Tamko la Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusiana na Muswada wa Mahakama ya Kadhi

Hatuwezi ongozwa ki ujanja ujanja tu,siku zinakwenda.nasema tamko limetulia nakwenda kula pasaka moyo ukiwa kwatu.kura ya katiba ya chenge na sita ni hapana/no.
 
tamko la jukwaa la wakristo tanzania kuhusiana na muswada wa mahakama ya kadhi

sisi, maaskofu kutoka tec, cct na cpct tumekutana leo tarehe machi 30, 2015 hapa dodoma ili kuomba kwa pamoja juu ya mgawanyiko unaodhihirika wa dini za kikristo na kiislamu kutokana na muswada wa mahakama ya kadhi. Maaskofu tuliokutana hapa hatuna hasira na wala hatuongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo wengine wanavyotutafsiri. Tunafikia maamuzi yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano.

Pia tumekuja kufuatilia kwa kina muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali ya 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya sheria ya tamko la sheria za kiislamu la mwaka 1964. Muswada huu unapendekeza kuanzishwa mahakama ya kadhi ambao utawasilishwa bungeni april 01, 2015 kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye kamati ya katiba na sheria ya bunge na kwa waziri mkuu hazijajibiwa.

Tangu tulipokutana machi 10, 2015 ambako tulitoa tamko letu kuhusiana na mahakama ya kadhi na katiba inayopendekezwa, tumekuwa tukiendelea kutafakari juu ya yale tuliyokuwa tumesema katika matamko yetu mbalimbali na jinsi amani na utulivu wa nchi yetu vinavyoendelea kumomonyoka siku zinavyokwenda.

kwanza tumeshangazwa na tabia ya viongozi wa serikali ya kuitisha na kuendesha mikutano wanayodai ni ya viongozi wa dini lakini isiyo rasmi.

machi 03, 2015 waziri mkuu aliitisha mkutano kupitia mchungaji mmoja ambapo hakuna hata kiongozi mmoja wa taasisi au kanisa aliyeshiriki. Jambo la kushangaza ni kile kilichotokea machi 28, 2015 ambapo mhe. Rais alishiriki kikao cha kikundi ambacho sio rasmi yaani kamati ya amani ya mkoa wa dar es salaam. Tunasema kamati hiyo siyo rasmi kwa sababu haina baraka za viongozi wa ngazi za juu wa kidini wa mkoa huo na haina mwongozo wa kazi zake.

Mikutano ya jinsi hii kati ya serikali na wale ambao imewaona kuwa ndio viongozi wa dini sio sahihi kwani viongozi wa dini wana taratibu zao za kualikwa au kuwakilishwa katika mikutano na viongozi wa serikali au wa dini au madhehebu mengine. Tunawashauri wanaohutubia na wanaoshiriki mikutano hii wajue kwamba washiriki hawana uwezo wa kuamua au kukubaliana na jambo lolote kwa niaba ya viongozi wao wa juu na pia viongozi husika wa serikali wasifurahi kwamba ujumbe wao umewafikia viongozi wa dini kwani hao washiriki sio wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa maamuzi au kukubaliana juu ya jambo fulani la kitaifa.

pili, tumekuwa tukifuatilia kwa karibu juu ya muswada wa mahakama ya kadhi na tumebainisha dhahiri kwamba kile tulichokuwa tunasema kitatokea kimeaanza kutokea bayana. Yale yaliyotokea kwenye semina kuhusu mahakama ya kadhi kwa waheshimiwa wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania machi 29, 2015 ambao ni wasomi, ni ishara ndogo sana ya kile kitakachotokea maeneo yote ya nchi yetu.

serikali kwa nia moja na kwa sababu tusizozijua inaanzisha vita vya kidini kati ya watanzania wakristo na waislamu
.

Tunashangazwa kuona jinsi serikali inavyonuia jambo hili ovu litakaloleta balaa kwa nchi yetu wakati huu wa kuelekea kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa na baadaye uchaguzi mkuu wa 2015.

Kutokana na mambo hayo makuu mawili hapo juu, sisi maaskofu wa jukwaa la wakristo tanzania tunatamka kama ifuatavyo :

Matamshi ya mhe. Rais akihutubia aliyowaita viongozi wa dini tarehe machi 28, 2015 kuwa mahakama ya kadhi ni ya waislamu wenyewe na serikali haitajihusisha wala kugharamia yanakinzana na kile kinachoendelea bungeni na nchini. Hapa tunajiuliza, endapo maneno ya rais ni kweli, mbona bunge linaendelea kujadili kitu ambacho serikali haitajihusisha wala kukigharimia ? Kwa mantiki hiyo, tunamtaka mhe. Rais aagize muswada huu uondolewe bungeni na usijadiliwe tena kwa kuwa utafiti wa tume ya kurekebisha sheria ulishaonyesha madhara ya uanzishwaji wa mahakama ya kadhi. Vinginevyo, kuendelea kujadiliwa kwa muswada huu maana yake ni kwamba serikali inajihusisha na itagharimia mahakama hiyo.

Serikali ijue kuwa endapo wabunge wa dini za kikristo na kiislamu watapigana na kisha baadaye wananchi nao wakafanya hivyo katika maeneo yao, serikali itakuwa ndiyo chanzo cha mapigano hayo. kama tulivyotamka hapo juu, kuhusiana na jambo hili tunamtaka mhe. Rais aiepushe nchi yetu na kuingizwa kwenye mapigano ya kidini ambayo kuyadhibiti itakuwa vigumu sana (tafadhali rejea kinachoendelea huko nigeria). Pia tunamwomba mhe. Rais akumbuke na kutafakari kile kilichotokea na kinachotokea nchi ya afrika ya kati kati ya kundi la seleka (waislam) na kundi la anti balaka (wakristo).

Tunaamini kuwa viongozi wa serikali wanafahamu viongozi rasmi wa dini na madhehebu ya dini. Kwa mantiki hiyo tunawashauri viongozi wa serikali waache kabisa kutumia vikundi visivyo rasmi kualika mikutano wanayodhani kuwa itakubalika na waumini wa dini hizo. Mikutano yote ya jinsi hiyo itakayoitishwa ni batili na maamuzi yake hatuyatambui na hatutayatambua.

Bado maaskofu tunasimamia tamko letu la machi 10, 2015 na tunawahimiza wakristo wajitokeze kwa wingi katika kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na zaidi wajitokeze kwenda kupiga kura ya hapana wakati wa kura ya maoni kwani katiba inayopendekezwa ilifikia hapo kwa njia ya ubabe, ilikosa uadilifu na mbaya zaidi ni rushwa ya ahadi ya mahakama ya kadhi ya iliyotolewa na waziri mkuu kwa waislamu wakati wa kupitisha katiba inayopendekezwa. Tunafanya hivyo kwa dhamiri safi kwa sababu ya imani yetu na kwamba sisi ni raia wa nchi hii na tuna haki ya kueleza mawazo yetu bila woga kama katiba ya jamhuri ya muungano ya mwaka 1977 inavyotupa haki.

Mwisho tunawaomba wakristo wote waendelee kufunga na kuomba kwa ajili ya utulivu na amani ya nchi yetu.

big up.
 
hawa maaskofu mbona hawaishi kutapatapa, hizo sheria zinazotambua mahakama za kadhi mbona zipo kitambo, ujinga tu wanaishia kupayuka payuka tu.

Imekula kwako mazima
Mwaka huu kama ni mimba itatimiza miezi kumi
 
Nasubiria na Tamko la Pengo bila kusahau na mrejesho wa Kamanda mpiganaji Gwajma.

Hahahaha Gwajma ni kiboko ya wasaliti.
 
Viongozi wa dini hamna sababu ya kulumbana na serikali.
Toeni elimu kwa umma na washirika wenu ili kuikataa katiba ya serikali ambayo ipo kwa manufaa ya wachache.
Rais amekuwa dhaifu sana hivyo uwezekano wa kutuletea majanga ni mkubwa.
Maaskofu kemeeni,karipieni,shaurini bila woga wowote.
Mwisho toeni ushauri wa kuiondoa serikali legelege na chama legelege.
Sawa kabisa mheshimiwa,na viongozi wote wa dini na wasiokuwa wa dini pia wahakikishe elimu inawafikia wafuasi wao popote walipo!ili tu wawe na hekima ya kuamua,hizi mbwembwe nyingine zitatuletea balaa.
 
Safari hii waislamu tutakomaa hadi kieleweke...hatutishwi na vitamko uchwara vya makafir.....

usimwite binadamu aliyeumbwa na Mungu kafiri! unafanya makosa sana! naomba utubu dhambi hii ya kuwaita wenzio kafir. shida nikwamba ulifundishwa vibaya. kama waislamu munaikubari torati iweje leo umwite mwenzio kafir? mi nafikiri kafiri ni mtu asie mucha Mungu! mashehe/ wanazuoni wa kislamu wafundisheni vizuri wezenu.
 
Kuwa na nidhamu mkuu,kikwete pia ni mwislamu(mwana wa mjakazi)na ndiye rais wenu hadi sasa!!kashfa weka mbali,tukubaliane kuikataa katiba pendekezwa tu!!na iwe ni kwa maslahi mapana na ustawi wa nchi yetu na imani zetu,ungeijua nguvu yetu waislam kwenye mustakabali wa taifa hili wala usingeandika utumbo huo,Mungu akupe hekima mpendwa.

Mkuu, achana na huyo jamaa amejilia 'chakula chake' hapa anabwabwaja tu.
 
Sasa naamini kwamba wakristo mna roho mbaya sanaa.haina shida lakini itajulikana tu.

Hivi Wakristo ndio wamekataa au Waislamu ndio wamekubali ulaghai wa CCM? Nakuhakikishia ktk hili, CCM wako tayari kuwatimizia Wakristo matakwa yao ili wakubali ghiliba zake.

Hapa tulipofikia, Wakristo wakisema wanataka Shule zao zilizobakia serikalini warejeshewe, CCM watakuwa wako tayari ili mradi Wakristo wasema 'ndio' na wakubali matakwa na mkakati wa CCM kuhusu hili suala.
 
usimwite binadamu aliyeumbwa na Mungu kafiri! unafanya makosa sana! naomba utubu dhambi hii ya kuwaita wenzio kafir. shida nikwamba ulifundishwa vibaya. kama waislamu munaikubari torati iweje leo umwite mwenzio kafir? mi nafikiri kafiri ni mtu asie mucha Mungu! mashehe/ wanazuoni wa kislamu wafundisheni vizuri wezenu.

Hata wewe pia ni KAFIR....unasemaje...??
 
Nyie makafir mwaka huu tunakomaa na nyinyi mpaka kieleweke...

Pumbavu kabisa, kafiri ni wewe na ukoo wako. Hizo sheria zenu za ki ISIL za kuoa watoto wa miaka 9 kama mtume wenu zipelekeni mnakokujua lakini si hapa tz, nyambaf!
 
I like ur comment...!!! U seem to hv very reasonable and fruitful discussion...!!!

Katiba pendekezwa ni bomu kwa kweli...!!! See below

1: Wabunge bado watakuwa mawaziri....wakati tulipendekeza ukiwa mbunge huwezi kuteuliwa kuwa waziri...hapa kuna mgongano wa mihimili...!!! Na bunge litashindwa kuisimamia serikali kikamilifu kama ilivyo sasa...

2: Tulipendekeza, mbunge awe na vipindi viwili tu, yaani 10 yrs, aondoke...bali katiba ya Chenge & 6..sasa ni 15 yrs....

3: Tulipendekeza wabunge wasioonekana ktk majimbo yao bila sbb za msingi kwa 6 months, wananchi walio mchagua wamtimue...hii ingefanya mbunge awajibike kwa walio mchangua..sasa ni kinyume...mbunge hawezi kufukuzwa na walio mchagua..bali CHAMA NDIO KINAWEZA KUFUKUZA UBUNGE NA KUMFUKUZA UANACHAMA HATA KAMA WANANCHI WANAMPENDA...tumeona kwa Zitto, Kafulila, Hamad Rashid..etc hadi wakaitwa wabunge wa mahakama..!!

5: Tulipendekeza PCCB iwe huru na kujitegemea...iweze kufanya uchunguzi, na kuwashtaki wala RUSHWA MAHAKAMANI WENYEWE....NA DPP AWE CHINI YA PCCB...OF WHICH HAIKO HIVYO TENA SASA...tumerudi kule kule..

6: Tulipendekeza Speaker wa Bunge asiwe MUUMINI WA CHAMA CHOCHOTE cha Siasa for the last 5 years ktk historia yake..ili awe fair sana ktk maamuzi...na awe atleast mwanasheria au judge...ila hili limegeuzwaaaa..tumerudi kule kule...

7: Tulipendekeza mbunge awe na minimum Qualification ya form 4 with pass credits..ili awe anajua nn kinaendelea bungeni..isiwe tunaona uchafu na taarab za kina Lusinde.....katiba pendekezwa ya
Chenge inasema, MBUNGE ANATAKIWA AJUE KUSOMA NA KUANDIKA...as entry point...yaani ni shida...Mbunge mwakilishi wa wananchi, kiongozi..awe standard 6 au 7 ni sawa tu..dunia ya leo kweli...!!? Alafu atunge sheria..!? Tunajidanganya saanaaa

8: Tulipendekeza KATIBU MKUU KIONGOZI....atachaguliwa na RAIS..BAADA YA TUME YA UTUMISHI WA UMMA kumpelekea majina 3 ya watu competent, na wasio na shaka ktk utendaji wao..ili RAIS ACHAGUE MMOJA KATI YAO...LAKINI KATIBA YA CHENGE IMEPIGA CHINI...!! imagine

9: Tulipendekeza idadi ya mawaziri iwe fixed ktk KatibA..ili Rais abane matumizi na sio achague apendavyo...hovyo hovyo...na wizara zinakuwa fixed...!! Sasa imegeuzwa...

10: Tulipendekeza, PM, mawaziri na manaibu waziri, IGP..KATIBU MKUU KIONGOZI, PCCB DIRECTOR, GOVERNOR, DPP, TRA CEO...wafanyiwe VETTING YA UHAKIKA NA BUNGE MARA TU BAADA YA KUTEULIWA NA RAIS...NA WATAKAO PITA WATAENDA KUAPISHWA NA RAIS..NA WATAO SHINDWA KUPITA VETTING YA BUNGE RAIS INABIDI ACHAGUE WENGINE...NA KISHA WAENDE BUNGENI KUFANYIWA VETTING...!! HILI NALO LIMEGUZWA...hakuna vetting...Rais atachagua tu hata shemeji yake...ndio maana unaona madudu kila kona..!!

Kuna mengi sina muda..ila sbb hizo hapo juu ZINATOSHA KUPIGA KURA YA HAPANA...BILA WASIWASI NA NI HAKI YETU SOTE....tuamke...!!! Tujue haki yetu...



Mimi ni mwislam safi! Na nitaikataa katiba pendekezwa for the sake of my country,si kwa ajili ya mahakama ya kadhi kuwepo ama kutokuwepo!!hata katiba isipokuwepo bado uislam wangu utakuwepo tu!katiba ipo kwa dunia uislam ni kwa dunia na akhera,na tuna namna njema tu ya kuhukumu ki uislam zaidi ya hiyo ya katiba ya kihuni,ninachokataa kwenye katiba hii ni pale mambo yote ya msingi yaanakosa majibu kikatiba na badala yake katiba tena ina direct kwa bunge kuyatungia kanuni(sheria?)Nilichojiuliza mimi ni kuwa ikiwa katiba hii itapita kwanza,then kanuni nyingine muhimu zaidi zije kutungwa na bunge baadaye ni nani tena atakayepiga kura kukubali au kukataa kanuni hizo za bunge wakati kura itakuwa imeshapita?kuna mtego hapo!! Na ndiyo maana naikataa katiba hii hadi pale itakapojikamilisha pasipo kuacha mianya mingine ya watu wasio waaminifu kuitia vidole,until then kura yangu ni HAPANA.
 
Back
Top Bottom