Tamko kuhusu Shutuma juu ya Kitila Mkumbo (Mjumbe Kamati Kuu ya CHADEMA)

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
TAMKO KUHUSU SHUTUMA JUU YANGU KITILA MKUMBO(MJUMBE KAMATI KUU YA CHADEMA)
TAR.10/11/2013

(https://www.facebook.com/kitila.mkumbo.3/posts/10152401804973289)

Kufuatia taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuhongwa kwa Zitto naye kuhonga watu wengine, nikiwemo mimi, ili kutoa siri za chama chetu (CHADEMA) kwa lengo ya kukivuraga watu, wengi sana wameniandikia email, sms na hapa fb ili nitoe ufafanuzi kuhusu ukweli wa mimi kuhongwa na Zitto na mahusiano yangu na mwanasiasa huyu nguli. Mwanzoni nilipuuzia na sikutaka kabisa nitoe maoni kuhusu jambo hili kutokana na kiwango cha ujinga kilichomo ndani ya waraka huo unaosambazwa. Hata hivyo kwa kuwa watu wengi wamenitaka nitoe ufafanuzi, napenda kueleza haya yafuatayo:

i) Mimi Kitila Mkumbo, pamoja na umaskini wangu, sijawahi kuhongwa popote na sitarajii kuhongwa. Taarifa zinazosambazwa juu yangu ni za uwongo wa kijinga na uzushi wa kitoto kwa malengo ya siasa nyepesi. Ni wazi kwamba wanaosambaza habari chafu juu yangu hawanijui na ndiyo maana wanaweza kudiriki kuzusha kwamba mie Kitila Mkumbo naweza kuhongwa sh. 200,000/=. Hakuna namna nyingine ya kuthibitisha kwamba waraka huu na maudhui yake ni mambo ya kutunga zaidi ya hilo la kuzusha kwamba nami ni miongoni mwa watu waliohongwa.

ii) Kuhusu mahusiano yangu na Zitto ni kwamba kijana huyu ni rafiki yangu wa miaka mingi tuliyejuana na kuanza urafiki kabla ya hata mie kuijua CHADEMA. Urafiki wetu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo ndani na/au nje ya siasa. Wasiopenda hili poleni sana. Mie ni mtu mzima na hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kunichagulia marafiki na/au maadui.

iii) Wanaosambaza waraka huu ni watu woga wa demokrasia na wasioijua CHADEMA. Chama hiki kimejipambanua kwa miaka mingi kwamba ni chama kinachopigania demokrasia ndani na nje ya chama. Matatizo yetu hushughulikiwa kikamilifu ndani ya vikao ambapo huwa tunajadili mambo kwa upana. Watu wenye makosa husutwa, huonywa na ikibidi huadhibiwa. Kama kweli haya yanayosambazwa yangekuwa na hata chembe ya ukweli, na kama kweli waraka huu umetoka makao makuu ya chama, sioni ni kwa nini jambo hili zito kiasi hiki haliletwi kwenye vikao vya chama na sisi tunaotuhumiwa kukivuruga chama tushughulikiwe kwa mujibu wa taratibu kama ambavyo watu wengi wamewahi kushughulikiwa ndani ya chama chetu kwa makosa waliyotenda.

iv) Ni vizuri tukajenga utamaduni wa kuhoji mambo badala ya kuyameza kana kwamba tunasoma msaafu. Hivi huyo mtu anayemhonga Zitto bilioni mbili (2,000,000,000) ili atoe siri za chama, ni siri gani hizo ambacho chama cha siasa kinazo ambazo ni za hatari hata itolewe hongo kama hiyo?

v) Ninasikitishwa na idara ya uenezi wa chama chetu kukaa kimya bila kutoa maelezo juu ya jambo hili, hasa pale ambapo tumeambiwa waraka huu umetoka makao makuu. Hii si kawaida kwa idara yetu hii nyeti iliyosheheni watu mahiri. Mara zote huwa wepesi kabisa kwa vijana wetu katika idara hii kutoa ufafanuzi, tena kwa mambo mepesi kabisa yanayokigusa chama, vipi makamanda kwenye jambo hili imekuwaje?

v) Mwisho kama kuna watu walidhani kwamba kwa uzushi huu watanikatisha tamaa na kunirudisha nyuma katika kutoa mchango wangu wa kuimarisha siasa ya vyama vingi hapa nchini, na kuijenga CHADEMA kama chama mbadala imara wamekosea. Nipo imara na nitaendelea kutoa mchango wangu kikamilifu. Poleni sana wote mliokwazwa na jambo na ufafanuzi wangu ndio huo.
 
Nafikiri Kitila naye ameingia kwenye mtego wa kuilaumu idara ya Uenezi badala ya kuweka wazi jambo hili ili lianze kuchunguzwa , kuna haja ya yeye kama mwalimu kuonyesha njia , ila alivyo jibu ni kama anata futz mtu wa kumsuta na kumlaumu, hii sio sahihi, kwa maoni yangu.

tuntemeke , mpasuko uko uko wapi hapo? Au hukutaka afafanue japo njia aliyotumia sio sahihi?
 
Yeah ni bora kamanda umeamua kusema mwenyewe, wale wote waoga wa chadema wanahangaika sasa kujaribu kuchonganisha watu bila sababu, Maafisa wa habari wa chadema kwa hapa mmepotoka kuzinyamazia hizi tuhuma mpaka leo na hiki kitu ndo kinachofanya huu mjadala usiiishe hata, hongera sana kamanda kwa kutoyumba kimsimamo
 
Hongera sana kamanda Mkumbo kwa ufafanuzi. Mimi najua wazi kuwa taarifa hiyo imeandaliwa kwa ustadi mkubwa na watu wa usalama wa taifa kwa ajili ya kuwakatisha tamaa baadhi ya watu, kujenga kutoaminiana, kujenga hofu na mwisho kukigawa chama. Ni vizuri chama kikawa makini katika kushughulikia jambo kama hili
 
I have seen people plough fields of evil and sow wickedness like seed, now they harvest wickedness and evil.

Nyie Viongozi mnaotuhumiwa jiulizeni nafsini mwenu, mlipanda nini? Kwani mwisho wa yote hakika mtavuna mlicho panda.
 
Aeleze ukweli sio kulaumu idara ya hbri,lkn ukifatilia kwa umakini na historia ya mkumbo akiwa daruso utapata shida kumwamini
 
Nakupongeza Bw.Kitila.lakini kwa nia njema tu naomba niulize;Je,Mh.Zito aliwahi kukutumia pesa kwa njia ya simu ya mkononi ktk kipindi kilichoelezwa kuwa alikuhonga?
 
Tuntemeke hivi wewe si ulifukuzwa chadema,mbona bado unashabikia tena,au roho inakuuma sanabukiona chadema bado ipo?na kwa heading yako unaonyesha ni fitina,mpasuko uko wapo hapo?kwani Kitilya amekwambia anajitoa chadema au umemuelewaje?
Omba msamaha na uombe uanachama upya labda utafikiriwa.
 
Dr Kimei naye anajiandaa kuwapeleka mahakamani wote walio mchafua kuwa alimpa Zitto alienda kuchukua pesa kwake.Vijana wa wanaodhani chadema ni yao na kusambaza habari za uongo kwenye mtandao watamtaja tu aliyewatuma.
 
Naona TUNTEMEKE ametoka mafichoni kutetea kundi haramu la Masalia lililokwisha kuzikwa siku nyingi zilizopita.

BTW:Mwl wangu Kitila umeonyesha hekima katika tamko lako.
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kamanda Mkumbo kwa ufafanuzi. Mimi najua wazi kuwa taarifa hiyo imeandaliwa kwa ustadi mkubwa na watu wa usalama wa taifa kwa ajili ya kuwakatisha tamaa baadhi ya watu, kujenga kutoaminiana, kujenga hofu na mwisho kukigawa chama. Ni vizuri chama kikawa makini katika kushughulikia jambo kama hili

Taarifa haina ustadi wowote ni ya kiwango cha chini sana haina hata chembe ya ukweli.Imeandaliwa na watu wenye akili ndogo ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom