Tamko la CHADEMA Wilaya ya Arusha: Hatutamabui muafaka wa madiwani

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Ndg, wana JF,

Katika kikao cha wilaya kilichofanyika katika Hoteli ya Stereo hapa Arusha, chadema wilaya ya arusha imetoa tamko kwamba haitambui muafaka wa madiwani, na kwa usaliti waliouonyesha hawatahitaji kuona katiba inapindishwa, wachukuliwe hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wale wote wenye nia mbaya na wasioendana na katiba ya chama.

Kikao hicho kilifanyika chini ya uongozi wa mkoa, ambayo ilikuwa chini ya mwenyekiti wake Ndg, Samson Mwigamba na Katibu wake wa mkoa pamoja na wajumbe wengine akiwepo mbunge wa jimbo la arusha ambaye ameingia kwa kofia ya kuwa mjumbe wa kamati kuu ya chama.

Msimamo huo uliungwa mkono na wajumbe wote, ambao kwa pamoja wamesema madiwani wote waliokiuka katiba wafukuzwe kabisa chamani wakatafute chama chao.


nawakilisha.
 
Kindly Mh Nanyaro Japhet Nanyaro aka baba Kamanda plse confirm the post.

pamoja na kwamba atacomfirm the post, ni kwamba katika kikao hicho kamati ya muda iliyoteuliwa kuongoza na kuratibu shughuli zote za wilaya walitambulishwa pale, ambapo kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mh. Nanyaro Ephata na wajumbe wengine kumi na tano hivi.
 
Madiwani wa arusha wangepewa onyo kali tu nadhani hilo ni jambo la muhimu sana. Kusudi wasirudia tena siku nyingine...
 
Nzuri sana hii, wawaachishe udiwani wote waliohusika na wawafukuze chama, zipigwe kura upya!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom