Tusiwalaumu wanaoilaumu CHADEMA kuhusu mafuriko Dar, ilaumiwe serikali kwa kuwanyima watanzania elimu ya uraia. Hawaelewe kazi ya Vyama vya siasa vya upinzani, kazi za mbunge na kazi ya mkusanya mapato ya watanzania. Hii ni moja ya sababu wabunge kudai posho kubwa ili kuwawezesha kuwa wafadhiri. "Pesa nyingine zinaishia milango ya Bunge wananchi wanakuja kuwaomba wabunge wao" sio maneno yangu kauli ya Pinda. Maana yake wabunge wa DAR wote(Mnyika, Zungu, Mdee,na wengine) , Dr SLAA, EL, Sitta, Sumaye watoe pesa kusaidia waathirika wa mafuriko. Anayekusanya kodi afanye nini?