Uchaguzi 2020 Tamko la chama cha Julius Malema wa EFF juu ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Kidogo kidogo dunia nzima inakuja Tanzania kuishinikiza serikali irudie uchaguzi huru na wa haki ikiwa na katiba mpya, si hii katiba ambayo wanaikanyaga wenye mamlaka halafu raia anaelipa kodi hio katiba haimlindi mbele ya vyombo vya serikali. We have to do something.
Malema ni mwanampotevu.
 
Ni kweli kuwa CCM ni chama kikongwe Afrika. Kitendo cha vijana wadogo akina Malema na wenzake akina Mbuyiseni Ndlozi kwa kushirikiana na wenzao akina Mnyika na Zitto kutaka kupambana na vyama vikongwe ni utovu wa nidhamu.

Angalia tamko lao kuhusu uchaguzi wa Tanzania lilivyojaa kibri.
View attachment 1618635View attachment 1618636
Wamwaga damu watatukana kwani ukweli unauma.
Unajifananishaje na Nyerere ewe mmwaga damu za raia wako?
 
Chama kinachoshindwa kutetea watu wake wenyewe kwenye nchi yao leo kinaongelea mambo ya TZ. Nonsense
Unakijua unachoongea?
Unajua kirefu cha EFF na wanachosimamia?
Au damu za watu uliowaua zinakuandama?
 
Sasa kama watanzania wameamua nyinyi mnataka muwalazimishe kuchagua upinzani? Kwa nini msiende mahakamani? Sasa nyinyi wakati wa kampeni mlikuwa mnahangaika na kuwaeleza watz jinsi utakavyoingia barabarani kupitia beberu Amsterdam. Kama hamjui watz hawapendi kibaraka hata siku moja.
Amsterdam ameshapeleka kesi kortini. Subirini kuitwa shaurini tu!
 
Wangewarudishia kwanza wazawa wa SA ardhi yao iliyoporwa kabla ya kuzungumzia masuala ya Tanzania. Katika uchaguzi huu, endapo wananchi wazalendo wasingeona mbali na kufanya uamuzi mzuri wa kuwakataa hawa vibaraka wa London & Washington, basi nchi yetu ingetumbukia na kuzama kwa mara nyingine tena katika minyororo ya utumwa na kwenye lindi la ukoloni ambamo Rais Magufuli amejitahidi kwa kiasi kikubwa kutunasua na kutunusuru.
Eti Wazalendo! Wizi mtupu!!!
 
Hata ukiwauliza wapinzani walete ushahidi wa kuibiwa hawana zaidi watakuletea karatasi za kupigia kura fake!
Hivi neno ushahidi uko wapi ndo the only weapon kuwapiga nalo wanaolalamika?
mengine hayahitaji kujua kusoma bali hata picha zinatosha kujua kitu
 
Unakijua unachoongea?
Unajua kirefu cha EFF na wanachosimamia?
Au damu za watu uliowaua zinakuandama?

Sihiitaji kuwajua ila najua walichoongea ni nonsense. Matamako yao ndo yatabadilisha matokeo?

TZ is a sovereign country haitaingiliwa na nchi yeyote, endeleeni kujipa moyo kama mlivyoamini mtashinda.
 
Wizi walifanya akina Mkapa na Kikwete lakini huu NI UJAMBAZI KABISA.
Lipumba anasema kuna mbunge wake alikwenda kupiga kura kwenye kituo akiwa na familia yake ya watu 7.
Cha ajabu huyo mbunge wake amepata kura 00000000..
Yaani mpaka kura yake watu wamepita nayo.
Basi huu ni ushahidi mkubwa mojawapo kwamba kweli mmepoteza kura kihalali, maana hadi watu wenu wa karibu hawakuwapigieni.

Aliyeanzisha utaratibu wa kura kuwa siri ya mpiga-kura mwenyewe, basi aliona mbali sana, na amesaidia kuokoa na kulinda heshima ya ndoa na mahusiano mengi baina ya watu: yaani kudumu na mtu hata kama hukubaliani naye.
 
Kumbuka kuna ushahidi wa mazingira na kuna ushahidi wa vielelezo!
Vielelezo tayari wapinzani wanavyo hadi vya picha na video, sema tu havijarushwa hapa sababu ya shinda ya mitandao! Au hukumuona mgombea wa CHADEMA akionyesha moja ya karatasi origional ilotumika kupigia kura ambayo walikamata katika moja ya majimbo hapa bongo?

Ushahidi wa mazingira nao ni mwingi tu:-
1.Rejea mgombea wa CUF jimbo la Temeke ambaye alipata kura 0 (SIFURI) kwenye kituo kwenye kituo ambacho alipiga kura yeye mwenyewe na wanafamilia 7, Na hapakuwa kura hata moja iliyoaharibika, Je hizi kura zote 8 zilienda wapi?

3.Hata riport za baadhi mashirika kama CIP zinaonyesha kwamba wananchi waliojitokeza kupiga kura mwaka huu walikuwa wachache sana,! Je kura milioni 15 zilitoka wapi???

3.Tangu tuanze mfumo wa vyama vingi CCM Zanzbar haikuwahi kushinda kwa Zaidi ya asilimia 69% inapochuana na Maalim Seif Au Seif hakuwahi kupata chini ya asilimia 40, Je kwa kuzingatia hali halisi ilivyokuwa wakati wa kampeni Je wewe unaona yale matokeo ni fair and just?

4.Kwa kuzingatia hali halisi ya kampeni zilivyokuwa na historia halisi ya mikoa kama Dasm, Mbeya,Kilimanjaro, Arusha, Lindi, Mtwara, Iringa,Njombe na Songwe, Je ni Wapinzani wanaweza kukosa jimbo hata moja kwenye mikoa hiyo???

........... Hapa hata bila miwani mbona kila kitu kinaonekana wazi? Tuweni na hofu ya Mungu, ni bora kukaa kimya kuliko kusuport kitu ambacho unajua kabisa si kweli!!!
Hapa hakuna ushahidi hata mmoja. Hizi ni tuhuma tu kama tashwishwi zingine; na ni jambo la kawaida kwa mfa-maji. Mfano: Mtu anaweza kuacha kujipigia kura makusudi, akipata sifuri iwe kisingizio kwamba kuna walakini kwenye mchakato mzima.

Karatasi zinazodaiwa kuwa halisi zinazozagaa mitaaani hazijathibitishwa na mamlaka husika kuwa ndivyo kweli. Wapinzani kukosa majimbo iliyozoeleka kuwa ya wapinzani ni suala la kawaida la kitu kinachoitwa mabadiliko. Mabadiliko hayana mazoea, hayadumu -- sifa kuu ya mabadiliko ni kubadilika.
 
Ni kweli kuwa CCM ni chama kikongwe Afrika. Kitendo cha vijana wadogo akina Malema na wenzake akina Mbuyiseni Ndlozi kwa kushirikiana na wenzao akina Mnyika na Zitto kutaka kupambana na vyama vikongwe ni utovu wa nidhamu.

Angalia tamko lao kuhusu uchaguzi wa Tanzania lilivyojaa kibri.
View attachment 1618635View attachment 1618636
Ameshindwa kupambana na mtoto ANC, ataliweza kweli baba lao CCM iliyowapa Uhuru SA? Malema ni kijana ila akili zake za kizee, akiwa mzee lazima awe mchawi!
 
SA watuachie mambo yetu wenyewe. Tuliwasaidia walipokuwa na matatizo sasa basi. Sio wao peke yao bali mataifa yote tuliyoyasaidia kusini mwa Afrika. Shukrani ya punda ni mateke.
 
SA watuachie mambo yetu wenyewe. Tuliwasaidia walipokuwa na matatizo sasa basi. Sio wao peke yao bali mataifa yote tuliyoyasaidia kusini mwa Afrika. Shukrani ya punda ni mateke.

Tuliwasaidia kupata uhuru kutoka kwenye makucha ya makaburu weupe na wao wanayodhima kutusaidia kupata uhuru kutoka kwenye makucha ya makaburu weusi wa CCM.
 
Hapa hakuna ushahidi hata mmoja. Hizi ni tuhuma tu kama tashwishwi zingine; na ni jambo la kawaida kwa mfa-maji. Mfano: Mtu anaweza kuacha kujipigia kura makusudi, akipata sifuri iwe kisingizio kwamba kuna walakini kwenye mchakato mzima.

Karatasi zinazodaiwa kuwa halisi zinazozagaa mitaaani hazijathibitishwa na mamlaka husika kuwa ndivyo kweli. Wapinzani kukosa majimbo iliyozoeleka kuwa ya wapinzani ni suala la kawaida la kitu kinachoitwa mabadiliko. Mabadiliko hayana mazoea, hayadumu -- sifa kuu ya mabadiliko ni kubadilika.

Pia kuna kura hazikuhesabiwa kwa sababu zilikuwa considered zimeharibika. Hata mtu aliyejipigia kura, kama hakufuata maelekezo ya upigaji kura yaliyowekwa, kura yake itahesabika imeharibika!
 
Sawaaa familia yake haikumpigia kura.
Basi wangembakishia hata kura yake mwenyewe nayo pia mmeondoka nayoo?
Basi huu ni ushahidi mkubwa mojawapo kwamba kweli mmepoteza kura kihalali, maana hadi watu wenu wa karibu hawakuwapigieni. Aliyeanzisha utaratibu wa kura kuwa siri ya mpiga-kura mwenyewe, basi aliona mbali sana, na amesaidia kuokoa na kulinda heshima ya ndoa na mahusiano mengi baina ya watu: yaani kudumu na mtu hata kama hukubaliani naye.
 
Hakuna statement ya aina hii,huu ni mwendelezo wa Chadema kuendelea kuipaka matope serikali na kuichafua nchi kwa kuwa wameshindwa.

Nimeongea na mmoja wa wanahama wakongwe wa EFF na amekanisha huu waraka. Home Main - EFF
 
Back
Top Bottom