Tamko la CCM: Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, yaipongeza Serikali ya awamu ya tano

Jana tarehe 07/12/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani hiyo.

Kamati Kuu kwa niaba ya Chama imeunga mkono hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 inatekelezwa kwa ufanisi. Aidha, inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika maeneo ya:-

(1) Kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali:

Kamati Kuu inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo. Juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana wazi.
Aidha, Kamati Kuu inawataka wahusika mbalimbali kwenye maeneo hayo ya udhibiti wa vyanzo vya mapato kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ili lengo liweze kutimia.

(2)Kudhibiti matumizi ya Serikali:

Kama ilivyoagizwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, Serikali ya Awamu ya Tano imeanza vizuri na kwa kasi kusimamia udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima katika Serikali, ili kutumia fedha hizo kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi. Kamati Kuu inaunga mkono juhudi hizi na kuwataka wote wanaohusika kwa namna moja ama nyingine na udhibiti wa matumizi hayo wamuunge mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika jitihada hizi.

(3)Uhimizaji wa wananchi katika kufanya kazi kwa bidii:

Kamati Kuu inawataka wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla nchini kumuunga mkono Rais na Serikali yake kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na uzalendo. Kamati Kuu inawahimiza watu wote kwenye maeneo yao ya kazi kujituma na kuchapa kazi ili kujenga nchi yetu na kumuunga mkono Rais Magufuli.

(4)Kusimamia na kuhimiza uwajibikaji katika Serikali, Taasisi na Mashirika yake:

Kamati Kuu pia inapongeza na kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji mkubwa Serikalini ili kuongeza kasi na ubora wa utoaji huduma. Katika kipindi cha muda mfupi matunda yake yameanza kuonekana na hivyo kuweka msingi mzuri wa kuboresha huduma kwa umma kwa njia endelevu.

(5)Juhudi na jitihada hizi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli zimeleta matumaini mapya kwa sehemu kubwa ya wananchi na kukuza imani kwa Serikali yao. Hivyo, kila Mtanzania ana wajibu wa kuunga mkono jitihada hizi.

Pamoja na kuunga mkono na kupongeza kasi waliyoanza nayo Rais Magufuli, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kamati Kuu inawataka Viongozi wengine wote kuiga mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ili kutekeleza kwa haraka zaidi Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Kamati Kuu inawatakia Watanzania wote kheri ya Krismas na mwaka mpya wa 2016, na inaamini mwaka ujao utakuwa wa kuchapa kazi na wenye mafanikio zaidi.

Imetolewa na:-

Abdulrahman O. Kinana,
KATIBU MKUU WA CCM08/12/2015

Ambatanisha scanned copy ya taarifa hii ili iwe na ukweli Zaidi
 
Mpelekeeni Rais Ilani yenu kama walivyofanya ACT...

Chama Tawala ni CCM na Ilani inayotekelezwa ni ya CCM...

Kusema kwamba Rais Magufuli anatekeleza Ilani ya CHADEMA/UKAWA ni kichekesho kama sio porojo...

Ni lini CHADEMA mmemkabidhi Rais Magufuli Ilani yenu mpaka mkaanza kujinasibu kwamba anatekeleza Ilani yenu?

Hivi wanaongelea ile Ilani ya webusaiti? hehehehe... Hao CHADEMA/UKAWA waendelee kuzungusha mikono, Magufuli ana Ilani, ya CCM!
 
Ni muhimu wakategua kitendawili cha uchaguzi wa Zanzibar!

Haiwezekani. Kwanza hawana nia, azma, uthubuta, uibavu na jeuri ya kutegua kitendawili rahisi.

Inaauma , tena sana,kupigwa mwelekana kitoto ulichozaa mwenyewe! chali kifo cha mende!
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitazungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali majira ya saa saba na nusu mchana huu katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

Updates:-

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ameshaingia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo za Makao Makuu na anazungumza na waandishi wa habari hivi sasa,

CVsi1-RUkAEgH7Q.jpg

Kinana akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya CCM, Lumumba.

CVse8W5VEAACocz.jpg

Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye Press ya Katibu Mkuu wa CCM.

=========================

Updates:-

huyu nae ni jipu kule kwenye mbuga atatumbuliwa tu muda ukifika
 
KWA HIYO UNAFIKI WA JK ndio ameutolea tamko?Tuliposema JK ziara zake za nje hazina tija tulimaanisha.

Kinana nae amesahau,angemtaka Waziri mkuu ataje makampuni yaliyokuwa kwenye list ya kutolipa kodi maana kuna kampuni moja ya "Almasi" Shipping.....

Pia inasikitisha Kinana kutokuwa mkweli katika umri huu.Ni ilani gani ya CCM ambayo magufuli ametekeleza? Ataje ni ibara gani ya ilani ya CCM?

Mtu anatekeleza Ilani ya Chadema na kutupilia mbali ya CCM halafu katibu mkuu anaibuka na unafiki wa kumpongeza.
Watu wa aina yako mnafurahisha kama siyo kusikitisha!

Kama Ilani yenu ingekuwa ni nzuri kwa nini haikuwapeleka Ikulu?

Unafiki wa kutaka kujinasibisha na Serikali ya CCM wakati wananchi walitupilia mbali unafiki na ulaghai wanu ni kupoteza muda.

Unaweza kupitia video za kampeni za CCM kama unataka kufahamu ni Ilani gani iliyoipeleka CCM kukabidhiwa nchi kuiongoza.

Kwa kukusaidia kidogo, Sehemu ya 11-13 ya Ilani ya CCM inasema,

Vita dhidi ya Rushwa
11. Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii hazitaleta manufaa kwa wananchi na kuondoa umasikini iwapo adui rushwa ataendelea kulitafuna Taifa letu. Rushwa ni adui wa haki pia ni adui wa maendeleo na ustawi wa wananchi, hivyo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla.

12. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa; ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

13. Sambamba na kupambana na tatizo la rushwa, Serikali pia zitatakiwa kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa umma.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jana tarehe 07/12/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ilifanya kikao chake cha kawaida mjini Dar es salaam kwa siku moja. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kamati Kuu pia ilipokea taarifa juu ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. Kwa ujumla na kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM Taifa iliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe. Kassim M. Majaliwa kwa kasi nzuri waliyoanza nayo katika utekelezaji wa Ilani hiyo.

Kamati Kuu kwa niaba ya Chama imeunga mkono hatua kadhaa zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 inatekelezwa kwa ufanisi. Aidha, inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali katika maeneo ya:-

(1) Kusimamia vyanzo vya mapato ya Serikali:

Kamati Kuu inapongeza na kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) zinasimamia ukusanyaji wa kodi za Serikali ipasavyo. Juhudi hizi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa muda mfupi zimezaa matunda yanayoonekana wazi.
Aidha, Kamati Kuu inawataka wahusika mbalimbali kwenye maeneo hayo ya udhibiti wa vyanzo vya mapato kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa Serikali ili lengo liweze kutimia.

(2) Kudhibiti matumizi ya Serikali:

Kama ilivyoagizwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, Serikali ya Awamu ya Tano imeanza vizuri na kwa kasi kusimamia udhibiti wa matumizi yasiyo ya lazima katika Serikali, ili kutumia fedha hizo kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi. Kamati Kuu inaunga mkono juhudi hizi na kuwataka wote wanaohusika kwa namna moja ama nyingine na udhibiti wa matumizi hayo wamuunge mkono Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali yake katika jitihada hizi.

(3) Uhimizaji wa wananchi katika kufanya kazi kwa bidii:

Kamati Kuu inawataka wanaCCM na wananchi wote kwa ujumla nchini kumuunga mkono Rais na Serikali yake kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na uzalendo. Kamati Kuu inawahimiza watu wote kwenye maeneo yao ya kazi kujituma na kuchapa kazi ili kujenga nchi yetu na kumuunga mkono Rais Magufuli.

(4) Kusimamia na kuhimiza uwajibikaji katika Serikali, Taasisi na Mashirika yake:

Kamati Kuu pia inapongeza na kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji mkubwa Serikalini ili kuongeza kasi na ubora wa utoaji huduma. Katika kipindi cha muda mfupi matunda yake yameanza kuonekana na hivyo kuweka msingi mzuri wa kuboresha huduma kwa umma kwa njia endelevu.

(5) Juhudi na jitihada hizi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Magufuli zimeleta matumaini mapya kwa sehemu kubwa ya wananchi na kukuza imani kwa Serikali yao. Hivyo, kila Mtanzania ana wajibu wa kuunga mkono jitihada hizi.

Pamoja na kuunga mkono na kupongeza kasi waliyoanza nayo Rais Magufuli, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kamati Kuu inawataka Viongozi wengine wote kuiga mfano huu mzuri na kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo ili kutekeleza kwa haraka zaidi Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Kamati Kuu inawatakia Watanzania wote kheri ya Krismas na mwaka mpya wa 2016, na inaamini mwaka ujao utakuwa wa kuchapa kazi na wenye mafanikio zaidi.

Imetolewa na:-

Abdulrahman O. Kinana,
KATIBU MKUU WA CCM08/12/2015

Hivi haya nayo yalihitaji kuita waandishi wa habari?!!!!
 
I swear, haipo kwenye ilani ya CCM, hii ni speed ya Serikali ya MAGUFULI, Alisema Chagua Magufuli na watu wakaamua. He is Magufuli. President asiye na utashi wa kichama. Nipishe Kinn
 
KWA HIYO UNAFIKI WA JK ndio ameutolea tamko?Tuliposema JK ziara zake za nje hazina tija tulimaanisha.

Kinana nae amesahau,angemtaka Waziri mkuu ataje makampuni yaliyokuwa kwenye list ya kutolipa kodi maana kuna kampuni moja ya "Almasi" Shipping.....

Pia inasikitisha Kinana kutokuwa mkweli katika umri huu.Ni ilani gani ya CCM ambayo magufuli ametekeleza? Ataje ni ibara gani ya ilani ya CCM?

Mtu anatekeleza Ilani ya Chadema na kutupilia mbali ya CCM halafu katibu mkuu anaibuka na unafiki wa kumpongeza.

Tunaamini kwamba ingekuwa vyema kwa Rais kama angeomba ushauri wa namna ya kutekeleza ilani hii ili kuepusha makosa ambayo tuliyoyainisha.Ukisoma Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kuanzia Ukurasa wa 10 hadi wa 16 utaona ahadi yetu kwa Watanzania tuliyoahidi endapo Mgombea wetu wa Urais angefanikiwa kutangazwa mshindi na kuunda serikali. Ambayo tuliahidi kuwa
''• Katiba ya wananchi ni kipaumbele namba moja,
hivyo serikali ya CHADEMA itaanzisha tena mchakato
wa katiba uliozingatia maoni ya wananchi. Lengo ni
kuhakikisha kwamba vifungu vinavyohusu tunu, maadili
na miiko ya uongozi vinakuwa kwenye katiba mpya ili
sheria na kanuni mpya ziweze kutungwa na kudhibitiwa
• Kujenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini
mchango wake kwa taifa kila siku
• Kuimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika
Sekta ya Umma
• Kupiga vita/kuondoa rushwa/ufisadi na ubadhirifu
katika sekta ya Umma na binafsi
• Kuimarisha mchango wa Wataalam katika uendeshaji
wa nchi
• Kusimamia ukusanyaji na matumizi mazuri ya kodi na
mapato ya serikali na kupunguza mzigo wa kodi kwa
wananchi
• Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa watumishi wa
Umma
• Ikiwa ni pamoja na kupunguza kodi kwa wafanyakazi
ili kupunguza ukali wa maisha
• Kulipa mshahara wa mwezi kwa awamu mbili katika
mwezi ili kwendana na uhalisia wa hali ya maisha
• Kudhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni
pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa
muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku
matumizi ya magari ya anasa serikalini (mashangingi)
• Kudhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa
madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
• Kuimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za
serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi
ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
ili watanzania waweze kuihakiki na Bunge lao liikubali
kabla ya kupitishwa na serikali
• Kuimarisha serikali za mitaa ili wananchi washiriki
kikamilifu katika maendeleo yao."

Ili kutekeleza hayo ni lazima kuufumua mfumo kupitia katiba mpya hasa kuanzia pale Rasimu ya Warioba ilipoishia.
Rais hapaswi hata mara moja kujihusisha na vitendo vya kusamehe wahujumu uchumi badala ya kuachia mhimili wa mahakama kufanya kazi yake.

Ben Saanane na wazungusha mikono wenzako,

Ilani ya CCM (2015 - 2020), mwanzo kabisa kwenye Utangulizi Ibara ya Nne inasema hivi:
Katika miaka mitano ijayo (2015 - 2020), CCM ikiwa madarakani, itazielekeza Serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendeleza kupambana na changamoto kubwa nne: Kwanza kuondoa umaskini; pili kupunguza tatizo la ukosefu ajira hasa kwa vijana; tatu kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na nne kuendelea kudumuisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

Acheni kudandia treni kwa mbele, mtaumia!
 
I swear, haipo kwenye ilani ya CCM, hii ni speed ya Serikali ya MAGUFULI, Alisema Chagua Magufuli na watu wakaamua. He is Magufuli. President asiye na utashi wa kichama. Nipishe Kinn
Hapana, hii ni spidi ya 120 km/h ya serikali ya Lowassa mabadiliko, mabadiliko Lowassa, wakati huo huo ukizingusha mikono!

Kwa kukusaidia kidogo, Sehemu ya 11-13 ya Ilani ya CCM inasema,
Vita dhidi ya Rushwa
11. Jitihada za kuinua uchumi na kuongeza huduma za jamii hazitaleta manufaa kwa wananchi na kuondoa umasikini iwapo adui rushwa ataendelea kulitafuna Taifa letu. Rushwa ni adui wa haki pia ni adui wa maendeleo na ustawi wa wananchi, hivyo ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili nchi yetu na dunia kwa ujumla.

12. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa; ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

13. Sambamba na kupambana na tatizo la rushwa, Serikali pia zitatakiwa kushughulikia kwa ukali zaidi tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa umma, kuchelewesha kutoa maamuzi yenye maslahi kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza masuala yenye maslahi kwa umma.
 
hakuna tofauti wangeongea wasingeongea still wana ukawa mngepayuka na kuropoka na kusema amnavosema na mnachokiona kuropoka kutoka midomoni mwenu.....mlisema magufuli anaendeshwa ikapita,mkaja mkasema nguvu ya soda ikapita,mkasema wanaisoma namba wao ccm ben saanane akaja akasema magufuli analipiza kisasi kwa waliokuwa wanashabikia ukawa,leo mnasema wanampongeza kinafiki nalo hilo litapita kwa kuwa ni nyie mlikuwa mkipiga kelele kwa nn ccm hawatoi tamko leo wantaka kutoa mnasema ni unafiki sasa hapo nani mnafiki??

Usishindane na walioshindwa hutashida. Waache wapayuke hasira za kushindwa ziwaishe
 
Ben Saanane na wazungusha mikono wenzako,

Ilani ya CCM (2015 - 2020), mwanzo kabisa kwenye Utangulizi Ibara ya Nne inasema hivi:
Katika miaka mitano ijayo (2015 - 2020), CCM ikiwa madarakani, itazielekeza Serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendeleza kupambana na changamoto kubwa nne: Kwanza kuondoa umaskini; pili kupunguza tatizo la ukosefu ajira hasa kwa vijana; tatu kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma; na nne kuendelea kudumuisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao.

Acheni kudandia treni kwa mbele, mtaumia!
Hawa vijana wa bavicha wanafurahisha sana!
 
KWA HIYO UNAFIKI WA JK ndio ameutolea tamko?Tuliposema JK ziara zake za nje hazina tija tulimaanisha.

Kinana nae amesahau,angemtaka Waziri mkuu ataje makampuni yaliyokuwa kwenye list ya kutolipa kodi maana kuna kampuni moja ya "Almasi" Shipping.....

Pia inasikitisha Kinana kutokuwa mkweli katika umri huu.Ni ilani gani ya CCM ambayo magufuli ametekeleza? Ataje ni ibara gani ya ilani ya CCM?

Mtu anatekeleza Ilani ya Chadema na kutupilia mbali ya CCM halafu katibu mkuu anaibuka na unafiki wa kumpongeza.

Tunaamini kwamba ingekuwa vyema kwa Rais kama angeomba ushauri wa namna ya kutekeleza ilani hii ili kuepusha makosa ambayo tuliyoyainisha.Ukisoma Ilani yetu ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kuanzia Ukurasa wa 10 hadi wa 16 utaona ahadi yetu kwa Watanzania tuliyoahidi endapo Mgombea wetu wa Urais angefanikiwa kutangazwa mshindi na kuunda serikali. Ambayo tuliahidi kuwa
??? Katiba ya wananchi ni kipaumbele namba moja,
hivyo serikali ya CHADEMA itaanzisha tena mchakato
wa katiba uliozingatia maoni ya wananchi. Lengo ni
kuhakikisha kwamba vifungu vinavyohusu tunu, maadili
na miiko ya uongozi vinakuwa kwenye katiba mpya ili
sheria na kanuni mpya ziweze kutungwa na kudhibitiwa
? Kujenga uzalendo ili kila Mtanzania aweze kutathmini
mchango wake kwa taifa kila siku
? Kuimarisha nidhamu, utendaji na uwajibikaji katika
Sekta ya Umma
? Kupiga vita/kuondoa rushwa/ufisadi na ubadhirifu
katika sekta ya Umma na binafsi
? Kuimarisha mchango wa Wataalam katika uendeshaji
wa nchi
? Kusimamia ukusanyaji na matumizi mazuri ya kodi na
mapato ya serikali na kupunguza mzigo wa kodi kwa
wananchi
? Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa watumishi wa
Umma
? Ikiwa ni pamoja na kupunguza kodi kwa wafanyakazi
ili kupunguza ukali wa maisha
? Kulipa mshahara wa mwezi kwa awamu mbili katika
mwezi ili kwendana na uhalisia wa hali ya maisha
? Kudhibiti na kupunguza matumizi ya serikali ikiwa ni
pamoja na kufuta safari za watumishi serikalini zisizokuwa
muhimu pamoja na zile za Rais na kupiga marufuku
matumizi ya magari ya anasa serikalini (mashangingi)
? Kudhibiti deni la Taifa kwa kuanza na ukaguzi wa
madeni ya serikali ili kuhakiki jinsi yalivyotumika
? Kuimarisha uwazi na kuondoa usiri katika shughuli za
serikali na kuweka bayana mikataba yote ya nchi
ikiwa ni pamoja na ile ya mafuta, madini na gesi asilia
ili watanzania waweze kuihakiki na Bunge lao liikubali
kabla ya kupitishwa na serikali
? Kuimarisha serikali za mitaa ili wananchi washiriki
kikamilifu katika maendeleo yao.?

Ili kutekeleza hayo ni lazima kuufumua mfumo kupitia katiba mpya hasa kuanzia pale Rasimu ya Warioba ilipoishia.
Rais hapaswi hata mara moja kujihusisha na vitendo vya kusamehe wahujumu uchumi badala ya kuachia mhimili wa mahakama kufanya kazi yake.

haya yalitakiwa kutekelezwa na lowassa?
 
Wanajukwaa, mtakumbuka leo Vuta-Nikuvute ameleta uzi humu ukionyesha kwamba rais magufuli amewekea speed gavana na CC. Lakini kinana amemwaga sifa tele. Vuta -Nikuvute unastahili kuwekewa ban angalao miezi mitatu ili ujifunze athari za kuumiza vichwa vya watu kwa taarifa zisizokuwa na mashiko. POle. Tingatinga anaendelea kutumbua majipu.
 
Back
Top Bottom