Tamko juu ya tiba asilia na tiba mbadala dhidi ya ugonjwa wa Corona litoke mapema

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Sera ya afya ya 2007 imekiri kuwa takribani asilimia sitini ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa na maradhi kabla ya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya. Aidha, hivi karibuni tiba mbadala imepata umaarufu miongoni mwa wananchi kutokana na uimarikaji wake duniani. Kadhalika, wagonjwa hutoka hospitalini na kwenda kutafuta tiba asilia au kutumia aina zote za tiba kwa pamoja.

Pamoja na madhumuni ya sera hiyo ya kuendeleza, kuratibu na kuboresha utoaji wa huduma za tiba asilia, mbadala na ukunga wa jadi. Na matamko ya sera juu ya kanuni na miongozo. Iko haja ya serikali kutoa tamko kwa kipindi hiki cha tishio la Corona ili hizi ‘pseudo means’ zisipewe nafasi kubwa wakati huu.

Siku za hivi karibuni mara baada ya ugonjwa wa corona kuanza kuonyesha makali yake, wachungaji na wanaojiita manabii walianza kuonyesha kuwa na uwezo wa kutibu corona huku wengine wakataka wapelekwe Wuhan, China ili wakasaidie.

Kwa kuwa imani hizi ziko nyingi sana kwetu kama sera ilivyokiri, iko haja ya serikali kutoa tamko la haraka ili itakapotokea kwa watanzania wakipata gonjwa hili wasianze kuamini tiba asilia na mbadala kabla ya tiba halisi.

Kwa kuwa ‘consipiracy’ kuhusu gonjwa hili zimeshaanza kuenea. Wakiaminishwa gonjwa lilitengenezwa na lilitabiriwa wakitumia kitabu cha Dean Khoontz, ‘The eyes of Darkness’, pia filamu ya ‘Contagion’ ya mwaka 2011 hali inaweza kuwa mbaya na watu wakagomea tiba kama wakongo walivyowahi kugomea tiba katika mlipuko wa ebola. Ni ngumu kwa sasa kuwafundisha watu kuhusu ‘Texas sharpshooters fallacy’.

Lakini watu hao wakiendelea kuamini gonjwa limetengenezwa, na wakawaamini wachungaji na watu wa tiba asilia na mbadala ipo hatari kubwa inaweza kutokea.

Hivyo kwa kuwa sera ya afya inajua imani za watu wake, ni muhimu kuweka mambo sawa apema kabla hali haijawa mbaya kivyovyote vile.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom