OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,339
WAKATI Mbunge wa Bahi, Omar Badwel anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kwa tuhuma za kupokea rushwa, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ameilipua Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) kuwa imekithiri kwa rushwa.
Kutokana na tuhuma hizo, Kafulila amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuvunja kamati hiyo, vinginevyo yeye atajiondoa.
Pia mbunge huyo ameitaka Kamati ya Maadili kulitumia Bunge kumvua ubunge, Badwel, kutokana na tuhuma za kupokea rushwa zinazomkabili.
Kafulila alisema hayo jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa, wananchi hawatakuwa na imani tena na kamati hiyo.
"Ikumbukwe Juni 13, 2011 nilieleza bungeni namna wabunge wa Kamati ya LAAC wanavyoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, huku nikimtaja kwa jina Mbunge wa Bahi, Omary Badwel kuwa ni miongoni mwao," alisema Kafulila ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo.
"Nilijitoa mhanga kwa kutaja majina ya wabunge wanaoomba rushwa kwa watumishi wa Serikali, lakini hatua hazikuchukuliwa, sasa leo Takukuru wamemtia mbaroni mmoja wao, bado hamuamini," alisema Kafulila.
"Sasa naomba niweke wazi kwamba kama Spika hataivunja kamati hii na kuunda nyingine nitajiondoa kwenye kamati kwa sababu itakuwa imepoteza imani kwa wananchi," alisema Kafulila.

TAMKO LA NDUGU DAVID KAFULILA KUHUSU MBUNGE WA JIMBO LA BAHI KUKAMATWA NA TAKUKURU KWA RUSHWA.
Kwanza niwashukuru ndugu zangu wanahabari kwa kuitikia wito wangu kukubali kuja kunisikiliza. Mtakuwa mmesikia na kusoma kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu taarifa ya aibu inayolikumba Bunge letu tukufu kufuatia taarifa kutoka vyombo vya dola kuwa mbunge mwenzetu kutoka jimbo la Bahi Ndugu Omary Badwel anashikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la jinai na la aibu sana la rushwa.JUNE 03, 2012
Ningependa kuwakumbusha wana habari kuwa nimepata kuzungumza Bungeni mwaka jana 2011 kuhusu tabia ovu kwa baadhi ya wabunge kuomba rushwa watumishi wa serikali katika mchakato wa kusimamia serikali. Ilikuwa ni Bunge la mwezi June, tarehe 13, 2011 wakati nikichangia hoja ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano. Hapa nilitoa taarifa iliyowahusu wabunge watatu akiwemo huyu anayeshikiliwa na vyombo vya dola sasa, Ndugu Omary Badwel. Kwakuwa hakuna hatua iliyochukuliwa, leo napenda niweke msimamo wangu wazi katika maeneo yafuatayo;
1. Kwakuwa nilijitahidi sana kwa kila namna kujenga heshima ya kamati hii ya LAAC bila kupewa ushirikiano toka kwa wadau wote, TAMISEMI pamoja na BUNGE, naomba kutamka rasmi kuwa sina imani tena na Kamati hii kwakuwa imepoteza uhalali kuweza kuendelea kuwa kamati ya kusimamia na kudhibiti hesabu za serikali.
2. Kwa kuzingatia hoja hiyo, Ni wajibu wa Spika kutafakari upya kuhusu hadhi ya Kamati hii na kuipanga upya kwa maslahi ya Umma, heshima na hadhi ya Bunge letu.
3. Nikiwa mjumbe wa Kamati ya Maadili ya Bunge, Na kwakuwa linayo mamlaka ya kumvua ubunge mbunge yeyote kwa azimio la Bunge, nitaiomba Kamati kushughulikia suala hili kibunge na kuhakikisha tunakwenda na azimio katika mkutano ujao wa Bunge kuhakikisha hatua stahiki zinachulikuwa kulinda heshima ya Bunge ili muhusika aendelee kuchukuliwa hatua za kijinai kama raia wa kawaida.
4. Kwakuwa suala hili linahusu heshima na hadhi ya Bunge, Ni muhimu Kamati ya Uongozi kuhakikisha suala hili linakuwa la kwanza katika ratiba za vikao vya mkutano ujao. Napenda kurudia kuwa, nilisema mwanzo na hakuna aliyechukua hatua. Hii ni mara ya mwisho na ninaahidi kutoendelea kushiriki tena vikao vya kamati hii ya aibu kama Mh. Spika hataona busara na umuhimu wa kuipangua kamati hii. Serikali legelege ni matokeo ya Bunge legelege kwakuwa ni kazi ya Bunge kusimamia na kuidhibiti serikali kikatiba. Watendaji wa serikali kujua bei za wabunge ni msiba.
…………………………………………
David Kafulila (MB).