TAMISEMI yapiga marufuku walimu kuweka rehani Kadi za Benki ili kujipatia mikopo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), imewataka walimu kujiepusha kuweka rehani kadi zao za benki(ATM), wanapokopa mikopo kwenye Taasisi za Fedha.

Aidha, imeagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kufukuzwa kazi mwalimu yeyote atakayebainika mlevi na mtoro kazini.

Naibu Katibu, Mkuu wa Ofisi hiyo, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Ilboru, jijini hapa Arusha.

Alisema kuna taarifa za walimu wanapokopa wanaacha ATM zao.

“Mara nyingi nilikuwa nikitembea kwenye Halmashauri nasikia kuna tatizo la walimu wanakopa hadi wanaacha ATM kadi, najua hapa hawapo, eti kuna wale wa kuacha ATM kadi hapa?, tukisema tuweke mezani zipo?,”alihoji.

Aliongeza “Nashukuru nilipofika hapa Ilboru nimeambiwa walimu wote wana ATM sio kama wale wa maeneo mengine kule wanapokopa, niwapongeze sana.”

Chanzo: IPP Media
 
Kwahio hili katazo ni kwa waalimu pekee ? Kwani waalimu wote wana ATM na kuwa na ATM ni kigezo cha kuwa waalimu?

Haya ni matatizo ni kukata matawi badala ya kuondoa mizizi, kama ni kuvunja sheria kwa wadai kuchukua ATM za watu kwanini wasiwakataze hao wadau?

Pili kama waalimu wamezidi kukopa (na hawana collateral ya kuweza kuacha) na inabidi wakope labda maisha yao na ya kila mtanzania kipato hakikidhi mahitaji.
 
Muhimu waboreshe maslahi yao

Mwalimu au Mtumishi wa Umma hajaongezewa mshahara kwa miaka 6 sasa ili hali gharama za maisha zikipanda, ataachaje kukopa na kuacha kadi za benki.

Siku hizi wanakopea hadi Salary advance seuse hizo ATM cards 😀😀
 
Naibu Katibu, Mkuu wa Ofisi hiyo, anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na walimu na watumishi wa Shule ya Sekondari Ilboru, jijini hapa Arusha.
Hajiongezi akajiuliza kwa nini walimu!

Kwanini siyo maafisa elimu?

Kwanini siyo wakurugenzi?

Mwalimu anatumia mshahara wake kwa nauli kwenda na kurudi kazini, mwalimu anatumia mshahara wake kulipa kodi ya nyumba, mwalimu anatumia mshahara wake kupiga simu juu ya masuala ya kazi, na zaidi ya hapo mshahara huohuo mdogo ndiyo atunzie familia nk

Lakini pia kwa kiwango kilekile cha elimu mwingine analipwa millions mwalimu analipwa laki kadhaa

Ningemwona huyo afisa ana akili angewapigania walimu waboreshewe maslahi badala ya kuwalaumu
 
Back
Top Bottom