Tamko la BAVICHA jimbo la Segerea kulaani mauji ya kinyama ya David Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la BAVICHA jimbo la Segerea kulaani mauji ya kinyama ya David Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jigoku, Sep 6, 2012.

 1. j

  jigoku JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Wanabodi,salaam kwenu
  Tafadhalini someni tamko la BAVICHA kuhusu mauaji ya kinyama ya mwandishi wa chanel Ten ambalo nimewabandikia kama lilivyo.

  [h=3][/h] [h=3]BARAZA LA VIJANA CHADEMA (BAVICHA) JIMBO LA SEGEREA[/h]
  TAMKO LA BAVICHA KULAANI MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI MAREHEMU DAVID MWANGOSI.
  1.UTANGULIZI
  Ndugu wanahabari,BAVICHA jimbo la Segerea limewaita hapa leo 06/09/2012,ili kutoa masikitiko,kulaani na kutoa tamko juu ya vitendo vinavyoendelea kushamiri vya mauaji dhidi ya raia wasio kuwa na hatia.vifo hivi vyenye mashaka vinavyoendelea kutokea mbele ya uwepo wa jeshi la polisi vimeendelea kwa muda mrefu sasa bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu,na vinazidi kuondoa imani ya jeshi hili lenye dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao.
  Matukio ya mauaji ya hivi karibuni yaliyotokea mbele ya jeshi la polisi,mkoani Morogoro (Morogoro mjini) Nyamongo mkoani Mara na tukio la kuuwawa kwa mwandishi wa habari kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ni baadhi tu ya matukio mengi yenye mashaka na yanayoleta sintofahamu juu ya utendaji kazi wa jeshi la polisi na kusababisha kutokuaminika tena kwa watanzania. BAVICHA jimbo la Segerea tunasikitishwa sana na mauaji ya KINYAMA ya mwandishi wa habari,marehemu DAVID MWANGOSI yaliyotokea 02/09/2012,akitekeleza majukumu yake ya kutafuta habari kwenye tukio la uzinduzi wa tawi la CHADEMA kijiji cha Nyololo,huku akiwa amezungukwa na polisi wengi na wasiweze kumuokoa na kifo hicho.Je kazi yao ilikuwa nini kama siyo kulinda usalama wa raia na kama ni kulinda ilikuwaje DAVID alikufa amemkumbatia moja ya wanausalama hawa?huku wengine wakimshambulia? Tunashangazwa sana na jeshi la polisi kuzuia mikutano ya ndani iliyokuwa ikifanywa na CHADEMA kwa kisingizio cha kupisha zoezi la sensa ya watu na makazi,wakati likiacha mikutano ya ndani ya CCM wakiendelea na chaguzi za viongozi wa UWT na UVCCM na mikutano ya hadhara wakati zoezi la sensa likiendelea,kwa mfano Uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa mbunge jimbo la BUBUBU UNGUJA( Uzinduzi huo ulifanywa na Dr Mohamed Ghalib Bilal,UVCCM wilaya ya Temeke na Kinondoni,UWT wilaya ya Temeke-Uchaguzi uliofanyikia PTA hall sabasaba,Mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jimbo la Mchinga(Mh.Said Mtanda alihutubia),Asha Suleiman Idd(mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Kaskazini B) aliekuwa akifungua mkutano wa UVCCM katika wilaya ya Kindunina mbunge wa Bumbuli mh.January Makamba aliefungua mkutano wa jumuia ya wazazi CCM wilaya ya Lushoto.Wakati matukio haya yote yakifanywa na CCM ni kipindi cha muda wa nyongeza wa sensa ulikuwa ukiendelea. BAVICHA jimbo la Segerea tunahoji,KATAZO LA POLISI LA KUZUIA MIKUTANO NA SHUGHULI ZOTE ZA SIASA NI KWA CHADEMA TU? Hali hii inatoa picha kwamba jeshi la polisi linatumika kisiasa kwa kuibeba CCM,ni kwa namna gani wataepuka kuitwa POLISISIEMU?hata hivyo kuna dalili tosha kwamba vyombo vya habari navyo vimeanza kujengewa hofu katika kutekeleza majukumu yao,kwa hili la kuuwawa kwa mwandishi akiwa amezungukwa na polisi akitafuta habari kwenye tukio la kisiasa za chadema,tunajiuliza ni kwa vipi walishindwa kulinda usalama wake ili hali wakijua ni mwandishi?ni nani hasa alimuua DAVID MWANGOSI?mbele ya wanausalama waliokuwa na silaha,magari, intelijensia,radio call,kofia za kujikinga,marungu,mabuti na vyote walivyotakiwa kuwa navyo? Mauaji haya ya KINYAMA katikati ya polisi wengi yanatudhihirishia kwamba wizara hii ya mambo ya ndani inayoongozwa na Emmanuel Nchimbi pamoja na mkuu wa polisi IGP MWEMA wameshindwa kabisa kukomesha tabia ya vifo vya raia vyenye utata na hasa pale vinapotokea mikononi mwa polisi,na kwamba wao ni wadau halali wa kifo cha marehemu DAUD MWANGOSI. BAVICHA SEGEREA TUNATAMKA KWAMBA 1.TUNAMTAKA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI EMMANUEL NCHIMBI AJIHUZULU KWA KUSHINDWA KUZUIA VIFO VYA RAIA WASIO NA HATIA VINAVYOTOKEA MIKONONI MWA JESHI LA POLISI ,HASA KWA MAUAJI YA MWANDISHI YALIYOTOKEA AKIWA AMEZUNGUKWA NA POLISI WENGI TU. 2.TUNAMTAKA RAIS JK AVUNJE UKIMYA SASA JUU YA TABIA HII YA MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA KUUWAWA MBELE YA POLISI, KWA KUWAFUKUZA KAZI MARA MOJA IGP SAID MWEMA,MKUU WA OPERATION PAUL CHAGONJA NA RPC WA IRINGA KAMUHANDA ,NAHATA HIVYO RAIS NI MWEPESI SANA KUTOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA MISIBA INAYOGUSA TAIFA, NI VIPI KWA KIFO CHA DAUD BADO YUKO KIMYA? 3.POLISI KAMA WANAJIFUNZA KUUA RAIA WASIO NA HATIA BASI NASISI TUTAHAMASISHANA KUJIFUNZA KUFA,NA HATUTAOGOPA TENA KUFA KWA KUWA TUNAJUA TUSIPOKUFA LEO,TUTAKUFA KESHO NA TUSIPOKUFA KESHO IPO SIKU TUTAKUFA. 4.SERIKALI YA CCM IACHE KUTUMIA NGUVU YA DOLA KUTISHA ,KULETA HOFU WALA KUDHOOFISHA WANANCHI WASIENDELEE KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA CHADEMA,NA TUNA MTAKA KATIBU WA UVCCM TAIFA,MARTIN SHIGELA AACHANE NA PROPAGANDA ZENYE LENGO LA KUPOTOSHA UMMA NA KUTISHA VIJANA WASIKIUNGE MKONO CHADEMA. 5.BAVICHA SEGEREA TUNATANGAZA KUTOKUWA NA IMANI NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA,NA TUNAMTAKA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA AUELEZE UMMA KUNA TOFAUTI GANI KATI YA KAULI YAKE,NA KAULI YA WASIRA NA KAULI YA WAZIRI MKUU BUNGENI(AMBAYO NI YA SERIKALI NA NI YA CCM PIA) ILIYOLENGA KUTISHIA KUIFUTA CHADEMA,ILI HALI WAKIJUA WANAOUA WATU SIO CHADEMA BALI NI JESHI LA POLISI? NA ATUELEZE JE TENDWA NAE ANAKOSA AMANI KUFUATIA CHADEMA KUUNGWA MKONO NA WANANCHI HUKO VIJIJINI? NA MAENEO MENGINE NCHINI. 6.BAVICHA JIMBO LA SEGEREA TUNATOA RAI KWA VIJANA WOTE TANZANIA WANAOHITAJI MABADILIKO NA WENYE MTIZAMO CHANYA WA UKOMBOZI KUTOKA MIKONONI MWA MAFISADI, KUWA TAYARI KUPAMBANA NA NAMNA YOYOTE YA UONEVU,UKANDAMIZAJI,UDHALILISHAJI NA UBAGUZI WA NAMNA YOYOTE ILE. Imetolewa leo na uongozi wa BAVICHA (J) SEGEREA
  Daniel Raymond​
  M/Kiti​
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  Matola hakosi kwenye hili tamko...big up ujumbe umefika
   
 3. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana makamanda waziri aache propaganda za kitoto ajitokeze ajibu kwa nini serikali ya ccm inatumia polisi kuua raia wasiokuwa na hatia kama ambavyo imefanya huko Iringa, Tarime, Morogoro, Arusha na maeneo mengine.
   
 4. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali ya ccm ielewe kuwa Leo mauaji haya yanatuuma ila hatufanyi kitu, IPO SIKU maumivu yatatuinua, tutadharau damu, risasi, vitu vizito na mabomu ya machozi ili tuondoe maumivu yetu ya muda mrefu. zen huyo Tendwa msajili wa vyama vya siasa akitaka dunia ijue aanze na kukifuta CHAMA CHA MAPOLISI (CCM)
   
 5. M

  Mendelian Inheritanc Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana makamanda waziri aache propaganda za kitoto ajitokeze ajibu kwa nini serikali ya ccm inatumia polisi kuua raia wasiokuwa na hatia kama ambavyo imefanya huko Iringa, Tarime, Morogoro, Arusha na maeneo mengine.
   
 6. s

  sad JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tendwa ni kada wa c.c.m hana jipya zaidi ya kujipendekeza, na hata hivyo hana uwezo kwani kuna siku nilimwona katika kipindi cha this week perspective anashindwa kujieleza hata kwa kiingereza. hana uwezo wowte
  . zaidi tuhoji uwezo wake
   
 7. t

  tenende JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ila kiswahili anaongea kwa mapoozi!. TENDWA ni JANGA LA TAIFA = na WASIRA!.
   
 8. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hongereni segerea, tuko pamoja makamanda, japo kigugumizi kwa ASENGA kilijitokeza mliman TV, nadhani mazoea, ila mmetuakilisha makamanda kusoma tu kilichoandikwa pale ilikuwa shughuli kubwa..., tukaze buti, mungu yuko pamoja nasi
   
 9. R

  Rare JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nimependa kitu kimoja "tuhamasishane kutokuogopa kufa" hii itasaidia hasa Tendwa wakili wa dili la kishetani la kuua mabadiliko CDM. Anyway death is a sure post for any man born from a womb of a woman. Ndio maana huwa nashangaa watu wanapoogopa neno kumwaga damu wakati wote wametokana na tendo la mwanamama mmoja kukubali kuwa na kiumbe miezi tisa na kisha kumwaga damu, watu wanatahiriwa wanamwaga damu. Mwagosi kamwaga damu na utumbo kwa nini asiwe chachu bora ya kutuaambia kuwa tuwe msingi imara kwa kizazi kijacho kwa kukubali kuumia.
   
Loading...