TAMISEMI yapiga marufuku walimu kuweka rehani Kadi za Benki ili kujipatia mikopo

Hajiongezi akajiuliza kwa nini walimu!!!!
Kwanini siyo maafisa elimu?
Kwanini siyo wakurugenzi?

Mwalimu anatumia mshahara wake kwa nauli kwenda na kurudi kazini, mwalimu anatumia mshahara wake kulipa kodi ya nyumba, mwalimu anatumia mshahara wake kupiga simu juu ya masuala ya kazi, na zaidi ya hapo mshahara huohuo mdogo ndiyo atunzie familia nk

Lakini pia kwa kiwango kilekile cha elimu mwingine analipwa millions mwalimu analipwa laki kadhaa

Ningemwona huyo afisa ana akili angewapigania walimu waboreshewe maslahi badala ya kuwalaumu
Aache longolongo kama wana akili walipe madeni ya hao walimu. Serikali inadaiwa haitaki kulipa huku inajifanya kuwa na huruma kwa walimu! Acheni unafiki huna cha kusema kaa kimya.!!
 
Walimu wengi wa Tanzania hawana akili, nikiweka kadi rehani, si naenda benki kuchukua kadi nyingine na mkopo umiza siulipi
Kuna mjanjamjanja kama wewe alikopa 20 elfu akawa anakwepa kulipa, riba ikapanda hadi laki 9. Siku hana hili wala lile , ndani ya arobaini za mwizi akabambwa .Alitaitiwa akalipa
 
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), imewataka walimu kujiepusha kuweka rehani kadi zao za benki(ATM), wanapokopa mikopo kwenye Taasisi za Fedha.

Aidha, imeagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi mwalimu yeyote atakayebainika mlevi na mtoro kazini.

Naibu Katibu, Mkuu wa Ofisi hiyo, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Ilboru, jijini hapa Arusha.

Alisema kuna taarifa za walimu wanapokopa wanaacha ATM zao.

“Mara nyingi nilikuwa nikitembea kwenye Halmashauri nasikia kuna tatizo la walimu wanakopa hadi wanaacha ATM kadi, najua hapa hawapo, eti kuna wale wa kuacha ATM kadi hapa?, tukisema tuweke mezani zipo?,”alihoji.

Aliongeza “Nashukuru nilipofika hapa Ilboru nimeambiwa walimu wote wana ATM sio kama wale wa maeneo mengine kule wanapokopa, niwapongeze sana.”

Ippmedia
Kuwachukulia nidhamu kwa kulewa upo sahihi. Kuhusu kadi za atm, sio sahihi, ni kuingilia uhuru binafsi. Tafuta chanzo cha tatizo, wakuu nyama ya kasungura mnakula pekee yenu, walimu mnawapa kapande ukubwa wa kaukucha ka mtoto.
 
Kuwachukulia nidhamu kwa kulewa upo sahihi. Kuhusu kadi za atm, sio sahihi, ni kuingilia uhuru binafsi. Tafuta chanzo cha tatizo, wakuu nyama ya kasungura mnakula pekee yenu, walimu mnawapa kapande ukubwa wa kaukucha ka mtoto.
Kulewa kwangu kuna muhusu nini!?
 
Huyu naibu hajielewi,kukopa ni hiari ya mtu.
Angejikita kwenye kupandisha madaraja na kuongeza mishahara sio huo utumbo
 
Walimu wengi wa Tanzania hawana akili, nikiweka kadi rehani, si naenda benki kuchukua kadi nyingine na mkopo umiza siulipi
Hiyo kadi mpya unapataje bila kukabidhi kadi ya zamani. Otherwise uwe na loss report.
Hali ya watumishi waliopo serikalini ni ngumu sana kuliko FORM 4 leaver aliopo TANESCO, TPA, TRA, TIC, NSSF, PSSSF, LAPF, WMA, TMA, ATCL, TTCL, TPB, NBC, TPS, TLS, TANAPA, NCAA, na mengine mengi.
Nimewahi piga kazi hotel moja kila siku tunapeleka breakfast na lunch kwenye ofisi za TANESCO na NSSF msosi wa bei kubwa wa adabu meanwhile mwalimu hata chai ya mkono mmoja hakuna fungu anawekewa. Na kama anaipata ni kwa njia ya magendo. Aiseeeeee nji hiiiiiii
 
Back
Top Bottom