Ukurasa wa Pili.
Wamezungumzia uwezo wa Msajili kuwa Hana uwezo wa kukataa kusajili kiholela.
Wamenukuu Ibara ya 10 ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992, inayotamka kuwepo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambapo Ibara ya 8(5) inamlazimisha Msajili lazima atoe usajili wa kudumu kwa kila chama cha siasa kilichotimiza masharti ya usajili na kuaninisha vizuizi vinavyoweza kupelekea chama kunyimwa usajili wa kudumu, lakini kipengele cha ofisi ya Msajili kukosa bajeti hakipo kwenye vizuizi, hivyo siyo kizuizi, hayo ni matatizo ya ofisi yake.
Pia wameshutumu tamko la Msajili ati ana shughuli nyingine, wamesisitiza kazi kuu ya Msajili ni kusajili, mengine yote yatafuata.
Hicho kipengele kimenivutia sana. Hivi Kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ana kazi nyingine zaidi ya kufanya usajili na kuhakikisha hivyo vyama vya siasa vinafuata taratibu na kanuni zinazoongoza vyama vya siasa?
Hoja za CCJ zimenivutia, naona wanaweza kumbana kwenye angle mbaya na akashindwa kuchomoka, ngoja tusubiri majibu yake.
Maana huu uhuni wa CCM kwa kushirikiana na NEC na Tendwa, sometimes unasikitisha sana.