Tamko la CCJ dhidi ya Kauli za Tendwa juu ya Usajili wa kudumu

wewe futa usemi wako hapo juu zaidi hakuna. Kuna vyama vya upinzani ambavyo vimethubutu vingi tu sawa?
Shalom, lengo la vyama vya siasa ni kushika dola, tuna vyama 19, kimoja tuu ndio kimeshika dola, vinaingia kwenye uchaguzi kwa mara ya 4 vikiwa fragmented, au huku ndiko unakokuita kuthubutu?. Tuendelee kuvilea vyama vinavyoendelea kuthubutu ama viunganishe nguvu vifanye kweli?.

Kama ulimaanisha just kuthubutu, basi nimefuta kauli yangu!.
 
Hadithi ni hii.
Mhalifu mmoja alishikwa akifanya uhalifu akapelekwa kwa Mfalme kuhukumiwa. Mfalme akamruhusu achague moja kati ya adhabu zifuatazo
1. Yeye amuue mkewe
2. Awape sumu watoto wake
3. Anywe pombe alewe.
Mhalifu akachagua pombe kwa imani haina madhara sana, hivyo alikunywa pombe, alipolewa alimuua mkewe na pia aliwapa sumu watoto wake.
Hadithi ndio imeishia hapo,
Ufafanuzi unafuatia.
 
Kadri serikali kupitia Msajili wa vyama inavyozidi kupambana na CCJ ndivyo inavyonifanya nianze kuamini kwamba CCJ is really opposition party!
 
Ufafanuzi wa Hadithi.
Kwa msajijili kukataa kuisajili CCJ ni shinikizo la serikali kwa kudhani kuikwamisha CCJ ni kueupusha CCM na matatizo madogo. Serikali ya CCM itakabiliwa na matatizo makubwa zaidi kwa kutoisajili CCJ kwani CCM inakabiliwa na siku ya kifo cha nyani, miti yote inateleza. Watanzania wamechoshwa na maisha duni, na mwaka huu wamepania kufanya mabadiliko kurejesha heshima ya taifa.

Wamesema kikulacho ki nguoni kwako, uovu unaitafuna CCM na serikali yake, uko ndani yake. Msajili ndiye yule mlevi aliyechagua madhara kidogo kumbe anataka kuliangamiza taifa.

Msajili na serikali ya CCM wamelewa madaraka, kwa uminyaji wa demokrasia, watapelekea wananchi ambao ndio msingi wa madaraka na mamlaka ya serikali kuamua kuchagua chama wanachokitaka (CCJ) kiongoze nchi.

My Take.
Hapa sasa CCJ, inachimba mkwala!.
 
Hadithi ni hii.
Mhalifu mmoja alishikwa akifanya uhalifu akapelekwa kwa Mfalme kuhukumiwa. Mfalme akamruhusu achague moja kati ya adhabu zifuatazo
1. Yeye amuue mkewe
2. Awape sumu watoto wake
3. Anywe pombe alewe.
Mhalifu akachagua pombe kwa imani haina madhara sana, hivyo alikunywa pombe, alipolewa alimuua mkewe na pia aliwapa sumu watoto wake.
Hadithi ndio imeishia hapo,
Ufafanuzi unafuatia.

Pasco, patamu hapo tupe busara ya hadithi hiyo, usiniambie msajili amechagua kunywa pombe, akalewa na kuifuta CCM kwenye orodha ya vyama. Tupe ufafanuzi haraka Pasco
 
Serikali na msajili wanaipatia CCJ Publicity ambayo baadae watakuja kujuta kwa nini walifanya maamuzi ya kukiminya CCJ. Ninaamini CCJ kina vichwa nyuma yake, kwa CCM kuanza kukizibia mkondo kwa magogo na makuti, wanapoteza muda bure wa kuangalia mikondo mingine (CUF, CHADEMA) inakwendaje watakuja jikuta tayari wamezuungukwa na maji kupitia mikondo ambayo hawaiangalii sana.

Watafanya nini CCJ itakapoamua kujiunga na CHADEMA katika uchaguzi mkuu na wagombea wa CCJ kusimama kama wa CHADEMA au CUF? itakuwa too late. Waache democrasia ifanye kazi yake, hii ni kwa maendeleo ya nchi siyo kundi la watu. Waache woga wa kitoto, kama wao wanaweza kuicheza kwa nini wanataka kuizima?
 
Unajua wakati Buyern Munich wanahangaika kumkaba Etoo, Millito akawapiga Mbili, sasa CCM waache kuhangaika na CCJ wakipe Usajili wa Kudumu! Nimeipenda hiyo hadithi yao. Ngoja tuangalie

Ila kwa sasa naweza sema kwamba kuelekea Uchaguzi mkuu CCJ ni Pace Maker, ndio maana kuna sehemu nilisema kwamba CCJ si CCJ
 
Hitimisho.
'Certiorari Mandamus' ambayo ni hati inayotolewa na mahakama kuu kuilazimisha serikali itimize wajibu wake.

Angalizo mzee, inaitwa 'writ of Mandamus' au kwa lugha nyepesi 'Mandamus Order'
 
Unajua wakati Buyern Munich wanahangaika kumkaba Etoo, Millito akawapiga Mbili, sasa CCM waache kuhangaika na CCJ wakipe Usajili wa Kudumu! Nimeipenda hiyo hadithi yao. Ngoja tuangalie

Ila kwa sasa naweza sema kwamba kuelekea Uchaguzi mkuu CCJ ni Pace Maker, ndio maana kuna sehemu nilisema kwamba CCJ si CCJ

Naomba mwogozo hapo kwenye bold!
 
Naomba mwogozo hapo kwenye bold!

Mkuu Masanilo CCM sio Wajinga they know that kukinyima Usajili wa Kudumu CCJ ni hatari zaidi kuliko kukipa. Amin Amin nakwambia kesho Tendwa atatoa tamko akisema alikuwa anatania tu media ili mquote vibaya na CCJ ianchukua Usajili wa Kudumu. Salama ya CCM ni kuipa CCJ usajili wa Kudumu
 
Mkuu kumbe nawe ni philosopher!
 
NImewawekea tamko lenyewe kwenye posti ya awali!

Na huu ni mwanzo tu.. CCJ itaenda na kufanya mambo ambayo hayajawahi kufanywa na opposition katika kudai haki katika miak 15 iliyopita. Believe me.. the bar is being raised as I said before.. "a notch or two higher".
 
Waaa,yale yale hakuna jipya ni blah blah kama wengine tu..Kuliko kwenda mahakamani bora wafanya maandamano ya nguvu au waende kwa wananchi..Kama Tendwa kawanyima je Serikali na mahakama wanaweza kuwatenganisha?
Exactly nilitegemea watatoa tamko tofauti kali kuwa kesho ni kesho kuandamana hadi kwa msajili, sasa kuna tofauti gani na vyama 18 vilivyopo naona wanapita mle mle walipopitia wengine kwa maana hiyo wako nyuma ya wakati, wakati Ccj wanainama kuokota kijiti kilichoteleza wakimbiaji wengine (vyama 18) ikiwemo CCM wanaelekea kumalizia mbio.
 
Luteni... fikra zako haziko mbali sana.. sasa huwezi kutoka tu na kusema unaandamana bila kutengeneza msingi wa maandamano au hatua nyingine. CCJ imetoa nafasi kwa Msajili kuwaelewa Watanzania kwanini isionekane yeye na CCM wamecollude kuinyima usajili kwani kauli zao zinafanana?

Inapofikia watu wanaandamana basi watanzania watajua kuwa njia nyingine zozote zimeshindikana.
 
Nitasikitika sana endapo Tendwa atakubali Kuisajili CCJ Kirahisi hivi, napenda iwe ni Nginjanginja, mpeleke huku mpeleke kule mpaka asalimu Amri, Lakini akiisajali kirahisi hivi CCM itakuwa imeruka Mtego wa CCJ, ni mtizamo wangu
 
Chama cha Jamii ambacho kimenuiwa kunyimwa usajili wa kudumu na Serikali inayodaiwa kuwa ni ya kidemokrasia ya Rais Jakaya Kikwete leo kimetoa majibu yasiyo na utata ya kwanini uamuzi huo ambao umekuwa ukifanyika kama njama kati ya serikali na uongozi wa juu CCM ni uamuzi wa kiwoga, usio na demokrasia na wenye lengu la kukipigisha magoti chama hicho kusalimu amri na kutupilia mbali wazo lake la kutaka kushiriki Uchaguzi Mkuu.

LIfuatalo ni tamko hilo.

Habari ndiyo hiyo...
MKJJ naona tamko limezingatia pia na mijadala ya hapa JF hususan mara baada ya kunyimwa usajili,hatua mliyochukua siyo mbaya,tusubiri majibu.
 
CCJ, fanyeni kazi na Ofisi ya Msajili wa Vyama, msifanye kazi na vyombo vya habari pekee! Mwandikieni Msajili na yeye awajibu kwa MAANDISHI. Kutafuta huruma kwa WATANZANIA kwa wakati huu hakutawasaidia sana. Mengi ya mnayoyatolea matamko ni yale mnayosoma kwenye magazeti kama mimi. Nendeni mbali zaidi. Tafuteni pia mtu makini wa kuwasaidia ushauri upande wa habari na mawasiliano.Ni kaushauri kangu ka bure.
 
MKJJ naona tamko limezingatia pia na mijadala ya hapa JF hususan mara baada ya kunyimwa usajili,hatua mliyochukua siyo mbaya,tusubiri majibu.

Usiwe na shaka tunazingatia sana maoni ya watu na hata suala la umoja endapo itafikia uko we want to be the one to set the agenda and facilitate it.
 
Back
Top Bottom