TAMISEMI yapiga marufuku walimu kuweka rehani Kadi za Benki ili kujipatia mikopo

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), imewataka walimu kujiepusha kuweka rehani kadi zao za benki(ATM), wanapokopa mikopo kwenye Taasisi za Fedha.

Aidha, imeagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi mwalimu yeyote atakayebainika mlevi na mtoro kazini.

Naibu Katibu, Mkuu wa Ofisi hiyo, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Ilboru, jijini hapa Arusha.

Alisema kuna taarifa za walimu wanapokopa wanaacha ATM zao.

“Mara nyingi nilikuwa nikitembea kwenye Halmashauri nasikia kuna tatizo la walimu wanakopa hadi wanaacha ATM kadi, najua hapa hawapo, eti kuna wale wa kuacha ATM kadi hapa?, tukisema tuweke mezani zipo?,”alihoji.

Aliongeza “Nashukuru nilipofika hapa Ilboru nimeambiwa walimu wote wana ATM sio kama wale wa maeneo mengine kule wanapokopa, niwapongeze sana.”

Chanzo: IPP Media
Haaaaa Anaongea wenyewe halafu anajijibu mwenyewe
 
Bila kuacha kodi maana yake hakuna mkopo.
Walimu wana madeni chungu nzima
Imefikia hadi wanaenda kukopa kwenye taasisi ndogondogo maana benki hawakopesheki

Huko sasa inawabidi waache kadi zao..
Mwisho wa mwezi anaenda kuchukua kamshahara huko,mwingine unalipa deni.
Kadi anarudishiwa akishamaliza makato ya deni.

Hii imepelekea hali kuwa mbaya zaidi,,ni vema wangeanza kwanza kutatua kiini cha tatizo.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Inaudhi na kusikitisha sana wakati kanunua mandege ya trillion 3 yanayopigwa na vumbi na kuingiza hasara ya mabilioni.
Walimu wana madeni chungu nzima
Imefikia hadi wanaenda kukopa kwenye taasisi ndogondogo maana benki hawakopesheki

Huko sasa inawabidi waache kadi zao..
Mwisho wa mwezi anaenda kuchukua kamshahara huko,mwingine unalipa deni.
Kadi anarudishiwa akishamaliza makato ya deni.

Hii imepelekea hali kuwa mbaya zaidi,,ni vema wangeanza kwanza kutatua kiini cha tatizo.
 
Biashara ya safari za anga ni ngumu sana ina ushindani mkubwa sana na mashrika yaliyoanza biashara hiyo kabla ya ATCL nayo bado yanaingiza hasara kubwa sana kama vile Kenya Airways na Rwanda.
Lakini nadhani ni kwa sababu ya hii Corona..
Baadaye mambo yatakuwa sawa
 
Biashara ya safari za anga ni ngumu sana ina ushindani mkubwa sana na mashrika yaliyoanza biashara hiyo kabla ya ATCL nayo bado yanaingiza hasara kubwa sana kama vile Kenya Airways na Rwanda.
Lakini isipokuwepo kabisa huoni kama ni hatari zaidi?
 
Huyo msela aliyeropoka huo utumbo hana akili kaabisa yaani!!

Yaani kwa ujumla yeye ni matope. Kwanza hajui kitu akikua pengine ataacha.
😈😈😈😈😈😈😈😈😈😈😈😈😈

Nimemind kinyama yaan.
 
Unajua viongz wa Afric wanadili Hadi na vitu binafsi

Kwann wasiwek sheria za kukataz mchakato huo Hadi kutOa kaul Kam hizo

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), imewataka walimu kujiepusha kuweka rehani kadi zao za benki(ATM), wanapokopa mikopo kwenye Taasisi za Fedha.

Aidha, imeagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi mwalimu yeyote atakayebainika mlevi na mtoro kazini.

Naibu Katibu, Mkuu wa Ofisi hiyo, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Ilboru, jijini hapa Arusha.

Alisema kuna taarifa za walimu wanapokopa wanaacha ATM zao.

“Mara nyingi nilikuwa nikitembea kwenye Halmashauri nasikia kuna tatizo la walimu wanakopa hadi wanaacha ATM kadi, najua hapa hawapo, eti kuna wale wa kuacha ATM kadi hapa?, tukisema tuweke mezani zipo?,”alihoji.

Aliongeza “Nashukuru nilipofika hapa Ilboru nimeambiwa walimu wote wana ATM sio kama wale wa maeneo mengine kule wanapokopa, niwapongeze sana.”

Chanzo: IPP Media
Kwanini viongozi hawatambui mishahara na marupurupu ya walimu ni kiduchu?!
Waongelee mbadala basi..?!
 
Walimu wengi wa Tanzania hawana akili, nikiweka kadi rehani, si naenda benki kuchukua kadi nyingine na mkopo umiza siulipi
Basi na wewe huna akili. Kwa kuwa wasio na akili ndiyo waliokufundisha mambo mengi yasiyo kuwa na akili.
 
Back
Top Bottom