Tamko la CHADEMA kuhusu Mafuriko lililotolewa na Dr. Slaa leo

Huyo Slaa anatuletea habari za Early Warning System wakati hata mafuriko hayajaisha? na kama ni kujuwa kuwa mabondeni huwa panafurika ni nani asiyejuwa?

Mkuu uwa unaniduwaza sana wakati mwingine. Kwa bandiko kama ilo hakika unakua sawa na ngumbaru tu!

Slaa hapa anataka serikali ijifunze;sasa kama suala la mafuriko Jangwani linajulikana,serikali imefanya nini katika kuepusha athari? Slaa anahimiza katika suala zima la disaster management;wewe unavyosema mafuriko bado hayajaisha, unataka kutuambia kwamba tusubiri hadi mafuriko yaishe ndo tutafute cha kujifunza?!
 
Safi sana Dr kwa tamko,serikali hi legelege ya CCM inafanya sherehe miaka 50 ya uhuru kwa kutumia mabilioni ya mapesa wakati miundo mbinu mibovu wala kuwasaidia waadhirika hakuna zaidi ya maneno ya uongo.
 
fisadi mkuu kikwete anakenua tu. alikenua mabomu mbgl na g la mboto na sasa anakunywa chai landani huku watz wanaangamia , wkt wmkuu wa uinglish anaahirisha ziara kukitokea tu maandamano nchini huyu fisadi wetu anatoa tamko kupitia mafisadi wenzake akina luhanjo na salva.laisi legheleghe huzaa serikali legheleghe.
 
ni matamko yaleyale ya kulalamika na kulaumu kama Jacob Zuma na Barack Obama kabla hawajashika Ikulu angalia wanavyopwaya Ikulu..... ngoja tuwape Ikulu kama hamjatugeuka
 
ni matamko yaleyale ya kulalamika na kulaumu kama Jacob Zuma na Barack Obama kabla hawajashika Ikulu angalia wanavyopwaya Ikulu..... ngoja tuwape Ikulu kama hamjatugeuka

Mkuu Ikulu sio sehemu ya majaribio...mfano mdogo umeona walivyokwenda Ikulu kwa JK wamepewa Juice ya Machenza na gahawa na tende za Yemen wanakenua meno tu huku waking'aa sharubu...

Je wakipewa nchi si watageuza Ikulu kijiwe cha kunywea Mbege na Mtori!
 
unasahau kodi unayolipa ili uweze kupata maisha bora sasa.. Kuna kitengo cha maafa na kina bajeti kila mwaka,maafa yawepo au yasiwepo. Kuna watu wana uelewa mdogo sana wa mambo..

Mkuu umenena vyema. DMD ni idara mfu.
 
Jamani hizo system zinazosemwa ni zipi hizo wajamani, hebu nielimisheni kidogo. Japani hawajakuwa nazo kweli? na juzi juzi miezi kadhaa zilizopita niliona watu wanasombwa kule amerika na mto misisipi. Hebu wajamani ni elimisheni hiyo alarm system ya mafuriko iko je?
 
Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?

kupewa ushauri pia ni msaada mkubwa sana kuliko pesa!
lazima kukosoa kwani kilichotokea(vifo na hasara) mostly vingeepukika iwapo sheria,kanuni na utekelezaji ungefuatwa .na hiyo ingewezekana iwapo ushauri uliotolewa ungekuwa ni wajibu wa dola!
 
Mathalani mpaka sasa hatujaona jitihada zozote ambazo zimechukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa katika kuonyesha juhudi za kukabiliana na janga hili kubwa kwa taifa letu,hii inaonyesha wazi kuwa kitengo hiki hakijaandaliwa kuweza kukabiliana na maafa kama ambavyo majukumu yake yanavyopaswa kuwa.
Vikao vinaendelea.
Pa diem kwanza....
 
Aliyekosea ni yule aliyewaacha watu wajenge mabondeni na unamjuwa ni nani. Kikwete alisema "very clear" waondoke mabindeni.

Huyo Slaa anatuletea habari za Early Warning System wakati hata mafuriko hayajaisha? na kama ni kujuwa kuwa mabondeni huwa panafurika ni nani asiyejuwa? asijitafutie umaarufu kwenye maisha ya watu.

Nadhani hao watu wanaoambiwa kila siku wasijenge huko sasa ndio itakuwa mwisho wa kujenga huko, hii hapa:

RAISI AMWAGIZA PROF ANNA TIBAIJUKA KUZUIYA UJENZI ENEO LA JANGWANI April 5, 2011


Makamba kishanhangaika sana na hao watu. Huyu Slaa asituletee habari za kutowa matamko mbiombio na kutafuta umaarufu hivi hana sera? au hajui hata wakati muafaka wakutoa haya matamko? Ni mbaya sana watu kujitafutia umaarufu kwenye matatizo.

Tuwaombee Mungu awasaidie hawa watu walioathirika na tuwasaidie kadri ya inavyowezekana na kuwasaidia zaidi ni kuhakikisha hawajengi mabondeni.

Mkuu,
Watu wanalaumu tu, wakipitishiwa jembe na Magufuli ndo wa kwanza kuponda mawe, yakiwakuta wanageuka. Hii ya kutojenga mabondeni ni miaka mingi sana, imeimbwa kama sijakosea kuna wengine walipelekwa pwani wakarudi wakagoma wakarudi.

Hii ya kuwa ambia wahame mabondeni na wasejenge mabondeni ndo early alarm system ya ukweli. Sijui huyu jamaa anataka ya aina gani.
 
Mkuu kwa ninavyojua helcopter ilikuwa ya kukodi kenya sijui ulitaka akakodi ije ikaokoe, na mpaka taratibu zote zilifuatwe sijui ingekuja kumwokoa nani maana maafa yangekuwa ndo yanaishia. Sjui kwanini Jk hajaitumia hiyo aloruka nayo leo kuangalia uaribifu uliotokea badala ya kuokoa kwanza

Hivi CDM wakileta helcopter kurescue wahanga wa mafuriko si ndio mtawaita wahaini kabisa kwa Kuingilia majukumu ya serikali?

Think Big
 
Kumbe Slaa bado anaexist? Jana nilijaribu sana kumtafuta kwenye maeneo ya matukio lakini sikumuona. Juhudi zangu pia ziligonga mwamba kumpata Mnyika na Mdee! Nashangaa leo Slaa anavyokuja kifua mbele kwenye makaratasi wakati kwenye eneo la tukio hakuwepo.

Ushauri wangu kwenu CDM..tunataka kuona vitendo na wala siyo propaganda! Kwa stahili yenu hii hamtakaa muitwe chama tawala kamwe!!

Wewe Rejao hautakaa uiite CDM Chama tawala lakini watanzania watakiita. Alafu,CDM Sio wanaokusanya kodi.
 
hv kule kwenu karatu umeweza mpakan mwa mbulu mea2 na ngorongoro au unarnpoka 2,hv we una sera unazi2mia wap wakati huna utawala cbir lada ukilud kanisan

Acha acheze na akili za waishio kwa matumaini....jamaa hali ngumu kwahiyo faraja yao kila siku ni maneno kama haya ambayo yanawafanya wajisikie ahueni...!!!
 
Kazi ya Vyama sio kutenda ya Serikali wewe usiyejua ulisemalo. Mwambie Rais wako asikusanye kodi basi kama unaona yeye ni wa kusaidiwa na Vyama na watu binafsi. Unakumbuka Sherehe za Uhuru ziligharimu zaidi ya Bilioni 64? Uliona Mbwembwe za Majeshi? Mara Karate, Mara wafundisha Mbwa, Mara ndege na mengine ya Mbwembwe tu si wangetoka huko kambini waje waokoe? Labda vitambi na miradi binafsi vimewazidi. Think b4 you talk
 
MKUTANO WA NNE
____________
MAJADILIANO YA BUNGE
___________
Kikao cha Arobaini – Tarehe 10 Agosti, 2006
(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)
D U A
Spika (Mhe. Samuel John Sitta) Alisoma Dua
HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI
Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:-
WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Taarifa ya Mwaka na Hesabu
za Taasis ya Utafiti wa Magonjwa Tanzania kwa Mwaka 2004/2005, (The Annual Report
and Accounts of the National Institute of Medical Research Tanzania for the year
2004/2005).
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:
Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa
Fedha 2006/2007.
MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO NA ARDHI: Maoni ya Kamati
ya Kilimo na Ardhi Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio
ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007.
MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI: Maoni ya Kambi ya Kambi
ya Upinzani Kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya
Wizara hiyo kwa Mwaka 2006/2007.



Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipoanzisha mpango huu wa kupima viwanja Dar es
Salaam, lengo letu kubwa lilikuwa kuondoa watu wa mabondeni ambao walikuwa karibu
na kaya 5,500 aliniambia Katibu Mkuu akiwa Mbunge kabla hajawa Katibu Mkuu



Mheshimiwa Mwenyekiti, inakadiriwa asilimia 70 ya wakazi wote wa Jiji la Dar
es Salaam, wanaishi katika maeneo yaliyojengwa kiholela na yenye msongamano
mkubwa na baadhi wamejenga sehemu za mabondeni na hivyo, kuhatarisha usalama wa
maisha na mali zao wakati wa mvua za masika
 
Back
Top Bottom