Tamko la CCM: Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, yaipongeza Serikali ya awamu ya tano

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitazungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali majira ya saa saba na nusu mchana huu katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Updates:-

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ameshaingia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Makao Makuu na anazungumza na waandishi wa habari hivi sasa,
attachment.php

Kinana akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba.

CVse8W5VEAACocz.jpg

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye Press ya Katibu Mkuu wa CCM.

=========================

Updates:-

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana tarehe 07/12/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani hiyo.

Kamati Kuu kwa niaba ya Chama imeunga mkono hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 inatekelezwa kwa ufanisi. Aidha, inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika maeneo ya:-

(1) Kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali:

Kamati Kuu inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo. Juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana wazi.
Aidha, Kamati Kuu inawataka wahusika mbalimbali kwenye maeneo hayo ya udhibiti wa vyanzo vya mapato kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ili lengo liweze kutimia.

(2)Kudhibiti matumizi ya Serikali:
Kama ilivyoagizwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, Serikali ya Awamu ya Tano imeanza vizuri na kwa kasi kusimamia udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima katika Serikali, ili kutumia fedha hizo kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi. Kamati Kuu inaunga mkono juhudi hizi na kuwataka wote wanaohusika kwa namna moja ama nyingine na udhibiti wa matumizi hayo wamuunge mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika jitihada hizi.

(3)Uhimizaji wa wananchi katika kufanya kazi kwa bidii:
Kamati Kuu inawataka wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla nchini kumuunga mkono Rais na Serikali yake kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na uzalendo. Kamati Kuu inawahimiza watu wote kwenye maeneo yao ya kazi kujituma na kuchapa kazi ili kujenga nchi yetu na kumuunga mkono Rais Magufuli.

(4)Kusimamia na kuhimiza uwajibikaji katika Serikali, Taasisi na Mashirika yake:
Kamati Kuu pia inapongeza na kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji mkubwa Serikalini ili kuongeza kasi na ubora wa utoaji huduma. Katika kipindi cha muda mfupi matunda yake yameanza kuonekana na hivyo kuweka msingi mzuri wa kuboresha huduma kwa umma kwa njia endelevu.

(5)Juhudi na jitihada hizi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli zimeleta matumaini mapya kwa sehemu kubwa ya wananchi na kukuza imani kwa Serikali yao. Hivyo, kila Mtanzania ana wajibu wa kuunga mkono jitihada hizi.Pamoja na kuunga mkono na kupongeza kasi waliyoanza nayo Rais Magufuli, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kamati Kuu inawataka Viongozi wengine wote kuiga mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ili kutekeleza kwa haraka zaidi Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Kamati Kuu inawatakia Watanzania wote kheri ya Krismas na mwaka mpya wa 2016, na inaamini mwaka ujao utakuwa wa kuchapa kazi na wenye mafanikio zaidi.Imetolewa na:-

Abdulrahman O. Kinana,
KATIBU MKUU WA CCM
08/12/2015

Updates:-

CVsnPyyVEAAtv-x.jpg

Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahaman Kinana akiwaaga wanahabari baada ya kumaliza Press.

Attachments

  • kinana.v01.jpg
    kinana.v01.jpg
    31.1 KB · Views: 9,173
Vizuri sana japo wanapaswa kufaham wananchi tumeridhika na kasi iliopo kuhusu serikali ya Magufuli
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitazungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali majira ya saa saba na nusu mchana huu katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Naamini Mwenyekiti aliongoza Kamati kuu kumpongeza Magufuli kufuta safari za nje.

Msisahau kukumbusha Waziri mkuu kuweka list ya wakwepa kodi pamoja na wamiliki wake ikiwepo ile ya Katibu Mkuu wako ya Almasi Shipping
 
mwenyekiti aseme kati ya yale makontena 349 yake ni mangapi , riziwani yake ni mangapi na mama salma yake ni mangapi halafu aendelee na ajenda nyinginezo
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitazungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali majira ya saa saba na nusu mchana huu katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Wanataka kujikosha na kumunga mkono JPM kinafiki.
 
Naamini Mwenyekiti aliongoza Kamati kuu kumpongeza Magufuli kufuta safari za nje.

Msisahau kukumbusha Waziri mkuu kuweka list ya wakwepa kodi pamoja na wamiliki wake ikiwepo ile ya Katibu Mkuu wako ya Almasi Shipping

Hiki ndio kitakuwa moja ya kipimo kikubwa cha uzalendo na dhamira ya Magufuli katika kupambana na ufisadi hasa ule unaowaohusu vigogo wakubwa wa chama na serikali.

Na hapa ndio pengo la UKAWA kutoshika dola litakapoonekana kwa wengi.

Hapo bado data za Escrow kupitia Stanbic hazijawekwa hadharani na Kubenea ndani ya Bunge.
 
Wanawaandaa Wananchi Kisaikolojia, Ili Washinde Chaguzi Za Ubunge.
 
Naamini Mwenyekiti aliongoza Kamati kuu kumpongeza Magufuli kufuta safari za nje.

Msisahau kukumbusha Waziri mkuu kuweka list ya wakwepa kodi pamoja na wamiliki wake ikiwepo ile ya Katibu Mkuu wako ya Almasi Shipping

Mkuu umesema sana, lkn tusitegemee kipya zaidi ya blaa blaa za miaka yote, kwa sababu watu ni wale wale na Mwenyekiti ni yule yule, ambaye wakati yote hayo yanafanyika alikuwa kiongoz wa nnchi
 
Naamini Mwenyekiti aliongoza Kamati kuu kumpongeza Magufuli kufuta safari za nje.

Msisahau kukumbusha Waziri mkuu kuweka list ya wakwepa kodi pamoja na wamiliki wake ikiwepo ile ya Katibu Mkuu wako ya Almasi Shipping

Wakiweka list yote hadharani sasa hivi si itaharibu uchunguzi, No?
 
Hiki ndio kitakuwa moja ya kipimo kikubwa cha uzalendo na dhamira ya Magufuli katika kupambana na ufisadi hasa ule unaowaohusu vigogo wakubwa wa chama na serikali.

Na hapa ndio pengo la UKAWA kutoshika dola litakapoonekana kwa wengi.

Hapo bado data za Escrow kupitia Stanbic hazijawekwa hadharani na Kubenea ndani ya Bunge.

Magufuli haendeshwi na hisia za upinzani, hayupo kupimwa na upuuzi wenu!
 
Wanataka kujikosha na kumunga mkono JPM kinafiki.

hakuna tofauti wangeongea wasingeongea still wana ukawa mngepayuka na kuropoka na kusema amnavosema na mnachokiona kuropoka kutoka midomoni mwenu.....mlisema magufuli anaendeshwa ikapita,mkaja mkasema nguvu ya soda ikapita,mkasema wanaisoma namba wao ccm ben saanane akaja akasema magufuli analipiza kisasi kwa waliokuwa wanashabikia ukawa,leo mnasema wanampongeza kinafiki nalo hilo litapita kwa kuwa ni nyie mlikuwa mkipiga kelele kwa nn ccm hawatoi tamko leo wantaka kutoa mnasema ni unafiki sasa hapo nani mnafiki??
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom