Katibu Mkuu, Kinana akiongea na vyombo vya habari katika ofisi za CCM, Lumumba.
Ndondoo za alichokisema:
-Kamati Kuu ilifanya kikao chake jana na kupokea taarifa ya utendaji wa Serikali katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015 -2020
-Kamati Kuu inaipongeza Serikali Chini ya Uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli, Makamu Mhe Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa
-CCM kupitia Kamati Kuu inaunga mkono hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano ktk utekelezaji wa Ilani katika maeneo yafuatayo:-
-Kamati Kuu inapongeza na kuunga mkono Juhudi kubwa ya Serikali ya kusimamia vyanzo vya mapato kwa kuimarisha utendaji wa mamlaka za TPA&TRA.
-CCM inaunga mkono hatua ya Serikali kudhibiti matumizi, kama ilivyoagizwa na Ilani ya CCM ya 2015 - 2020 ili kuboresha huduma kwa wananchi.
-CCM inaunga mkono Juhudi za kuwataka wanaohusika na kudhibiti matumizi ya Serikali kumuunga mkono Rais Magufuli katika jitihada hizi.
-Kamati Kuu inawataka wanaCCM na wananchi kumuunga mkono Rais na Serikali kwa kuitikia wito wa kufanya kazi kwa bidii, Maarifa na Uzalendo.
waandishi gani hao hata mvuto hawana, sio presentable kabisa wamevaa kama wanataka kwenda sokoni.