Tamko la CHADEMA kuhusu Mafuriko lililotolewa na Dr. Slaa leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la CHADEMA kuhusu Mafuriko lililotolewa na Dr. Slaa leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiranja, Dec 22, 2011.

 1. K

  Kiranja JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 754
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA POLE KWA WANAFAMILIA NA WANANCHI KUHUSIANA NA JANGA LA MAFURIKO YALIYOKUMBA JIJI LA DAR ES SALAAM, MBEYA NA DODOMA .

  Usiku wa kuamkia tarehe 20.12.2011 Maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, Mbeya na Dodoma yamekumbwa na maafa makubwa ya mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa ambazo zimeendelea kunyesha mfululizo katika maeneo hayo.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kutoa pole za dhati kwa wanafamilia na wananchi wote ambao wamekumbwa na janga hili kubwa , kwani limesababisha maafa makubwa sana ya vifo, kupoteza mali na miundombinu mbalimbali kuharibiwa vibaya kwenye maeneo husika. Tunapenda kuwahakikishia wananchi hawa kuwa tutakuwa nao pamoja katika kipindi hiki kigumu katika maisha yao kutokana na madhara waliyopata yaliyosababishwa na maafa haya.

  Kutokana na janga hili limetukumbusha jambo moja kuwa kama Taifa hatujajiandaa kikamilifu kuweza kukabiliana na majanga kama haya pindi yanapotokea na hata vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeonyesha dhahiri kuwa havijaandaliwa kimfumo na kinyenzo katika kuweza kukabiliana na majanga kama haya na huu ni udhaifu mkubwa sana kwa taifa lenye miaka 50 baada ya uhuru wake .

  Mathalani mpaka sasa hatujaona jitihada zozote ambazo zimechukuliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa katika kuonyesha juhudi za kukabiliana na janga hili kubwa kwa taifa letu,hii inaonyesha wazi kuwa kitengo hiki hakijaandaliwa kuweza kukabiliana na maafa kama ambavyo majukumu yake yanavyopaswa kuwa . Na hii ni hatari kwani kama chombo cha kukabiliana na maafa hakiwezi kufanya hivyo kwa wakati ni kuendelea kuwaacha wananchi waendelee kupata madhara makubwa zaidi. Na haswa ikizingatiwa kuwa idara ya hali ya hewa ilishatahadharisha kuhusiana na mvua hizi.

  CHADEMA tunapenda kuikumbusha serikali kuhusiana na ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo ilieleza wazi kuhusiana na kukosekana kwa mifumo thabiti ya kujulisha umma kuhusiana na majanga mbalimbali katika miji yetu (Early Warning Systems) kama ambavyo ipo katika nchi nyingi , mfumo huu ni muhimu sana katika kuweza kuufanya umma uwe na elimu ya jinsi ya kuweza kujikinga na majanga haya kwa lengo la kupunguza madhara yasiwe makubwa kama ambavyo taifa hivi sasa linashuhudia.

  CHADEMA inapendekeza hatua zifuatazo ziweze kuchukuliwa haraka na serikali ili kuweza kukabiliana na majanga/maafa mbalimbali hapa nchini yanapojitokeza;

  I) Kuandaa mfumo wa awali wa kutahadharisha umma juu ya ujio wa majanga (Early Warning Systems) kwa kutumia vyombo na nyenzo mbalimbali ili kuepusha madhara makubwa kwa watu na mali zao.

  II) Kutunga sheria mpya ya ujenzi na kuweka viwango vya ujenzi viwe vyenye hadhi ya kimataifa na haswa ujenzi wa kuta mbalimbali na majengo marefu na kuhakikisha kuwa ujenzi holela haujitokezi kwenye miji na majiji yetu hapa nchini.

  III) Kuhakikisha kuwa kwenye miji yote mikubwa mtandao wa mabomba ya maji ya dharura unawekwa ili kuweza kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapotokea.

  IV) Serikali ijiandae mara moja kukabiliana na magonjwa ya milipuko kama vile kuhara ,kipindupindu na mengineyo ambayo yatajitokeza kutokana na mafuriko haya kuharibu miundombinu ya kusambaza maji, makazi ya watu n.k.

  V) Kitengo cha maafa kiwe na vifaa wakati wote , na haswa vifaa kwa ajili ya uokoaji na wawe na utaratibu wa kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuweza kutumia vifaa hivyo kuweza kujiokoa na sio kuacha hali iwe kama ambavyo imejionyesha Dar Es Salaam jana baada ya baadhi ya majaketi okozi kufikishwa kwa wahanga na kushindwa kuyatumia kikamilifu.

  VI) Serikali itoe elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa ya milipuko kwa wananchi waliokumbwa na mafuriko haya ili kuepusha wananchi wengi kukumbwa na magonjwa hayo pindi yakijitokeza.

  Mwisho tunapenda kuendelea kutoa pole kwa wanafamilia wote na wananchi kwa ujumla kutokana na madhara makubwa waliyoyapata , Mungu awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu.
  Tamko hili limetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA .

  ……………….

  DR. Willbroad P. Slaa.

  Katibu Mkuu –CHADEMA.


  22/12/2011.
   
 2. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Rais Wangu amenena, Je Fisadi Kikwete atatekeleza?
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tunashukuru kwa tamko, lakini pia wangekumbshwa kuhusu kujenga madaraja ya dharura ambayo yamekatwa na maji hasa kwa wakazi wa Tegeta, Bunju, Boko, Kunduchi nk. Sasa hivi magari hayavuki kwenda ngambo ya pili na maeneo ya mjini
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Rais anayeongoza kwenye mioyo ya Wananchi ametoa Tamko.
  Tunasubiri tamko kutoka kwa Rais anayetawala.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  tunashukuru
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni tamko zuri sana la kuwakumbusha na kuwapa mbinu walioko madarakani!
  Fedha za kutekeleza mapendekezo hayo ya CDM zipo kabisa!...shida ni misappropriation tu!
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Watu wanatumia pesa nyingi sana kukusanya watu kwa ajili ya mikutano, lakini kutumia hizo pesa kwa ajili ya kuwasaidia watu wahame haraka au kuwatangazia basi kuwa kuna hatari inakuja hakuna. We have to change, and the changes start now.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Anasubiri aandaliwe hotuba/tamko. zamani alikuwa anaandaliwa na January Makamba, siku hizi sijui nani anamwandalia.
   
 9. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Jana kuna vitu viwili vilinishangaza
  1. TBC1 kukusanya habari na kuziweka sandukuni kusubiri saa 2 usiku kama tunavyofanyaga tunaponunua nguo za watoto
  2. Mkazi mmoja kujitosa na mtumbwi wake kuokoa raia, yaani serikali haina?!
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Safi sana Dr. Slaa... ila toeni na chopa ikaokoe wahanga maana serikali hii legelege kutwa kulala... yani waziri mkuu anamsubiri rais aseme...mkuu wa jeshi nae hajiongizi mpaka rais hata kutoa chopa ili iokoe ama kuweka daraja la dharura wanajeshi wamelala,... wazee wa intelejensia ndio kabasa hawana hata vifaaa... kazi kweli kweli... kumbe hii issue ilikuwepo kwenye ilani ya chadema .. sasa magamba kwenye ilani yao kulikuwa na nini? katiba hakuna walikuwa na nini?
   
 11. k

  kipinduka Senior Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Helkopta ya kukod ipo wapi hata ruzuku imeisha
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  jk haelewi hata aanzie wapi
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  kutoka pale pfisini kwako manyanya hadi jangwani watu walipopatwa na mafuriko ni kilometa moja.kwanini hujaonekana ukiokoa watu unasubiri kutuhadaa na tamko kwenyevyombo vya habari?
   
 14. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  asante kwa pole yako doctor. Mungu aendelee kukulinda na kukubariki. safi dr. mia
   
 15. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #15
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Siku zote wakati wa mechi mashabiki ndiyo huwa wanatoa maelekezo utafikiri wao ndio wanaojua soka kuliko wachezaji. Subiri sasa akipewa mpira halafu aambiwe piga danadana. Doooooohhhh!
   
 16. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mtasema yote lakini mimi sintosahau utendaji wa huyu jamaa alikuwa anakwenda mwenyewe na kutoa maelekezo kwenye tukio si kuhutubia watu kwenye TV.

  [​IMG]
   
 17. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera sana rais wetu mtarajiwa 2015...
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Nimesoma Tamko la Chadema hakuna cha maana zaidi ya kukosoa...cha kujiuliza Chadema wamechangia nini kwa waathirika wa mafuriko? Au ni porojo tu? Tuliona kule Japan walichangangia dola 2000..

  Hapa nyumbani mmewasaidia nini au ndio ilo Tamko?
   
 19. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "mficha maradhi, kifo humuumbua"
  zile za kwenu mbili si zipo?
   
 20. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "Chloroquine ni chungu lakini ni dawa"
  Ulijihadaa mwenyewe,uliambiwa chagua serikali makini,ukachagua vilaza.hata kwenye Ilani haikuwepo kuboresha hico kitengo.Lakini ndio mkome kung'ang'ania kukaa kwenye mabonde.
   
Loading...