Tamko la ACT-Wazalendo baada ya Kongamano lao kuzuiwa na Polisi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866

Baada ya Jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa Chama Cha ACT- Wazalendo kilipanga kufanya kongamao Jumapili ya June 12 2016 kwa lengo la kujadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017.

Taarifa iliyotolewa na chama cha ACT-Wazalendo kupitia kwa Mwenyekiti wa chama hicho Anne Mghwira imesema kwamba kongamano hilo lililenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa katika hali isiyo ya kawaida walipewa taarifa na mwenye ukumbi (LAPF Millenium Tower) kwamba polisi walikuwa wametanda katika eneo la ukumbi tangu saa kumi mbili asubuhi na ilipofika saa nne kamili asubuhi mwenye ukumbi aliwataarifu rasmi kuwa amepewa taarifa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kinondoni kwamba chama chao hakina kibali cha kufanya kongamano hilo na hivyo asiwafungulie ukumbi huo.

Hivyo kupitia taarifa hiyo chama ACT-Wazalendo kimesema kimesikitishwa sana na hatua hiyo ya polisi na wanaitafsri kuwa ni mwendelezo wa hatua za uhakika katika kufifisha demokrasia katika nchi.
 
Kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge hakukutoa fursa kwa zitto kufanya press namna hiyo!
 
Kwani hao ACT hawana Ofisi? Si wangefanyia kwenye ofisi yao? Wameyataka wenyewe
wengine walipojaribu kupita japo kusalimia ofisi zao Shinyanga walikuta tayari polisi walishatanda na kuzuiwa kuingia hata offisini kwao tu mkuu, japo kunywa hata maji. Sasa Ushauri ungefeli tu siku ya kutoa tangazo tutakuwa offisini kwetu ACT. Labda ungewashauri wakafanyie Chimwaga mpya au Lumumba.

Najaribu kuwaza
 
Itabidi wafanye ziara ya kushitukiza wakiambatana na kamera kujadili hiyo bajeti kama waheshimiwa wengine wanavyofanya wakiwa "wanatekeleza" majukumu yao au na yenyewe hairuhusiwi kwa vyama vya upinzani?
 
Vyama vya kwenye briefcase navyo vinatafuta umaarufu kwa nguvu
Zitto alituambia ndege hazitapaa mwezi huu,naona tu midege inaingia na kutoka
 
Back
Top Bottom