Tamko la CHADEMA Kanda ya Ziwa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU NA BARAZA KUU LA CHADEMA NA VIONGOZI WA BARAZA LA VIJANA MIKOA YA GEITA, MWANZA, SIMIYU NA KAGERA .
UTANGULIZI:
Ndg.waaandishi awali ya yote nichukue nafasi hii kuwashukuru wote kwa mwitikio wenu katika kikao hiki muhimu kwa mstakabali wa Taifa letu kama nilivyo jitambulisha hapo huu mimi ni Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Geita pia kamanda wa Redbragete kanda ya ziwa na Mwenyekiti wa Makatibu wa Mabaraza kanda ya ziwa Magharibi. Nipo hapa kusoma maazimio ya wajumbe wa Baraza kuu, mkutano mkuu na viongozi wa Baraza la vijana la Chadema mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu na Kagera kupinga na kulaani kile kilichoitwa UKAWA.
UDHAIFU WA UONGOZI WA CHADEMA
Tunaungana na kuwapongeza wajumbe wenzetu wa mikoa ya PWANI, DSM na TANGA waliokemea upuuzi huu mapema wiki hii.
Kwa kweli suala hili halivumiliki na si la kulichekea hata kidogo.
Ndg.Wanahabari itakubukwa kuwa chama chetu ni chama makini kinachoamini katika nguvu ya umma na siyo nguvu ya viongozi sasa cha kushangaza hapa viongozi wetu wameendelea kutuburuza sisi wanachama na viongozi wa ngazi za chini bila kushirikishwa katika maamuzi ya chama.Kwa mfano kitendo cha ubabe wa M/Kiti wetu kuendelea kufikiri kwa niaba yetu na kufanya maamuzi peke yake ni kutudhalilisha sisi kama viongozi na watanzania kwa ujumla.
Tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha viongozi wetu wa juu kufanya maamuzi ya kihuni na ya kifedhuri cha kususia bunge la KATIBA na sasa hivi kuanza kutoa masharti ya kitoto kwamba ili warudi Bungeni ni lazima yatekelezwe masharti hayo.
Tunasikitishwa na unafiki huu uliiopitiliza, viongozi wetu wamekubali kuwa sehemu ya matapeli wa kisiasa, wamekwenda kwenye BUNGE LA KATIBA wamekula posho zinazotokana na kodi zetu walala hoi, halafu wameacha kufanya walichotumwa.
Kuanzisha UKAWA na kususia BUNGE LA KATIBA ni muendelezo wa siasa za kinafiki, huu ni muendelezo wa mipango ile ile ya kuwahadaa Watanzania kupitia misimamo yetu isiyosadikika.
Njia bora na nzuri kwetu ni kupambana kupitia Hoja, na wabunge wetu wa katiba walipaswa pia kupambana kupitia Hoja na sio kukimbia Bungeni,
Kuungana na washirika wa CCM, ambao ni CUF na NCCR-MAGEUZI kwenye kufanya harakati hizi kunatupa wakati mgumu sisi wananchi na viongozi wa huku chini na Tunaamini kwamba kama imewezekana kwa viongozi wetu KUUNGANA NA CCM-B, kamwe haitashindikana siku moja MBOWE akituambia TUUNGANE NA CCM, na kwamba kwenye SIASA HAKUNA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU. Huu ni upuuzi na uzembe mkubwa wa kisiasa unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa.

Kususia vikao vya bunge la katiba kwa sababu tu SERIKALI TATU zinakataliwa na CCM, ni kudhihirisha kiasi gani kwamba viongozi wetu hawa ni WAROHO WA MADARAKA na kwamba wanataka kuutumia mchakato huu wa KATIBA MPYA kama ngazi yao ya kupata madaraka kiurahisi.
Kwanini CCM wao hawakususa na kutoka nje ya bunge baada ya kuona CHADEMA na CUF na wengineo wanapinga uwepo wa SERIKALI MBILI?. Kwanini tumewaruhusu wenzetu waendelee kupata platform ya bure kiasi hiki?. Viongozi wetu kwenye hili wameboronga na wanapaswa sio tu kujiudhuru lakini pia wanachapwe viboko hadharani kwa kutusaliti na kuzisaliti nafsi zao.
Tunapenda kuwakumbusha WALAFI HAWA WA MADARAKA, kwamba huku mikoani IDADI YA NAMBA ZA SERIKALI SIO AGENDA, huku kwetu tuna shida ya Mbolea, shida za ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla, migogoro ya mipaka, mkiundo mbinu, Afya na nyinginezo, mmesusa kushiriki vikao vya kuandaa katiba nani atatusemea haya maswala kama kweli mnajiita UKAWA ni umoja wa katiba ya wananchi?. ACHENI UNAFIKI
kwa kuwashirikisha CUF na NCCR Kwenye kambi rasmi bungeni kwani sisi kuna viongozi wa chama ngazi mikoa na wilaya tuliwahi kuhoji pale vionozi wetu waliposema hatuwezi kuwashirikisha CUF na NCCR kwani wao ni CCM .B na sisi tuliamini hivyo na kuona CUF na NCCR ni kikwazo kwetu sasa tunashangaa leo bila hata kuja kwetu sisi kama viongozi na wanachama kuelezwa kilichoibadilisha CUF na NCCR ghafla kutoka kwa CCM B.na kuwa wapinzani lmala? Sisi wanachama na viongozi bado tunaamini CUF na NCCR bado ni CCM B. tena iliyo kubuhu.Hatukubali hatukubali kuungana na vyama vinavyotumiwa na CCM.

Tunalaani kwa nguvu kubwa ujanja ujanja huu wa kisiasa, hatuwezi kukubali kutumiwa kila siku na mabwana wakubwa hawa na sisi tuendelee kuwavumilia na kuwakalia kimya kila uchao, tunataka waache kuendelea kutufanya sisi viongozi wa chini kama mandondocha wa kisiasa kama walivyo wao.

HITIMISHO.
Sisi kama viongozi wenye machungu na chama chetu tunaonya na kulaani kitendo cha chama chetu kuungana na CUF na NCCR kwa sababu vyama hivyo vinatumwa na CCM. Hatuko tayari kuendelea kubaliki upuuzi kama huu wa viongozi wetu kutumwa na kujinufaisha na familia zao huku sisi tukiishia maisha ya kuhangaika iko taarifa ya viongozi wetu kuhongwa na CUF ili kudhoofisha upinzani Tanzania kwa mwendelezo uleule wa upinzani maslahi.
Tunawataka viongozi wetu hawa waitishe mkutano wa BARAZA KUU haraka iwezekanavyo ili tulijadili swala hili na ikiwezekana tuwawajibishe kwa kujitwisha madaraka yasiyo yao.
Mkutano huo wa Baraza kuu uitishwe haraka iwezekanavyo na usisimamiwe na Mbowe wala Dkt.Slaa na badala yake usimamiwe na BARAZA LA WAZEE LA CHAMA kwa kuwa Mbowe, Dkt. Slaa na waganga njaa wenzake kwenye hili wao ni watuhumiwa.
Vile vile Tunatoa siku kumi na nne viongozi wetu kujitoa mala moja ndani ya genge hilo la UKAWA ili kunusuru upinzani nchini.
na wanandeni warejeshe kwani kwa chama chetu maana imani tayari imeshaanza kupotea baada ya siku hizo 14 kupita bila utekelezaji wa matakwa ya wanachama tuliowengi basi tutashawishi na kanda zingine nazo ziungane nasi kususia kushiriki shughuli za chama ikiwemo migomo na maandamano.
Nawashukuruni sana kwa kunisikiliza
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA;- wajumbe wa Baraza kuu na mkutano mkuu wa CHADEMA na wajumbe wa BARAZA LA VIJANA BAVICHA wa mikoa ya Geita, Simiyu, Kagera Na Mwanza.
Na limesomwa leo tqrehe 21.05.2014 hapa mkoani Geita nami

FIKIRI MIGIYO
………………………………

KATIBU WA BAVICHA MKOA GEITA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI TENDAJI BAVICHA TAIFA.
MWENYEKITI WA MAKATIBU WA MABARAZA YA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI
MKUU WA REDBRIGADE KANDA YA ZIWA.

TAARIFA YA BAADHI YA WAJUMBE WA BARAZA KUU NA MKUTANO MKUU CHADEMA MIKOA YA DSM, PWANI NA TANGA KUPINGA UHUNI WA KISIASA UNAOITWA UKAWA.

UTANGULIZI.
Ndugu wanaHabari, Tunapenda mtusaidie kufikisha ujumbe wetu huu kwa umma unaotokana na malalamiko na manung'uniko ya wanachama wenzetu wa CHADEMA kuhusu udhaifu mkubwa wa kiuongozi unaoendelea kwa sasa chini ya mwavuli wa UKAWA.
Kwa wiki kadhaa sasa, kumeibuka msamiati mpya wa kisiasa wa UKAWA uliopelekea mpaka kuundwa kwa BARAZA KIVULI LA UKAWA pale Bungeni bila kufuata Utaratibu.

Sisi viongozi ambao miongoni mwetu ni Wajumbe wa vikao halali vya chama, ambavyo ni Baraza Kuu na Mkutano mkuu wa chama kutoka mikoa ya Tanga, Pwani na DSM kwa masikitiko makubwa tunasema kuwa hatupendezeshwi na mwenendo huu wa chama unaofanywa na viongozi wetu wakuu.

KUSUSIA BUNGE LA KATIBA.
Ndugu wanaHabari,
Kwa namna ambavyo tumepambana kwa miaka mingi kudai na kuishinikiza serikali kuridhia uandikaji wa katiba mpya, ni -------- pekee anayeweza kususia fursa ya uandishi huo tena kupitia chombo huru (BUNGE LA KATIBA) kwa sababu tu ya mgongano wa kimaslahi.

Tunasikitika sana kuwaona viongozi wetu na wabunge wa chama chetu cha CHADEMA wamesahau kazi tuliyowatuma ya kwenda kuandika katiba mpya yenye kuzingatia maslahi ya wananchi badala yake wamekwenda kupigania vyeo.

Tumefedheheshwa sana na namna ambavyo wawakilishi hawa wamekubali kutanguliza mbele maslahi yao na kuyaacha maslahi ya wananchi ambao ndio waliuowatuma, kwenye Rasimu yenye sura zaidi ya 18 ni uzezeta kususia sura 2 tu za mwanzo kisa tu maslahi yao ya kugawana vyeo wanaona hayawezi kutekelezeka.

Tunaomba ifahamike kwamba, hakujawahi kukaliwa kikao chochote halali cha chama chetu kilichoazimia na kuwaagiza wajumbe wanaotokana na chama chetu wasimamie katiba yenye SERIKALI TATU, na ikionekana haiwezekaniki WASUSE NA KUTOKA NJE YA BUNGE.-

Huu ni udhaifu unaotawaliwa na uroho wa madaraka, sisi kama viongozi halali wa kikatiba wa chama hatujawahi kuwaza wala kuamua kuhusu ujinga huu, siku zote tumekuwa tukiwasisitiza wajumbe wetu kwenye fursa yoyote watakayoipata kwenda kusimamia mawazo na misimamo ya wananchi ambao ni wanyonge,

-Tunawatuma wajumbe wetu kuhakikisha tunapata katiba itakayosimamia na kuzitunza Rasilimali zetu, na wala si kweli kuwa Idadi ya Serikali kama ni 3 au 2 au 5 au zozote inaweza kuwa muarobaini wa changamoto zetu.

Daima dumu tumekuwa tukiamini kwenye mapambano ya Hoja ambayo ndio msingi mkuu wa demokrasia ya kweli Tunayoisimamia kama CHADEMA.

Hivyo Basi tunasema, si sahihi hata kidogo kwa wajumbe wetu wa Bunge la katiba kususia vikao vile na ndio maana hata baadi ya wabunge wengi wa chama chetu wamekuwa wakilalamika chini chini kwetu sisi wajumbe wa baraza kuu kwamba wamechoka sasa kuburuzwa na viongozi wakuu wa chama na kwamba wao nao wana mawazo na misimamo yao, sasa kwa niaba yao pia tumeona kama viongozi wa chama -tulikemehe hili.

- Nipo tayari kuyataja majina ya wabunge hawa wanaolalamika kuburuzwa ambao ni zaidi ya wabunge 31 wa kuchaguliwa na wa viti maalum.

Muungano wetu huu wa UKAWA ni muungano wa kinafiki usiokuwa hata na hadidu za rejea, hakunaga muungano duniani kote ambao waunganaji wake wanaungana kiujanja ujanja tu kama walivyofanya viongozi wetu hawa. Hatuungi mkono na tunawataka wasiendelee na upuuzi wao huu, warudi bungeni kama hawataki wajitoe tuchague wabunge wengine watakaowawakilisha wananchi wanaotuamini.

Ni sawa na ndoa ya mkeka, hakuna maridhiano, hakuna vikao, asubuhi wapenzi jioni wana ndoa, ndoa ya namna hii kamwe haiwezi ikadumu hata kidogo.

BARAZA KIVULI LA UKAWA.
Tunasikitika sana na kitendo cha mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe, kutufanya sisi wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu hatuna maana kwenye kufanya maamuzi ya chama.

Walituaminisha kwamba CUF wamefunga ndoa na CCM na kwamba wao ni sehemu ya serikali hivyo hawawezi kushirikiana na chama ambacho ni sehemu ya serikali, kwa msingi huu tukaazimia kwenye vikao vya chama ambavyo ni halali kwamba chama chetu hakitashirikiana na chama kingine chochote cha siasa kwa kuwa ni washirika wa CCM na kwamba wao ni CCM-B

Tumemkashigu na kumtuhumu James Mbatia na NCCR nzima kuwa ni Tawi la CCM na ndio maana hata Mbatia ameteuliwa kuwa Mbunge, inakuwaje leo tunashirikiana na watu hawa ambao wanatumiwa na CCM?.

Ni lini Muungano wa CCM na CUF umevunjika rasmi?.

Ni lini ushirikiano wa NCCR ya MBATIA na CCM umekufa rasmi?.

Je mazingira yaliyofanya tuwahesabu wenzetu hawa kuwa ni CCM B leo yamebadilika?, na kama yamebadirika yamebadilika lini na yamebadilikaje?.

Je sio kweli kwamba tuliwatenga wenzetu na kuwakashifu kwa sababu tu ya uchu wa madaraka?.

Yaani sio kweli kwamba tuliwafedhehesha wenzetu hawa kwa sababu ya UWAZIRI KIVULI?. Na leo tunawasafisha wenzetu hawa kwa UWAZIRI KIVULI HUO HUO.

Kwanini viongozi wetu wanakuwa na UCHU na UROHO wa MADARAKA kiasi hiki?.-

Kama tunaweza tukawaita wenzetu MASHETANI asubuhi na jioni tukawaita MALAIKA kwa sababu ya UWAZIRI KIVULI, je tukipewa nchi na kushika dola, si Tutawaita wenzetu majina mabaya zaidi?.

Si tutakuwa na serikali mbovu nay a ajabu zaidi ya hivi sasa tulivyo kwenye siasa za upinzani tu tulio nao?.

Kwa misingi huu, Tunaamini kuwa UKAWA ni UNAFIKI WA KISIASA, na umebuniwa kwa sababu moja tu nayo ni kugawana vyeo, hakuna sababu yoyote yenye mantiki iliyopo kwenye uundwaji wa UMOJA huu na ndio maana hauna hadidu za rejea wala hauna hati za makubaliano miongoni mwetu.

Napenda kuwaambia watanzania kuwa sisi baadhi yab wajumbe wa Baraza kuu na mkutano mkuu wa mikoa ya Pwani, Dsm na Tanga hatuungi mkono upuuzi wowote wenye lengo la kusimamia ugawanaji wa vyeo na madaraka, watu wa namna hii tunawaita WALAFI wa MADARAKA.

Tunaunga mkono watanzania wote wanaoitakia heri Tanzania yetu.
Mungu ibariki Tanzania
Imeandaliwa na-
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Mikao ya Pwani,-
DSM na TANGA

Na imesomwa nami
……………………………………………………
JOSEPH YONA PATRICK
+255713802226

Mwenyekiti wa CHADEMA WILAYA YA TEMEKE
Mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa TEMEKE
MJUMBE WA BARAZA KUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI YA UTENZAJI BAVICHA TAIFA
haki at Monday, May 19, 2014​

  • Mbona font zinafanana format ya uandishi au ndio wasaliti wanawafundisha kuandika ........................................................

    wito kwa ndugu zangu wa CHADEMA hawa jamaa ni wa kuwapuuza na lengo kubwa ni kutaka kuwatoa watanzania kwenye malengo makubwa ambayo ni bajeti na katiba

    NB
    Kamwambie wanaokutuma kuwa vijana wa chadema we are very smart than how they can think , na tupo makini sana thus why zitto and their fallow they have decided to run from Jamii forum despite the fact they are getting support from some of the modes

Chadema kinakera lakini kwa upande mwingine hebu tuangalie kwa umakini haya mambo hivi hawa siyo mapindikizi kweli ambayo yanavuruga chadema hasa baada ya kuonekana kuwa chama kinashikwa na familia moja pengine watu wameamua liwalo naliwe sasa.
 
UKAWA ndio mpango mzima,subirini iwaingie sawasawa
Mtu anayetaja neno ukawa namuona kama kichwani hayuko sawa ni genge la wachumia tumbo fulani halafu wengine ndiyo mmekomaa nao kweli kutojitambua ni jambo baya sana pole mkuu.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAARIFA YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU NA BARAZA KUU LA CHADEMA NA VIONGOZI WA BARAZA LA VIJANA MIKOA YA GEITA, MWANZA, SIMIYU NA KAGERA .
UTANGULIZI:
Ndg.waaandishi awali ya yote nichukue nafasi hii kuwashukuru wote kwa mwitikio wenu katika kikao hiki muhimu kwa mstakabali wa Taifa letu kama nilivyo jitambulisha hapo huu mimi ni Katibu wa Baraza la Vijana Chadema Mkoa wa Geita pia kamanda wa Redbragete kanda ya ziwa na Mwenyekiti wa Makatibu wa Mabaraza kanda ya ziwa Magharibi. Nipo hapa kusoma maazimio ya wajumbe wa Baraza kuu, mkutano mkuu na viongozi wa Baraza la vijana la Chadema mikoa ya Geita, Mwanza, Simiyu na Kagera kupinga na kulaani kile kilichoitwa UKAWA.
UDHAIFU WA UONGOZI WA CHADEMA
Tunaungana na kuwapongeza wajumbe wenzetu wa mikoa ya PWANI, DSM na TANGA waliokemea upuuzi huu mapema wiki hii.
Kwa kweli suala hili halivumiliki na si la kulichekea hata kidogo.
Ndg.Wanahabari itakubukwa kuwa chama chetu ni chama makini kinachoamini katika nguvu ya umma na siyo nguvu ya viongozi sasa cha kushangaza hapa viongozi wetu wameendelea kutuburuza sisi wanachama na viongozi wa ngazi za chini bila kushirikishwa katika maamuzi ya chama.Kwa mfano kitendo cha ubabe wa M/Kiti wetu kuendelea kufikiri kwa niaba yetu na kufanya maamuzi peke yake ni kutudhalilisha sisi kama viongozi na watanzania kwa ujumla.
Tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha viongozi wetu wa juu kufanya maamuzi ya kihuni na ya kifedhuri cha kususia bunge la KATIBA na sasa hivi kuanza kutoa masharti ya kitoto kwamba ili warudi Bungeni ni lazima yatekelezwe masharti hayo.
Tunasikitishwa na unafiki huu uliiopitiliza, viongozi wetu wamekubali kuwa sehemu ya matapeli wa kisiasa, wamekwenda kwenye BUNGE LA KATIBA wamekula posho zinazotokana na kodi zetu walala hoi, halafu wameacha kufanya walichotumwa.
Kuanzisha UKAWA na kususia BUNGE LA KATIBA ni muendelezo wa siasa za kinafiki, huu ni muendelezo wa mipango ile ile ya kuwahadaa Watanzania kupitia misimamo yetu isiyosadikika.
Njia bora na nzuri kwetu ni kupambana kupitia Hoja, na wabunge wetu wa katiba walipaswa pia kupambana kupitia Hoja na sio kukimbia Bungeni,
Kuungana na washirika wa CCM, ambao ni CUF na NCCR-MAGEUZI kwenye kufanya harakati hizi kunatupa wakati mgumu sisi wananchi na viongozi wa huku chini na Tunaamini kwamba kama imewezekana kwa viongozi wetu KUUNGANA NA CCM-B, kamwe haitashindikana siku moja MBOWE akituambia TUUNGANE NA CCM, na kwamba kwenye SIASA HAKUNA ADUI WALA RAFIKI WA KUDUMU. Huu ni upuuzi na uzembe mkubwa wa kisiasa unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa.

Kususia vikao vya bunge la katiba kwa sababu tu SERIKALI TATU zinakataliwa na CCM, ni kudhihirisha kiasi gani kwamba viongozi wetu hawa ni WAROHO WA MADARAKA na kwamba wanataka kuutumia mchakato huu wa KATIBA MPYA kama ngazi yao ya kupata madaraka kiurahisi.
Kwanini CCM wao hawakususa na kutoka nje ya bunge baada ya kuona CHADEMA na CUF na wengineo wanapinga uwepo wa SERIKALI MBILI?. Kwanini tumewaruhusu wenzetu waendelee kupata platform ya bure kiasi hiki?. Viongozi wetu kwenye hili wameboronga na wanapaswa sio tu kujiudhuru lakini pia wanachapwe viboko hadharani kwa kutusaliti na kuzisaliti nafsi zao.
Tunapenda kuwakumbusha WALAFI HAWA WA MADARAKA, kwamba huku mikoani IDADI YA NAMBA ZA SERIKALI SIO AGENDA, huku kwetu tuna shida ya Mbolea, shida za ajira kwa vijana na jamii kwa ujumla, migogoro ya mipaka, mkiundo mbinu, Afya na nyinginezo, mmesusa kushiriki vikao vya kuandaa katiba nani atatusemea haya maswala kama kweli mnajiita UKAWA ni umoja wa katiba ya wananchi?. ACHENI UNAFIKI
kwa kuwashirikisha CUF na NCCR Kwenye kambi rasmi bungeni kwani sisi kuna viongozi wa chama ngazi mikoa na wilaya tuliwahi kuhoji pale vionozi wetu waliposema hatuwezi kuwashirikisha CUF na NCCR kwani wao ni CCM .B na sisi tuliamini hivyo na kuona CUF na NCCR ni kikwazo kwetu sasa tunashangaa leo bila hata kuja kwetu sisi kama viongozi na wanachama kuelezwa kilichoibadilisha CUF na NCCR ghafla kutoka kwa CCM B.na kuwa wapinzani lmala? Sisi wanachama na viongozi bado tunaamini CUF na NCCR bado ni CCM B. tena iliyo kubuhu.Hatukubali hatukubali kuungana na vyama vinavyotumiwa na CCM.

Tunalaani kwa nguvu kubwa ujanja ujanja huu wa kisiasa, hatuwezi kukubali kutumiwa kila siku na mabwana wakubwa hawa na sisi tuendelee kuwavumilia na kuwakalia kimya kila uchao, tunataka waache kuendelea kutufanya sisi viongozi wa chini kama mandondocha wa kisiasa kama walivyo wao.

HITIMISHO.
Sisi kama viongozi wenye machungu na chama chetu tunaonya na kulaani kitendo cha chama chetu kuungana na CUF na NCCR kwa sababu vyama hivyo vinatumwa na CCM. Hatuko tayari kuendelea kubaliki upuuzi kama huu wa viongozi wetu kutumwa na kujinufaisha na familia zao huku sisi tukiishia maisha ya kuhangaika iko taarifa ya viongozi wetu kuhongwa na CUF ili kudhoofisha upinzani Tanzania kwa mwendelezo uleule wa upinzani maslahi.
Tunawataka viongozi wetu hawa waitishe mkutano wa BARAZA KUU haraka iwezekanavyo ili tulijadili swala hili na ikiwezekana tuwawajibishe kwa kujitwisha madaraka yasiyo yao.
Mkutano huo wa Baraza kuu uitishwe haraka iwezekanavyo na usisimamiwe na Mbowe wala Dkt.Slaa na badala yake usimamiwe na BARAZA LA WAZEE LA CHAMA kwa kuwa Mbowe, Dkt. Slaa na waganga njaa wenzake kwenye hili wao ni watuhumiwa.
Vile vile Tunatoa siku kumi na nne viongozi wetu kujitoa mala moja ndani ya genge hilo la UKAWA ili kunusuru upinzani nchini.
na wanandeni warejeshe kwani kwa chama chetu maana imani tayari imeshaanza kupotea baada ya siku hizo 14 kupita bila utekelezaji wa matakwa ya wanachama tuliowengi basi tutashawishi na kanda zingine nazo ziungane nasi kususia kushiriki shughuli za chama ikiwemo migomo na maandamano.
Nawashukuruni sana kwa kunisikiliza
TAARIFA HII IMEANDALIWA NA;- wajumbe wa Baraza kuu na mkutano mkuu wa CHADEMA na wajumbe wa BARAZA LA VIJANA BAVICHA wa mikoa ya Geita, Simiyu, Kagera Na Mwanza.
Na limesomwa leo tqrehe 21.05.2014 hapa mkoani Geita nami

FIKIRI MIGIYO
………………………………

KATIBU WA BAVICHA MKOA GEITA
MJUMBE WA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA TAIFA
MJUMBE WA KAMATI TENDAJI BAVICHA TAIFA.
MWENYEKITI WA MAKATIBU WA MABARAZA YA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI
MKUU WA REDBRIGADE KANDA YA ZIWA.

Kama kweli mtoa mada ni kiongozi, hafai kabisa kuongoza hata wanyama!
Na kama ni kijana basi ni mchawi au hajui kabisa nyumba za ibada wala kufika!
Binadamu gani unaependa kuchochea chuki watu wachukiane na kugombana.
Kuna kosa gani waliokosana wakapatana, siku zote tunaomba Mungu ccm waache dhambi tuungane ili tuwe kitu kimoja, nakushangaa mtoa mada unachukia viongozi wako kupatana na waliokosana, ama kweli wewe umevurugwa
Mungu akusamehe.
 
mwenye akili timamu anajua wazi kuwa tamko hili ni la ccm kwa kutumia mamluki wao...
 
Sasa chadema waungane na ccm, chama cha amani na mshikamano
kwenye mshikamano haki hutendeka lkn cyo ccm ambako dhuluma ni maisha ya kawaida kwa kifupi ccm ni genge la wahalifu,wauza madawa ya kulevya,majangili,wezi wamali za umma,na mambo mengine ya ovyo.
 
Wewe Mleta mada huna akili. nasijui waliwezaje kukupa vyeo vyote hivyo wakati unaonekana kabisa amnazo.kama kiongozi mwenye maadili na anaejua thamani ya chama chake, ungelitambua ni wapi ungetakiwa kupeleka malalamiko yako.minaona kama vile unajipalilia ili angalau usikike,ungekuwa na vijisenti kidogo basi kutwa tungekuona kwenye magazeti.jina halijengwi kupitia migongo ya wenzako.unaongelea nguvu ya hoja,wewe mbona ukupeleka hiyo hoja sehemu usika na kuitetea,matokeo yake unaileta uku.upate msaada gani? mpaka sasa hujajua ni nani mmiliki wa katiba mpya.pole sana kaka.kwatabia hii sitoshangaa siku ukianika hadharani matatizo yako na mkeo.mtageuka sana wachumia tumbo kisa 2015,ndugu CCM inawenyewe,nyie mtatumiwa kama kond....m nakisha kutupiliwa mbali.chezea CCM wewe

Baba Anjela,huyu jamaa si lolote ni nape baada yakuona habari ya ukanda, udini na ukabila kwenye ukawa hautaeleweka wamebuni huu mpango mpya wa kuchonganisha viongozi na wanachama,taarifa kwa nape,mwigulu na jangili sugu jipangeni upya hii haina mashiko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom