Tamko la Kamati Kuu ya CCM kuhusu DOWANS na hali ya kisiasa nchini

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Taarifa ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi

CCM1-1.JPG

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ilikutana jana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Katika kikao hicho Kamati Kuu ilijadili na kutolea maamuzi kuhusu masuala mbalimbali kama ifuatavyo:-

1. SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA CCM KUTIMIZA MIAKA 34

Kamati Kuu imejadili na kupitisha ratiba ya Sherehe za CCM kutimiza miaka 34 ambazo Kitaifa sherehe za Uzinduzi zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 1/2/2011 na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Mhe. Aman A. Karume na kilele cha maadhimisho Kitaifa yatafanyika Dodoma ambako Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni rasmi. Kila Mkoa na Wilaya wataandaa ratiba zao kulingana na mazingira ya maeneo yao. Katika wiki hiyo ya sherehe wana CCM na wanachama wa Jumuiya za Chama watafanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Uwakilishi na Madiwani.

Aidha sherehe hizi zitatumiwa kufanya mikutano ya Matawi na Kata kufanya tathmini kuhusu Uchaguzi uliopita na kuweka mikakati ya kujiandaa kwa Uchaguzi ujao.

Sherehe hizi pia zitaambatana na Matembezi ya Mshikamano yatakayofanywa nchi nzima asubuhi ya siku ya kilele, yaani tarehe 5/2/2011; haya ni matembezi yanayofanywa kila mwaka wakati wa sherehe hizi ili kudumisha umoja na mshikamano ndani ya chama na nchi kwa jumla; pia huwa ni fursa kwa wana CCM kuchangia Chama chao.

2. VURUGU KATIKA MANISPAA YA ARUSHA

Kamati Kuu imesikitishwa na tukio la vurugu za kisiasa zilizotokea tarehe 5 Januari, mwaka huu katika Manispaa ya Arusha ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa pamoja na uharibifu mali. Kamati Kuu inawapa pole waliofiwa, waliojeruhiwa na wale ambao mali zao ziliharibiwa. Aidha ni matumaini ya Kamati Kuu kwamba tukio hili halitarudiwa tena hapa nchini kwani lengo letu sote ni kudumisha amani na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao. Kuhusu maandamano yaliyozuiwa na Jeshi la Polisi lakini baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakachochea yafanyike na hatimaye kusababisha wananchi kupoteza maisha yao, na wengine kujeruhiwa na uharibifu wa mali, kwa vile suala hili sasa lipo Mahakamani Kamati Kuu haitapenda kulizungumzia kwa undani. Imetoa angalizo kwa viongozi wa siasa wa vyama vyote kuwa wajibu wao wa kwanza ni kulinda amani na utulivu, na kujiepusha kabisa na uchochezi wenye kuleta chuki na ubabe wa kutunishana misuli na vyombo vya dola ambavyo ndiyo muhimili wa ulinzi na usalama wa nchi yetu na wananchi wote na mali zao.

3. UCHAGUZI WA MEYA MANISPAA YA ARUSHA
Kwa kuzingatia kwamba umekuwepo upotoshaji mkubwa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, na hata kusababisha malalamiko mengi na vurugu, Kamati Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-

Kwanza:
· Matokeo ya Udiwani Manispaa ya Arusha yalikuwa ifuatavyo: Madiwani wa Kata: CCM 10, CHADEMA 8 na TLP 1 – Jumla viti 19.
· Madiwani Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
· Wabunge Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.

Matokeo ya jumla: CCM – Viti 16, CHADEMA 14 na TLP 1. Jumla Viti 31.

Pili:

Siku ya kupiga kura (tarehe 18/12/2010) Mkutano ulipoanza wajumbe 14 wa CHADEMA hawakuwepo. Waliofika ni wajumbe 16 wa CCM na 1 wa TLP, jumla wajumbe 17 ambao ni zaidi ya nusu ya wajumbe wanaotakiwa ili mkutano uwe halali kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira haya Msimamizi wa Uchaguzi aliendesha uchaguzi ambapo Ndugu Gaudence Vicent Lyimo wa CCM alipata kura 17, hivyo kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Umeya na Ndugu Michael Kivuyo wa TLP alipata kura 17 na kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Naibu Meya.

Kwa hiyo wanaosema uchaguzi huo haukuwa halali ama hawajui sheria au wanajiingiza tu katika ushabiki wa kisiasa.

Tatu:

CHADEMA wanadai katika wale wajumbe 16 wa CCM, mmoja wao (Mhe. Mary Chatanda) hakuwa mjumbe halali kwa kuwa katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum aligombea kupitia Mkoa wa Tanga.

CHADEMA, kupitia Msimamizi wa Uchaguzi waliomba ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume ya Uchaguzi, Katibu wa Bunge na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Ofisi zote hizo tatu zilitoa jibu kwamba Mhe. Mary Chatanda alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, na kwamba Wabunge Viti Maalum ni Wabunge wa Kitaifa na vyama vyao ndivyo vinawapangia Halmashauri za kufanyia kazi. Mhe. Mary Chatanda anaishi Arusha akifanyakazi kama Katibu wa CCM wa Mkoa huo hivyo CCM ilimpangia hapo hapo Arusha ndipo afanyie kazi za Halmashauri kama Diwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliarifiwa kuhusu uamuzi huu kama sheria inavyotaka.

Ni ufafanuzi huo huo ndio CHADEMA waliutumia kushinda kiti cha Halmashauri ya Hai baada ya kuwapangia kufanyakazi katika Halmashauri hiyo Wabunge 2 wa Viti Maalum na ambao si wakaazi wa Wilaya hiyo. Kura hizo mbili ndizo ziliwapa CHADEMA ushindi; na CCM tumekubali matokeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo CHADEMA hawakuvunja sheria.

Uhalali wa Mhe. Mary Chatanda kupiga kura Manispaa ya Arusha ni sawa sawa na uhalali wa Wabunge wawili wa Viti Maalum wa CHADEMA walivyopiga kura Hai.

Jambo hili CHADEMA wanalijua vizuri lakini wanapotosha umma kwa makusudi wakitumia vyombo vya habari ambavyo bila kufanya utafiti navyo vimekuwa vinashabikia suala hili.

Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.

4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.

5. MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU

Kamati Kuu imejadili hali inayojitokeza ya migomo ya wanavyuo na Wahadhiri katika vyuo mbali mbali kwa madai ya mikopo, na Wahadhiri kupunjwa mishahara. Kamati Kuu imeitaka Serikali ifuatilie kwa karibu sana madai ya Wanavyuo na Wahadhiri na yale matatizo ya dhati hatua za haraka zichukuliwe kuyapatia ufumbuzi ili wanavyuo na wakufunzi watumie muda wao madarasani na sio barabarani kwenye maandamano.

6. SEMINA YA WABUNGE WA CCM

Kwa kuzingatia maelekezo ya Kamati Kuu, CCM imeaandaa semina ya siku 3 ya Wabunge wake wote 260 itakayoanza tarehe 22 hadi 24/1/2011. Semina itafanyika Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, na itafunguliwa na Mhe. Mizengo Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu; na itafungwa na Mwenyekiti wa Chama Dkt. Jakaya M. Kikwete.

Mada kuu zitakazojadiliwa ni kuhusu Wajibu wa Ubunge na pia kuhusu Kanuni za Bunge. Kwa kuwa karibu asilimia 60% ya Wabunge wa CCM ni wapya, semina hii ina lengo la kuwapa uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya Ubunge.

7. MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika uliofanyika mjini Luanda, Angola tarehe 7-10 Desemba 2010 Vyama hivyo ni: ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), MPLA (Angola), ZANU-PF (Zimbabwe) na CCM (Tanzania). Kamati Kuu imeyapokea mapendekezo yote yaliyotolewa na Makatibu hao ambayo baadaye yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kimkakati wa vyama vilivyoongoza mapambano ya kudai uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na uwepo wa haja ya kukusanya, kuratibu na kuhifadhi historia ya harakati za ukombozi ili kutunza vizuri urithi wa historia ya ukombozi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na:-

Capt (Mst) John Z. Chiligati (Mb.),

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

ITIKADI NA UENEZI

21/01/2011

Kimsingi wanaheshimu maamuzi ya ICC.Lakini wanasubiri uamuzi wa mahakama kuu juu ya pingamizi la wanaharakati.
Kwa mengineyo bofya www.ccmtz.org
 
Hakuna msingi wowote wao kama Chama Cha Majambazi waje wazi sio kutegemea nguzo za wengine. Hawawezi kutoa kauli ili waweze kuhesabiwa wakati ule wa kuhesabiwa walikuwa hawapati kigugumizi. Chama hiki sasa ni tambala bovu wamekuwa makuwadi wa RA na genge lake la wahuni likiongozwa na rais Mwizi.
 
Naona CCM wanakoelekea sasa ni kubaya zaidi yaani dowans kwao ni okey
 
Kwa nini CCM wanafanyia mikutano ya chama chao Ikulu ? Je ikulu ni mali ya CCM? Hivi kweli Obama anaweza kuendesha mkutano wa chama cha Democrat pale white house bila kuraruliwa na raia walipa kodi?
 
Mkubwa... nachelea kusema kama tuna ikulu nchi hii.... lile kwa sasa ni pango la wanyang'anyi tu!!!!
 
Kwa nini CCM wanafanyia mikutano ya chama chao Ikulu ? Je ikulu ni mali ya CCM? Hivi kweli Obama anaweza kuendesha mkutano wa chama cha Democrat pale white house bila kuraruliwa na raia walipa kodi?
Nami nimeangalia hiyo meza na mwonekano wa ofisi nikaona vinafanana sana na pale Ikulu ambapo baraza la mawaziri hukutanika... Yaani kama mkutano haukufanyikia Lumumba CCM HQ na hapo kweli ni Ikulu, basi hii ni kashfa nyingine ya kujitakia!
 
Taarifa ya Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi

CCM1-1.JPG

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ilikutana jana jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Katika kikao hicho Kamati Kuu ilijadili na kutolea maamuzi kuhusu masuala mbalimbali kama ifuatavyo:-

1. SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA CCM KUTIMIZA MIAKA 34

Kamati Kuu imejadili na kupitisha ratiba ya Sherehe za CCM kutimiza miaka 34 ambazo Kitaifa sherehe za Uzinduzi zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam tarehe 1/2/2011 na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Mhe. Aman A. Karume na kilele cha maadhimisho Kitaifa yatafanyika Dodoma ambako Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni rasmi. Kila Mkoa na Wilaya wataandaa ratiba zao kulingana na mazingira ya maeneo yao. Katika wiki hiyo ya sherehe wana CCM na wanachama wa Jumuiya za Chama watafanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi kwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika ngazi ya Urais wa Muungano, Urais wa Zanzibar, Ubunge, Uwakilishi na Madiwani.

Aidha sherehe hizi zitatumiwa kufanya mikutano ya Matawi na Kata kufanya tathmini kuhusu Uchaguzi uliopita na kuweka mikakati ya kujiandaa kwa Uchaguzi ujao.

Sherehe hizi pia zitaambatana na Matembezi ya Mshikamano yatakayofanywa nchi nzima asubuhi ya siku ya kilele, yaani tarehe 5/2/2011; haya ni matembezi yanayofanywa kila mwaka wakati wa sherehe hizi ili kudumisha umoja na mshikamano ndani ya chama na nchi kwa jumla; pia huwa ni fursa kwa wana CCM kuchangia Chama chao.

2. VURUGU KATIKA MANISPAA YA ARUSHA

Kamati Kuu imesikitishwa na tukio la vurugu za kisiasa zilizotokea tarehe 5 Januari, mwaka huu katika Manispaa ya Arusha ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa pamoja na uharibifu mali. Kamati Kuu inawapa pole waliofiwa, waliojeruhiwa na wale ambao mali zao ziliharibiwa. Aidha ni matumaini ya Kamati Kuu kwamba tukio hili halitarudiwa tena hapa nchini kwani lengo letu sote ni kudumisha amani na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao. Kuhusu maandamano yaliyozuiwa na Jeshi la Polisi lakini baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakachochea yafanyike na hatimaye kusababisha wananchi kupoteza maisha yao, na wengine kujeruhiwa na uharibifu wa mali, kwa vile suala hili sasa lipo Mahakamani Kamati Kuu haitapenda kulizungumzia kwa undani. Imetoa angalizo kwa viongozi wa siasa wa vyama vyote kuwa wajibu wao wa kwanza ni kulinda amani na utulivu, na kujiepusha kabisa na uchochezi wenye kuleta chuki na ubabe wa kutunishana misuli na vyombo vya dola ambavyo ndiyo muhimili wa ulinzi na usalama wa nchi yetu na wananchi wote na mali zao.

3. UCHAGUZI WA MEYA MANISPAA YA ARUSHA
Kwa kuzingatia kwamba umekuwepo upotoshaji mkubwa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha, na hata kusababisha malalamiko mengi na vurugu, Kamati Kuu inapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:-

Kwanza:
· Matokeo ya Udiwani Manispaa ya Arusha yalikuwa ifuatavyo: Madiwani wa Kata: CCM 10, CHADEMA 8 na TLP 1 – Jumla viti 19.
· Madiwani Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.
· Wabunge Viti Maalum: CCM 3, CHADEMA 3.

Matokeo ya jumla: CCM – Viti 16, CHADEMA 14 na TLP 1. Jumla Viti 31.

Pili:

Siku ya kupiga kura (tarehe 18/12/2010) Mkutano ulipoanza wajumbe 14 wa CHADEMA hawakuwepo. Waliofika ni wajumbe 16 wa CCM na 1 wa TLP, jumla wajumbe 17 ambao ni zaidi ya nusu ya wajumbe wanaotakiwa ili mkutano uwe halali kwa mujibu wa sheria.

Katika mazingira haya Msimamizi wa Uchaguzi aliendesha uchaguzi ambapo Ndugu Gaudence Vicent Lyimo wa CCM alipata kura 17, hivyo kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Umeya na Ndugu Michael Kivuyo wa TLP alipata kura 17 na kutangazwa mshindi halali wa kiti cha Naibu Meya.

Kwa hiyo wanaosema uchaguzi huo haukuwa halali ama hawajui sheria au wanajiingiza tu katika ushabiki wa kisiasa.

Tatu:

CHADEMA wanadai katika wale wajumbe 16 wa CCM, mmoja wao (Mhe. Mary Chatanda) hakuwa mjumbe halali kwa kuwa katika kugombea Ubunge wa Viti Maalum aligombea kupitia Mkoa wa Tanga.

CHADEMA, kupitia Msimamizi wa Uchaguzi waliomba ufafanuzi wa kisheria kutoka Tume ya Uchaguzi, Katibu wa Bunge na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Ofisi zote hizo tatu zilitoa jibu kwamba Mhe. Mary Chatanda alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, na kwamba Wabunge Viti Maalum ni Wabunge wa Kitaifa na vyama vyao ndivyo vinawapangia Halmashauri za kufanyia kazi. Mhe. Mary Chatanda anaishi Arusha akifanyakazi kama Katibu wa CCM wa Mkoa huo hivyo CCM ilimpangia hapo hapo Arusha ndipo afanyie kazi za Halmashauri kama Diwani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa iliarifiwa kuhusu uamuzi huu kama sheria inavyotaka.

Ni ufafanuzi huo huo ndio CHADEMA waliutumia kushinda kiti cha Halmashauri ya Hai baada ya kuwapangia kufanyakazi katika Halmashauri hiyo Wabunge 2 wa Viti Maalum na ambao si wakaazi wa Wilaya hiyo. Kura hizo mbili ndizo ziliwapa CHADEMA ushindi; na CCM tumekubali matokeo kwa kuwa kwa kufanya hivyo CHADEMA hawakuvunja sheria.

Uhalali wa Mhe. Mary Chatanda kupiga kura Manispaa ya Arusha ni sawa sawa na uhalali wa Wabunge wawili wa Viti Maalum wa CHADEMA walivyopiga kura Hai.

Jambo hili CHADEMA wanalijua vizuri lakini wanapotosha umma kwa makusudi wakitumia vyombo vya habari ambavyo bila kufanya utafiti navyo vimekuwa vinashabikia suala hili.

Kwa kifupi Kamati Kuu inasisitiza kwamba Uchaguzi wa Meya wa Arusha ulifuata sheria kwa ukamilifu, na washindi walishinda kihalali na hakuna sababu ya kurudia kufanya uchaguzi mwingine. Iwapo kuna watu hawaridhiki na mchakato wa uchaguzi huo wanayo nafasi ya kupinga katika vyombo vya sheria bila ya kufanya fujo wala kuleta uvunjifu wa amani kama ule uliotokea tarehe 5/1/2011 kule Arusha.

4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.

5. MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU

Kamati Kuu imejadili hali inayojitokeza ya migomo ya wanavyuo na Wahadhiri katika vyuo mbali mbali kwa madai ya mikopo, na Wahadhiri kupunjwa mishahara. Kamati Kuu imeitaka Serikali ifuatilie kwa karibu sana madai ya Wanavyuo na Wahadhiri na yale matatizo ya dhati hatua za haraka zichukuliwe kuyapatia ufumbuzi ili wanavyuo na wakufunzi watumie muda wao madarasani na sio barabarani kwenye maandamano.

6. SEMINA YA WABUNGE WA CCM

Kwa kuzingatia maelekezo ya Kamati Kuu, CCM imeaandaa semina ya siku 3 ya Wabunge wake wote 260 itakayoanza tarehe 22 hadi 24/1/2011. Semina itafanyika Dar es Salaam katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, na itafunguliwa na Mhe. Mizengo Pinda (Mb.) - Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu; na itafungwa na Mwenyekiti wa Chama Dkt. Jakaya M. Kikwete.

Mada kuu zitakazojadiliwa ni kuhusu Wajibu wa Ubunge na pia kuhusu Kanuni za Bunge. Kwa kuwa karibu asilimia 60% ya Wabunge wa CCM ni wapya, semina hii ina lengo la kuwapa uelewa mpana kuhusu majukumu yao ya Ubunge.

7. MKUTANO WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Kamati Kuu ilipokea na kujadili taarifa ya Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika uliofanyika mjini Luanda, Angola tarehe 7-10 Desemba 2010 Vyama hivyo ni: ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), MPLA (Angola), ZANU-PF (Zimbabwe) na CCM (Tanzania). Kamati Kuu imeyapokea mapendekezo yote yaliyotolewa na Makatibu hao ambayo baadaye yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kimkakati wa vyama vilivyoongoza mapambano ya kudai uhuru katika nchi za Kusini mwa Afrika pamoja na uwepo wa haja ya kukusanya, kuratibu na kuhifadhi historia ya harakati za ukombozi ili kutunza vizuri urithi wa historia ya ukombozi kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na:-

Capt (Mst) John Z. Chiligati (Mb.),

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

ITIKADI NA UENEZI

21/01/2011

Kimsingi wanaheshimu maamuzi ya ICC.Lakini wanasubiri uamuzi wa mahakama kuu juu ya pingamizi la wanaharakati.
Kwa mengineyo bofya www.ccmtz.org

Inaonekana CCM wana kiburi sana, hizi taarifa wapeane kwenye chama chao. Wananchi wa Tanzania wanategemea Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa tamko kuhusu Vurugu za Arusha , malipo kwa Dowans nk. mambo yao ya kichama wapeane huko huko kwao. Serikali inafanya makosa kwa kutegemea Wanaharakati kufanya kazi ambayo wametumwa na wananchi, hivi wanafahamu maana ya Serikali kweli au ni kanyaga twende tu?
 
4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.
hapa ndipo wametuthibitishia kumbe CC ya CCM ndiyo wamiliki halali wa DOWANS...................................hivi malipo ya wastaafu wa Afrika mashariki ambayo yana sheria ya Bunge mbona majibu mepesi kama ya DOWANS CC ya CCM haiyatoi????????????????????????????????????????????

Jibu ni kuwa wastaafu hao hawana cha kuwahonga............JK na timu yake ya mafisadi...........eti Tanesco walivunja mkataba........................Je waliouvunja mkataba mnawachukulia hatua gani?

Na mkataba upi waliuvunja wakati Richmond iliyorithi mkataba ni kampuni hewa????????????????????????

Only impeachment of Kikwete will end impunity and official graft in this country we all call home.....................
 
Mods thanks kwa kuiweka vizuri.technology ilinisumbua kidogo.
 
hili la kufanyia mikutano ya chama ikulu ni sawa na matumizi ya magari ya serikali wakati wa kampeni yaliyokemewa na msajili wa vyama vya siasa. nadhani sasa ni wakai mzuri wa kumwomba mh. tendwa akemee na hili pia.

halafu nimeona wameitisha maandamano ya mshikamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kuwashukuru wanachi kwa kukipigia kura chama. mikutano ya namna hiyo na maandamanano ya vyama vya upinzani yamepigwa marufuku mara kadhaa na jeshi la polisi likiwamo tukio la arusha la hivi karibuni kutokana na taarifa za kiintelijensia kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani. hivi haya ya ccm hakuna taarifa za kiintelijensia kama hizo? afande mwema yuko wapi afafanue hapa please.

ama kweli kutawala wanachi wapole kama watanzania raha sana!
 
Ukisoma maelezo haya kutoka hapo juu:

4. HUKUMU YA KUILIPA KAMPUNI YA DOWANS

Kamati Kuu imetafakari kwa makini suala la TANESCO kuilipa kampuni ya DOWANS Shs. 94 bn. na kubaini kuwa huu ni uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Biashara kwamba TANESCO ilivunja mkataba kinyume cha makubaliano na katika hali ya kawaida, kama hakuna njia nyingine ya kujiondoa kwenye kosa, ni busara na ni wajibu kwa muungwana [isomeke - wahujumu uchumi]kuheshimu maamuzi ya Mahakama. Hata hivyo, Kamati Kuu imeona kuwa kwa vile wapo Watanzania [wazalendo wa kweli] walioamua kupinga Mahakamani uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa TANESCO kuilipa DOWANS fidia ya Sh. bilioni 94, basi ni vema Serikali isubiri uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya pingamizi hili.

Tafadhali sana soma na maelezo yafuatayo kuhusiana na Rex Attorneys (Wanasheria wakubwa nchini wa Tanesco na Serikali):

Rex Attorneys ambayo ushauri wake umegeuka gharama kwa Taifa. Je, kampuni hii ilitoa ushauri usiongiliwa na maslahi ya pamoja kati ya wamiliki wa Dowans na kampuni husika?

Lakini pia ashinikize uchunguzi wa uhusiano kati ya kampuni hii na viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Waziri Mkuu iliyoipamba kampuni hiyo bungeni.

Ikumbukwe, kwa mara nyingine kampuni hii imefuatwa tena baada ya hukumu ya ICC ili kushauri kama Dowans ilipwe au la. Wameshauri ilipwe.

Ni kama vile kampuni hiyo mwanzo ilitoa ushauri wenye malengo ya kuandaa mazingira ya Dowans kushinda kesi na kulipwa.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari wiki iliyopita, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema; "Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO ilishauriwa na kampuni ya Rex Attorneys Advocates kukubaliana na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Usuluhishi bila kuipinga endapo itasajiliwa kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania."

Hapa, Rex Attorneys ndiyo iliyosifiwa na Waziri Mkuu bungeni, ikatoa ushauri wa kuvunja mkataba. Baada ya kuvunja mkataba, TANESCO ‘imehukumiwa' kulipa mabilioni.

Lakini baada ya hukumu kutoka, TANESCO imerudi kwa kampuni iliyotoa ushauri wa kuvunja mkataba, kampuni hiyo inashauri tena TANESCO ifanye malipo?!

Je, vigezo vya awali vya Rex Attorneys kushauri mkataba uvunjwe vimepotelea wapi hadi wakimbilie kushauri TANESCO ifanye malipo? Je, kuna uhusiano gani au kunaweza kuibuka uhusiano gani kati ya mabilioni itakayolipwa Dowans na kampuni hii ya kisheria? Je, kuna mgawo wa malipo hayo baadaye?

Kwa nini kampuni iliyoshauri kwa vigezo vya kisheria mkataba uvunjwe, baadaye igeuke ikipuuza vigezo hivyo na kutoa ushauri mpya wa kulipa mabilioni? Kwa mbunge makini bila shaka hapa kuna jambo la kuhoji.

Serikali kupitia TANESCO imevunja mkataba kwa ushauri wa kampuni hii, leo inakwenda kulipa faini kwa ushauri pia wa kampuni hii, je, kuna nini?
Kutoka thread hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ttorneys-ni-kashfa-kubwa-zaidi-ya-dowans.html
 
CCM1-1.JPG

Hii ndiyo timu ya walaji na wachakachuaji wa kura zetu sasa kujipongeza kwa kazi nzuri ya kuuchakachua mlo kupitia DOWANS lakini ninakuhakikishia future wikileaks zitatueleza JK alipata ngapi........................Rostam Aziz alipata mgao kiasi kipi..................
 
Back
Top Bottom