Tamko la BAVICHA kuhusu ajira za hivi karibuni kwa Kada za Afya na Ualimu

BAVICHA Taifa

Verified Member
Jul 25, 2013
105
500
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR - TAMISEMI) Mei 09, 2021 imetangaza ajira za Watumishi wa Kada mbalimbali za Afya 2,726 kwa ajili ya Hospitali za Halmashauri, vituo vya afya na Zahanati pamoja na Walimu 6,949 wa Shule za Msingi na Sekondari watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Ni maoni yetu kuwa Ajira zilizotangazwa siyo toshelevu kwani kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ya utawala wa Hayati John Magufuli aliweza kuajiri walimu 26,181 tu, na ajira 14,479 tu kwa kada za afya, wakati vijana waliomaliza vyuo vikuu na vya kati kwa kada hizo mbili ni zaidi ya vijana 300,000 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Kada ya Afya, kwa mujibu wa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Ummy Mwalimu aliwahi kukiri kuwa kuna uhaba mkubwa wa Watumishi katika kada hiyo, alisema “bado ipo changamoto ya rasilimali watu, pengo ni takribani asilimia 52.” Upungufu huu ni mkubwa sana hasa katika mazingira haya ambapo kuna magonjwa ya mlipuko kama Uviko-19.

Serikali inajinasibu kuwa ilijenga vituo vya kutolea huduma za Afya lakini vimebaki havina watumishi wala vifaa tiba na vitendanishi.

Bavicha tunaitaka Serikali kupunguza upungufu wa Wataalamu katika kada ya Afya kupitia bajeti ya Serikali ya 2021/2022 kutoka asilimia 52 angalau mpaka asilimia 20 kwa kuanzia na mwaka huu was fedha. Hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira pia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa Uviko-19.

Aidha, katika kada ya elimu, kwa mujibu wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali Za Mitaa Mhe. Mwita Waitara, aliwahi kusema kuwa kuna upungufu wa Walimu 80,000, ambapo Shule za Msingi ni Walimu 66,000 na Walimu 14,000 kwa Shule za Sekondari.

Serikali inategemea kuajiri asimia 8.6 tu ya mahitaji ya Walimu nchini ambao ni kiasi kidogo sana kulinganisha na mahitaji halisi yaliyopo nchini.

Hii inaonyesha ni jinsi gani Serikali haijajipanga kuboresha sekta ya elimu na kutatua tatizo la ajira kupitia kada ya elimu nchini.

Bavicha tunaitaka Serikali kupunguza upungufu wa Walimu katika Shule za Sekondari na Msingi kwa kuajiri Walimu angalau kufikia asilimia 50 ya mahitaji kwa kuanzia na mwaka huu wa fedha.

Nchi yetu haina uhaba wa Wataalamu wa kada ya Ualimu bali Serikali haipi kipau mbele tatizo la ajira na upungufu wa Walimu katika Shule mbalimbali nchini.

Bavicha tupo tayari kuikabidhi Serikali Sera yetu ya Vijana toleo la 2020, ili kuisaidia Serikali kutatua tatizo la ajira nchini, ambayo wameshindwa kulitatua kwa muda mrefu, kwani katika Sera hiyo tumeeleza namna tutakavyotatua tatizo la ajira nchini endapo wananchi watatupa Chadema ridhaa ya kuongoza Serikali.

“Chadema itawaunganisha watafutaji wa ajira na waajiri kupitia vituo vya taarifa za ajira ambavyo vitaanzishwa katika Halmashauri zote nchini. Chadema inaamini kwamba kujua mahitaji ya ajira za baadae na kupanga mkakati wa kutengeneza ajira hizo ni ufumbuzi endelevu wa kutatua tatizo la ajira nchini.”

Vijana Nguvu ya Mabadiliko.

Imetolewa leo Mei 11, 2021

Twaha Mwaipaya
Mratibu wa Uhamasishaji,
Bavicha Taifa.

IMG-20210511-WA0003.jpg
IMG-20210511-WA0001.jpg
 
Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,361
2,000
Lawama yote apewe Jiwe ,huyu mtu alikuwa wa ajabu Sana , Mungu alisaidie hili Taifa lisipate kiongozi wa hovyo namna Ile tena ......
Hzi Kada zilikuwa za kimkakati na ndo mana wahitimu walikuwa wengi , Kikwete alikuwa mwaminifu alikuwa habakizi mhitimu mtaani , japo alidokeza pia kuwa baada ya miaka kadhaa watastisha vipaumbele kwenye hzi Kada ili atakayesomea asome Kwa utashi wake maana serikali itakuwa inaajili Kwa kuziba mapengo......

Jiwe ameingia akapiga chini na kuvunjilia mbali ajira Kwa hzi Kada,mbali na kwamba Kikwete alikuwa ametenga tayar bajeti ya wahitimu 46000 education and Health combined together .....

Bila kutoa warning yyte akawa anawalundika Tu mtaani , huku akiwasisitiza wawe wanyonge , wawe machinga huku yeye alikimbilia kununua madege , Tulikuwa na Raisi wa Hovyo saana ....
Huyu mama naye ajikune tu anapoweza Ila tatizo ni kubwa Sana na limeweka mwanya mkubwa wa rushwa
 
Ivan said

Member
Feb 14, 2021
52
125
Sawa ujumbe umefika ila siku nyingine jitahidi kuandika kwa muhtasari maana lengo ni ujumbe umfikie mlaji. Pia ungejaribu kuonesha hiyo mikakati uliyosema ya namna ya kutatua tatizo la ajira badala ya kusubiri kukabidhi nyaraka kwa sababu yawezekana ikahitajika au lahasha!
 
mshale21

Senior Member
Apr 8, 2021
117
500
Lawama yote apewe Jiwe ,huyu mtu alikuwa wa ajabu Sana , Mungu alisaidie hili Taifa lisipate kiongozi wa hovyo namna Ile tena ......
Hzi Kada zilikuwa za kimkakati na ndo mana wahitimu walikuwa wengi , Kikwete alikuwa mwaminifu alikuwa habakizi mhitimu mtaani , japo alidokeza pia kuwa baada ya miaka kadhaa watastisha vipaumbele kwenye hzi Kada ili atakayesomea asome Kwa utashi wake maana serikali itakuwa inaajili Kwa kuziba mapengo......

Jiwe ameingia akapiga chini na kuvunjilia mbali ajira Kwa hzi Kada,mbali na kwamba Kikwete alikuwa ametenga tayar bajeti ya wahitimu 46000 education and Health combined together .....

Bila kutoa warning yyte akawa anawalundika Tu mtaani , huku akiwasisitiza wawe wanyonge , wawe machinga huku yeye alikimbilia kununua madege , Tulikuwa na Raisi wa Hovyo saana ....
Huyu mama naye ajikune tu anapoweza Ila tatizo ni kubwa Sana na limeweka mwanya mkubwa wa rushwa
Umenena vyema mkuu!
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Hii nchi sehemu ambayo haisumbui kwa upande wa ajira ni vyeo vya kisiasa huwezi kuona gap hata siku moja.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
16,784
2,000
Lawama yote apewe Jiwe ,huyu mtu alikuwa wa ajabu Sana , Mungu alisaidie hili Taifa lisipate kiongozi wa hovyo namna Ile tena ......
Hzi Kada zilikuwa za kimkakati na ndo mana wahitimu walikuwa wengi , Kikwete alikuwa mwaminifu alikuwa habakizi mhitimu mtaani , japo alidokeza pia kuwa baada ya miaka kadhaa watastisha vipaumbele kwenye hzi Kada ili atakayesomea asome Kwa utashi wake maana serikali itakuwa inaajili Kwa kuziba mapengo......

Jiwe ameingia akapiga chini na kuvunjilia mbali ajira Kwa hzi Kada,mbali na kwamba Kikwete alikuwa ametenga tayar bajeti ya wahitimu 46000 education and Health combined together .....

Bila kutoa warning yyte akawa anawalundika Tu mtaani , huku akiwasisitiza wawe wanyonge , wawe machinga huku yeye alikimbilia kununua madege , Tulikuwa na Raisi wa Hovyo saana ....
Huyu mama naye ajikune tu anapoweza Ila tatizo ni kubwa Sana na limeweka mwanya mkubwa wa rushwa
Acheni usenge, siyo kila kitu ni siasa.

Mbona Magu kapiga bench watu miaka 5 mlikuwa kimya tu.

Madai yenu ni katiba mpya, bunge Live, mikutano ya hadhara.

Sasa leo shobo za nini ?
 
am 4 real

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
465
1,000
umeandika kirefuuuuu yote uliyoandika yalikuwa yatoshe paragraph moja tu

Tamko lilitakiwa kuwa na paragraph moja tu
Mkuu mitume wote wali hubiri injili Kwa kutoa mifano..... Sikupangii Cha kuandika ila Tengeneza tamko lako lenye paragraph Moja tulione mkuu.....Hilo ni la twaha mwaipaya@ bavicha Taifa....wewe toa lakwako tulione.
 
Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
3,782
2,000
Wanateuana tu.
Nawakumbusha tu watumishi wenzangu kuwa Maafisa wa Jeshi wanapanda vyeo kila leo kwa mujibu wa kanuni zao za utumishi. Sisi watumishi tunaendelea kuhakikiwa
 
Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,447
2,000
Accumulation ya watu kutoajiriwa in 5 yrs leo waje waajiriwe kwa mara moja, hiyo ni akili au matopetope. Acheni kumchosha Mama....
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom