavyuo na wakufunzi watumie muda wao madarasani na sio barabarani kwenye maandamano.

6. SEMINA YA WABUNGE WA CCM

Kwa kuzingatia maelekezo ya Kamati Kuu, CCM imeaandaa semina ya siku 3 ya Wabunge wake wote 260 itakayoanza tarehe 22 hadi 24/1/2011. Semina itafanyika Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, na itafunguliwa na Mhe. Mizengo Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu; na itafungwa na Mwenyekiti wa Chama Dkt. Jakaya M. Kikwete.

Mada kuu zitakazojadiliwa ni kuhusu Wajibu wa Ubunge na pia kuhusu Kanuni za Bunge. Kwa kuwa karibu asilimia 60% ya Wabunge wa CCM ni wapya, semina hii ina lengo la kuwapa uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya Ubunge.

7. MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika uliofanyika mjini Luanda, Angola tarehe 7-10 Desemba 2010 Vyama hivyo ni: ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), MPLA (Angola), ZANU-PF (Zimbabwe) na CCM (Tanzania). Kamati Kuu imeyapokea mapendekezo yote yaliyotolewa na Makatibu hao ambayo baadaye yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kimkakati wa vyama vilivyoongoza mapambano ya kudai uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na uwepo wa haja ya kukusanya, kuratibu na kuhifadhi historia ya harakati za ukombozi ili kutunza vizuri urithi wa historia ya ukombozi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na:-


Capt (Mst) John Z. Chiligati (Mb.),


KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA


ITIKADI NA UENEZI


21/01/2011




Kimsingi wanaheshimu maamuzi ya ICC.Lakini wanasubiri uamuzi wa mahakama kuu juu ya pingamizi la wanaharakati.
Kwa mengineyo bofya www.ccmtz.org

Wajumbe wa Chadema hawakuwepo kwa sababu gani?Kamati kuu halikujiuliza swali hili?
Maelezo kuwa mahudhurio ya zaidi ya nusu ya wajumbe yalikuwa yanahalalisha maamuzi ya kikao kisheria bila kueleza ni sheria ipi yanatusaidia nini? Waseme ni sheria ipi ili tupate mwanga.
 
Great thinkers bana - yaani mnashangaa saaaana as IF mlitegemea kitu kipya na tofauti kutoka kwa chama kinachoongozwa na Mkwere na Yusufu Makamba!

Majibu rahisi rahiiiiiiisi kwa issue za moto ndio motto ya CCM.

I just hope huu upuuzi ni wa CC ya CCM na sisi wananchi tunasubiri tamko rasmi la SERIKALI juu ya current burning issues i.e DOWANS, Mauaji ya kinyama ya Arusha, kupanda kwa gharama za umeme, jinsi gani mchakato wa Katiba mpya utaendeshwa to mention just a few.
 
Hawa wazee kinachowafanya wasijue kwamba swala la umeme ndo litakalo wachimbia kaburi nini??
Nishati ni kitu ambacho kinaumiza wananchi wa kila tabaka ...sasa kwa nini wanashindwa kufanya maamuzi?

Mimi siamini kama nchi yetu hatuna uwezo wa kujenga kituo kikubwa cha kufua umeme na kumaliza tatizo ambalo linaumiza wananchi na wawekezaji kiasi hichi.
Kikwete mbona hasomi alama za nyakati? Mbona mkapa yeye alifanya maamuzi makubwa tu na katuachia mambo mengi sana ya kujivunia na ambayo ni kumbukumbu bila blaa blaa kama huyu jamaa!!!
 
kwani ccm ndio waamuzi wa kura zirudiwe au la? Wao ni ccm na ni wapinzani wa Cdm . Ngoja tuone huyo Meya atafanyaje kazi

Nafikiri Meya amejiandaa kufanya kazi na madiwani 16 wanaomuunga mkono,hao wengine wa Chadema itabidi wasubiri mpaka 2015 uchaguzi mwingine utakapofanyika kama hakutakuwa na maandamano ya kumkimbiza JK Ikulu kabla ya mwaka huo.

Kwa uamuzi huu wa kamati kuu imeonyesha wazi kwamba Kamati kuu inakumbatia ufisadi na haijali sauti za watanzania kabisa kwa kweli chama kimeshika hatamu.Sasa suala ni moja tuu kuandamana mpaka serikali ya kifisadi isalimu amri hakuna kulala kama tunataka kuikomboa nchi yetu.
 
mbona hizo topic nyingine hazina breakdown kama hiyo ya kwanza?...mi nilikuwa nataka kuona vipengele vya dowans.
 
Hivi mimi naomba kuuliza maamuzi ya DOWANS ni maamuzi ya CCM au SERIKALI mbona mimi nachanganyikiwa. CCM wanaongea wao kama nani?? Swala la Dowans ni swala la taifa haijalishi chama gani sasa kwa nini CCM watoe maamuzi wao. Huu upumbavu utaisha lini. Wao kuandamana ruksa upinzani mwiko kwa vile wataleta vurugu. Haya tuone sasa leo mmetueleza ukweli wa mambo HAPA HALIPWI MTU KIKWETE NA WATU WAKO MSITUUDHI IKAWA BALAA. MMELOGWA NINYI WATU HUYU RA ATAWALIZA MUDA SI MREFU. Nachoka mie napatwa na kizunguzungu kupita maelezo. Kikwete Kikwete utakuja juta siku moja unajua yaliyopo mbele au ni kibri kwa kwenda mbele
 
Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.

4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.

Hapa kuna chenga ya mwili. Wanaretreat ili wawe na nguvu kubwa ya kujilipa. Wametuaminisha kuwa kosa ni la Tanesco ambayo siyo kweli, kama kuna kosa ni la serikali hii ni ili wasiwajibike. Wamedhihirisha lazima kulipa Dowans wanasubiri tu muda muafaka. Kwa sababu ya umuhimu wa kesi hii ningependekezwa iendeshwe live na TV stations watanzania wajue haki imetendeka
 
Great thinkers bana - yaani mnashangaa saaaana as IF mlitegemea kitu kipya na tofauti kutoka kwa chama kinachoongozwa na Mkwere na Yusufu Makamba!

Majibu rahisi rahiiiiiiisi kwa issue za moto ndio motto ya CCM.

I just hope huu upuuzi ni wa CC ya CCM na sisi wananchi tunasubiri tamko rasmi la SERIKALI juu ya current burning issues i.e DOWANS, Mauaji ya kinyama ya Arusha, kupanda kwa gharama za umeme, jinsi gani mchakato wa Katiba mpya utaendeshwa to mention just a few.

Serikali ni nini na CCM ni nini? Am not sure why unasubiri tamko!
 
Hawa viongozi wetu wana nishangaza kweli, wanalaani matokeo ya yalio sababishwa na maandamano, lakini wanabariki mambo ambayo yatasababisha maandamano na pengine maafa zaidi. Hivi inahitajika akili na busara gani ya ziada kuelewa kuwa kulipwa kwa hawa dowans kutasababisha maandamano na pengine macha fuko?
 
mbona hizo topic nyingine hazina breakdown kama hiyo ya kwanza?...mi nilikuwa nataka kuona vipengele vya dowans.

Vipengele vya Dowans ni utata, havielezeki kwa lugha nyepesi kwa sababu

  1. wahusika wa dowans ni wajumbe wa CC, sijui kama walitoka nje wakati hoja inajadiliwa
  2. Mkataba wa Dowans ulivunjwa ukiwa umebakisha miezi 3, wanaolielewa hili vizuri ni wajumbe humo cc
  3. Rex attorney walioshauri mkataba uvunjwe, ndo hao sasa wameshauri pesa ilipwe
  4. waliobariki dowans irithishwe mkataba wa Richmond baadhi ni wajumbe wa hiyo CC
Sasa watajadili hoja gani inayohusu Dowans ambayo labda walikuwa hawaijui
 
I just hope huu upuuzi ni wa CC ya CCM na sisi wananchi tunasubiri tamko rasmi la SERIKALI juu ya current burning issues i.e DOWANS, Mauaji ya kinyama ya Arusha, kupanda kwa gharama za umeme, jinsi gani mchakato wa Katiba mpya utaendeshwa to mention just a few.

Mbona na wewe unanifanya nipate mashaka, kwani kwa mawazo yako wewe serikali ni ya chama gani ili iweze kutofautiana na upuzi wa cc ya ccm?
 
Hapa nanusa mbinu ya kutaka mjadala wa dowans usianzishwe bungeni kwa kigezo Kua wanasubiri tamko la mahakama ya tz... Kwa mtindo huu kweli serikali inategemea mianya ya kutolipa kodi itazibika kweli? Au vita ya rushwa itafanikiwa?
 
There is something very wrong into that party, CCM. Ukisoma kwa makini tamko hili na lile la umoja wa vijana utagundua yafuatayo:

1. They are full of vague sentences andd generalization. Issues hazielezewi with specifics and objectively. No solutions provided it's just business as usual.

2. Uandishi wa hayo matamko ni so poor especially at a national level of a party as old as CCM. Kama mnakumbuka matamko ya enzi zile za chama kimoja pamoja na propaganda lakini yalikuwa yanaandikwa kiumahiri na kiuandishi haswaa.

3. The main topic ni CHADEMA, hayo mambo mengine wanababia babia tu. Mfano hilo la migomo ya vyuo vikuu wanashindwa nini kumuamuru Pinda ahakikishe say in 3 months madai ya wanafunzi na wakufunzi yanapatiwa suluhisho.

4. Wamelewa madaraka, in the same old way kwamba wao wakisema basi ndiyo mwisho. Wanashinddwa kuelewa kwamba kuna fikra mbadala na wananchi hawafurahishwi tu eti kwa kuwa raisi kasema, bali they need the facts.

5. JK hana weledi hata wa kuongoza chama chake, anachofanya ni mazoea tu.
 
Yaani hili suala la kiserikali, lakini serikali iliyopo madarakani badala ya kuitisha kikao cha baraza la mawaziri au kumtaka mwana sheria mkuu alipitie suala hili wao wanaona ni vyema kwenda kujadiliwa na Makamba and the group, suala lenyewe technical, yaani hapa ccm wamewatusi/wametutusi kweli kweli sisi wananchi na wataalamu wa mambo ya sheria
 
Mbona Ni rahisi tu kuelewa CCM imeamua ku- invest kwa kuiba kabla ya kuondoka madarakani. Ilianzia kwenye EPA tumewakurupusha, waliiba pale AirPort zilikuwa chache wamegundua kuiba kwa kuishitaki serikali yake yenyewe kama kiini macho walidhani Ni siri sasa Waungwana na wapendanchi wameiweka hadharani na bado Aluta Kontinua !!!!!!!
 
Nami nimeangalia hiyo meza na mwonekano wa ofisi nikaona vinafanana sana na pale Ikulu ambapo baraza la mawaziri hukutanika... Yaani kama mkutano haukufanyikia Lumumba CCM HQ na hapo kweli ni Ikulu, basi hii ni kashfa nyingine ya kujitakia!
Mwenyekiti wa CCM ni nani vile?
 
Then utawasikia wakisema Wa tz tunaongea saaaana, YEEEEESSS TUNAONGEA, TUTAONGEA, SANA NA TENA SANA, MAFISADI NYIE HATUWATAKI, TUTAPIGA
KELELE USIKU NA MCHANA, NA KUPAMBANA KWASBB MMETUIBIA KURA
SASA MNATUIBIA FEDHA ZETU WAZI WAZI kawaida ya mwizi haachi,
AHADI hewa during campaign mmesha sahau, sasa mnaongelea jinsi ya
kutuibia thru Dowans, ingekuwa nchi nyingine leo mngekuwa hell au mahakamani,
mantuumiza saaaana tena hamna huruma na nchi hii, wananchi fukara hata nyie
mmepita vijijini na helicopter 3, mioyo yenu wote VIPOFU, & the worst of all you have
deaf, no vision, no mission mind, mnaudhi CCM
 
hivi sisi em ilihusika na ukombozi wa nchi gani hadi iwekwe ktk level ya Frelimo and the co? TANU hatunayo tena na ndiyo iliyohusika! Hawa sisi em wengi wao ni wakoloni weusi!
 
Back
Top Bottom