Tamko la Jumuia la MAIMAMU Z'Bar kuhusu Uvunjaji wa Amani Vilivyotokea kwenye Jimbo la BUBUBU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la Jumuia la MAIMAMU Z'Bar kuhusu Uvunjaji wa Amani Vilivyotokea kwenye Jimbo la BUBUBU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 25, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]Monday, September 24, 2012[/h][h=3]JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR – JUMAZA[/h]


  Nd. Waislam,
  Nd. Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam.
  Nd. Waandishi wa habari.
  Assalaamu alaykum warahmatullaah,
  TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR KUHUSU VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU VILIVOTOKEA KATIKA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA BUBUBU
  NAFASI YA UWAKILISHI TAREHE 16/9/2012.


  Sifa njema zote zinamstahikia Mwenyezi Mungu, wingi wa Utukufu na Mwenye nguvu zisizoshindika na Mlezi wa viumbe. Sala na salamu zimshukie Mtume wetu Muhammad ( salallahu alayhi wa sallam ) ambaye ameletwa na dini ya haki ili izishinde dini nyengine zote hata kama makafiri watachukia. Rehema na Allah ziwafikie jamaa zake, Masahaba na wale wote waliowafuata hao na kusimama kuinusuru dini yao hadi mwisho wa ulimwengu huu.


  Jumuiya ya Maimamu Zanzibar ( JUMAZA) imesikitishwa mno na vitendo vya uvunjifu wa amani na utulivu vilivyotokea katika uchaguzi mdogo jimbo la Bububu uliofanyika tarehe 16/9/2012.


  JUMAZA inawakumbusha Wazanzibari wote kuwa ni kosa kubwa mno kuibeza na kudharau neema ya amani na utulivu alivyotutunuku Allah (S.W) baada ya muda mrefu kuishi katika migogoro, uhasama na chuki zilizotokana na siasa za chuki kama tulivyowahi kutanabisha katika tamko letu tulilolitoa siku tatu kabla ya uchaguzi kufanyika tarehe 14/9/2012. Kila Mzanzibari ni shuhuda juu ya maafa yaliyotokea kutokana na siasa hizo za chuki ikiwemo kuharibu mali za watu, kususiana kupoteza heshima za watu na kupoteza maisha ya Wazanzibari wengi katika kilele cha vurugu hizo mwaka 2001.  JUMAZA inalani vikali matumizi ya nguvu kupita kiasi kulikofanywa na vikosi vya SMZ hususan KMKM kwa hatua yao ya kutumia hata risasi za moto kwa kuwashambulia raia wasio na hatia. Aidha na hatua ya KWTZ ya kutumia nguvu na vitisho vilivyopelekea khofu katika eneo la uchaguzi. Aidha JUMAZA inalani vitendo vilivyofanywa na watu wasiojulikana waliofunika nyuso zao na kubeba silaha kuwashambulia raia. Ndugu Wazanzibar wapendwa vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani na utulivu vilivyotokea katika uchaguzi mdogo katika jimbo la Bububu vimeleta maafa makubwa yakiwemo kuwajeruhi watu, kuleta khofu ndani ya jamii, kuharibu mali za watu, kuvunja heshima za watu na kusadikiwa kupotea kwa maisha ya kijana wa Kizanzibari asiye na hatia kwa kupigwa risasi. Matukio haya kwa hakika yametia doa kubwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyopatikana kwa gharama kubwa na taufiq ya Allah (S.W)


  JUMAZA inaamini kuwa vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani na utulivu vilivyotokea katika uchaguzi huo ni miongoni mwa mikakati inayotekelezwa na kikundi cha watu wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na kupatikana mamlaka kamili ya Dola ya Zanzibar.


  Kutokana na vitendo hivi, JUMAZA inaiomba SMZ kumuwajibisha kamanda Mkuu wa KMKM pamoja na Afisa wa operesheni kwa kuliingiza jeshi hilo katika kadhia ya kuvuruga uchaguzi katika jimbo la Bububu.


  JUMAZA inamuomba Rais wetu mpendwa wa Zanzibar Mheshimiwa Dr Ali Muhamed Shein na Makamo wa kwanza wa Rais Mheshimiwa Seif Sharif Hamad watekeleze ahadi yao waliyoichukua pale Bwawani na JUMAZA ni mshahidi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu 2010 ambapo waliahidi mbele ya Allah (SW) kuwa watadumisha amani na utulivu na kuwalinda Wazanzibar. Kwa nia njema tunawakumbusha viongozi wetu hawa wawe na yakini wataulizwa siku ya malipo kwa kiasi gani wameitekeleza ahadi hiyo.


  JUMAZA inawaomba Wazanzibari wote wasikubali kurejeshwa walikotoka bali wawe na subra na kudumisha mapenzi na mshikamano wao ili kufikia malengo makubwa waliyojipangia. Aidha Jumuiya inawaomba Wazanzibari wote kuiunga mkono Serikali ya Umoja wa Kitaifa pamoja na kuwaunga mkono viongozi wetu wa ngazi za juu. JUMAZA kwa upande wake itasimama kidete kuilinda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Aidha Wazanzibari wote bila ya kujali sera za vyama vyao wanaombwa kuwa tayari kupigania mamlaka kamili ya Dola ya Zanzibar kwa gharama yoyote ile .


  Mola wetu Mtukufu tunakuomba uinusuru Zanzibar na watu wake dhidi ya maadui wa ndani na nje wasioitakia mema nchi yetu.


  at 3:18 PM
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ina Maana BUBUBU ni Waislamu tupu ? Kwanini hata Wasianze na Ndugu Waislamu halafu Wananchi wote

  kwa Ujumla!!! Kweli huu sio UBAGUZI ?


  * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT...
   
 3. b

  bagwell Senior Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ASilimia 99 ya Zanzibar ni Waislamu...Inshallah Mwenyezi Mungu amuangamize yeyote ambae haitakii mema Zanzibar....AMIN.
   
 4. a

  abousalah2 Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata wakawepo ni wageni wasiokuwa na sifa hata ya ukazi wa bububu
  \
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  nasubiri tamko la bakwata likfuatiwa na la ponda issa ponda
   
 6. G

  Gene Senior Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wameshapoteza uTANZANIA WAMEBAKI NA ALLAH NA MUHAMMAD
   
 7. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35

  utanzania hautakufikisha mbinguni...
   
 8. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  QUOTE=nngu007;4691671]
  Ina Maana BUBUBU ni Waislamu tupu ? Kwanini hata Wasianze na Ndugu Waislamu halafu Wananchi wote

  kwa Ujumla!!! Kweli huu sio UBAGUZI ?


  * LOVE COMES NATURALLY; HATE IS TAUGHT...
  [/QUOTE]
  :wink::wink::wink:Hata makafiri kwani wamezuiwa kutoa tamko?
   
 9. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Same times unapaswa uwe na akili za kiwendawazimu?
   
 10. O

  Ongeauchoke Senior Member

  #10
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumuia hizo zilikaa kimya wakati makanisa yanachomwa moto. Kama ni wapenda amani mbona walikaa kimya. wadini kwelikweli.
   
 11. J

  Jadi JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 1,402
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Dola kamili ya zanzibar ndio nini?wamesahau wao ni mkoa?
   
 12. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #12
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuna tatizo kubwa sana katika jambo hili na katika katiba mpya linatakiwa kuwekwa wazi maana haiwezekani mzanzibar aliye bara asibughudhiwe na kuonekana ni mkazi halali wakati kwa zanzibar hali ni tofauti.
   
 13. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #13
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ..........Safi sana KMKM, komesha magaidi hao hadi wanyooke.
   
 14. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #14
  Sep 25, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Mimi hapa ndio huwa siwafahamu [baadhi ya] Waislamu wenzangu. Kwa mafundisho niliyopewa. moja ya imani za Uislamu ni kuwatambua na kuwaheshimu mitume wote wa Mwenyezi Mungu. Kuwatambua na kuwaheshimu ni pamoja na uwepo wao na dini zao, katika hao ni Mitume waliopewa vitabu na dini zao - "Tunamuamini Mwenyezi Mungu, na katika yale yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim, Ismail, Isaka, Yakub, na makabila, na [tunaamini] katika (Vitabu waliyopewa) Musa, Yesu, na manabii, kutoka kwa Mola wao. Hatutafautishi baina ya mmoja na mwingine miongoni mwao ." [Surah 3:84]. Sasa kusema kuwa Mtume Muhammad ameletwa kuzishinda dini nyengine, dini za hao hao ambao imani yetu inatulazimisha kuwatambua na kuwaheshimu, lakini sisi tunageuka na kuwaita makafiri na kutaka kulazimisha imani yetu juu ya wengine. Iko wapi amani na kuvumiliana ambavyo ndio maana na msingi wa Uislamu?
   
 15. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  .......kujitoa muhanga je?
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kulikuwa na watu wa CUF kwenye Zanzibar Leo wakilalamika kuwa kuna wakristo bububu Wamechagua CCM

  Ndio Maana CCM Imeshinda kwa hizo kura 58
   
 17. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #17
  Sep 25, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  u seem to BE an intelligent guy! A gentleman indeed! Imani haimfikishi mtu peponi bali matendo yake, utamuita mwenzio kafiri na wewe kujiona mtakatifu!!! Ni maandiko ya wapi hayo na ya dini gani, yanayohubiri chuki?????
   
 18. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #18
  Sep 25, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red, naomba kwa anayejua, anifahamishe. Hiki ni kiswahili? Na nini maana yake?
   
 19. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #19
  Sep 25, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Taratiibu maada inaanza kugeuzwa.
   
 20. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #20
  Sep 25, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Mcheza karate yeye bado hajatoa tamko?
   
Loading...