Tamko la CHADEMA kukanusha madai ya CUF kufanyiwa vurugu Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la CHADEMA kukanusha madai ya CUF kufanyiwa vurugu Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Sep 28, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  TAMKO LA CHAMA KUKANUSHA SHUTUMA ZA CHAMA CHA CUF KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA.

  Ndugu wananchi na wanahabari,

  Siku ya terehe 27 Alhamisi Septemba 2012 chama cha wananchi CUF walitoa taarifa ya malalamiko kwa vyombo vya habari na mitandao kuwa wanachama wa CHADEMA wamewafanyia vurugu kwa kuwapiga mawe na kuwa jambo hilo limehamasishwa na viongozi wa chama katika mkoa wa Arusha pamoja na Mhe Godbless Lema.

  Wote tunafahamu kuwa siku hiyo hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero wafanyabiashara ndogo ndogo walikuwa wamevamia na walikuwa wakijigawia maeneo, baada ya eneo la awali walilopewa la viwanja vya NMC kushindwa kuwachukua wafanyabiashara wote na halmashauri kushindwa kutoa majibu kwa wafanyabiashara hawa ambao waliwaambia wote waende NMC.

  Kwanza tunapenda kutoa pole kwa viongozi wa CUF kwa jambo hili lililowapata. Wao kama watu na Watanzania wenzetu tunawapa pole sana.

  Pili, CHADEMA inakanusha kuhusika na jambo hili. Hii si tabia ya CHADEMA na kamwe haiwezi kuwa tabia ya CHADEMA kufanya siasa chafu za namna hiyo. CHADEMA tunajali sana amani na upendo, na hii ndiyo tabia na makuzi yetu Watanzania.

  Katika mazingira haya, CHADEMA tunachukua fursa hii kuvikaribisha vyama vyote mathalani CUF, Arusha ni yetu sote na tutumie demokrasia vizuri kufanya kazi nzuri ya siasa kwa ajili ya kusababisha na kuleta matumaini kwa Watanzania hawa ambao serikali ya chama cha mapinduzi imeshindwa kuwaletea.

  CHADEMA hatuna shida na ushindani wa kisiasa katika mazingira ya kidemokrasia kwa maana ndio wakati pia wa wananchi kupima na kujua nani mkweli na ama nani anafanya kwa dhati ya kweli. Hivyo tunawakaribisha CUF karibuni Arusha na wala wasitafute kisingizio cha kuegemea ili CUF ianze kutajwa tajwa kwa kutumia mgongo wetu.

  Sambamba na hili, CHADEMA mkoa wa Arusha tumesikitishwa sana na tamko la CUF lilitolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na haki za BInadamu Mhe Abdul Kambaya, tamko lenye matisho na lugha isiyofaa.

  Moja na maneno ya tamko hilo wamesema, nukuu "Uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwa sababu wameanza tunaweza kumaliza". Wakazi wa Arusha na Watanzania wapime na waone, haya si maneno yanayoweza kutoka kwenye kichwa cha mtu anayefikiri vizuri, mtu anayeipenda nchi yake na kuheshimu utawala wa sheria. Zaidi ya hapo tamko hilo limesema pia, "Ile ngangari kwa polisi tunaweza kuwahamishia wao wakose pa kukaa".

  Katika yote haya, niwaombe wakazi wa Arusha, Wanachadema na hata wanachama wa vyama vingine tuwapende na tuwakaribishe CUF Arusha na sote tufanye kazi ya siasa kwa nguvu za hoja. CUF wanaweza kufanya hicho wanachotaka kufanya lakini CHADEMA kamwe hatupo tayari kwa vurugu ya aina yoyote, aidha tunawakaribisha kwa moyo mmoja na kama wapo tayari basi tufanye siasa zenye tija na manufaa kwa wakazi wa Arusha.

  Aidha nitoe onyo kali sana kwa mamluki ambao wamekuwa wakijifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Mara kadhaa watu hawa wamekuwa wakisababisha fujo ili kukifanya CHADEMA kionekane kuwa ni chama cha vurugu. MAMLUKI ni sumu, tukimgundua na kumthibitisha mtu wa aina hiyo katikati yetu tutamtangaza mbele ya jamii kuwa yeye ni sumu na kuomba wananchi wamtenge maana anapingana kwa kuleta hila na unafiki kwenye kazi ya kuwakomboa Watanzania. Niwatangazie mamluki hamtatuweza na tutawagundua tu.

  Mwisho, tunapoelekea kwenye marudio ya uchaguzi mdogo kwenye kata za Daraja II kwa Arusha mjini na Bangata kwa wilaya ya Arumeru Magharibi, nirudie kusema maneno ya Mhe Lema kuwa iwapo viongozi na watumishi wa umma watajihusisha na kushiriki kwa kufanya kampeni za kisiasa wakiwa wanatumia magari na vifaa vingine vya serikali watu hawa tutawakamata na tutawapeleka huko wanakostahili kupelekwa wezi na vibaka wengine.

  Hii ni tahadhari tunamaanisha kweli na wananchi wote wawe makini "wakamate mwizi" lengo likiwa ni kuweka adabu kwa watumishi na viongozi umma wanaovunja sheria ya utumishi wao kwa umma na matumizi ya rasilimali kwa namna isivyotakiwa kisheria. CHADEMA tutashiriki chaguzi hizi na tunawaomba wakazi wote wa maeneo haya tushiriki kwa utulivu na amani.

  WANACHADEMA wote tuendelee kuwa majasiri, tusiwe waoga na tusimamie kweli na haki.
  "Hakuna kulala Mpaka Kieleweke"

  Amani Sam Golugwa
  KATIBU WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA: golugwa@gmail.com

   

  Attached Files:

 2. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Kuwajibu au kuwatolea tamko hawa wapumbavu wa bondeni ni kupoteza muda!

  They better keep silent!
   
 3. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  CDM wangesema lipi zaidi ya hayo?
   
 4. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa
   
 5. h

  hans79 JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Fanyia kazi taarifa sio kukurupuka tu, kama pana kikundi kilifanya fujo walifungua mashitaka?
   
 6. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  ameshakwambia kwamba kama wapo wanaitwa mamluki na watashughulikiwa. Kukurupuka iko wapi?
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Mbona cdm wamefanya mikutano kwenye ngome za cuf kwa amani? Kwa hakika haukua ustaarabu.
   
 8. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kweli CUF ndio kiboko ya CHADEMA, Mkwara wa nguvu wamelegea kama mtoto wa kike, CUF sio CCM fujo wafanyieni CCM sio CUF. sawa sawa?
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hivi zile vurugu za jana za Wamachinga Arusha walikuwa ni CDM? CUF wanatia aibu.
   
 10. Kalumbesa

  Kalumbesa JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,009
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nilikuwepo arusha siku hiyo, ninachoshangaa mpaka sasa ni kwamba wale vwafanyabiashara waliovamia lile eneo ni CHADEMA? au walitumwa na CHADEMA? ni vipi CUF wawahusishe CHADEMA moja kwa moja huku waliopiga mawe pale ni wafanyabiashara,au msafara wa CUF ukipita mahali popote ukapigwa mawe,basi wahusika watakuwa ni CHADEMA?
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Safi sana, cuf karibuni sana arusha tushindane kwa siasa zenye tija.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 12. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Tamko lao mkuu la kusema wanaenda kuvunja ngome ya chadema, ndiyo iliwatia wana Arusha hasira. Maneno yao ya kipumbavu pumbavu ndiyo malipo yao hayo. Hivi Cuf wanaweza wafanya nini cdm? Ratio ni chadema 10:1 cuf. Cuf acheni kututishia, hatupendi ugomvi si kawaida yetu. Ila kamwe hatuwezi kuwaogopa wake wa mtu nyie kwa kelele zenu.
   
 13. Monyiaichi

  Monyiaichi JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 1,825
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Unafikiri ni kulegea kwa mkwara! wala, ustaarabu tu dear, unafikiri nani hawezi ukichaa akiamua? hapo pana mambo mengi sana ila basi tu. jinsi huo mkwara ulivyoongelewa ndio jinsi wananchi nao wanapima aina ya chama.

  Mwanamume jasiri ni yule ambae hata akikataliwa na mwanamke, anaendelea kumuheshimu na kujiheshimu pia. Lakini ukiona anayeanza kutishia na kumpakazia mwanamke anazidi kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa kupendwa au kukubaliwa. So watch out
   
 14. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CUF+ CCM=Janga la kitaifa
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Wakuu, nadhani kuna kitu hakiko sawa hapa.

  Je hao wamachinga ndio CHADEMA au kulikuwa na wamachinga pamoja na wanachama ktk eneo hilo la soko?

  Nafikiri taarifa hii pia haijakidhi haja ya maswali niliyonayo. In fact sielewi mantiki yake.
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Rest in everlasting fire CUF!
   
 17. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Hawa cuf wanatakiwa watambue juzi hakukuwa na mkutano wa chadema Arusha ilikuwa ni wavuja jasho wanatafuta haki yao.Haikuwa busara kwa cuf kwenda pale kuwatangazia mkutano wangesubiri wamachiga wapate haki yao ndio waanze matangazo yao.

  Kitendo walichokifanya Cuf ni sawa na kwenda msibani na kutangaza kuwa kutakuwa na disko kwa mfiwa usiku.Je nani kawambia wamachiga wote wa Arusha ni Chadema.

  Je mawe yaliyorushwa yalikuwa na bendera za Chadema Kama kithibitisho?
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Watu wametumia ustaarabu wewe unaleta utoto unadhani hayo maneno yako yana tija gani!

   
 19. M

  MTK JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Kaluli za "tunaweza kuwafanya chochote zinaonyesha kuwa CUF ni Jihadists! to them revenge, murder and violence is justifiable whereas Modernists like CDM persues inclusivity, peace and values the sanctity of life; anyway; ndoa ya mkeka na CCM imewakengehua, ignore them, If they can not put up then they should shut up, period.
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Karejee taarifa ya Cuf utaelewa mantinki ya habari hii!
   
Loading...