Tamko la CCJ dhidi ya Kauli za Tendwa juu ya Usajili wa kudumu

Hao nao si walizungumza kwa mitazamo yao?mbona hata sisi humu JF tumekisema vibaya CCJ kwa mitazamo yetu?hivi Chiligati,Msekwa kuzungumza hivyo ndio kukihujumu CCJ?jamani hawa walijisemea kama watanzania wengine ambao hatukuwa na imani na CCJ mimi nikiwa mmoja wapo..Hebu tupeni exactly walichokizungumza hasa..Na mwelekeo wao nini?

GS ninavyofahamu maneno anayoongea Msekwa, ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM na spika mstaafu, hayawezi kuwa na uzito sawa na unayoongea wewe humu ndani ya JF. Msekwa na Chiligati ni viongozi wa juu sana wa chama tawala na wanachosema wao kinachukuliwa kama ni maagizo na watendaji wa serikali akiwemo Tendwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
 
GS ninavyofahamu maneno anayoongea Msekwa, ambaye ni makamu mwenyekiti wa CCM na spika mstaafu, hayawezi kuwa na uzito sawa na unayoongea wewe humu ndani ya JF. Msekwa na Chiligati ni viongozi wa juu sana wa chama tawala na wanachosema wao kinachukuliwa kama ni maagizo na watendaji wa serikali akiwemo Tendwa na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

tena tungeuliwa wao kina Chiligati na Msekwa walijuaje kuwa CCJ haitopewa usajili wa kudumu hata kabla ya kupewa usajili wa muda?
 
Sasa huyu Tendwa pesa za kusafiri ovyo ovyo mwenyewe kama habari inavyosema kuwa hakusema kitu kwani alikuwa ametoka safari zipo za kumwaga lakini kuwapa maofisa wake kwenda kufanya uhakiki hana! Kama hiyo ilikuwa ni safari ya nje ya nchi na ya kikazi basi per diem, incidental, accommodation, transport, return air ticket kwa ajili yake na kaujumbe kake ni tosha kwa kufanya uhakiki! Kwanza registrar wa vyama vya siasa unaenda nje kufanya nini?
 
Sasa huyu Tendwa pesa za kusafiri ovyo ovyo mwenyewe kama habari inavyosema kuwa hakusema kitu kwani alikuwa ametoka safari zipo za kumwaga lakini kuwapa maofisa wake kwenda kufanya uhakiki hana! Kama hiyo ilikuwa ni safari ya nje ya nchi na ya kikazi basi per diem, incidental, accommodation, transport, return air ticket kwa ajili yake na kaujumbe kake ni tosha kwa kufanya uhakiki! Kwanza registrar wa vyama vya siasa unaenda nje kufanya nini?

yaani wewe umeenda mbali kweli kufikiria.. binamu yangu mmoja alikuwa akiniona nimetoa mawazo ambayo hayajaenda mbali sana aliniambia nina "akili za kuku"... hadi leo sijaelewa maana yake lakini natamani ningemwambia Tendwa kuwa maelezo yake yanayonesha yana akili za kuku..
 
Hii yote ni drama tu ya kutaka kuhujumu mageuzi, CCJ itapewa tu usajili wa kudumu lakini kwanza ni lazima wahakikishe kuwa sasa kwenye media ni CCJ na tendwa tu. Harakati zingine za ukombozi ziko kimya kabisa. Ndiyo maana wenye akili wanauliza chama kipya miezi 8 kablaya ya uchaguzi kweli ina maana gani. Kwa ccm ina maana zifuatavyo

- Itatuliza movement ambayo ilishaanza ku take place (mawaziri kuzomewa na watu kuwa na kauli) sasa watu wako njia panda
- ita divert attention kutoka kwenye issue kwenda kwenye marumbano ya kijinga kama ya jana
- kutaka kuja kuwaambia watu kwa vitendo kuwa upinzani ni ujinga kwa kuja kufanya bonge la kituko
- Kuwatosa (wapiganaji wa ufisadi kwa mdomo) ili kuwaingiza mkenge kama (mpendazoe).

Hizi njia zimeweza kutumiwa sana hapa dunia na watawala, kumbuka clinton kulusha mizinga kule Afghanistan ili kudivert attention kutoka kwa monica kwenda kwenye khali ya kuwa tuko vitani pia kumbuka kuwa hiyo action lazima ingemkuna Joe lieberman ambaye alikuwa ni critic mkubwa wa clinton at a time. CCM haiiogopi CCJ hata kidogo bali wanaiogopa CHADEMA na ukweli utabaki kuwa ukweli daima.
 
Unajua hii nchi imeoza mi nazani tuwaombee Mungu hawa viongozi wetu.
hivi kazi za Msajili wa vyama ni nini? > Si kusajili vyama kama jina lenyewe lilivyo.
Sasa huyu Tedwa huko nje anaenda kusajili vyama gani?
Huyu angekuwa anaishi Rwanda Angesha sekwa Ndani (Magereza) maana hawajibiki hata kidogo!
Na akicheza huyu Tedwa CCJ watakwenda mahakamani na uchaguzi utasitishwa. Sasa sijui hizo gharama atafidia yeye!
 
Lakini tuwe wa kweli jamani, CCJ inaweza kuwa tishio kwa CCM? Siamini

Kama kweli CCJ sio tishio kwa CCM, kwa nini wanawazungusha kuwapa usajili wa kudumu ilhali masharti yote waliyopewa wanadai wameyatimiza? Tendwa anaonekana anaifanyia kazi CCM kwa kuilinda isipatwe namabaya. Lakini awe macho maana hamjui bosi wake anayefuata ni nani. Unaweza kumfanyia kibaya mtu ambaye kesho utamwendea kumwomba mkate, itakuwaje Tendwa????

Be kind to people when you climb up because you don't know who will be kind to you when you climb down.
 
chama cha jamii, sauti ya jamii inayotaka kufichwa shimoni, sisijei inakuwa kama mzimu kwa sisiem.!
Lini hawa viongozi wataacha woga katika kutekeleza majukumu yao.? na hivi ndivyo hali ilivyo kwenye serikali ya jeikei wpo wapo kujiendesha wao na familia zao tabaka la walio wengi hawapewi haki yao, ni hicho kimvuli ndio wanachokiogopa kwani sisisjei ikikamata usukani hali yote hii takataka itachomwa moto iteketee kabisa.
Tendwa acha woga ipe usajili sisisjei ili usije kujuta hapo mbeleni.( sio kama tutakulipa fadhila ila utaishi kwa haki kama mtanzania)
 
Mkuu Mwanakijiji CCJ ina ugomvi na Mengi maaana jana nimecheki taarifa ya Habari ya ITV usiku sikuona Press Release yenu, just curous maana as I know kuna uhusiano mkubwa sana kati ya ya Mengi na Wanamgambo wa CCM
 
Gazeti la Jana la Mwananchi lina hii article ambayo inajieleza vilivyo:

Tendwa usiendekeze urasimu, wape usajili CCJ
Wednesday, 26 May 2010 10:58 0diggsdigg

Na George Maziku

MSAJILI wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa amejidhihirisha mwenyewe kuwa hana utaalamu wa kutosha wa fani ya sheria, na hata inawezekana akawa kihiyo kabisa wa fani hiyo muhimu kwa kazi yake.

Kilichonishawishi kuanza kutilia shaka uwezo wake katika usomi wa fani ya sheria ni matamshi yake ya hivi karibuni kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayohusiana na wajibu wake wa kusajiri vyama vya siasa, ambayo kusema kweli yanaonyesha darasa la sheria "linamgonga".

Mvutano wake usio wa lazima dhidi ya Chama Cha Jamii (CCJ), hususan kuhusu kauli yake kwamba ofisi yake haiwezi kushughulikia maombi ya usajili wa kudumu wa CCJ eti kwa kukosa fedha za kumwezesha kuzunguka mikoani kuhakiki orodha ya wananchama wa chama hicho, ni ushahidi wa kutosha kuwa Tendwa ni mbumbumbu wa sheria.

Sheria ya vyama vya siasa inamtaka msajiri kukipatia usajiri wa kudumu chama cha siasa kilichotimiza masharti ya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, sharti kuu likiwa ni kutimiza idadi ya wanachama 2000 kwa mikoa 10, yaani wanachama 200 kutoka kila mkoa.

Kuhusu suala la chama kuwa na wanachama 2000, sheria haijaweka kipindi maalum cha msajili kuzunguka mikoani kuhakiki wanachama hao, na wala sheria haijasema kuwa chama kitasajiriwa baada ya msajiri kuhakiki na kujiridhisha juu ya orodha ya wanachama wa chama kinachoomba usajili wa kudumu, hivyo hoja ya msajili kwamba hawezi kutoa usajili wa kudumu kwa CCJ kwa kuwa hajahakiki orodha ya wanachama wa CCJ haina nguvu za kisheria, ni urasimu wake tu unaojengwa na ukereketwa wake kwa chama tawala nchini-CCM.

Halafu sababu anayoitoa msajili kuhalalisha urasimu wake ni ya kipuuzi kabisa, ofisi ya msajili kukosa fedha za kuzungukia mikoani si tatizo la CCJ na haliwezi kuwa sababu ya kutokisajili chama hicho au chama kingine chochote, hilo ni tatizo la serikali na ofisi ya Tendwa.

Kama ofisi ya msajili ilipewa fedha kiduchu ambazo hazikidhi mahitaji ya kuendesha ofisi hiyo, aibu kwao, kwanini chama cha siasa kiadhibiwe kwa makosa ya watu wengine?.

Namshauri Tendwa kukisajili CCJ kama kilivyoomba, na kama hapo baadaye itabainika kuwa chama hicho kilimdanganya msajiri, basi anaweza kukifuta katika daftari lake la vyama vya siasa na kuwafikisha mahakamani viongozi wake.

Kama msajili ataendelea kushikilia msimamo wake huo na kuamua kutokisajili CCJ, basi tutajua kuwa ana ajenda yake ya siri dhidi ya CCJ, ajenda kutoka kwa wakubwa ndani ya serikali na CCM kutokisajili chama hicho kinachodaiwa kuwa na msukumo wa baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM.

Itakumbukwa kuwa Tendwa alishatangaza mara tu baada ya CCJ kuomba usajiri wa muda kuwa chama hicho hakitashiriki uchaguzi mkuu ujao wa rais, wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi Oktoba, mwaka huu.

Wakati akitoa tangazo hilo Tendwa alidai eti CCJ lazima kwanza watimize sharti la kukaa muda wa siku 180 (miezi 6) za usajiri wa muda, na baadaye ofisi yake ifanye uhakiki wa wanachama 2000 wa chama hicho, ndipo "afikirie" kukipatia (CCJ) usajiri wa kudumu kama kitakuwa kimetimiza matakwa ya sheria.

Tendwa anapaswa kuelewa kuwa muda wa siku 180 (miezi) unaotajwa katika sheria ya vyama vya siasa unahusu uhai wa usajiri wa muda wa chama cha siasa, si sharti la kupata usajiri wa kudumu wa chama cha siasa.

Sheria ya vyama vya siasa haijasema kuwa "chama cha siasa lazima kitimize siku 180 tangu kipatiwe usajiri wa muda ndipo kiwe na sifa ya kupata usajiri wa kudumu", hakuna maelezo kama haya katika sheria hiyo.

Mantiki ya kisheria ya kuweka uhai wa usajiri wa muda wa chama cha siasa ni kuwapa watu walioomba kusajiri chama, muda wa kutimiza masharti ya kupata usajiri wa kudumu likiwemo sharti la kupata idadi ya wanachama 2000 kutoka mikoa 10 kama sheria ya vyama vya siasa inavyotaka.

Kwahiyo, muda wenyewe pekee yake (siku 180) hausimami kama sharti linalojitegemea la kusajiri chama cha siasa, hitaji la lazima hapa ni chama kukamilisha masharti yaliyowekwa na sheria likiwemo sharti la kupata wanachama 2000 kutoka mikoa 10.

Kwa msingi huo, chama cha siasa kinaweza kupata usajiri wa kudumu hata baada ya mwezi mmoja (siku 30) tangu kipatiwe usajiri wa muda kama kitaweza kutimiza masharti yaliyowekwa hususan hili la la kupata wanachama 2000 kwa mikoa 10.

Uthibitisho wa hoja hii ni kusajiliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambacho kilisajiriwa siku ile ile uliporuhusiwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini, yaani Julai Mosi, 1992, kwasababu tayari kilikuwa na wanachama zaidi ya hao 2000 wanaotakiwa kisheria.

Kama Tendwa anang'ang'ania msimamo wake wa kutaka CCJ wakae siku 180 katika usajiri wa muda kabla ya kuomba usajiri wa kudumu, hata kama wamekamilisha masharti yote ya kisheria, basi anapaswa kutueleza kwanini CCM haikufuata utaratibu huo iliposajiliwa mwaka 1992?

Hoja hii ya Tendwa inafanana na ile ya Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye Februari 8, mwaka huu, alihoji uhalali wa kisheria wa uamuzi wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa, Augustino Ramadhan, wa kupanga majaji saba (7) badala ya watatu (3) kusikiliza rufaa ya serikali dhidi ya hukumu ya Mahaka Kuu ya Tanzania katika kesi ya kikatiba ya Christopher Mtikila.

Jaji Mkuu alimjibu Naibu Mwanasheria Mkuu kuwa halikuwa kosa kisheria kutumia majaji saba (7), kwani majaji watatu (3) waliotajwa katika sheria ni idadi ya chini inayotakiwa kisheria (minimum number), yaani sheria imesema kuwa "Angalau wasipungue majaji watatu (3)", lakini sheria hiyo haijasema "wasizidi majaji watatu", hivyo halikuwa kosa kuongeza idadi na kuwa saba (7).

Kwa hiyo madai ya Tendwa kwamba lazima CCJ watimize siku 180, ndipo wawasilishe maombi ya usajili wa kudumu, si hoja ya kisheria bali ni urasimu wake tu na nia mbaya dhidi ya CCJ.

Kama Tendwa anataka kuheshimika na watanzania, ni bora akaacha kutekeleza majukumu ya kazi yake kwa kutaka kufurahisha watawala na CCM, aache ukereketwa kwa CCM, atende kazi yake kama msomi, kama mwanasheria, na kama "jaji" kama anavyojiita mwenyewe, vinginevyo watu hawatamtofautisha na katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.
 
Nimeipenda CCJ kwani imeweza kuifanya serikali ya CCM kuonyesha woga na sasa inaanza kujiumbua na kujikuta iko uchi hadharani. Kitendo cha Msajili cha kushindwa kutimiza wajibu wake kama ilivyoainishwa kwenye katiba kinatoa maswali mengi kuliko majibu. Hivi sasa ni wazi kuwa Tendwa kama alivyo Jaji Makame ni wakereketwa wa CCM na kama kawaida yao ya ulafi wako pale kuhakikisha huu utawala wa kifisadi hauondoki madarakani kwani wananufaika nao. Kwa bahati mbaya wameshindwa kwenda na wakati na kutambua kuwa huwezi kudanganya watu wote wakati wote - sana sana utajikuta unajidanganya mwenyewe kama Tendwa anavyojidanganya sasa. Tofauti na mbinu za vyama vilivyotangulia ambavyo vimejizatiti zaidi katika kukata matawi ya huo mbuyu (CCM) kwa dhana ya kuuangamiza, CCJ wameelekeza zaidi nguvu zao katika kukata mizizi ya huo huo mbuyu (CCM). Pamoja na vyama vingine kuendelea kuivua nguo serikali ya CCM, CCJ inataka kuhakikisha wenyewe wanazivua nguo zao kama anavyoanza kufanya Msajili Tendwa kama zezeta vile - patamu hapo.
Mimi nimeshampelekea text message, wewe hapo ulipo unasubiri nini ?

Asante kwa kutukumbusha kutuma ujumbe! Nimetuma!!
 
Umenikumbusha enzi za Mrema na CUF ya ngangari na ngunguli mambo yalikuwa nginjangija mabomu ya machozi nje nje siku hizi sioni vitu hivyo, tukitoka pale jangwani au mwembe yanga kwenye mkutano tumejazwa upepo na Marando na Mtikila mtu hakatizi mbele tunakwenda mchaka mchaka hadi chuo mambo yalikuwa hot kweli kinginjanginja.

Luteni, huko nyuma nilikua nakuona una mchango 'uliokwenda shule' humu JF lakini kwa hii michango yako kwenye posts zinazohusiana na ujio wa CCJ unadhihirisha jinsi usivyoelewa maana nzima ya uwepo wa vyama vingi vya siasa.
 
Mkuu Mwanakijiji CCJ ina ugomvi na Mengi maaana jana nimecheki taarifa ya Habari ya ITV usiku sikuona Press Release yenu, just curous maana as I know kuna uhusiano mkubwa sana kati ya ya Mengi na Wanamgambo wa CCM

Huku ndiyo kuunganisha nukta nako kutaka! Hii ccm wamekuja na kali kuliko EPA kila mtu hajui afanye nini
 
Mpaka leo bado tu hajatengeneza huo msingi wa maandamano wakati muda umekwisha,leo ni tarehe 26 Mei sasa kama mko slow kiasi hicho maana yake hata mkipata usajili mtakuwa mmeshachelewa kujiandaa na uchaguzi mkuu kwa hali hii mlipaswa kuwa very fast ili mkimbizane na muda..Mtajipanga saa ngapi ili mshiriki uchaguzi Mkuu kama hata usajili wenyewe mnautafuta kwa mapozi hivyo..Sheria mpya ya uchaguzi inawataka kukusanya fedha pamoja na vifaa vyote vitakavyotumika wakati wa uchaguzi si chini ya siku 90 nyie bado mnajikongoja tu..Inakula kwenu!by the time mnapata usajili hamuwezi tena kushiriki uchaguzi kwa kuwa mmeshindwa kumeet matwaka ya sheria ya gharama za uchaguzi..Itakuwa imekula kwenu.

Sidhani kwamba CCJ kimeanzishwa kwa ajili ya kushiriki uchaguzi mkuu peke yake. Naamini kina agenda na mikakati mingi endelevu kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kwa mustakabali wa Taifa kwa ujumla.
 
Luteni, huko nyuma nilikua nakuona una mchango 'uliokwenda shule' humu JF lakini kwa hii michango yako kwenye posts zinazohusiana na ujio wa CCJ unadhihirisha jinsi usivyoelewa maana nzima ya uwepo wa vyama vingi vya siasa.
Boramaisha

Unataka kuniambia ubora wa michango wangu hadi nisapoti unachokitaka au hadi nisapoti Ccj, hapana ndugu yangu mimi huwa si wa aina hiyo huwa sifuati upepo nasticky kwa ninachokiamini, leo kuna Ccj kesho mtu atakuja na Cck unataka tena nianze kuamini hiyo CCk? Binafsi siamini ujio wa Ccj kwa kipindi hiki cha lala salama kinachofanyika ni mazingaombwe tu, tatizo liko kwa CCM wanakijengea Ccj publicity ya bure kwa kukicheleweshea usajili pindi kitakapopewa hutasikia cha Ccj wala nini.
 
"CHAMA cha Jamii (CCJ) kimesema kitamkopesha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa fedha za kuwapa maofisa wake 10 wafanye uhakiki wa wanachama wa chama hicho mikoani ili kipate usajili wa kudumu." Habari Leo
Naombeni msaada wa kuelimishwa kwenye hili..Hivi Serikali inaweza kukopa pesa toka kwa mtu binafsi au kutoka kwenye chama cha Siasa mbali na taasisi za fedha? Maana kama ni hivyo mi nataka niikopeshe fedha ili kupanua hospitali mama zetu waache kuzalia chini! Nafkili hayo ni matumizi mazuri ya fedha kuliko usajili wa CCJ.
 
Ingawa siamini ujio wa Ccj lakini jana walitoa point mbili muhimu ambazo hata Tendwa itabidi aziangalie mara mbilimbili, kwanza ni bajeti ya kuhakiki wanachama, kama kweli wanavyosema Ccj mwaka huu hakuna chama chochote kilichofanyiwa uhakiki sasa bajeti yake imekwenda wapi. Point ya pili ni ile ya kazi ya Msajili, kama kazi kuu ya ofisi ya Tendwa ni kusajili vyama inakuwaje atingwe na kazi zingine zaidi ya ile aliyoajiriwa? ni sawa na walimu mkuu kutingwa na shughuri za shamba la shule wakati kuna upungufu wa walimu shuleni haiingii akilini.
 
Back
Top Bottom