Tamko la chadema geita juu ya mh. Godbless lema_04/11/2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la chadema geita juu ya mh. Godbless lema_04/11/2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyota Njema, Nov 4, 2011.

 1. N

  Nyota Njema Senior Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA WOTE WA WATANZANIA

  TAMKO LA CHADEMA WILAYA YA GEITA JUU YA UNYANYASWAJI WA HAKI YA KIDEMOKRASIA ANAYOFANYIWA MH.GODBLESS LEMA (MB) NA WANACHADEMA WOTE WA ARUSHA KWA UJUMLA HATA KUPELEKEA MBUNGE LEMA KUAMUA KUJIPELEKA RUMANDE KWA HIARI. 4 NOVEMBA 2011
  [FONT=Arial,Arial Narrow][FONT=Arial,Arial Narrow]Katibu wa Chadema wa wilaya ya Geita Mh. Rogers J Ruhega ametoa tamko la kulaani vikali juu ya mwenendo wa wa utendaji wa jeshi la polisi Tanzania na hususani Mkoa wa Arusha unaoonyesha wazi kwamba wanatekeleza kazi zao si kwa weledi wa taaluma yao waliyoapa kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwatumikia watanzania bali inaoonekana wazi wanafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya watawala walioko madarakani na viongozi Chama cha Mapinduzi kwa ujumla wasio na nia njema na maendeleo ya kweli ya wananchi wanyonge. Kwa niaba ya CHADEMA Wilaya ya Geita na Wananchi wote wapenda haki, maendeleo na mabadiliko , tumesikitishwa sana na utendaji kazi wa jeshi la polisi hususani OCD wa wilaya ya Arusha unaoonekana unakandamiza kwa makusudi ya wazi kabisa haki ya kisheria kwa Mbunge wa Arusha Mh. Godbless Lema na Chadema Mkoa wa Arusha katika kutimiza mjkukumu yao ya kimsingi ya kusimamia na kuwaletea maendeleo Watanzania wa Arusha. CHADEMA tumesikitishwa na tunaendelea kusikitishwa sana kwani mkakati huu unaoonekana ni makusudi ya wazi wa serikali legelege na chama chake vinavyoonekana kushindwa kabisa kuwatimizia mahitaji yao ya kimsingi ya kimaendeleo kama walivyoahidi kwenye ilani yao ya uchaguzi,kama kudhibiti mfumuko wa bidhaa muhimu kama sukari iliyopanda na kufikia wastani wa Tsh. 2500 hadi 4500/=, sabuni mwichi mmoja kufikia 2,000/= mafuta ya taa lita moja inafikia Tsh. 2050/= n.k ndani ya Nchi yetu na hivyo kutafuta uungwaji mkono wa huruma za wananchi kwa kujikita katika siasa za propaganda za kuwahadaa kupitia kuvipaka matope vyama vyetu vya mageuzi na viongozi wetu wa vyama na wawakilishi wa wananchi kama Mh. Godbless lema eti wanahamisisha vurugu,hawafuati sheria na kwamba hii inaweza kupelekea kuhatarisha amani ya Nchi.
  Katibu huyo wa Wilaya ambaye pia ndiye aliyesimama kwa tiketi ya chadema kwa nafasi ya ubunge jimbo la Geita Mh. Rogers Ruhega alihoji, Watanzania wenzangu tuwe wawazi na wahalisia pasipo kuwa na unafiki wowote ndani ya mioyo yetu ni lini viongozi wetu wa Chadema ama wanachama wamekuwa ni chanzo cha kuvunja sheria za Nchi kama siyo Viongozi wa CCM na serikali yao iliyoko madarakani kwa kiburi cha madaraka na nia mbaya ya kuvikandamiza vyama vya siasa vya mageuzi ya kweli kama chadema vilivyo mstari wa mbele katika kupigania haki za wanyonge vijijini na mijini katika kuelekea uhuru wa kweli na maendeleo ya kweli ili kujihalalishia kubaki madarakani kwa nia ya kulinda maslahi ya matumbo yao na familia zao.
  Ukandamizaji na unyanyasaji wa jeshi la polisi unaoonekana kila mahali hapa Nchini na unaoonekana wazi unatekelezwa kwa maagizo ya watawala walioko madarakani na Chama cha mapinduzi kwa ujumla, haya yametokea pia Mjini mpanda pale Mh. Diwani wa Chadema kata ya makanyagio Ndugu Idd Nziguye alipofungwa Gezerani juzi eti kwa sababu tu ya kuwahamasisha Wananchi wa Kata yake wasihamie soko jipya lililo mbali na makazi ya wananchi na kubakia eneo la wazi na kuendelea kufanya biashara zao. Hapa tujiulize watanzania wenzangu ni maeneo mangapi CCM na Serikali yake wamewapa mafisadi kwa rushwa na mpaka sasa wanayashikilia bila faida yoyote kwa Watanzania na hawajafikishwa mahakamani na hawajafungwa?. Kwa mujibu wa Mh. Ruhega Maelekezo haya ya manyanyaso yanayofanywa kwa maelekezo ya Uongozi wa CCM kwa jeshi la polisi kwa Wanachama wetu na viongozi wa chadema kwa yametokea pia katika kata za Kasamwa na Rwamgasa zote zilizomo ndani ya wilaya ya Geita Mkoa wa Mwanza na mahali pengi ndani ya Wilaya ya Geita. Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kutoka kwa Wanachadema wenzetu wa Arusha, kwa makusudi kabisa Ijumaa ya Tarehe 28, polisi alivamia ofisi ya Mbunge akiwa na zaidi ya polisi 80, kwenye magari matatu na kuanza kuwapiga,na kuwadhalilisha wapiga kura waliokuwa ofisini,tendo hili ovu lilifanyika kwa kisingizio kuwa kuna maandamano na mkutano, hatimaye hawa wananchi walifikishwa polisi na kufunguliwa mashtaka ya kuandamana bila kibali. Wengi wa waliokamatwa alikuwemo diwani wa CHADEMA kutoka DSM aliyekuja Arusha kwa safari yake binafsi na aliamua kwenda ofisini kwa mbunge kumsalimia. Mhe Azuri (Diwani) huyu akakutana na azama hii na sasa nae ana kesi mahakamani ya maandamano na kufanya mkutano wa hadhara, aibu tupu hii kwa jeshi la polisi kufanya kitendo hiki.
  Jumatatu tarehe 31.10.2011 wananchi pamoja na mbunge walifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya kufanya mkutano kinyume cha sheria, hatimaye wapiga kura 19 walitoka kwa dhamana hadi 19 Novemba. Mbunge wa Arusha mjini alikataa dhamana kama njia ya kukataa uonevu, ukandamizaji,na dhuluma inayofanywa na polisi dhidi ya raia wema wa Arusha na Tanzania kwa ujumla. Kimsingi ni maamuzi magumu ila lazima yafanyike. Polisi wamekuwa na tabia na utamaduni wa kutisha wananchi,na kuwaogofya kuwa watawapeleka ndani(GEREZANI) kama vile gerezani ni adhabu kubwa sana. Mbunge Lema ameamua kwa hiari yake mwenyewe kutangulia CHADEMA tunatambua mbinu na mikakati yote inayofanywa na Serikali kwa kutumia polisi na usalama wa taifa mipango hii ina lengo la kukwamisha maendeleo ya Arusha, ili wananchi wakate tamaa na kuichukia CHADEMA, lakini pia kuna mipango michafu ya kuwabambikia Kesi viongozi wa CHADEMA pamoja na vijana na wanachama walio msitari wa mbele. CHADEMA Wilaya ya Geita tunaupongeza ujasiri huu wa Mbunge wa Arusha mjini,na tunawataka wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi wote wa Tanzania kuamka na kupinga dhuluma, uhuni, ukandamizaji na ukiukwaji huu wa sheria kwa vitendo. Ni wajibu wa kila mmoja mpenda haki kuungana na harakati za Chadema Nchi nzima na Mh. Lema katika kipindi hiki cha kuelekea ukombozi wa kweli wa kifikra na kimaendeleo ifikapo 2014.2015.
  [/FONT]
  [/FONT]Mwisho kabisa bwana Rogers Ruhega alimalizia kwa kutoa mapendekezo yafuatayo kwa utekelezaji juu ya suluhu za hali ya kisiasa za Arusha mjini;
  1. Watawala na Chama cha mapinduzi wawe makini sana katika kuwatumikia Watanzania kama walivyong`ang`ania kubaki madarakani kupitia uchaguzi mkuu uliopita pamoja na dallili zote zilizoonyesha kuwa walikuwa wamepoteza ushawishi kwa watanzania kwa kiasi kikubwa sana na wakijua wazi kwamba wakati wa kuwaburuza watanzania umekwishapita,Watanzania wa leo si wale wa miaka ya ndiyo mzee kwa kila jambo bila kuwa na uwezo wa kuhoji umeshapita.
  2. Chadema sasa ni Chama kikuu cha upinzani na kilchoenea Nchi nzima na chenye ushawishi mkubwa karibu kwa watanzania wote wasio na vyama pia wanaohitaji haki ya kimsingi ya kimaendeleo ya kweli yanayotokana na rasilimali nyingi sana na utajiri wa kutisha kupitia maliasili tuliopewa na mwenyezi Mungu na ambayo tumeyakosa kupitia Serikali legelege ya CCM,na maendeleo haya Watanzania wanayoshauku na matumaini makubwa sana kuyapata kupitia Serikali ijayo ya Chadema kwa ridhaa yao wenyewe ifikapo 2014/2015, `kwa maana hiyo basi tunaitaka Serikali kwa ujumla kumtendea haki stahiki na heshima anayostahili Mh, Mbunge Godbless Lema kama mwakilishi wa Wananchi katika kuwatumikia Wananchi wa Jimbo lake la Arusha mjini na kuepuka kunyanyasa kwa namna yoyote tena ili mradi havunji sheria. Kinyume cha kufanya hayo na kendelea kwanyanyasa wanachama, viongozi na wawakilishi wa wa Wananchi kupitia Chadema kutapelekea nguvu kubwa ya UMMA iliyo nyuma ya Chadema kuidai haki hiyo kwa nguvu ya Umma Nchini kwote.

  3. Chadema wilaya ya Geita inamtaka OCD wa Arsha afanye kazi zake kwa mujibu wa sheria na siyo kwa maagizo ya watawala wenye hila na haki za watanzania wapenda haki za wanyonge na viongozi wa Chama cha Mapinduzi na kisha amfutie makosa yote aliyoyaongoza katika kumbambikizia kesi Mh. Godbless Lema (MB) kabla ya siku aliyopangiwa kufikishwa mahakamani.Kinyume cha hapo OCD huyu aangalie asitumike vibaya hata kupelekea kuleta Wanachadema na wapenda haki wote Nchini kuanza kidai haki ya Mh. Lema, Viongozi wote wa Chadema,Wanachama na Wananchi wanyonge wanaokandamizwa kwa mabavu na Jeshi la Polisi kwa maelekezo ya watawala na viongozi wa CCM kwa kutumia nguvu ya umma, na ikumbwe kwamba hata wahenga wetu walisema ` Hata mti wa aina ya Mbuyu ulianza na ukubwa wa mmea wa Mchicha’. [FONT=Arial,Arial Narrow][FONT=Arial,Arial Narrow]Naomba kuwasilisha;Mungu wabariki Watanzania,
  Mungu Ibariki Tanzania.
  [/FONT]
  [/FONT]Rogers J. Ruhega
  KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA – GEITA
  [FONT=Cambria,Cambria][FONT=Cambria,Cambria]
  My take; Matamko kama haya yanategemewa nchi nzima, sipati picha ni nini kitatokea baada ya hapo! Mungu ibariki Tanzania.[/FONT][/FONT]
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  VIPI HILI LA USHOGA HAWALITOLEI TAMKO? AU HALIMA MASLAHI KWA TAIFA? thehe thehe thehe, mnisamehe mimi nimeuliza tu. Najua mh. MBOWE angakuwa karibu na mimi angeamuru nikatwe kichwa.
   
 3. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ujumbe utakua umewafikia hao 'mangimeza'
   
 4. M

  Maswi JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 897
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  watakuwa wameupata ujumbe wao
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Leo nilikutana na OCD Mwombeji tumezungumza naye kwa muda kuhusu usalama, huku nikiwaza alivyoniita Panya siku ile. Kweli utawala wa sheria Tanzania ni ndoto!
   
 6. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,514
  Likes Received: 2,066
  Trophy Points: 280
  Ushoga hawataki kuutolea tamko au wanapima upepo wabongo 2po upande gan.?
   
 7. j

  jigoku JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Message sent kamanda,na mafisadi wameupata,kupitia JF maana kuna vibaraka wa kuwapelekea habari walafi hawa
   
 8. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Ushoga unawahausu hao serikali wanaosubili msaada toka uk! By the way wameshatolea tamko
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Na bado tutasikia matamko mengi sana safari hii
   
 10. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Tanguliza ubongo mbele halafu hisia zifuate nyuma mkuu, hii thread haihusiani na ushoga kama vipi mbona kuna thread nyingi humu zinazoongelea suala la ushoga, ua ulipotea njia?
   
 11. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Kila apandae upepo huvuna tufani, serikali ya ccm kama itaendelea kupanda huu upepo na wajiandae kuvuna hilo tufani
   
 12. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Ushoga ni hiari ya mtu kuamua kubanduliwa au kubandua.
   
 13. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu jamaa si nasikia alishinda ubunge ila akapewa pesa ili aachie jimbo? Leo katoa wapi ujasiri wa kusemea maovu ya watu aliokubali kuwaacha waendelee kutafuna nchi yetu, wakati angeliweza kuungana na watetezi wengine wa wanyonge akiwa mjengoni.
   
 14. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ninaimani matamko yatakoma kama uovu ukikoma
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kwa mjibu wa nape kuwa nchi hii inawenyewe...lakini bahati mbaya hawa wenye nchi dalili zote zinaonyesha kuwa ni mashoga mfano kujichupua, kulipiwa vyumba vya kulala wageni na kununuliwa na waarabu..
   
 16. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CDM ni chama tawala mbadala ni muda umebaki ikabidhiwe nchi 2015.Hivyo utegemee ijiingize kwenye mitego ya magamba.
   
 17. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Bado tamko la Arusha na Moshi.
   
 18. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  hizo ni ndoto za mchana. Hatuwezi kuwapa nchi watu wanaodhaminiwa na mashoga.
   
 19. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  miaka 50 tanzania inadhaminiwa nahao mashoga sijajua unamanisha nini huwataki ccm au cdm mkuu funguka
   
 20. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuuu, Gadafi hakujua kama yatamkuta yaliomkuta.OCD HUYO ajui kesho itakuwa vip mtumemsiki kwa kauli yake
   
Loading...